THE OFFICIAL JOHN SHABANI AND GOSPEL IN AFRICA BLOG

Welcome to the official blog of the the gospel singer, songwriter and teacher John Shabani. If you are one of the fans among the millions, feel free to get connected with John Shabani and stay updated on this blog.To learn more about John Shaban and his Ministry, please click the about button above.

GET THE LATEST FROM JOHN SHABAN AND THE GOSPEL NEWS COMMUNITY

You will be able to read and review the latest news on John Shabani's tour and other specials. You will also come across the best articles of news on Gospel from all across Africa and the International Community.Please do feel free to review our categories of news and events.

FEEL FREE TO LEARN MORE ABOUT JOHN SHABANI AND HIS MINISTRY

If you wish to learn more about John Shabani and his ministry, please feel free to connect with John Shabani on the social networks. You can keep up with John Shabani and the Gospel in Africa community on both twitter, facebook, google plus and many other more.

STAY UPDATED WITH INTERNATIONAL AND LOCAL GOSPEL NEWS

Gospel in Africa Blog is a comprehensive gathering place for African Gospel music fans. Offering the latest news and information about Local and International Gospel music and news, Gospel in Africa Blog also shares the spotlight with other genres of Christian music that more than ever, seemingly overlap musical genre lines, such as Bluegrass Gospel, Christian Country and others. Singing News, the leading African Gospel and International music Blog, features African and international Gospel lyrics, radio, news, Christian concerts, songs, artists, and more.

GET IN TOUCH AND STAY CONNECTED WITH JOHN SHABANI

If you are interested in contacting and staying in touch with John Shabani then here are the contacts. E- mail: touchingvoice@yahoo.com or , princejohntz@yahoo.com, Mob: +255 754 818 767 or +255 716 560 094, www.facebook.com/john.shabani.

20 June 2014

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI DEBORA SAID AFARIKI DUNIA



Mama Askofu, mwimbaji wa injili na mjumbe wa chama cha muziki wa injili, debora John Said hatunaye tena kimwili!...
Gospel in Africa imepokea kwa masikitiko makubwa sana juu ya kifo cha Debora, tunawapa pole wafiwa na Watanzania wote na kupotelewa na mtumishi wa Mungu na kipenzi cha wengi, mama Askofu John Said, mwimbaji na mjumbe wa chama cha muziki wa Injili Tanznzania, ambaye amefanya kazi yake kwa upendo na uaminifu. Mungu azidi kuipigania familia  na wale wote waliokuwa wakimtegemea kiroho na kimwili. Ni wakati wa waimbaji wa nyimbo za injili kujifunza jambo, kurudiaha umoja na upendo aliotuachia Yesu. Sisi tuliobaki tuzidi kumtumikia Mungu kwani hatujui vilivyombele yetu.
 Huu ni wakati wa kuungama na kutubu makosa tunayoyafanya katika maisha yetu hapa duniani. Mungu amekupa kipaji fulani kwa kazi yake basi kitumia na usiache. Debora amefanya kazi ya Mungu kwa njia ya uimbaji kwa umaminifu mwingi, bila skendo, bila majivuno wala majigambo, amekuwa ni mshauri mzuri, hakuwa na wivu kabisa, na sasa ametangulia.

IBADA YA KUMUAGA ITAFANYIKA JUMATATU SAA NNE ASUBUHI KATIKA KANISA LA MAISHA YA USHINDI MABIBO EXTERNAL NA BAADAYE SAA NANE MCHANA MAZISHI KATIKA MAKABURI YA MABIBO JESHINI.

John Shabani
Katibu chama cha muziki wa injili Tanzania

17 June 2014

CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA KUKULETEA MBEYA GOSPEL FESTIVAL

Hawa ni wachache kati ya wengi watakaomtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji, maigizo pamoja na neno la Mungu siku hiyo.

Uongozi wa Chama cha muziki wa Injili Tanzania unawakaribisha wakaaji wote wa mbeya na maeneo ya jirani, kuja kubarikiwa na waimbaji mbalimbali wa injili kutoka mikoa mbalimbali. Lengo likiwa kwanza ni kumtumikia Mungu, kuhamasisha watu kujiunga na chama ili kudumisha umoja wetu; Kumbuka umoja ni nguvu.
Karibuni sana.

MUME MWEMA NI YUPI?

Ni maswali ambayo majibu yake yana utata mwingi, wengine wakidhani kuwa wamepata mwisho wa siku ni majuto, na wengine wakionekana kuwa ndivyo sivyo kumbe wamepatia...


Swali langu ni hili:
Hivi unapoomba Mungu akupe mume mwema, una maanisha nini?
Je ni mume ambaye anajali familia pia ana upendo kwa familia yake? Ni msomi, mwenye kipato kizuri, mtanashati au aliyeshikilia dini sana au mtu wa sala? . Mungu anajibu maombi kwa aina nyingi sana lakini wanadamu huwa tunapingana na mpango wa mungu

Mume mwema hatoki kwa ATM ao sio awe kama ATM eti ndo mume mwema , mume mwema sio muonekano ao kuwa anamilika nyumba, magari, kazi ya juu, ao kabila . Tumeshuhudia mara nyingi watu walikimbilia kuolewa na masupasta, matajiri au vijana watanashati lakini mwisho wake ni vilio, na wengine kupelekana kaburini. Sijapinga  suala la kuwa na chagua la aina ya mwenzi unayemtaka, lakini Mungu apewe nafasi ya kwanza katika maamuzi

Ebu angalia picha hii jinsi wanavyopendeza.
kila mtu  vyovyote vile alivyo anaweza kuwa mume mwema!...

15 June 2014

ON FATHER’S DAY MWANZILISHI WA KANISA LA T.A.G MAGOMENI AMEKABIDHIWA ZAWADI YA GARI

Hapa Mch. Sasali akijiandaa kukata utepe wa zawadi ya Gari alilokabidhiwa na kanisa la T.A.G Magomeni





Hilo hapo gari lenyewe



 Sasali family: Mch. Sasali, Mch. Matthew Sasali, 
                                      Happy Sasali, Mama yetu, Samuel Sasali na Joel Sasali

Natanguliza ujumbe huu kutoka ukura wa facebook wa  Sam Sasali:
On Father's Day Dad and Mum wamepokea zawadi ya Toyota Xtrail kutoka kwa Kanisa la Magomeni TAG Magomeni Kama Ishara ya Kutambua Ubaba wake. Happy Fazas Day. God bless u Pastor Dunstan Kanemba. Happy Birthday”.

Ninachoweza kukisema ni kama vile ambavyo wengine wameshasem; Katika vitu ambavyo vimenibariki leo ni kupata taarifa ya habari njema sana kwangu kwamba Mch. Sasali (Sr.) amepewa zawadi ya gari 4WD na kanisa ambalo amelilea sana kwa miaka mingi, Magomeni TAG. Nakumbuka Miaka kadhaa iliyopita nikiwa mwalimu wa kwaya na shemasi katika kanisa la T.A.G Mwanga Kwa Askofu Mulenda Omary, Kati ya watumishi walinibariki sana ni Mch. Nathaniel Sasali, kipindi hicho akiwa mwinjilisti wa kitaifa wa Tanzania Assemblies Of God. 

Nilijikuta nikiwa na Spiritual connection na mtumishi huyo; na baada ya muda mfupi nilijielekeza Dar na ghafla nikawa mwalimu wa kwaya ya hapohapo magomeni T.A.G

Moja ya watumishi walionifanya niwe hivi nilivyo na nitakavyokua, ni Mzee Nathanieli Sasali. Kuna kitu kizuri sana pale tunapotambua michango ya wachungaji na watumishi wa Mungu ambao ni genuine, katika ujana wao na utu uzima wao, hawa wazee wamekuwa wanamtumikia Mungu sio kwa sababu "huduma inalipa" ila kwa sababu wana wito.


Ahsanteni sana Magomeni TAG,  kwa kutambua mchango wa Baba!

12 June 2014

WAIMBAJI WA INJILI WALIOOA NA KUOLEWA

 Mr & Mrs John Lisu

 Jojo Jose & Matilda

 Stella Joel & husband

 Mr & Mrs David Robert

Mr &Mrs Addo November

 Mr & Mrs Joshua Makondeko



 Mr & Mrs Jangalason

Jesca BM & Husband

 Mr & Mrs Bony Mwaitege









Upendo Nkone & Husband

Mr & Mrs Victor Aron



Nimeweka habari hii baada ya kuambiwa mara nyingi eti karibu waimbaji wengi wa injili Tanzania hawajaoa au kuolewa, mimi nasema si kweli, kwa kuthibitisha hilo hawa hapa chini ni baadhi ya waimbaji wachache kati ya wengi wenye ndoa zao.

Kuoa ni mpango kamili wa Mungu, hivyo wenzangu namimi foleni hii imesogea sasa ebu tuingie katika taasisi hii ili kutimiza haki yote na pia kujihepusha na maswali yasiyokuwa na sababu…
Kwa wale nilioweka picha zao, samahani kama nimemkwaza mtu, hasa kwa wale wasiotaka kujulikana kwamba ameoa au kuolewa, lakini pia picha hizi sijazipata mbinguni, 
ni humuhumu mtandaoni

Mungu awabariki wana ndoa
Mungu wasaidie wale ambao bado
Amen!

9 June 2014

WAJANE WATOKWA NA MACHOZI YA FURAHA BAADA HUDUMA YA RLM KUWAKUMBUKA



 Mtumishi wa Mungu, Mary Lutumba akitoa zawadi ya upendo kwa wajane

 Mtumishi David Lutumba akiwatia moyo kina mama hao baada ya kuwapa pesa za kujikimu ki maisha

 Mama akitokwa na machozi ya furaha




Ni katika semina kubwa iliyoandaliwa na huduma ya River of Life – Mlima wa mabadiliko ikiongozwa na watumishi wa Mungu, Mary na David Lutumba. Ujumbe wa semina ulikua:
“KUKOMESHA  MSIBA WA MWANAMKE” (marko 5:34)Wanawake na kinamama  wengi wamefunguliwa katika semina hiyo.

Kama ilivyo kawaida ya blogu hii yenye wapenzi wengi duniani, lengo letu ni kutangaza huduma mbalimbali, tutaendelea kukujulisha mengi zaidi kuhusu huduma hiyo na wapi wanapatikana, endelea kufuatilia hapahapa!...

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP