THE OFFICIAL JOHN SHABANI AND GOSPEL IN AFRICA BLOG

Welcome to the official blog of the the gospel singer, songwriter and teacher John Shabani. If you are one of the fans among the millions, feel free to get connected with John Shabani and stay updated on this blog.To learn more about John Shaban and his Ministry, please click the about button above.

GET THE LATEST FROM JOHN SHABAN AND THE GOSPEL NEWS COMMUNITY

You will be able to read and review the latest news on John Shabani's tour and other specials. You will also come across the best articles of news on Gospel from all across Africa and the International Community.Please do feel free to review our categories of news and events.

FEEL FREE TO LEARN MORE ABOUT JOHN SHABANI AND HIS MINISTRY

If you wish to learn more about John Shabani and his ministry, please feel free to connect with John Shabani on the social networks. You can keep up with John Shabani and the Gospel in Africa community on both twitter, facebook, google plus and many other more.

STAY UPDATED WITH INTERNATIONAL AND LOCAL GOSPEL NEWS

Gospel in Africa Blog is a comprehensive gathering place for African Gospel music fans. Offering the latest news and information about Local and International Gospel music and news, Gospel in Africa Blog also shares the spotlight with other genres of Christian music that more than ever, seemingly overlap musical genre lines, such as Bluegrass Gospel, Christian Country and others. Singing News, the leading African Gospel and International music Blog, features African and international Gospel lyrics, radio, news, Christian concerts, songs, artists, and more.

GET IN TOUCH AND STAY CONNECTED WITH JOHN SHABANI

If you are interested in contacting and staying in touch with John Shabani then here are the contacts. E- mail: touchingvoice@yahoo.com or , princejohntz@yahoo.com, Mob: +255 754 818 767 or +255 716 560 094, www.facebook.com/john.shabani.

13 September 2015

NGUVU YA KUSIFU NA KUABUDU

NGUVU YA KUSIFU NA KUABUDU
              John Shabani
 
Baada ya kukamilisha kitabu "MARUFUKU KUKATA TAMAA" Sasa niko mbioni kukuletea kitabu kipya kiitwacho "NGUVU YA KUSIFU NA KUABUDU". Najua umesoma vitabu vingi vinavyohusu habari ya kusifu na kuabudu, lakini mimi nakuhakikishia, kitabu hiki kitakusaidi sana. Lakini pia utaelewa tofauti iliyopo kati ya kusifu, kuabudu na kutumika, na zaidi utaimarika sana.

Pamoja na kwamba bado kinaendelea kuhaririwa, lakini acha nikupe utangulizi:


Somo la Kusifu, kumwabudu Mungu ni moja ya masomo muhimu na la kupewa kipaumbele cha kwanza katika kanisa. Lakini pia ni mojawapo ya somo lililosahauliwa hasa katika kizazi hiki, japo katika miaka ya karibuni Mungu amekuwa akirejeza huduma hii kwa watu wake.
Tangu mwanzo Mungu alipomuumba mwanadamu, lengo kuu la Mungu ni kwamba mwanadamu amwabudu na kumtumikia. Hii ni sababu kuu ya Mungu kumuumba mwanadamu tafauti na kiumbe chochote. Mungu wetu anahitaji kuwa na ushirika na mwanadamu, ibada ni njia pekee na kuu ya kuwa na ushirika na Mungu. Wapo wanaoabudu hawataki kutumika pia wanaotumika hawaabudu. Katika kitabu cha kutoka sura 20: 16, hii ni sehemu ya maandiko yaliyoandikwa na Mungu mwenyewe tofauti maandiko mengine yalioandikwa na waandishi 40 walioandika Biblia. Sehemu hiyo ni amri, hivyo si ombi, ni lazima kumwabudu Mungu na kumtumikia Yeye peke yake.
Ukweli ni kwamba, wakristo wameitwa kuabudu. Bwana anahitaji hilo kwanza kabla ya kitu kingine chochote, Ndio sababu za kuandika kitabu hiki ili kuwasaidia wakristo na kila mwenye pumzi ya uhai, afahamu au kuelewa umuhimu wa kumwabudu Mungu.
Kama lilivyo jina la kitabu hiki “Nguvu ya kusifu na kuabudu” Ni ukweli usiopingika kwamba kusifu na kuabudu kunamfanya Mungu akutembelee katika hali zako na kuleta mabadiliko sawa sawa na uweza wake na mapenzi yake. Mimi nimeona nguvu hii na nimeionja. Ninaposifu mambo mengi sana yanafanywa upya ndani yangu na hata mazingira yanayonizunguka. Hiyo ndio nguvu ya kusifu na kuabudu katika roho na kweli, hakuna kitakachobaki jinsi kilivyo maana Mzee wa siku akishuka yote yanabadilika. Hiyo ndio nguvu iliyo katika sifa. Wewe huoni hata ukimsifia mtu wa kawaida utaona hata hali mwitikio wa mtu huyo. Wakati mwingine tumepewa kile tulichokuwa tunakihitaji kwa watu fulani baada tu ya kutanguliza sifa fulani. Hujui kwanini? Sifa ina nguvu na ndio maana Mungu hataki kushirikiana sifa zake na watu wala utukufu wake hatampa mwingine.

Fahamu kuwa uwepo wa Mungu unaleta amani, furaha, pumziko, unawavuta na kuvutia watu sahihi, unaleta baraka, unaleta nguvu, unaleta hekima heshima, uponyaji wa kiroho na kimwili, maono na ufunuo. Kwa kifupi kabisa uwepo wa Mungu kwetu ni suluhisho na majibu ya mahitaji yetu yote hapa duniani sasa na hata milele. kumbuka tutakuwa naye uso kwa uso milele na milele yote maana yeye ndiye ukamilifu wetu. Najua utajiuliza, kwanini kwa wakati mmoja ninachanganya kusifu, kuabudu na kutumika! Huu ni utangulizi tu, kadri utapoendelea kuzisoma kurasazingine, ndipo utakapo elewa zaidi.

Yesu aliwaambia wazi wanafunzi wake kwamba Baba anawatafuta waabuduo “… Baba anawatafuta watu kama hao wamwabudu”. (Yohana 4 : 23). Kumbuka, Baba hatafuti ibada bali watu wanaoabudu. Kuabudu ndio wito wetu wa kwanza tafauti na watu wengine wanavyodhani kwamba hoja kuu ya Mungu ni ya watendaji, hii si kweli. Waabuduo wa kweli mara nyingi huwa watenda kazi au watumishi wa kweli. Yesu pamoja na shughuli nyingi alizokuwa nazo, Biblia inasema alikuwa hana budi kupita katikati ya samaria japo safari yake ilikua ya kwenda Galilaya, ili tu kumsaidia mtu mmoja kuhusu uhalisi wa kuabudu (Yn 4.3-4) tafsiri ya King James katika mstari huo wa nne inasema “And He must needs go through Samaria”, ikimaanisha kuwamba, kulikuwa na uhitaji wa Yesu kulazimika kupitia samaria. Tafsiri ya kisasa ya Amplified Bible inasema “It was necessary for Him to go through samaria” ikimaanisha kulikuwa na umuhimu wa Yesu kufika samaria. Kama nilivyotanulia kusea, tukiwa na waabuduo halisi, hatutapata shida ya watenda kazi wazuri, hivyo Yesu alijua fika kwamba mtu huyo mmoja akibadilishwa ataweza kubadilisha maelfu ya watu.
(Yohana 4:19-24) Historia ya mwanamke huyu, yeye hakuwa myaudi, alikuwa mtaifa. Upatikanaji wa maji wakati huo ulikua mgumu, watu walijenga desturi ya kuchota maji asubui sana. Lakini ilikuwa ni vigimu kwa mwanamke huyu kuamkia kuchota maji kulingana mfumo wa maisha yake ya uovu, alikuwa ni mtu wa kusutwa, alikua mwizi wa waume za watu. Mpaka anakutana na Yesu alikua na wanaume watano. Mwanamke huyu alifahamu fika kuhusu historia ya kuabudu kwa kidini, kuabudu kusikokuwa na hofu ya Mungu. Ndio maana sasa anamwambia Yesu kuwa baba zao waliabudu katika mlima huu ingawa wayahudi waliwaambia wanatakiwa kwenda kuabudu Yerusalemu maana ndiko mahali kuwapasako kuabudia. Yule mwanamke alimuuliza Yesu swali la siku nyingi juu ya mahali panapofaa kwa ibada. Elewa kwamba, kwa karne saba Wayaudi na Wasamaria wamekuwa wakibishana juu ya swala hilohilo, juu ya mahali panapofaa kwa ibada.Yesu hakumbishia mwanamke yule, maana aliyaelewa hayo. Hapa Yesu anasema kwamba mahali hapakuwa na maana sana, cha muhimu ni hali ya moyo wa kila mtu, na jinsi anavyomheshimu Mungu. Hayo ndiyo yanaamua jinsi ibada yake ilivyo. Lakini akamwonyesha na kumfundisha kwa usahihi juu ya hilo. Jambo la ajabu lililo mtokea mama yule baada ya kuelewa ukweli na kumjua mtu anayeongea naye kuwa si mkuu wa dini fulani, sio mtu wa kawaida; Kwanza kiu yake ya uovu ilikatika maana aliyapata maji yaliyo hai. Pili alitubu dhambi zake, maisha yake yakabadilishwa kabisa. Tatu mfumo wake wa ibada ulibadilishwa kabisa maana alifundishwa uhalisia wa kuabdu, aliabudu sasa katika roho na kweli, na baada ya hapo ndipo nne, bila kusukumwa, kusukwasukwa, kuhimizwa wala kubembelezwa, akamtumikia Mungu, akawa mtenda kazi mzuri. Hakika utumishi ukajitokeza ghafla (Yohana 4:28). Hakika huwezi ukawa mwabudu mzuri na usitumike. Katika kizazi tulichonacho mifumo yetu ya ibada imebadilika kabisa, tumeabudu kidini, tuna hitaji kuujua ukweli huu utakao tufanya tubadilishwe kabisa na tuwe waabuduo halisi. Mazingira ya kumwabudu ni muhimu sana yakaeleweka kwa uzuri. Napenda niseme hapa kuwa mahali popote panafaa kumwabudu Mungu, Kwanini? kwasababu Mungu ni Roho na wote wanaotaka kumwabudu imewapasa kumwabudu yeye katika hali hiyo hiyo, yaani katika roho na kweli. Fahamu kuwa roho yoyote haifungwi na mazingira. Kuabudu katika Roho inamaana kuabudu ukiongozwa na Roho. Tukijua ukweli huu na kuufanyia kazi, hakutakuwa na shida ya kuwapata watumishi au watenda kazi wazuri, maana kila mtu atajuwa wito wake na bila kusukumwa wala kubembelezwa, atawajibika mwenyewe, hoo haleluya!
Nikiwa nachukuwa digrii yangu ya Biblia, moja ya somo lililonigusa sana ni la kusifu na kuabudu. Niliguswa sana na kufuatilia kwa ukaribu habari za mmoja wa wandishi wazuri wa vitabu vizuri vya kiroho dunia na aliyetunukiwa tuzo mbalimbali za heshima, Dr. Aiden Wilson Tozer (April 21, 1897 - May 12, 1963). Katika kitabu chake kiitwacho Ibada: Hazina iliyosahauliwa katika kanisa, alisema: “ Kusudi la Mungu kumleta mwanae afe na kufufuka aketi mkono wake wa kuume, ni ili aturejeshee ile hazina iliyopotea, ile hazina ya ibada: Ili turudi na kujifunza kufanya tena kile ambacho tuliumbwa kukifanya tangu mwanzo: Kumwabudu Bwana katika uzuri wa utakatifu….Tuko hapa ili kwanza tuwe watu wanaoabudu na kuwa watendakazi ni jambo la pili”
Narudia tena kusema, ibaba ndiyo wito wetu wa kwanza kwa kila mwamini katika kila taifa “Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu (Kuabudu) mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa” (Ufunuo 15:4)
Daudi anasema “Na wewe U Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israeli “(Zab 22: 3). Katika tafsiri nzuri ya Amplified Bible inasema “But You are holy, O You Who dwell in [the holy place where] the praises of Israel [are offered]. Sasa niruhusu nikufafanulie kidogo hapa! Kuketi huko kwa Mungu kunakozungumziwa katika mstari huo, kwa kiebrania kunamaanisha Yashab (Yeu – Shab), yaani ni kuketi, kuishi mahali fulani, kudumu mahali fulani, kukaa, kuendelea, kuishi, kutembelea mara kwa mara, kufanya makao, kujificha au kujibanza mahali, kubaki mahali, kurejea au kungojea.
Ina maanisha, ukitaka kumuona Mungu na ukuu wake, wema wake, mafanikio yake, neema yake, rehema zake, fadhili zake, ebu jawa na sifa zake ; maana Yeye hukaa (inhabit), hudumu/huishi juu ya sifa za watu wake, na maali alipo Mungu hapo pana kila jawabu. Shida ya wakristo wwa kizazi hiki, wanakimbilia majawabu, ishara na miujiza bila kuzifuata kanuni za ki-Mungu; matokeo yake watu wamenyweshawa au kulishwa vitu vya ajabu. Acha kutangatanga, sio kila nabii, mtume au mchungaji ametokana na Mungu. Naamini, ukijawa sifa za ki-Mungu, ukawa mwaduo halisi, hakika huwezi kujichanganya.
Katika matendo 13 :1-2 “Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho mtakatifu akasema, nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia “. Hapo kulikuwa na manabii na waalimu katika kanisa. Hapa tunaona kwamba kipaumbele cha huduma hakikuwa kutoa unabii au kufundisha, bali “ ibada “. Ni kwamba kila mtu alikuwa akiabudu, ndipo kutoka kwenye huduma ya ibada likatoka neno la unabii.
Hii inamaanisha tunapojawa na mioyo ya sifa na kuabudu, Mungu mwenyewe katika utatu mtakatifu hujihudhurisha pamoja nasi, huongea nasi, hutuhimarisha na kututenga kwa ajili ya huduma (utumishi au kutumika), maana Mungu wetu ni wakuabudiwa na kutumikiwa. Haisaidii kuwa na huduma kubwa wakati wewe mwenyewe huna moyo wa ibada, huduma hiyo itakuwa ya kukunufaisha wewe na sio Mungu wetu, Ndio maana katika kizazi hiki watu wameweka masharti mengi ndipo wamsifu Mungu; Mungu hayupo katika hilo na wala huwezi kusema umefanikiwa kwa hizo baraka za kuweka masharti ndipo upande madhabauni, lakini pia Kumbuka Mungu wetu ni Mungu mwenye wivu.
Katika kitabu cha Zekaria 14 : 17 anasema “ Tena itakuwa ya kwamba mtu awayeyote… asiyekwea kwenda Yerusalemu ili kumwabudu Mfalme, Bwana wa majeshi, mvua haitakunya kwao “. Hapana ibada-Hapana mvua”, inaamaana tusipokuwa na mioyo ya kumsifu na kumwabudu Mungu, mvua ya baraka haiwezi kamwe kunyesha juu yetu, maana Yeye hukaa juu ya sifa.
Ukisoma (Ezra 1:1-11), Taifa la Israeli baada ya kuishi utumwani huko babeli, baada ya utawala wa mfalme Nebukadreza kuwatesa na kuharibu kabisa nchi yao, kuvunja ukuta, kubomoa makazi yao pamoja na hekalu na kuchukuwa baadi ya watu mateka pamoja baadhi ya vitu muhimu katika nyumba ya Bwana, lakini muda ulipowadia, Bwana akamwamsha roho mfalme Koreshi aliyetawala wakati huo. Kwa ufupi nikwamba, mfalme huyo aliwaruhusu wana wa Israeli warejee kuijenga upya nchi yao, yaani Yerusalemu. Katika kujenga upya, mambo manne yalihitajika yafanyike
a. Kujenga ukuta (Ili kuwakinga na maadui)
b. Kujenga nyumba zao (kwa ajili ya kujihifadhi)
c. Kujenga hekalu (mahali pa kukusanyikia)
d. Madhabau (Kumwabudia Mungu)
Katika yote hayo, Mungu aliwataka waanze na jambo moja muhimu. Kwa mtazamo wetu wa kibinadamu hasa katika mfumo wa ujenzi, labda ingefaa sana kuanza na ukuta au nyumba ya kuishi. Lakini ukisoma Ezra 3:1-4, Mungu anaelekeza kwamba waanze kujenga madhabau
Mungu anataka sana kuwa na ushirika na Yeye kuliko kitu kingine, yaani kuwa na ibada na Yeye na hayo mengine atayazidisha (Luka 12:31). Madhabau ndipo maali pa uhusiano wa mtu na Mungu, ndio maali pa kutengeneza, maali pa kutua kila mzigo. Mwanadamu wa asili mara zote huwa na madhabau fulani katika moyo wake, hivyo tuspojenga madhabau ya Mungu basi tutajenga madhabau ya ibilisi.
Katika kitabu cha Danieli sura ya 3, Hapo tunawaona watu waliojua uwezo wa kumtumikia na kumwabudu Mungu (Dan 3:11-28). Kina Shadraka, Meshaki na abednego wanashutumiwa kwa kutokukubali kutumika na kuiabudu sanamu. Katika tafsiri moja ya King James inasema “They serve not your gods nor worship the golden image).
Mfalme Nebukandreza akaghadhibika kwa hasira kwasababu watu hao hawakutaka kuitumikia na kuisujudia sanamu (Dan 3:14-16). Nakumbuka jibu la wanaume waliomjua Mungu wao wanasema (Dan 3:7) “ Mungu wetu tunaye mtumikia atatuokoa na hilo tanuru liwakao Moto”. Lakini katika ule mstari wa 28, Mfalme anagundua siri ya kumtumiki na kubwabudu Mungu wa Mbinguni. Ninapomalizia kipengele hiki cha utangulizi, nataka uelewe jambo hili kwamba; kumsifu Mungu ni jambo lingine na kumwabudu ni jambo lingine tena muhimu sana, lakini pia kumtumikia ni jambo lingine. Mambo yote hayo matatu ni muhimu sana, hawa ni mapacha watatu.

Ni utangulizi tu, mengine kama:

1. Nini maana ya kusifu kuabudu na kutumika
2. Baraka na vikwazo vya kusifu, kuabudu na kutumika
3. Mambo muhimu ya kuzingatia katika maisha ya kusifu na kuabudu
4. Sadaka au dhabiu ya sifa
5. Maana halisi ya ibada au kuabudu
6. Umuhimu wa kuabudu
7. Chimbuko la ibada
8. Misingi ya kuabudu
9. Picha halisi ya ibada
10. Muziki katika kusifu na kuabudu
11. Kuongoza ibada au kipindi cha kuabudu
12. Mambo muhimu ya kuzingatia ili kuwa kundi bora la sifa na kadhalika utayapata ndani ya kitabu.

Nakupenda lakini Mungu anakupenda zaidi.


24 August 2015

JOHN SHABANI BOOK LAUNCHING - UZINDUNZI WA KITABU CHA JOHN SHABANI


Hatimaye kile kitabu kilichokua kinasubiriwa kwa hamu; kilichoandikwa na John Shabani​ sasa kinapatikana madukani.

Marufuku kukata tamaa ni kitabu kilichobeba majibu ya maswali mbalimbali yanayomkabili mwanadamu, ni kitaba chenye siri ya kuondoka kwenye Umaskini na kuwa tajiri, kwenye Ujinga na kuwa mwerevu, kwenye unyonge/dhaifu na kuwa jasiri, kwenye magonjwa na kuwa mzima, kwenye huzuni na kuwa mwenye furaha, kwenye taabu na shida na kuwa mwenye mafanikio, kwenye kushindwa na kuwa mshindi, kwenye kilio na kujaa kicheko, kwenye aibu, kuchekwa, kudharauliwa na kuitwa mheshimiwa fulani, kwenye dhambi/uovu na kuwa mcha Mungu.

Jipatie nakala yako sasa. Nakushauri mnunulie yule unayempenda, unayetamani afanikiwe kiroho, kiuchumi nk.

Lakini pia unaweza kututumia pesa yako kwa njia ya tigo pesa 0716560094 au mpesa 0759778778 nasi tutakufikishia popote ulipo Tanzania. Bei ni shilingi elfu kumi tu.

kwa mawasiliano zaidi 0713 778778, 0759 778 778









21 June 2015

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAJANE DUNIANI TAASISI YA RITA KUTOA DARASA KWA JAMII KUHUSU KUFAHAMU KUHUSU UANDISHI WA WOSIA NA FAIDA ZAKE





 Wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika banda la rita, wakijifunza mabo mbalimbali hasa yale yahusuyo kuandika wosia na, vyeti vya kuzaliwa na sheria mbalimbali


Labda nikudikeze darasa kwa kwa ufupi

WOSIA

1.  Wosia ni nini?

Wosia ni tamko analotoa mtu wakati  wa uhai wake akieleza jinsi anavyotaka mali yake igawanywe au wapewe watu gani  baada ya kifo chake.

2.  Nani anaweza kuandika wosia?

Ni mtu yeyote mwenye umri wa miaka 18 au zaidi  na mwenye akili timamu.

3.  Faida za wosia.

-         Kuepusha  watoto au mke/mume  kunyang’anywa mali.
-         Kuepusha  migongano katika  familia, ndugu au jamaa zake.
-         Kuepuka kumrithisha mtu yeyote ambaye kisheria hapaswi kurithi mali yako.
- Unakupa uhakika wa maisha bora ya baadae ya warithi wako kulingana na mali ulizo nazo
- Kupunguza gharama/usumbufu wakati wa kuendesha mirathi.


4.  Sababu za kuandika  wosia

-         Kuweka msimamizi wa mirathi  na mlezi wa watoto  wako au mwangalizi wa familia.
-         Kutoa maelekezo kuhusu  mali zako  kama  upendavyo na kwa kufuata sheria.

5.   Wosia unaokubalika kisheria

-         Uwe na wa maandishi au matamshi

-         Ushuhudiwe na watu wawili ikiwa ni wa maandishi.
-         Ushuhudiwe na watu wa nne ikiwa ni  wa matamshi.
-         Uwe wosia usiomnyima mrithi halali mali bila sababu zinazotambulika kisheria.

6.  Ni nani mrithi halali kisheria?

-         Mke au mume
-         Watoto waliozaliwa ndani ya ndoa
-         Watoto waliohalalishwa  kisheria
-         Wazazi na ndugu wa karibu ambao walikuwa tegemezi kwa mtoa wosia wakati wa uhai wake.

7.  Hali ya mwandika wosia

Anayeandika wosia ni lazima athibitishwe kuwa ana akili  timamu wakati akiandika au kutamka wosia wake.

8.  Mambo muhimu ya kuzingatia katika  kuandika wosia.

·        Majina ya wanaonufaishwa
·        Orodha ya mali za mtoa wosia  na mahali zilipo na stakabathi / hati za ununuzi  / Umiliki wa mali hizo.
·        Majina na anuani za msimamizi wa  mirathi na mwangalizi  wa watoto
·        Maelezo mengine ya kuweka kwenye wosia.

9.  Ni wapi wosia uhifadhiwe?

-         Wosia uhifadhiwe mahali ulipoandaliwa.
-         Kwenye taasisi za dini kama vile kanisa au msikiti.
-         Kwa mwanasheria yeyote
-         Kwa mtu yeyote asiyemrithi katika wosia husika na awe na sifa za kuaminika za kutunza siri.
                 
 Hayo ni machache tu kati ya mengi ambayo yatafundishwa katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam, jumanne ya tarehe 23 Juni 2015
Watu wote mnakaribishwa.


MENGINEYO

KWA watu wengi wa jamii za Kiafrika, mtu kuandika au kutoa wosia juu ya mali zake, ni kitu ambacho inachodhaniwa ni mkosi..., Pia hudhani kwamba anayeandika wosia ni mtu anayejichulia au kujitabiria kifo cha karibu!

Ukweli ni kwamba, wosia ni mojawapo ya vitu vinavyosaidia kuilinda familia na jamii inapotokea mtu aliyeandika wosia huo amefariki dunia. Wakati fulani, uandishi wa talaka unasaidia sana kusaidia usuluhishi wa matatizo ya kifamilia kuhusu mali na fedha za marehemu pindi kifo cha mtu aliye na mali akifariki dunia .
Kwa mujibu wa kifungu cha 2 cha sheria ya Usimamizi wa Mirathi ya Tanzania, wosia ni tamko la mwisho la mtu anayetoa tamko hilo, akielezea jinsi gani mali zake zitunzwe au kufanyiwa kazi pindi atakapofariki dunia. Kwa ajili hiyo, mtu aliyetoa tamko hilo, anatakiwa kutoa tamko ambalo ni la mwisho katika matamko yote aliyowahi kuyatoa wakati wa maisha yake juu ya mali na fedha zake zinapaswa kufanywa pindi atakapofariki dunia. Wosia unaweza kuwa wa maneno ya mdomo na vilevile wosia unaweza kuwa wosia uliondikwa kwa maandishi. Kati hali yoyote ile, wosia wa mdomo na wosia wa maandishi unakuwa na nguvu sawa kisheria, ili mradi tu masharti yanayopaswa kuzingatiwa yakitimizwa.

Hata hivyo, kwa wosia wa maandishi au ule wa mdomo, kuna masharti kadhaa yanayohitajika kutimizwa kwa wosia huo kuwa na nguvu kisheria. Mtu anayeandika wosia kimsingi anatakiwa kuwa na mali anayoimiliki yeye binafsi (si ya anayoimiliki kwa ubia au aliyopewa kutokana na wadhifa wake labda kiserikali au kampuni). Vilevile wosia lazima uoneshe nia ya mtamkaji kuhusu kutoa mali zake (pamoja na fedha) kwa watu au mtu fulani na vilevile ndugu msomaji unatakiwa ujue kwamba wosia utakuwa na nguvu kisheria pale tu ambapo mwandishi/mtoa wosia huo atakapokuwa amefariki dunia.
Kwa wosia wa mdomo mpaka uwe una nguvu kisheria, ni lazima ushuhudiwe na watu au kwa maneno mengine mashahidi wasiopungua wanne na kati ya hao, wawili ni lazima wawe watu kutoka katika ukoo wake. Hali hii si tofauti sana kwa upande wa wosia unaoandikwa kwa maandishi, kwani wosia huu ni lazima ushuhudiwe na watu wasiopungua wawili na kati ya hao mmoja ni lazima awe ni mtu kutoka katika ukoo wa mtoa wosia. Hawa wanaweza kuwa wajomba, mashangazi, kaka au dada wa mtoa tamko la wosia.

Zaidi ya hayo, wosia hauwezi kuwa na athari yoyote kisheria kama mtoa tamko la wosia hatatia saini yake aidha kwa maandishi au kwa kuweka dole gumba katika karatasi yake ya wosia. Hii ina maana kwamba mahakama haitautambua wosia huo kama hautakuwa na sahihi ya mtoaji wa tamko hilo. Hata hivyo, wosia hata kama utakuwa na vigezo vyote vinavyotakiwa lakini kama mtoaji wake alitoa tamko lake akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa akili au kulazimishwa/kushurutishwa, hii ni mojawapo ya vigezo vya kukataa kuidhinisha wosia au mirathi kwa mtu yeyote na mahakama. Wosia vilevile ni lazima umtaje mtu atakayeutekeleza. Huyu ni mtu ambaye mtoa wosia atamchagua katika wosia wake na ndiye atakayepewa majukumu yote ya kuangalia jinsi gani matakwa ya mtoa wosia yatavyotimizwa. Ni kweli kwamba mtu anaweza kuandika wosia na kuufuta wakati wowote na mara zote anazotaka. Sheria haina pingamizi juu ya jambo hilo.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba mtoa wosia anaweza kubadilisha mawazo yake wakati wowote ule. Hata hivyo, wakati wowote mtu atakapokuwa anaandika wosia, ni lazima aandike kwamba wosia huo ni wa mwisho kabisa kati ya wosia mwingine aliowahi kuuandika. Hata hivyo, mahakama imepewa uwezo kisheria kutengua au kubatilisha wosia wowote kama haukidhi vigezo vya kisheria kuufanya uwe halali. Katika hali kama hii, familia itatakiwa kumchagua mtu asimamie mirathi kana kwamba marehemu hakuacha wosia wowote kwani wosia wake hautakuwa na nguvu yoyote kisheria. Ikiwa baada ya kifo cha mtu aliyeandika wosia, kutakutwa wosia mbili tofauti na ulioandikwa siku na tarehe tofauti, basi wosia wa tarehe ya mbele ndio utahesabika kuwa halali na si wa tarahe ya nyuma yake. Hapa sheria inatumia busara kwamba mpaka wosia mwingine uandikwe ina maana marehemu alibadili mawazo yake na ndiyo maana akaandika wosia mwingine.

Wosia unapata nguvu kisheria pale tu aliyeandika akifariki dunia. Hii ina maana kwamba, hata kama mathalani, mtoto wa marehemu ndiye aliyeandikwa atarithi shamba la marehemu, mtoto huyo hatakuwa mmiliki halali wakati mwandishi wa wosia huo atakapokuwa hai, ila tu pale atakapofariki dunia ndipo mtoto huyo ataweza kuwa mmiliki halali wa shamba hilo. Kimsingi, ni haki ya mwandika au mtoa wosia kubadilisha wosia wake wakati wowote autakao. Vilevile ni haki yake kumpa urithi mtu yeyote atakayekuwa amemchagua katika wosia wake. Hata hivyo, mwandishi wa wosia ni lazima azingatie watoto ambao ni wategemezi kwake pale atakapokuwa anaandika/anapotoa wosia wake.
Unafahamu masharti ya Wosia...?
- Mtoa wosia lazima awe na akili timamu.
- Awe ametimiza miaka kumi na nane (18) na kuendelea.
- Uonyeshe tarehe ,mwezi na mwaka ulioandikwa.
- Uonyeshe majina ya warithi.
- Mtoa wosia ahusishe mali zake binafsi na si za mtu mwingine.
- Wosia ni siri wanufaika hawatakiwi kuujua.
- Mtoa wosia lazima aweke saini yake, na kama hajui kusoma na kuandika aweke alama ya dole gumba la mkono wa kulia.
- Mashuhuda lazima waweke saini zao tena kwa wakati mmoja.

20 June 2015

NAIBU WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, ANGELA KAIRUKI KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WAJANE DUNIANI





 Mwenyekiti wa Chama cha Wajane Tanzania, Rose Sarwatt na katibu wa chama hicho bwana John Shabani, wakizungumza na waandishi wa habari juu ya madhimisho ya siku ya wajane duniani. kulia ni mjumbe wa chama hicho, bi Mwajua Mwinyimkuu
 Mheshimiwa Ajnjela Kairuki, mgeni rasmi katika maadhimisho ya kwanza Tanzania, ya siku ya wajane Duniani.


NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wajane Duniani.
Tunategemea pia kuwa na wadau mbali mbali, kama vile viongozi wa serikali, viongozi wa kidini, wawakilishi wa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, waandishi wa habari pamoja na wasanii mbalimbali, wamesema.



Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Juni 23 mwaka huu, yaani siku ya jumanne, ambapo kimkoa yatafanyika  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza na waandishi leo Jijini Dar, Mwenyekiti wa Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA), Rose William Sarwatt na katibu mkuu wa chama hicho, bwana John Shabani, wamesema, siku hiyo itawakutanisha wajane wote nchini. Katika maadhimisho hayo pia wataweza kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili pamoja na utatuzi wake.

Maadimisho hayo ambayo yanafanyika Dunia nzima kwa hapa nchini yatabeba kauli mbiu isemayo, “Andika wosia kuepusha migogoro isiyokuwa na lazma”. Yataanzia stendi ya stesheni hadi sehemu husika. “Kauli mbiu hiyo imekubalika na takrbani ya wajane wote nchini, kutokana na changamoto zetu kufanana, ikiwemo ya kushuka kwa uchumi ndani ya familia pindi mume anapofariki,” amesema Sarwatt.  
Aidha amesema, changamoto kubwa wanayoipigia kelele wajane wengi nchini ni uchumi kuporomoka pindi wakiondokewa na wenza wao, hivyo tatizo hilo pia huongeza   idadi ya watoto yatima mitaani.

Mbali na kupata changamoto hizo Sarwatt amesema, uwepo wa TAWIA umekuwa msaada mkubwa na kimbilio la wajane wengi kwani kimekuwa msari wa mbele kuwasaidia. Licha ya wajane wengi kuonekana kukata tamaa ya maisha, TAWIA ilianzisha miradi mbalimbali ya kuweza kuinuana kimaisha ikiwemo ya kufanya biashara ndogondogo. Na kwamba biashara hizo na michango mbalimbali imewasaidia kuwapeleka watoto shule pamoja na kujikimu katika maisha yao.
“Tuchukue fursa hii kuwakumbusha wadau mbalimbali ambao wanaweza kutusaidia, ili tuweze kuwafikia wajane wengine waliopo vijijini ambao hatuwezi kuwafikia. Pia tunaomba serikali itusaidie kupata takwimu ya wajane  wote nchini, ili iwe rahisi kuwafikia,” wamesema.


Mwisho, watanzania wote wanaalikwa kuhudhuria siku hiyo, kwani licha ya maadhimisho, Pia, kutakuweo na elimu mbalimbali kama sheria, afya, uchumi n.k. Pia, kutakuwepo na bidhaa mbalimbali kutoka kwa wajane.

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP