Taasisi
hiyo itajikita katika kutafuta ufumbuzi katika kuwasaidia watoto, vijana na
kina mama wanaoishi katika mazingira magumu. Hivi karibuni John alifanya ziara
huko Turkana Kenya maali ambapo kuna jamii ya watu wanaoishi katika mazingira
magumu sana na walioshikilia mila na tamaduni zilizo kinyume na haki za
binadamu, pia alitembelea katika moja ya kambi kubwa ya wakimbizi barani
Afrika; kambi hiyo inaitwa KAKUMA, yenye wakimbizi kutoka Uganda, Rwanda, DRC
Kongo, Burundi, Somalia, Rwanda n.k.
Pia John alitembelea vijiji kadhaa huko Sudan, na kujionea jinsi maisha
yalivyo magumu hasa kutokana na vita vya mara kwa mara katika nchi hiyo amba yo
hivi karibuni imegawanyika na kuwa nchi mbili.
Kwa upande wa Tanzania, John amekuwa akifanya ziara mbalimbali,
akitembelea jamii ya watu wanaoishi katika mazingira magumu na hasa wale
waliokumbatia mila zinazorudisha nyuma maendeleo. Katika ya makabila hayo ni wa
Hadzabe, wa Mang’ati, wa Masai na makabila mengine madogomadogo.
Kwa msaada wa Mungu, John amepanga kutembelea huko Somali, Kongo, Misri
na nchi zingine barani Afrika.
Pia ili kuibua vipaji kwa vijana na watoto na kuviendeleza, ameanzisha
kituo cha kuibua vipaji, na kwa kuanza, ameanzisha kituo cha kuibua vipaji vya
uimbaji na uigizaji. Mpaka sasa kituo hicho kimeibua vipaji vya watoto 35,
vijana 105 na watu wazima 22.
Unapoomba, usisahau kulitaja jina la John Shabani, mwana harakati
aliyejitolea kwa nguvu zake, Vipaji vyake pamoja na uwezo wake mdogo kuwasaidia
watu wengine.
Watu hawa wanahitaji msaada wa kila aina ili
waweze kuishi kama mwanadamu mwingine.
Wito wangu, ni kwa kila mtu kuguswa na na hali
hii na kuungana namikatika kuwasaidia ndugu zetu hawa. Usiulize serikali
imekufanyia nini, bali jiulize umechangia nini katika serikali yako. Kumbuka amsaidiaye
maskini humkopesha Mungu, na Mungu wetu hawezikukaa na deni la mtu,yeye hulipa
mara mia. Ukitaka kujua maisha magumu, tembelea vijijini. Kumbuka mchango wako
wa hali na mali ni wa muhimu sana. Mchango wako na wangu hakika unaweza
kuwasaidia ndugu zetu hawa.
Jamii ya waturkana wanaishi mpakani mwa kenya na sudan
Hapo juu Mch. John Akiwa katika mlango wa kuingilia wa nyumba za waturkana. Nyumba hii wanaishi Baba, mama, watotot, ndugu wa familia pamoja na mifugo (One of the Turkan's house)
John Akigawa msaada wa chakula na mavazi kwa watotot yatima huko soudan
(Giving Foods and others needs to the orphans in Sudan)
hapo juu, John akiwa katika lango la kuingilia katika moja ya kambi kubwa za wakimbizi barani afrika, ijulikanayo kwa jina la Kakuma (John visits Kakuma Refugee Camp)
Hii ndio kambi ya kakuma
(Kakuma Refugee Camp)
John Akicheza Ngoma za kihadzabe (Hadzabe dance)
John katika mpango wa kuinua vipaji kwa vijana
John na mkakati wa kuwasaidia watoto (Help Youth and children program)
0 comments:
Post a Comment