7 October 2015

YOU MUST NEVER FORGET WHO WAS THERE FOR YOU WHEN NOBODY ELSE WAS!

 John Shabani na Alex Msama wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya kutambulishwa kama watendaji wa kampuni ya Msama Promotions, ni katika tamasha lililo andaliwa na kampuni ya hiyo miaka kadhaa iliyopita.

 John Shabani akiwajibika ofisini



Nimekumbuka miaka kadhaa iliyopita tangu mwaka 2004 nikifanya kazi kama msaidizi wa Msama na baadaye nikiwa kama mtaalam na mwalimu wa nyimbo za injili nikiwashauri waimbaji na kuakiki kazi za waimbaji waliokuwa wakizileta katika kampuni ya Msama Promotions.

Nimekumbuka tukiwa kwenye chumba kimoja pale mwananyamala na baadaye kuhamia kinondoni, nimekumbuka wakati ambao nilitembea kwa mguu nikitokea ofisini baada ya kutokuwa na nauli ya kurudi nyumbani na wakati mwingine nililazimika kulala ofisini bila kumwambia mkurugenzi wangu kwani hali ya kifedha ilikuwa mbaya, nimekumbuka wakati nilipobaki ofisini peke yangu wakati wafanya kazi wengine wakishindwa kuvumilia pale ambapo hali ya mshahara haikuwa vizuri, kuna wakati nilifanya kazi kama msaidizi, wakati mwingine kama katibu, wakati mwingine kama mratibu wa masuala Fulani ya kiofini; 
na leo hii Msama Promotions imekuwa ni moja ya makapuni makubwa inayoweza kuandaa matamasha makubwa yanayohudhuriwa na maelfu ya watu.

Ujumbe wangu kwako:
“USIMSAHAU  YULE ALIYESIMAMA NA WEWE KATIKA MWANZO WAKO MDOGO”

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP