THE OFFICIAL JOHN SHABANI AND GOSPEL IN AFRICA BLOG

Welcome to the official blog of the the gospel singer, songwriter and teacher John Shabani. If you are one of the fans among the millions, feel free to get connected with John Shabani and stay updated on this blog.To learn more about John Shaban and his Ministry, please click the about button above.

GET THE LATEST FROM JOHN SHABAN AND THE GOSPEL NEWS COMMUNITY

You will be able to read and review the latest news on John Shabani's tour and other specials. You will also come across the best articles of news on Gospel from all across Africa and the International Community.Please do feel free to review our categories of news and events.

FEEL FREE TO LEARN MORE ABOUT JOHN SHABANI AND HIS MINISTRY

If you wish to learn more about John Shabani and his ministry, please feel free to connect with John Shabani on the social networks. You can keep up with John Shabani and the Gospel in Africa community on both twitter, facebook, google plus and many other more.

STAY UPDATED WITH INTERNATIONAL AND LOCAL GOSPEL NEWS

Gospel in Africa Blog is a comprehensive gathering place for African Gospel music fans. Offering the latest news and information about Local and International Gospel music and news, Gospel in Africa Blog also shares the spotlight with other genres of Christian music that more than ever, seemingly overlap musical genre lines, such as Bluegrass Gospel, Christian Country and others. Singing News, the leading African Gospel and International music Blog, features African and international Gospel lyrics, radio, news, Christian concerts, songs, artists, and more.

GET IN TOUCH AND STAY CONNECTED WITH JOHN SHABANI

If you are interested in contacting and staying in touch with John Shabani then here are the contacts. E- mail: touchingvoice@yahoo.com or , princejohntz@yahoo.com, Mob: +255 754 818 767 or +255 716 560 094, www.facebook.com/john.shabani.

28 June 2018

SIKU YA TUKIO KUBWA LA WATANZANIA WOTE KUKUSANYIKA PAMOJA KUMSIFU MUNGU




 WAPENDWA, ILE SIKU YA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI DINI ZAO AU DHEHEBU, KUKUSANYIKA PAMOJA KUMSIFU MUNGU WETU IMEFIKA SASA.
NAWAKARIBISHA RASMI ILI TUMTUKUZE MUNGU WETU.

 NI SIKU YA UJIO MPYA WA PST. JOHN SHABANI, YULE MWALIMU MAARUFU 
WA NYIMBO ZA INJILI ALIYEFUNDISHA KWAYA NYINGI NA WAIMBAJI WENGI BINAFSI. 
JOHN SHABANI ATAWAONGOZA MAMIA YA WATU KATIKA KUSIFU, 
PIA SIKU HIYO DVD YAKE ILIOANDALIWA KWA VIWANGO ITAWEKWA WAKFU. ZAIDI YA KWAYA KUMI NA WAIMBAJI BINAFSI WATAHUDUMU. 








NI PALE NDANI YA KANISA LA WCC KEBBY'S HOTEL MWENGE MKABALA NA KITUO CHA ITV. NI TAREHE 1/7/2018, KUANZIA SAA NANE MCHANA.
NI TUKIO LITAKALOHUDHURIWA NA MAASKOFU, WACHUNGAJI, MITUME NA WATU WA DINI ZOTE.MGENI RASMI NI MISS NGUSE NYERERE, WAGINI MAALUM NI MADAME LUUNDO KUTOKA CANADA NA MCHUNGAJI NA MWALIMU PETER MITIMINGI, ATATOA UJUMBE MAALUM KWA WAIMBAJI NA KWA KILA MWENYE KIU YA KUMTUMIKIA MUNGU. 
HAKUNA KIINGILIO, NJOO NA ELFU KUMI KWAAJILI YA KUNUNUA DVD. RANGI YA TUKIO NI NYEUSI NA NYEKUNDU
KWA MAWASILIANO ZAIDI 0759778778 NAMAANISHA 0759778778 
NJOO WEWE NA RAFIKI ZAKO, PIA NISAIDIE KUSHARE TANGAZO HILI.

15 June 2018

TUKIO KUBWA LA UZINDUZI WA WCC CHOIR, KWAYA YA KANISA LA WAREHOUSE CHRISTIAN CENTRE (GHALA LA CHAKULA) LINALOONGOZWA NA MCH. NA MWL. PETER MITIMINGI

Zawadi pekee ya kwaya kwa baba na mama
Mwalimu John Shabani, Mtumishi Peter Mitimingi, saa ya kuabudu.




 Hawa ni mamia ya watu waliohudhuria siku ya tukio.
 Praise team ya kanisa wakimtukuza Mungu

 Baada ya tukio lililotikisa jiji la Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla la uzinduzi wa kanisa "GHALA LA CHAKULA - WARE HOUSE CHRISTIAN CENTRE", baada ya miezi michache limefanyika tukio lingine kubwa zaidi ndani ya kanisa hilo, si ligine bali lile la uzinduzi wa kwaya pekee ya kanisa hilo (WCC CHOIR).

Hakika haijawahi kutokea kwa kanisa linaloanza kuwa na kwaya ya zaidi ya watu 50, tena wakiimba kwa ufanisi wa hali ya juu. Hii ni kutokana na mafunzo maalum kutoka kwa mtaalam wa sauti na mwalimu John shabani. Ni kwaya pekee yenye watu wa rika zote.

Tunasababu zote za kumpongeza Mtumishi Peter Mitimingi kwa maono haya makubwa ya kuanzisha huduma itakayoleta ukombozi kwa jamii.

HACK MOYO WA MPENZI WAKO USIHACK SIMU YAKE - UJUMBE MUHIMU KWA WANANDOA NA WALIO KWENYE MAHUSIANO

    Huu ni ujumbe muhimu kwa wanandoa na walio 
kwenye muhusiano kutoka kwa
Winnie Nzobakenga

Nimewahi kusikia wanawake wengi wanaulizia jinsi ya kuhack simu za waume zao ili wawe wanasoma meseji za waume zao. Haya yapo pia hata kwa wachumba.  Mmh! hivi ninyi wamama au wan awake wenzangu, mnajipenda kweli? Sasa ukishahack simu yake then what?

Ukikuta msg za wanawake wengine then what,inakusaidia nini??ukishajua mmeo anamchepuko utachukua mapanga na visu na panga kwenda kupigana?utaweza kweli?ukishajua kuna mwanamke kazaa naye na amempangishia nyumba utapata nguvu za kwenda kumpiga huyo mwanamke?? Ukishajua utaongeza mapenzi kwa mme wako au ndio utaenda kuvunja ndoa na kubeba vilago na kuondoka?watoto utaawaacha au utaondoka nao,nani atawalea,nani atawapa matumizi??ninawambia kabisa ninyi ambao mnahangaika kujua namna ya kuhack simu ya mme wako kujua kinachoendelea.
NISIKIE NIKWAMBIE
Hapo tatizo sio simu,tatizo ni moyo ,unatakiwa udeal kuurudisha moyo wake.Ukihangaika na simu,simu haina shida wanaweza wakaacha kuwasiliana mme akahamia kabisa kwa mchepuko utamfanyaje?mbona simu ni kitu kidogo saaana.Wewe fanya juu chini huo moyo wake usikuponyoke,moyo ukishaponyoka hata uhack nini hamna kitu. Kuna mwingine anataka akishakuta msgs kwenye simu ya mme wake ndio aanze kufunga na kuomba,kuombea ndoa yake.Sikia tu nikupe siri sio rahisi kuomba ukishajua kuna anayekuzunguka utachemsha,utaishia tu kulia.Askari yeyote huwa hafanyi mazoezi siku ya vita,siku ya vita huwa anaenda kufanya alichofanyia mazoezi miaka au miezi kadhaa iliyopita ya maandalizi.
Huna haja ya kukamata msgs za mapenzi za mwenzi wako ndio uanze kuomba,anza kuomba sasa,wewe omba kabisa kwa nguvu zako zoote.Biblia inasema kuwa "Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.(1 Wathesalonike 5:3). Kumbe kati ya watu wanaotakiwa kuombea ndoa zao kwa mzigo mkubwa ni wale ambao saivi wanaona kuwa ndoa zao zina amani.Amani uliyonayo na furaha visikufanye ukajisahau na kulala omba omba hayo maombi yatatumika wakati wa vita.Wala haina haja ya kukuta msgs za mcheps ndo uanze kuomba .Yafanye maombi kuwa maisha yako,usiishi bila maombi,usiongeje maombi ya zima moto. Jambo jingine Biblia inasema kwamba Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia; Na wenye haki watapewa matakwa yao.(Mithali 10:24)
Kuna wanawake wao masaa 24 wanawaza kuhusu michepuko,hawana imani kabisa na waume zao,kila wakati kila saa anawaza mme yuko na mtu mwingine,akichelewa tu kurudi nyumbani anawaza mme wangu yuko kwa mwanamke,simu ya mwanaume isipopatikana tu kidogo hewani mke anajua mme yuko kwa mchepuko,pesa asipoona matumizi yake anajua kapewa mchepuko. Yaani mwanamke anaishi hayo maisha ya wasiwasi wakati wote utafikiri kuku mtetea anayetafuta sehemu ya kutaga.Mara ashike simu ya mme atafute msgs na dialled calls na received calls,mara aende kwenye messenger ya facebook na whatsup,mara atafute jinsi ya kuhack number ya mmewe,mara anunue number mpya aanze kumtumia mmewe msgs na kujifanya mwanamke mwingine ili mradi tu afanye fujo.Mme akirudi ananuswa hadi nguo za ndani hadi mdomo utanuswa hahaha utafikiri mbwa wa usalama,kwa madai ya kuwa mke ni mlinzi.
Rafiki wala hatulindagi hivyo,ulinzi ni kufanya majukumu yako kama mke na kusugua goti.Hayo mengine mwachie Mungu ashugulike naye,ukisugua vizuri goti hakuna kitu ambacho kitafanyika kinyume Mungu asikujulishe.Lolote kabla halijatokea ktk ulimwengu wa mwili,Mungu atakuonyesha ktk ulimwengu wa roho na utakisambaratisha kabla hakijatokea juu kwa juu.Ndio maana nasema usighulike sana kwa namna ya mwili kuhack sijui simu na msg,shugulika magotini.Kuna mambo ukiyafanya kwa mmeo automatically utauhack moyo wa mwanaume na kikubwa ni #Unyenyekevu.,vingine nitakupa siku nyingine.Ila ukweli ni kwamba unaweza kuuteka moyo wa mmeo,kama Delila aliweza na wewe unaweza.Stop hacking your husbands phones,kwanza huo muda mnapata wapi??
Winnie Nzobakenga

6 June 2018

MWALIMU NA MCHUNGAJI DKT. PETER MITIMNGI AANZISHA HUDUMA IJULIKANYO KWA JINA LA GHALA LA CHAKULA - WCC

 Baada ya kulitumikia kanisa la TAG kwa miaka mingi kama mchungaji msaidizi na baadaye kuanzisha huduma ya injili vijijini - VHM, hatimaye Mwalimu na Mchungaji Peter Mitimingi aanzisha kanisa lijulikano kwa jina la Ghala la chakula au kwa kimombo; Warehouse Christian Centre - WCC
 Mchungaji Peter Mitimingi akiwa katika picha ya pamoja na wahudumu siku ya uzinduzi wa kanisa.
 Maelfu ya watu waliohudhuria siku hiyo


Na John Shabani - Dar es salaam

Baada ya kutumika katika kanisa la Tanzania Asseblies of God  (TAG ) zaidi ya miaka ishirini Mchungaji na mwalimu Dr Peter Mitimingi azindua kanisa lake rasmi  Kebbys Hotel Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika uzinduzi wa kanisa hilo uliohudhuriwa na zaidi ya watu elfu tatu  Dr Mitimingi amesema kuwa yapo malengo matatu ambayo yamepelekea yeye kuanzisha WCC ikiwa ni pamoja watu kukua kiroho ,wawe na Ufahamu,waijue kweli ambao utamsafirisha kupata majibu ya changamoto mbalimbali pamoja na Uhuru

Amesema kuwa wengi waneokoka na wapo makanisani miaka mingi lakini hawajakua kiroho,amesema kuwa mtu akilifahamu tatizo ni jibu sahihi kuliko kutokujua tatizo.

"Kwakutolifahamu tatizo unaweza ukatibu ugonjwa ambao siyo kabisa ila ukilifahamu tatizo utajua uanzie wapi kulitatua,kwani ratizonlinaanzia kwenye kulijua tatizo lenyewe " alisema Mitimingi

Ameeleza kuwa katika malengo hayo endapo angeendelea kuwa katika kanisa la TAG malengo hayo yasingekamilika kutokana na taratibu za Kanisa hilo.

"Sijatoka kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG )kwa ugomvi kama watu wanavyozusha bali nilikwenda kwa viongozi wa juu wa Kanisa wakanisa nilianza na nyumbani Mwenge TAG
ambapo nilikuwa mchungaji msaidizi, nikaenda kwa mchungaji wa wilaya , nikaenda kwa Makamu wa Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dkt. Magnus Mhiche ,wote hawa walinikubali ,wakaniombea na kuniwekea mikono tayari kwa kutumika." Alisema Mitimingi.
 

Mungu akubariki Mtumishi kwa maono haya makubwa.

5 June 2018

KARIBU SJ STUDIO

 SJ STUDIO na SJ VOCAL TRAINING 
KIMBILIO LA WANAOTAKA KUORESHA SAUTI ZAO, WANAOTAKA 
KUIMBA NA KUREKODI KWA VIWANGO. 
KARIBUNI SANA



 KWA MAWASILIANO:
CALL/WHATSAPP
+255716560094

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP