Mama Askofu, mwimbaji wa injili na mjumbe wa chama cha muziki wa injili, debora John Said hatunaye tena kimwili!...
Gospel in Africa imepokea kwa masikitiko makubwa sana juu ya
kifo cha Debora, tunawapa pole wafiwa na Watanzania wote na kupotelewa na
mtumishi wa Mungu na kipenzi cha wengi, mama Askofu John Said, mwimbaji na
mjumbe wa chama cha muziki wa Injili Tanznzania, ambaye amefanya kazi yake kwa
upendo na uaminifu. Mungu azidi kuipigania familia na wale wote waliokuwa wakimtegemea kiroho na
kimwili. Ni wakati wa waimbaji wa nyimbo za injili kujifunza jambo, kurudiaha umoja
na upendo aliotuachia Yesu. Sisi tuliobaki tuzidi kumtumikia Mungu kwani
hatujui vilivyombele yetu.
Huu ni wakati wa kuungama na kutubu makosa
tunayoyafanya katika maisha yetu hapa duniani. Mungu amekupa kipaji fulani kwa
kazi yake basi kitumia na usiache. Debora amefanya kazi ya Mungu kwa njia ya
uimbaji kwa umaminifu mwingi, bila skendo, bila majivuno wala majigambo,
amekuwa ni mshauri mzuri, hakuwa na wivu kabisa, na sasa ametangulia.
IBADA YA KUMUAGA ITAFANYIKA JUMATATU SAA NNE ASUBUHI KATIKA
KANISA LA MAISHA YA USHINDI MABIBO EXTERNAL NA BAADAYE SAA NANE MCHANA MAZISHI
KATIKA MAKABURI YA MABIBO JESHINI.
John
Shabani
Katibu
chama cha muziki wa injili Tanzania
0 comments:
Post a Comment