12 October 2012

Vurugu za Kidini Mbagala: Mtoto akojolea msahafu; makanisa yachomwa

Kanisa baada ya kuchomwa moto


 
Taarifa na maoni ya watu mbalimbali


Chanzo cha fujo hizo ni mabishano ya watoto wawili wenye imani tofauti mmoja akimwambia mwenzake kwamba eti ukikojolea msaafu unakua chizi yule dogo mwingine kaukojolea kweli na hajawa chizi, Yule mwenzake alivyoona kashindwa ikabidi aende msikitini akawatonya waislamu kwamba kuna dogo kakojolea msaafu, Si unajua tena wakatoka waislamu wenye siasa kali wakataka kumuua dogo polisi wameingilia kati na kumuokoa huyo dogo sasa ni vita ya mabomu ya machozi ya Polisi na mawe yanayorushwa na waislamu, Hali sio shwari kabisa magari kibao yamevunjwa vioo na fujo bado inaendelea mpaka sasa

Source: Clouds Fm
QuoteBy Bob G View Post
Polisi wanapiga mabomu ya machozi kuwatawanya Waislamu waliokwenda kuchoma moto kituo cha polisi na kumtoa mtoto alie kojojea Kuran.

Huyo mtoto ni wa kidato cha kwanza walikua wanabishana na mwezie kwamba ukikojolea Kuraan utakuwa kichaa ndipo huyo kijana alipokojolea na hakuwa kichaa na mwenzie alivoona hivo akawataarifu watu kuwa mwenzie kakojolea kuraani, watu wakamkimbiza polisi kumwokoa na ndipo wananchi walipokwenda kituo cha polisi kutaka kutoa kipigo kwa mtoto huyo na polisi wakaja kumlinda na mabomu yakatumika kutawanya watu.

Source: Radio Clouds dk chache zilizopita
QuoteBy PakaJimmy View Post
Nimesikiliza Redio Cloudz hapa taarifa zinasema hadi sasa makanisa 3 yameshachomwa kutokana na vurugu huko Mbagala.

Makanisa hayo ni pamoja na Anglikana, Sabato na Pentekoste yote ya Mbagala.

Taarifa inasema vurugu zinazidi kusambaa maeneo mbali ya jirani
QuoteBy A VILLAGER View Post
Ni kweli waislamu wameharibu mali katika makanisa matatu Mbagala - Kova on ITV
- Vurugu sasa zimehamia Chang'ombe karibu na Uwanja wa Taifa kwenye kiwanja kilichouzwa na Bakwata.
- Polisi wamefika wameona hakuna tatizo Waislamu wamevunja ukuta wameweka jukwaa wanahutubia; polisi wapo jirani wanawafuatilia
QuoteBy Gurudumu View Post
Kova, mkuu wa Mkoa wa DSM, na Shehe mkuu wa mkoa wa DSM wako live ITV kipindi maalum wanaelezea hilo tatizo na mkuu wa mkoa anakemea watu wachache ambao wanavizia matatizo madogo madogo na kuchochea chuki za kijamii
QuoteBy Pumba View Post
Mkuu wa mkoa anawasihi dini zote kutolichukulia jambo hili kwa jazba kwasababu ni jambo lililoanzishwa na watoto katika hali yao ya utani....pia anasema kuna watu watachukulia advantage hii kufanya uharibifu...

Shehe mkuu anasema kila mtu anabeba mzigo wake mwenyewe hivyo si haki kuuhukumu ukristo kwa jambo lililofanywa na mtoto hata kama ni mkristo si wakristo waliomtuma






 Magari yavunjwa
 FFU wakiwadhibiti watu mbalimbali
 
OMBEA NCHI YETU

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP