25 November 2019

UANDISHI AU UTUNZI WA NYIMBO (SONG WRITING/COMPOSITION)

Ebu tuangalie misingi ya utunzi wa nyimbo

JE UNAWAJUA WATU MUHIMU KWENYE KWAYA, BENDI AU KWA MWIMBAJI BINAFSI?

Ili wimbo uweze kukamilika huwa unakuwa na vipengele kadhaa ndani yake.
-       Kuna maneno au mashahiri, au kwa lugha ya siku hizi ‘mistari’ na kwa kiingereza Lyrics.
Nyimbo inaweza kuandikwa na mtu mmoja au wawili au Zaidi, tunawaita kwa kimombo Song writers. Mwandishi wa nyimbo anayeweka maneno ya wimbo (lyrics) eitha kwa kwa maneno ya kawaida au kwa nota huitwa Lyricict
-       Mistari huhitaji kupewa sauti ya kuimbia, Melody. Na huyo anayebuni au kutengeneza melody huitwa Composer. Lakini kama mtu atatengeneza vyote nilivyotaja hapo juu, kwa ufupi anatambulika kama mwandishi wa nyimbo (songwriter)
-       Baada ya hapo hutengenezwa arrangement, au mpangilio wa muziki huo, nini kinakuja wapi, waimbaji waimbe vipi na kujumlisha kazi zote hizi unapata wimbo mmoja.

Kwa uzoefu wa bendi au kwaya zetu, mara nyingi, Lyrics huletwa na mtu mmoja, anaweza akaleta mistari yenye melody au akaleta mistari peke yake na kutaka msaada wa wanamuziki wenzie watafute melody. Kazi inafuata ya arrangement pia hufanywa kwa ushirikiano na hatimae kukapatikana wimbo ambao kwa utamaduni wetu huwa tunatangaza kuwa mtunzi ni yule aliyekuja na mistari.

Si kila mtu ana kipaji cha kutunga, japo hiyo ndio imani ya wengi kuwa kila anaejua kuimba hujua kutunga. Waimbaji wengi maarufu duniani waliimba nyimbo zilizotungwa na wengine, na halikadhalika si kila anaetunga anajua kuimba, watunzi hata wa mashahiri huwaachia watu wengine waghani mashahiri yao, mtunzi akilazimisha kuimba wakati hana kipaji hicho matokeo ni madudu tu na hali kadhalika muimbaji asiye na kipaji cha kutunga aking’ang’ania kutunga kipawa chake cha kuimba kinaweza kisionekane kutokana na utunzi kuwa hafifu.
Na hali kadhalika si kila mtu ni arranger, tatizo ni pale asiekuwa na kipaji anaamua kufanya hiyo kazi, kinachotoka hakieleweki kama kinakwenda au kinarudi. Hali hii ipo pia kwa waimbaji binafsi(solo artist), wanataka kujionyesha wanajua kila kitu au wanafanya kila kitu, haiwezekani. Kuna wakati unahitaji aina fulani za tungo kutuko kwa  watunzi wazuri, una hitaji mwalimu au mtu wa kukuongoza kuwa bora zaidi, lakini pia zaidi ya hilo, unamwitaji arranger. Kama wewe umebahatika kufanya kila kitu basi mshukuru Mungu kwa hilo.
Kama nilivyosema awali katika bendi arrangement huwa ni mchango wa mawazo, lakini ukifanya utafiti kidogo utagundua hata katika kazi inayoonekana ya kikundi kuna mtu au watu ndio wanaoongoza nini kipigwe wapi. Nichukulie mfano wa bendi zilizopita, katika kutaka kujua undani wa jambo hili, nilipata maelezo ya kina kutoka kwa mkongwe wa muziki wa dansi hapa nchini, ndugu yetu John Kitime. Yeye anasema “Katika bendi nilizopitia kama vile Orchestra Mambo Bado, Orchestra Makassy au Vijana Jazz enzi hizo kulikuwa na mtu ana sauti ya mwisho kuhusu arrangement”
Kupendwa kwa wimbo ni mkusanyiko wa haya niliyoyataja hapo juu. Nyimbo nyingi zinazopendwa sasa hazitachukua muda kusahaulika kutokana na kuwa na arrangement hafifu sana. Mfumo wa sasa wa waimbaji kujaza wimbo wote bila kuweko na hata nafasi ya vyombo kutamba ni aina moja ya arrangement, lakini kwa mtazamo wangu nyimbo hizi zitasahaulika katika kipindi kifupi.
Katika mfumo wa uajiri au utafutaji wa wanamuziki katika vikundi vyetu, umuhimu hutolewa kwa wapiga vyombo na waimbaji, nadra kusikia mtunzi anatafutwa na nadra zaidi kusikia anatafutwa arranger, hivyo huwa bahati tu akatokea arranger mzuri au mtunzi mzuri katika kwaya au bendi na si kutokana na mipangilio. Pia nawajua arrangers wengi ambao hata wao hawajui kuwa ni arrangers, hivyo ‘majembe’ kama hayo yakifukuzwa au kuhama kwaya au bendi, basi vikundi hivyo vinaanza kudorora, na si mara moja nimekuta hata kwaya/bendi zenyewe hazijui kwanini ghafla kuna ukame wa tungo nzuri, pengine yule msanii aliyeitwa mzigo, kwa kuwa hakuwa muimbaji mzuri alikuwa ndie arranger bora wa kikundi hicho!!!
Labda niseme kwa kifupi, arrangement ndio ule mpangilio wa kuamua nini kipigwe na kipigwe wapi. Muziki unasheria za msingi kama vile hesabu.2+2=4, si nne na nusu wala na robo, arranger anakuwa na kipaji cha kupanga nini na anaweza kukueleza kwa nini pale kipigwe kinanda na gitaa liwe kimya au pale vipigwe vyote na kwanini iwe hivyo.
Muziki wetu wa wa kwaya au waimbaji wa siku hizi wakiwamo pia wale wa Bongoflava, umetawaliwa na waimbaji kwani swala la utunzi wa muziki na arrangement (kunakotambuliwa kama kutengeneza beat), huachiwa ‘producer’. Ni wazi ukisikiliza mfululizo wa nyimbo zinazotoka kila siku ni wazi kuwa maproducer wachache sana wanakipaji cha kuarrange, utasikia vyombo vinalia katika wimbo bila kuwa na mpangilio wala sababu ya kuwepo, hapa utasikia filimbi, mara saksafon, mara rimba, mara gitaa. Ninapo yasema hayo, sijawasahau wale waongozaji wazuri au masoloist, ambao ni watu pekee tena wenye mchango wa pekee kwenye vikundi vyetu vya uimbaji. Hawa nao wakiondoka huachapengo kubwa sana.

ZANA ZA UTUNZI
Mtunzi au mwandishi wa nyimbo, popote alipo anashauriwa kuwa na zana muhimu kama; Kifaa chochote cha kurekodia, daftari au notebook na kalamu. Kwa dunia ya leo, ukiwa na simu yako ya mkononi au tablet inatosha. Kwa lugha nyingine tunasema; Ikiwa kweli unataka kuchukua uandishi au utuzi wako wako wa wimbo kwa umakini mkubwa, unapaswa kujenga tabiaya kubeba zana au vifaa vya utunzi/uandishi wa nyimbo popote ulipo. (If you want to take your songwriting seriously and create authentic music, you should do your best to carry songwriting materials with you everywhere).

UANDISHI WA WIMBO.
MWANZO BORA WA UANDISHI BORA WA WIMBO.
Ifahamike ya kwamba kuna aina nyingi za kuanza kuandika wimbo, ila njia MAKINI ni ya kuanza na MADA ambayo itakupa JINA/TITLE.
UMUHIMU WA JINA/TITLE/MADA.
1. Jina la wimbo ni moyo wa wimbo.
2. Jina huelezea wimbo mzima.
3. Jina/Mada itakuongoza vyema ktk kuandika mistari na kukufanya usiandike nje ya mada.
Unda au chagua jina ambalo ni fupi si zaidi ya maneno matano (5) ili iwe rahisi kukumbukwa na mashabiki hata iwe rahisi kuiomba redioni au kuisema kwa marafiki au washikaji zao. Juu ya hili unaweza fanya uchunguzi wa kupitia majina ya nyimbo mbalimbali ili uone ufupi wa majina ya nyimbo unavyokuwa na madhara chanya kwa mashabiki.
Endelea kufatilia hii kitu tafadhari,na uwape habari marifiki. Wakati ujao tutaangalia kuhusu INTRO, CHORUS, VERSE, CHORUS, VERSE, CHORUS, OUTRO

Ukitaka Huduma ya kuandikiwa au kutungiwa limbo mzuri wasiliana namimi mwalimu wak wa Sauti Afrika Masahriki.


Kocha John Shabani

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP