Hapa Mch. Sasali akijiandaa kukata utepe wa zawadi ya Gari alilokabidhiwa na kanisa la T.A.G Magomeni
Hilo hapo gari lenyewe
Sasali family: Mch. Sasali, Mch. Matthew Sasali,
Happy Sasali, Mama yetu, Samuel Sasali na Joel Sasali
Natanguliza ujumbe huu kutoka ukura wa facebook wa Sam Sasali:
“On Father's Day Dad and Mum wamepokea zawadi ya Toyota
Xtrail kutoka kwa Kanisa la Magomeni TAG Magomeni Kama Ishara ya Kutambua Ubaba
wake. Happy Fazas Day. God bless u Pastor Dunstan Kanemba. Happy Birthday”.
Ninachoweza kukisema ni kama vile ambavyo wengine wameshasem;
Katika vitu ambavyo vimenibariki leo ni kupata taarifa ya habari njema sana
kwangu kwamba Mch. Sasali (Sr.) amepewa zawadi ya gari 4WD na kanisa ambalo
amelilea sana kwa miaka mingi, Magomeni TAG. Nakumbuka Miaka kadhaa iliyopita
nikiwa mwalimu wa kwaya na shemasi katika kanisa la T.A.G Mwanga Kwa Askofu
Mulenda Omary, Kati ya watumishi walinibariki sana ni Mch. Nathaniel Sasali,
kipindi hicho akiwa mwinjilisti wa kitaifa wa Tanzania Assemblies Of God.
Nilijikuta nikiwa na Spiritual connection na mtumishi huyo; na baada ya muda
mfupi nilijielekeza Dar na ghafla nikawa mwalimu wa kwaya ya hapohapo magomeni
T.A.G
Moja ya watumishi walionifanya niwe hivi nilivyo na
nitakavyokua, ni Mzee Nathanieli Sasali. Kuna kitu kizuri sana pale
tunapotambua michango ya wachungaji na watumishi wa Mungu ambao ni genuine, katika
ujana wao na utu uzima wao, hawa wazee wamekuwa wanamtumikia Mungu sio kwa
sababu "huduma inalipa" ila kwa sababu wana wito.
Ahsanteni sana Magomeni TAG, kwa kutambua mchango wa Baba!
0 comments:
Post a Comment