4 October 2012

SHEREHE YA KUMPONGEZA MCHUNGAJI BENJAMAIN BUKUKU KWA KUHITIMU DEGREE YA UDHAMIRI (MASTER OF DIVINITY- MD)


Dr. Barnabas Mtokambali (Askofu mkuu wa T.A.G) akimwombea Mchungaji Benjamin Bukuku na mke wake

Chuo alichosomea Mch. B. Bukuku - International Theological Seminary

Baada ya kumaliza masomo yake huko marekani, Mchungaji Banjamini Bukuku wa Amani Christian Center – Moshi, hatimiaye leo mamia ya watu wakiwemo maaskofu, wachungaji, pamoja na viongozi kutoka idara mbalimbali za serikali wamehudhuria sherehe ya kumpongeza Mtumishi huyo wa Mungu katika kanisa hilo. Mgeni rasmi katika sherehe. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikua Dr. Barnabas Mtokambali (Askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God). Kwaya mbalimbali pamoja na waimbaji binafsi kutoka Dar es salaam, John Shabani na stella Joel wamepamba sherehe hiyo kwa nyimbo za kiroho.

Akihutubia katika sherehe hiyo, Askofu B. Mtokambali amempongeza Mchungaji bubuku kwa uamuzi wake wa kujiendeleza ki-elimu hasa kusomea degree ya udhamiri ambayo katika T.A.G ni wachungaji watano tu waliofikia kiwango hicho. Pia Chuo alichosomea INTERNATIONAL THEOLOGICAL SEMINARY kilichopo Los angeles California marekani, ni chuo chenye hadhi ya kimataifa na kinachojulikana duniani kote.

Mchungaji B. Bukuku amekuwa akigusa mioyo ya watu mbalimbali kwa mosomo mazuri ya kiroho. Mamia ya watu wamefunguliwa kupitia huduma yake kwa njia ya radio kama vile Upendo Radio Dar es salaam kila juma tano saa 3:00 usiku, Radio sauti ya injili Moshi kila juma tano saa 3.30 usiku. Mamia ya watu wamebarikiwa na kufunguliwa na huduma ya Mchungaji Bukuku.

Katika sherehe hiyo, Wachungaji, Viongozi mbalimbali wa kanisa pamoja na washirika, wameshauriwa kujiendeleza ki-elimu kulingana na Neno la Mungu linavyosema, mtafute elimu umshike sana, usimwsche aende zake.. Akitoa ushauri huo, Askofu Mtokambali amesema, katika dunia ya sayansi na teknologia, wakristo wasibweteke ili kuufikia ulimwengu pamoja na kujiandaa kushika nyazifa kadhaa katika serikali.
 Mchungaji Benjamin Bukuku na wanafunzi wenzake huko Los angeles siku ya kuhitimu chuo

 
 Askofu B. Mtokambali pamoja na watumishi kadhaa wakati wa kufungua sherehe kwa maombi

 John Shabani akimtukuza Bwana katika sherehe hiyo

 Mwimbaji John Shabani kutoka Dar es salaam akimpongeza Mch. B. Bukuku


 Bishop B. Mtokambali akimmpongeza Mch. B. Bukuku

John Shabani katika picha ya pamoja na Mch. Benjamin Bukuku

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP