THE OFFICIAL JOHN SHABANI AND GOSPEL IN AFRICA BLOG

Welcome to the official blog of the the gospel singer, songwriter and teacher John Shabani. If you are one of the fans among the millions, feel free to get connected with John Shabani and stay updated on this blog.To learn more about John Shaban and his Ministry, please click the about button above.

GET THE LATEST FROM JOHN SHABAN AND THE GOSPEL NEWS COMMUNITY

You will be able to read and review the latest news on John Shabani's tour and other specials. You will also come across the best articles of news on Gospel from all across Africa and the International Community.Please do feel free to review our categories of news and events.

FEEL FREE TO LEARN MORE ABOUT JOHN SHABANI AND HIS MINISTRY

If you wish to learn more about John Shabani and his ministry, please feel free to connect with John Shabani on the social networks. You can keep up with John Shabani and the Gospel in Africa community on both twitter, facebook, google plus and many other more.

STAY UPDATED WITH INTERNATIONAL AND LOCAL GOSPEL NEWS

Gospel in Africa Blog is a comprehensive gathering place for African Gospel music fans. Offering the latest news and information about Local and International Gospel music and news, Gospel in Africa Blog also shares the spotlight with other genres of Christian music that more than ever, seemingly overlap musical genre lines, such as Bluegrass Gospel, Christian Country and others. Singing News, the leading African Gospel and International music Blog, features African and international Gospel lyrics, radio, news, Christian concerts, songs, artists, and more.

GET IN TOUCH AND STAY CONNECTED WITH JOHN SHABANI

If you are interested in contacting and staying in touch with John Shabani then here are the contacts. E- mail: touchingvoice@yahoo.com or , princejohntz@yahoo.com, Mob: +255 754 818 767 or +255 716 560 094, www.facebook.com/john.shabani.

28 May 2021

FAIDA ZA KUIMBA



FAIDA ZA KUIMBA

Kuna aina mbili kuu za faida:

1.              Faida za kuimba ambazo zinamsaidia mtu kiafya.

2.              Faida za kuimba kwenye jamii

Kwanza kabisa naomba nikueleze maana ya kuimba. 

KUIMBA ni kutoa sauti yenye ulinganifu, sauti hiyo inatakiwa kufuata mapigo ya ki muziki na ni zaidi ya kughani. Zamani mababu zetu walikuwa wanaimba kwenye kazi mbalimbali ili kurahisisha kazi yenyewe iliyokuwa ikifanyika, mpaka sasa watu wengi huimba ili kuburudisha, kufundisha, kukosoa au kuelimisha kikundi fulani cha watu.

Kuimba ni faida kwa mwimbaji kwani kuna faida nyingi saana ambazo mwimbaji anazipata kama vile kuburudika, kuburudisha, kuinjilisha, kuhamasisha, kufariji, kufurahisha n.k

Leo nitakueleza faida za kuimba ambazo zinamsaidia mwimbaji kiafya:

  1. Kuimba ni mazoezi. Unapoimba unafanya mazoezi ambayo pia ni kinga kwa magonjwa mbalimbali yanayoweza kumuathiri mtu ambaye hafanyi mazoezi. Mazoezi ambayo nayasemea hapa ni Kupanua kiwambo (diaphragm), mwanakwaya anatumia nguvu nyingi sana wakati anaimba ili kupanua mapafu na kiwambo. Hii itamsaidia mwimbaji ku zuia magonjwa yanayoweza kuathiri mapafu kama vile kikohozi, mafua.
  2. Inasaidia kuboresha mfumo wa upumuaji mwilini kwani msukumo wa damu utakuwa mkubwa ambapo ndani ya chembe za damu huwa kuna hewa safi ya Oxygen ambayo husambazwa mwilini pote na chembe za damu katika mzunguko. 
  3. Inasaidia kupunguza mawazo. Hili liko wazi kabisa  kwa mwanakwaya au mwimbaji yeyote yule, ukiimba unapunguza mawazo. Mtu mwenye mawazo anaweza kuugua hata magonjwa ya akili na kisaikolojia.
  4. Husaidia kusimama vizuri. Mwimbaji huwa ana staili yake ya jusimama ambapo kifua chake anakiweka mbele, mabega yanakuwa yameinuka kidogo ili kumsaidia kutoa sauti, mgongo pia unakuwa umenyooka vizuri. Hii inamsaidia kuufanya uti wa mgongo usijikunje. Kwa hiyo mwanakwaya anapoimba kwa muda mrefu huwa na tabia ya kusimama kama anataka kuimba na hivyo kumsaidia yeye kutunza na kukinga uti wa mgongo.
  5. Huimarisha mfumo wa kinga mwilini. (strengthen the immunity system) Kwenye mwili wa binadamu kuna kinga (protini) ambayo ina jina la kitaalamu ambalo ni Immunoglobulins, kwa hiyo mtu anapoimba anafanya mazoezi (kama nilivyosema hapo juu) na unapofanya mazoezi ina maana kwamba unaongeza kinga mwilini tofauti na mtu ambaye amekaa tu bila kufanya mazoezi


Kwa ufupi sasa kuimba kuna faida kiafya, faida zingine nimezitaja hapa chini ambazo ni:

  • Kuimba nidawa ya asili ya mawazo (natural annti-depresant)
  • Kuimba kunapunguza mawazo kwa kiasi kikubwa sana (ni dawa kwa mtu mwenye mawazo)
  • Kuimba kunaongeza uwezo wa kufikiri na kuchukua maamuzi.

Faida za kuimba kwenye jamii.

Kuimba humsaidia mtu kuongeza idadi ya marafiki.

Kuimba kunamwongezea mtu kujiamini katika kila kitu anachokifanya kwa faida yake na jamii kwa ujumla.Kuimba kunapanua wigo wa mawasiliano.

Lakini zaidi ya hapo kuimba ni ajira kubwa.

Naamini masomo haya yamefungua ufahamu kwako. Ukitaka kujifunza zaidi tuwasiliane, ili nawewe uwe mmoja wa wanafunzi wangu katika darasa letu la mafunzo ya sauti na uimbaji.

Whtspp/call +255716560095

Facebook: John Shabani (Mtoto wa Mfalme)

Instagram: sjvocaltraining

E-mail: jshabani2011@gmail.com

Web: www.johnshabani.blogspot.com

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP