Wakati wimbi la kuvamiwa Makanisa likiendelea na Makundi ya
watu wanaosaidikika ni Waislam, Usiku wa kuamkia leo majira ya saa 3 usiku
kundi la Watu wanakadiriwa kuwa zaidi ya 20 wakiwa na mapanga walivamia kituo
Cha Television Cha Agape, Maarufu kama ATN kwa lengo la kutana kuiba katika
Kituo hicho.
Kundi hilo la watu waliokuwa na Silaha hizo lili wazidi nguvu walinzi na Kufanikiwa kuingia ndani ya Ofisi na kwenda kubeba Flat Screen ya nchi 32, Monitor pamoja na laptop. Kabla hata kundi hilo halijatawanyika mmoja wa walinzi alifanikiwa kubonyeza kitufe za "Alarm" kutaarifu mashirika ya Ulinzi ambayo yalifika kwa wakati pamoja na Polisi katika eneo husika.
Hii sio kawaida ya wezi kwenda kuiba na mapanga wakiwa zaidi ya 20, tena hawana hata gari la kubebea mizigo watakayoiba hasa unapoenda kuiba kwenye kituo cha TV kisha ukaiba Flat Screen na Laptop ambazo hata uswazi zipo. Yamkini hawa watu walikuwa wamekwenda kwa lengo lingine katika kituo hicho sababu hata Ofisi ya Mchungaji na Vitu vingine Vya thamani havikuguswa.
Hiki ni Kipindi cha kuwa macho, vibaka pia hawakawii kujifanya "Wanauamsho" wakafanya uhalifu kwa kutumia upepo uliopo sasa hivi wa Kuchoma Makanisa.

0 comments:
Post a Comment