John Shabani akisalimiana na viongozi wa umoja wa wanafunzi wakristo wa vyuo vikuu iringa
SEMINA YA NENO LA MUNGU KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU
IRINGA YAFANA.
Mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iringa wamefurika
katika ukumbi wa Ruco, katika semina ya Neno la Mungu. Ni semina iliyoandaliwa
na umoja wa wanafunzi wakristo wa vyuo vikuu vya Iringa. Umoja huo ujulikanao
kama Joint Fellowship umeundwa na wanafunzi wa vyo vikuu vitatu:
Chuo kikuu cha Ruaha (RUAHA UNIVERSITY COLLEGE – RUCO)
Chuo kikuu cha Mkwawa (MKWAWA UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION-
MUCE) na chuo cha Tumaini (TUMAINI UNIVERSITY)
Chuo kikuu cha Ruaha (RUAHA UNIVERSITY COLLEGE – RUCO)
Chuo kikuu cha Mkwawa (MKWAWA UNIVERSITY COLLEGE OF EDUCATION-
MUCE)
chuo cha Tumaini (TUMAINI UNIVERSITY)
Watumishi wa Mungu, JOHN SHABANI, MCH. EFRAHIMU
MWANSASU na Emmanuel Mgogo na kundi lake (Sayuni bandi) kutoka mbeya waligusa
mioyo ya wanafunzi kwa nyimbo za sifa na kuabudu. Pia vikundi vya uimbaji
kutoka vyuo vyote vitatu waliimba.
Mnenaji katika semina hiyo alikua Mwinjilisti wa
kimataifa Daniel Mwankenja. Baada ya Kongamano hilo la siku mbili, uongozi wa
umoja huo ukiongozwa na mwnyekiti Mr.
Lameck Mtaka na makamu wake mr. Emmanuel Kibona, wamewashukuru bwana John
Shabani, Mch. Efrahimu Mwansasu na watumishi wote kwa kukubali kuungana nao na
kuifanya semina hiyo kuwa ya Baraka na kuacha gumzo Iringa.
Lengo kuu la umoja huo ni kuhimarisha umoja wa kiroho kwa
wanafunzi wa vyuo vikuu vya Iringa.
John shabani akiwa katika picha na viongozi wa umoja wa wanafunzi pamoja na mlezi wa semina hiyo Mhe. diwani wa Iringa na mwenyekiti wa CCM iringa mjini - Madame Jesca
John Shabani akimtukuza Bwana
Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu iringa wakiongozwa na John shabani,
wakicheza mbele za Bwana
Mch. Efrahimu Mwansasu akimtukuza BwanaJWajjWakabbbMMwa
Emmanuel Mgogo na kundi lake (Sayuni bandi) kutoka mbeya, Wakimwimbia Bwana
John shabani akiwa katika picha na viongozi wa umoja wa wanafunzi pamoja na mlezi wa semina hiyo Mhe. diwani wa Iringa na mwenyekiti wa CCM iringa mjini - Madame Jesca
0 comments:
Post a Comment