4 June 2014

MUNGU ANAWEZA! HATIMAYE MCHUNGAJI ALIYEHUKUMIWA MIAKA 30 JELA AACHIWA

 Huyu ndiye Mch. Daniel Mwasumbi aliyekuwa amehukumiwa miaka 30 jela, lakini yuko huru kwa msaada wa Mungu.

Baadhi ya magazeti yalivyoandika habari hiyo, siku alipo hukumiwa



Imekuwa ni siku ya furaha na shangwe kwa familia, marafiki pamoja na ndugu na jamaa wa Mchungaji Mwasumbi aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma za Kubaka na kisha kuhukumiwa miaka 30 jela, na sasa yuko huru.
Ninawashukuru wote ambao walisimama bega kwa bega kusimama katika zamu ya Maombi. Ninapenda kuwataarifu kuwa kupitia taarifa ya habari napia ukurasa wa Facebook wa rafiki yetu Mtoto wa Mchungaji Mwasumbi Gama Daniel Mwasumbi ametujuza kuwa Baba Yao ameshinda Rufaa Yake na Sasa yuko nje ya Gereza.
Mchungaji huyu anaondoka gerezani huku akiwa ameacha Kanisa ndani ya Gereza ambalo alikuwa amelianzisha mnamo mwaka jana mwezi Julai alipokuwa amehukumiwa kifungo hicho. Mchungaji Mwasumbi atakuwa akiwahudumia Wafungwa Kila Jumapili kama mojawapo ya Branch Ya kanisa.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP