John akiwa na uso wa furaha baada ya kumaliza masomo yake kwangazi ya degree (Bachelor of arts in Biblical Studies)
Mmoja wa wakurugenzi wa chuo hicho, Dr. Lee, akiwapiga wanafunzi msasa wiki moja kabla ya mahafali
John Shabani na mwandishi wa habari, George Kabula
Elimu haina umri, huyu hapa ni bibi wa miaka 80 akifurahia kumaliza masomo yake
Mary B. Nyerere
Imekuwa siku ya
furaha na shangwe kwa wanafunzi, ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria katika
mahafali ya pili ya chuo cha kimataifa cha Biblia (International School of
ministry – ISOM), tawi la Tanzania. Kwa mara ya pili sasa, lakini pia ni mara
ya kwanza kwa ngazi ya degree au BA (Bachelor
of arts in Bible knowledge)
Chuo cha ISOM
kikishirikiana na chuo kikuu cha uongozi (Christian Leadership University)
vyenye makao makuu huko Marekani, kwa mara ya kwanza Tanzania, wametoa vyeti
kwa ngazi ya shahada na stashahada (Diploma and BA).
John Shabani ni kati
ya wanafunzi waliotunukiwa cheti kwa ngazi ya degree. Kabla ya kuhitimu, chuo
kilipata bahati ya kutembelewa na mmoja wa viongozi wa ISOM kutoka Marekani,
Dr. Lee. Kiongozi huyo aliwapiga msasa wanafunzi kwa muda wa siku tatu.
Usajili wa wanafunzi
wapya unaendelea.
0 comments:
Post a Comment