Wengi wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho ni wachanga na watu wenye ulemavu. Taasisi mbalimbali za serikali na binafsi pia zimekuwa zikipeleka watoto katika kituo hicho.
Muonekano wa nje wa jengo la Shalom
Picha juu ni John Shabani alipokitembelea kituo hicho kilichopo kilomita 160 kutoka arusha mjini, ni mkakati wa kuibua vipaji vya watoto na kuviendeleza. Watoto hawa wanahitaji kurekodi nyimbo zao mbalimbali kwa mfumo wa CD na Video, pia kuwezeshwa vifaa mbalimbali vya mazoezi. Ungana na John Shabani katika kuviendelea vipaji vya watoto hao
Hivi ni baadhi ya vitanda vya watoto hao
Watoto wengine wanauwezo mkubwa wa kusakata soka
Watoto wakipata chai ya asubui
Waotot wakiwa katika hali ya furaha
John Shabani akiurahi na watoto
Hawa ni baadhi ya watoto wa shalom Shalom Orphanage center ambao wamekuwa wakisomeshwa katika shule mbalimbali
Watoto hawa wanaolelewa na kituo cha shalom Orphanage Center, walikutwa katika mapori ya karatu wakiishi nje tu, maisha yao ni ya kuzurura maeneo mbalimbali na sehemu zinazotupwa taka ilikujiokotea mabaki ya vyakula. cha kusikitisha, mzazi pekee anayeishi na watoto hao baada ya mama yao kuingia mitini, Baba huyo ni mlevi na amekuwa akiwabaka na kuwalawiti watoto hao kwa zamu.
John shabani akiwa akimsaidia mtoto kupiga ngoma. viongovyote vya mtotot huyo havina uwezo wakufanya chocho, vimesababishwa kupooza na mzazi wa watoto huyo, ambaye baada ya kujifungua mtoto huyo aliamua kuwa akimfungia mtoto huyo ndani na kumpa madawa ya usingizi, huku akiendelea na biashara ya kujiuza. Pembeni ni Mchungaji Johnson Lugenge ambaye ndiye msaidi wa mama Warra katika kuwalea watoto hao.
Mmoja wa wazungu wanaokuja mara kwa mara wakijitolea kuwahudumia watoto hao, hapa amemkumbatia mtotot huyo ambaye mikono, miguu na mdomo wake vimepooza.
JE ungependa kuwa sehemu ya baraka kwa hao watoto kwa kujitolea (Volunteer), au kuchangia pesa zako, chakula, mavazi, elimu? Wasiliana na uongozi wa Shalom Orphanage Center kwa simu namba:
O767904608 au 0755244117.
Mungu akubariki sana!
0 comments:
Post a Comment