THE OFFICIAL JOHN SHABANI AND GOSPEL IN AFRICA BLOG

Welcome to the official blog of the the gospel singer, songwriter and teacher John Shabani. If you are one of the fans among the millions, feel free to get connected with John Shabani and stay updated on this blog.To learn more about John Shaban and his Ministry, please click the about button above.

GET THE LATEST FROM JOHN SHABAN AND THE GOSPEL NEWS COMMUNITY

You will be able to read and review the latest news on John Shabani's tour and other specials. You will also come across the best articles of news on Gospel from all across Africa and the International Community.Please do feel free to review our categories of news and events.

FEEL FREE TO LEARN MORE ABOUT JOHN SHABANI AND HIS MINISTRY

If you wish to learn more about John Shabani and his ministry, please feel free to connect with John Shabani on the social networks. You can keep up with John Shabani and the Gospel in Africa community on both twitter, facebook, google plus and many other more.

STAY UPDATED WITH INTERNATIONAL AND LOCAL GOSPEL NEWS

Gospel in Africa Blog is a comprehensive gathering place for African Gospel music fans. Offering the latest news and information about Local and International Gospel music and news, Gospel in Africa Blog also shares the spotlight with other genres of Christian music that more than ever, seemingly overlap musical genre lines, such as Bluegrass Gospel, Christian Country and others. Singing News, the leading African Gospel and International music Blog, features African and international Gospel lyrics, radio, news, Christian concerts, songs, artists, and more.

GET IN TOUCH AND STAY CONNECTED WITH JOHN SHABANI

If you are interested in contacting and staying in touch with John Shabani then here are the contacts. E- mail: touchingvoice@yahoo.com or , princejohntz@yahoo.com, Mob: +255 754 818 767 or +255 716 560 094, www.facebook.com/john.shabani.

25 October 2016

MTAZAMO NA USHAURI WA JOHN PAZIA KWA WAIMBAJI
Anayeonekana kwenye picha hii ni John Pazia, kijana mwenye vipaji vingi, mcha Mungu na mwenye ndoto na maono makubwa

MFAHAMU MTANGAZAJI JOHN PAZIA

John Pazia mwenye makazi yake mkoani Arusha ni mmoja baadhi kati ya watangazaji wenye ushawishi mkubwa Tanzania, na ameinua muziki injili kwa upande wa kaskazini kwa asilimia kubwa na mchango wake umeonekana. Amekuwa sauti ya wengi waliokuwa na kilio cha kuinuka na kutambulika. Ni mtangazaji wa kituo cha radio Radio Habari Maalum kilichopo Jijini Arusha.


MTAZAMO WA JOHN PAZIA KWA MWAKA JANA 2015 NA KINACHOTAKIWA MWAKA HUU
“Mwaka 2015 ulikuwa ni mwaka mzuri ambao ulileta changamoto kwakuwa kuna waimbaji waliofanya kazi nzuri na kuleta changamoto kwa waimbaji wengine, video pia audio na matamasha pia” Alisema John Pazia.
“Pia ulikuwa ni mwaka ambao umewafanya baadhi ya waimbaji wa Injili kujiingiza katika siasa na kuwagawa mashabiki wa muziki wa injili kwa kuingia na kuwaimbia wanasiasa na kuleta gumzo kwa watu na pia gumzo kwa waimbaji wenzao, huenda ikawa walikuwa na malengo yao siwahukumu” na “pia swala la ngazi maana ya makundi ya waimbaji wana mashabiki fulani kama wa Sebene na Hip Hop walikuwa hawachangamani lakini hivi sasa wengi wameanza kuelewa, pia waimbaji wa muziki wa injili wamekuwa karibu wao kwa wao tofauti na kipindi cha nyuma na pia hata kushirikiana katika nyimbo zao.

Pia Wachungaji wameanza kutambua huduma hizi na kukubaliana na kile hususani vijana na kuwaruhusu kumtumikia Mungu katika madhehebu tofauti tofauti na sehemu nyingine nyingi za huduma”. Pia kuna waimbaji waliokurupuka na kufanya kazi mbovu na kutokukubali ushauri, na wengine hawana ushirika mzuri na watangazaji, wengine hutafuta watangazaji wakiwa na shida tu bila hivyo hawana ushirika wa zaidi, wengine hawakubali kuambiwa ukweli wakikosea na hawapendi kuthubutu pia kama kushiriki katika tuzo, pia wengine hawapendi kujitangaza kimitandao, vituo tofauti tofautio vya habari, pia uongozi (management) husema Bwana ataonekana huku wamebweteka, ni jambo la kuthubutu.
Waimbaji wasitoe nyimbo ovyo bila malengo , watazame mbele na pia hii huchangia kutofanya kazi nzuri na zenye viwango, pia video nzuri na zenye viwango.
Pia waimbaji kuwa na ushirika mzuri na makanisa na Baba zao wa kiroho, pia kutodharau waimbaji wadogo ama wenzao lakini ni vyema kuwashauri kwa kutumia njia nzuri ili tuweze kujengana.
Swala muhimu sana ambalo ni vyema watu waelewe si kama wanavyofikiria, uimbaji wa injili ni swala linaloanzia rohoni, na ukitaka wimbo wako usikike  na kuongea na mioyo ya watu na kuponya walioumia, wanaohitaji kutiwa moyo. Usifanye kazi kama kuhudumia watu ila imguse kwanza Mungu na yawe yatokayo kwa Mungu, jenga mahusiano mazuri na Mungu, Mungu hutoa ili awaguse watu wengine kupitia uimbaji.
1.       Ushirika na Mungu, kuomba sana kuliko kuimba sana. Unaweza kutoa nyimbo nyingi lakini zisiguse watu kabisa, kama kiukopi nyimbo za duniani na kuweka maneno ya Mungu kama Mungu haweza kukupa ufunuo.
2.       Waweza kutoa nyimbo nyingi lakini zisiwe na uwepo wa Mungu na Roho Mtakatifu asionekane . Tunza uhusiano na Mungu wako na pia maneno uyazungumzayo kila wakati.

Malengo ya mwaka 2016:
“Malengo ni kuendelea kuusukuma muziki wa Injili na kuwasaidia waimbaji kupitia tasnia yangu, kuwatangazia kazi zao na pia kuwashauri. Haya yote nitayafanya na walio tayari kupokea na kutoa panapostahili, kwakuwa wote tunaujenga mwili wa Kristo. Nitatumia taaluma na kazi yangu kitaifa na kimataifa, nahitaji tu ushirikiano wao” alisema JOHN Pazia.KIJIJI KIMOJA HUKO INDONESIA HUFUKUA MAITI KILA MWEZI AGOSTI Baadhi ya maiti zikiwa zimefukuliwa, kusafishwa na kuvishwa nguo mpya


Wananchi wa kijiji cha Toraja, huko Sulawesi ya Kusini, nchini Indonesia, kila baada ya miaka mitatu, hufukua na kusafisha maiti ya ndugu zao.

Ieleweke kuwa hawafukui maiti hiyo hiyo kila miaka mitatu ila kila maiti inapozikwa, kwa wale wanafuata utamaduni huu, hufukuliwa mara moja na kusafishwa na kuzikwa tena. Na sherehe hiyo inafanywa kila miaka mitatu katika mwezi wa Nane.

Sherehe hiyo inaitwa Ma'nene na wananchi wa kijiji hicho wanaamini kuwa kufanya hivyo inawaletea baraka kwa kuwakumbuka marehemu na kuwasafisha na kuwavalisha nguo ili wapendeze na kuwabariki.

Haijulikani imeanza lini hii sherehe na serikali haiingilii zoezi hili kulinda utamaduni wa watu wa kijiji hiki.
 Wananchi wa kijiji cha Toraja, huko Sulawesi ya Kusini, nchini Indonesia, kila baada ya miaka mitatu, hufukua na kusafisha maiti ya ndugu zao.

Ieleweke kuwa hawafukui maiti hiyo hiyo kila miaka mitatu ila kila maiti inapozikwa, kwa wale wanafuata utamaduni huu, hufukuliwa mara moja na kusafishwa na kuzikwa tena. Na sherehe hiyo inafanywa kila miaka mitatu katika mwezi wa Nane.

Sherehe hiyo inaitwa Ma'nene na wananchi wa kijiji hicho wanaamini kuwa kufanya hivyo inawaletea baraka kwa kuwakumbuka marehemu na kuwasafisha na kuwavalisha nguo ili wapendeze na kuwabariki.

Haijulikani imeanza lini hii sherehe na serikali haiingilii zoezi hili kulinda utamaduni wa watu wa kijiji hiki.

UBORA WA SAUTI KWA MWIMBAJI, MUHUBIRI, MSEMAJI KWENYE MATUKIO MBALIMBALI
Nianze kwa kusema, nimekuwa mmoja kati ya waalimu wa sauti na uimbaji, niliyewezesha watu wengi, vikundi vingi, na kwaya nyingi kuimba vizuri.
Lakini pia nashangaa wapo watu wengi wanaokimbilia studio, wanatengenezewa studio lakini ukweli ni kwamba hawajawa waimbaji wazuri, ni waimbaji wa kuimbia CD. Jamani kuimba vizuri kuna gharama zake.
Ikumbukwe kuwa, ili uimbaji wetu au muziki wetu uwe wa viwango vya kimataifa yapo mambo yanayotakiwa kufanyika:
Kwanza ni uandishi mzuri, ubunifu zaidi, studio bora (quality of studio), kuandaa video yenye viwango (quality of video).
Nimekua nikifundisha kwa kina kuhusu hatua nne za kuelekea kuwa na albam bora ya audio, ikiwa ni pamoja na: mwimbaji kuwa bora, tungo bora, muziki bora na studio bora.
Nikualike tena kuhudhuria mafunzo yetu ya sauti yanayoendelea maeneo ya Ukonga. Kwa kuchangia kidogo tu nitakufundisha mbinu za kuwa mwimbaji bora. Tuwasiliane.
Tuendelee na somo:
Unahitaji kufanya nini?
Unahitaji kuboresha sauti yako kwa kupumua vizuri na kutuliza misuli yako badala ya kuiga mtu mwingine.
Kwa Nini Ni Muhimu?
Sauti nzuri hufanya wengine watulie na kufurahia kusikiliza. Sauti mbaya huaribu mawasiliano, na inaweza kumfadhaisha mwimbaji/msemaji na wasikilizaji.
KWA KAWAIDA watu hawavutiwi tu na mambo yanayosemwa, bali wanavutiwa pia na jinsi yanavyosemwa. Ikiwa mtu anayezungumza nawe au anayeimba mbele yako ana sauti nzuri, changamfu, ya kirafiki, na yenye fadhili, utafurahia kumsikiliza kuliko kama ana sauti kali isiyo ya kirafiki, sivyo? Kukuza sifa hizo nzuri hakutegemei tu kuboresha sauti. Kunaweza kuhusu utu wa mtu pia.
Nyakati nyingine sauti isiyofaa inaweza kusababishwa na kasoro fulani ambayo mtu amezaliwa nayo au ugonjwa uliodhuru zoloto. Huenda kasoro hizo zisiweze kurekebishwa katika mfumo huu wa mambo. Lakini, unaweza kuboresha sauti yako ukijifunza kutumia vizuri viungo vya usemi. Kwanza, tufahamu kwamba sauti za watu hutofautiana. Kwa hiyo, usijaribu kuiga sauti ya mtu mwingine. Badala yake, boresha sauti yako mwenyewe pamoja na hali zake. Unawezaje kufaulu? Kuna mambo mawili makuu. Pumua Vizuri. Ili sauti yako iwe nzuri, unahitaji hewa ya kutosha na unahitaji kupumua vizuri. Bila kufanya hivyo, sauti yako inaweza kuwa dhaifu mno na unaweza kukata-kata maneno katika hotuba yako.
Sehemu kubwa za mapafu haziko juu kifuani; sehemu hizo huonekana kubwa kwa sababu tu ya mifupa ya mabega. Lakini, sehemu za mapafu zilizo pana zaidi ziko chini, juu tu ya kiwambo. Kiwambo kinashikana na mbavu za chini na kinatenganisha kifua na tumbo.
Ukivuta pumzi na kujaza tu sehemu za juu za mapafu, utakosa pumzi haraka. Sauti yako itakosa nguvu na utachoka haraka. Ili uvute pumzi vizuri, unahitaji kuketi au kusimama vizuri na kurejesha mabega nyuma. Jaribu sana usipanue sehemu ya juu pekee ya kifua unapovuta pumzi. Kwanza vuta pumzi kabisa. Sehemu za chini za mapafu zikijaa hewa, mbavu zako za chini zitapanuka. Kwa wakati huohuo, kiwambo kitasonga chini, kikisukuma chini kwa utaratibu sehemu za tumbo hivi kwamba utasikia mkazo kwenye mshipi wako au kwenye vazi katika eneo la tumbo. Lakini mapafu hayako kwenye eneo la tumbo; yamefunikwa na mbavu. Unaweza kuthibitisha jambo hilo kwa kuweka mkono mmoja kila upande wa mbavu za chini. Kisha vuta pumzi kabisa. Kama unavuta pumzi vizuri, utaona kwamba huingizi hewa tumboni na kuinua mabega. La, badala yake, utasikia mbavu zikisonga juu kidogo na kupanuka.
Kisha, jaribu kushusha pumzi. Usishushe pumzi kwa ghafula. Ishushe polepole. Usijaribu kuzuia pumzi kwa kukaza koo kwa sababu sauti itajikaza au itakuwa nyembamba sana. Mkazo wa misuli ya tumbo na mkazo wa misuli iliyo kati ya mbavu huondosha pumzi, lakini kiwambo hudhibiti mwendo wa pumzi hiyo.
Msemaji anaweza kudhibiti jinsi anavyopumua kwa kujizoeza kama vile tu mwanariadha anavyofanya mazoezi ya mbio. Simama vizuri kama umerejesha nyuma mabega, vuta pumzi kabisa ili sehemu za chini za mapafu zijae hewa, kisha shusha pumzi polepole na kwa utaratibu ukihesabu kwa kadiri uwezavyo kabla ya kuvuta tena pumzi. Kisha jizoeze kusoma kwa sauti ukipumua kwa njia hiyo.
Tuliza Mkazo wa Misuli. Jambo jingine muhimu linalotokeza sauti nzuri ni utulivu! Unaweza kuboresha sana sauti yako ukijifunza kutulia unapozungumza. Ni lazima akili na mwili zitulie, kwa kuwa mkazo wa akili husababisha mkazo wa misuli.
Ifikirie misuli ya koo na kujaribu kuituliza. Kumbuka kwamba nyuzi zako za sauti hutikisika zinapopitisha hewa. Sauti hubadilika misuli hiyo ikikazika au ikitulia kama tu vile uzi wa gitaa hubadili sauti ukikazwa au ukilegezwa. Sauti hurudi chini nyuzi za sauti zinapotulia. Kutuliza misuli ya koo pia hufanya mianzi ya pua ibaki wazi, na hiyo huboresha sauti.
Tuliza mwili wako mzima—magoti, mikono, mabega, na shingo. Ukifanya hivyo, utaweza kuvumisha sauti vizuri ili isikike wazi. Sauti huvumishwa wakati mwili wote unapohusika kuitokeza, lakini mkazo huizuia. Sauti hutokezwa kwenye zoloto nayo huvumishwa katika mianzi ya pua, kwenye mifupa ya kifua, meno, na kaakaa ya mdomo na mianya iliyo katika mifupa ya pua. Sehemu hizo zote zinaweza kuchangia ubora wa sauti. Ukiweka kitu kwenye kibao cha gitaa cha kupaazia sauti, sauti itafifia; ni lazima kibao hicho kisiwe na kitu ili kitikisike na kutoa sauti vizuri. Ndivyo ilivyo pia na mifupa ya mwili wetu ambayo imeshikiliwa na misuli. Uvumishaji mzuri wa sauti unakuwezesha kuwa na ubadilifu wa sauti na kuweza kuonyesha hisia mbalimbali unapoimba au kuzungumza. Pia utaweza kuimbia au kuhutubia watu wengi zaidi bila kukaza sauti.
JINSI YA KUFAULU
Fanya mazoezi ya kuvuta pumzi, ukijaza sehemu za chini za mapafu kwa hewa.
Unapozungumza, tuliza misuli yako ya koo, shingo, mabega, na mwili wote mzima.
MAZOEZI: (1) Kwa dakika chache kila siku katika juma, fanya mazoezi ya kuvuta pumzi kabisa mpaka uzijaze sehemu za chini za mapafu yako. (2) Jaribu kutuliza misuli ya koo unapoongea, angalau mara moja kwa siku.
SAUTI HUTOKEZWAJE?
Sauti zote hutokezwa na hewa inayotoka mapafuni. Mapafu hupiga hewa kama pampu kupitia koo na kuingia ndani ya zoloto ambayo iko katikati ya koo. Ndani ya zoloto mna misuli miwili midogo inayoitwa nyuzi za sauti, msuli mmoja uko upande mmoja na msuli mwingine upande mwingine. Nyuzi hizo za sauti ndizo vitokezaji vikuu vya sauti. Misuli hiyo hufungua na kufunga njia ya hewa katika zoloto ili kuingiza hewa na kuitoa na vilevile kuzuia vitu visivyotakikana visiingie kwenye mapafu. Tunapopumua kwa njia ya kawaida nyuzi za sauti hazitokezi sauti wakati hewa inapopita. Lakini mtu akitaka kuimba au kuzungumza, misuli hufinya nyuzi za sauti, na nyuzi hizo hutikisika wakati hewa inayotoka mapafuni inaposukumwa kuzipitia. Utaratibu huo hutokeza sauti.
Kadiri nyuzi za sauti zinavyokazika, ndivyo zinavyotikisika kwa kasi zaidi na ndivyo sauti inavyoinuka. Na kadiri nyuzi hizo zinavyolegea, ndivyo sauti inavyopungua. Mawimbi ya sauti yanayotoka kwenye zoloto huingia sehemu ya juu ya koo inayoitwa koromeo. Kisha mawimbi hayo hupitia mdomo na pua. Hapo sauti nyinginezo huongezwa ili kurekebisha, kukuza, na kuimarisha sauti ya awali. Kaakaa la mdomo, ulimi, meno, utaya, na midomo huungana pamoja ili kutawanya mawimbi ya sauti, na kutokeza usemi unaoeleweka.
Sauti ya mwanadamu ni ajabu sana, na haina kifani ikilinganishwa na chombo chochote kile ambacho binadamu ametengeneza. Ina uwezo wa kuonyesha hisia mbalimbali kama vile upendo na chuki kali. Sauti ikikuzwa na kuzoezwa vizuri, inaweza kubadilikana sana na kutokeza nyimbo tamutamu na semi zinazogusa mioyo.
KUSHINDA MATATIZO FULANI HUSUSA
Sauti dhaifu. Sauti ndogo huenda isiwe dhaifu. Ikiwa nzuri na yenye kuvutia, wengine wanaweza kufurahi kuisikiliza. Lakini ni lazima sauti iwe yenye kiasi kinachofaa ili iweze kufaidi wengine.
Ili uboreshe ukubwa wa sauti yako, unahitaji kuivumisha zaidi. Unahitaji kutuliza mwili wote mzima, kama ilivyoonyeshwa katika somo hili. Pamoja na kutuliza mwili, fanya mazoezi ya kuimba hali umefunga midomo. Midomo inapaswa kugusana kidogo, isishikane sana. Unapoimba kwa njia hiyo, sikia mitikisiko ya wimbo huo akilini na kifuani. Nyakati nyingine sauti husikika kuwa dhaifu au kukazika kwa sababu ya ugonjwa au kukosa usingizi. Bila shaka, hali hiyo ikiboreka, sauti itaboreka.
Sauti inayoinuka juu sana. Mkazo kwenye nyuzi za sauti hufanya sauti iinuke. Sauti yenye mkazo hufanya wasikilizaji wawe na mkazo. Unaweza kupunguza sauti nyembamba kwa kutuliza misuli ya koo ili kupunguza mkazo kwenye nyuzi za sauti. Jaribu kufanya hivyo, ukifanya mazoezi kila siku unapozungumza. Pia ni vizuri kuvuta pumzi kabisa.
Sauti ya kubana pua. Nyakati nyingine pua iliyofungika hutokeza tatizo hilo, lakini mara nyingi hali hiyo husababishwa na jambo jingine. Nyakati nyingine kwa kukaza misuli ya koo na mdomo, mtu hufunga mianya ya pua na kuzuia hewa isipite vizuri. Jambo hilo hutokeza sauti inayobana pua. Unahitaji kutulia ili kuepuka jambo hilo.
Sauti nzito na kali. Sauti kama hiyo haitokezi mazungumzo ya kirafiki. Inaweza kutisha wengine. Katika hali fulani, jambo muhimu ni kuendelea kujitahidi kubadili utu wako. Ikiwa tayari umefanya hivyo, kujaribu kutumia kanuni za kurekebisha sauti kunaweza kusaidia. Tuliza koo na taya. Kufanya hivyo kutafanya sauti yako ipendeze zaidi na kufanya maneno mengine yasitokee vibaya kwa kuyalazimisha kupitia meno.
Karibu katika darasa la sauti, ili ufanyike kuwa mwimbaji, muhubiri, msemaji bora. Kumbuka, sauti yako ndio wewe!
John Shabani

24 October 2016

TANZANIA’S JOHN MAGUFULI ANNOUNCED AS WORLD’S BEST PRESIDENTPresident of Tanzania John Pombe Joseph Magufuli has been announcd the best President in the World by the United Nations Economic & Social Council during their annual review which was published on August 12, 2016
www.theguard1an.com

A Technical Committee made up of experts from reputable International Civil Service Organisations and Think Tanks adjudged Mr. Magufuli as the best President during the period under review. He has been in office since November 05, 2015 and is tipped to rule the country for another term of office.
Many have welcomed the recognition as Tanzania has seen rapid development since he assumed office.
The outcome of the report which was based on the Political, Economic and Social indexes of the country and the President tops the list. World leaders acknowledge the reports, opposition parties still object to it as they criticize every move by the government.
“I am very honored with such a prestigious recognition. I believe this feat has been achieved through hard work and transparency of my government. I thank the good people of Tanzania for creating the enabling environment for me to perform my duties creditably as their President”. – Mr. Magufuli said.

23 October 2016

JOHN SHABANI NDANI YA TABIBU TV.

KIPINDI: MAPITO YANGU
Tabibu Television

Usikose kuangalia kipindi cha mapito yangu kitakachoanza kurushwa hewani hivi karibuni na Aneth Nyoni @annienyoni kupitia Tabibu Television. Kutana na mwana saikolojia Dr. Nkwabi Sabasaba akiwa na Rachel Mwegisa. #tabibu tv #startimes #channel 116

 John Shabani akiwa na bi Aneth Nyoni, akieleza yale aliyopitia ikiwa ni pamoja na maisha ya ufukara, kuwekwa maabusu kwa kosa la kusingiziwa, kufiwa na mke, malezi ya watoto bila mama n.k.

Mwana saikolojia, DK. Nkwabi Sabasaba akikipitia kitabu kilichoandikwa na John Shabani, chenye jina la "MARUFUKU KUKATA TAMAA"
HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP