VOCAL TRAINING - DARASA LA UIMBAJI BY JOHN SHABANI

John Shabani akiwa na baadhi ya wanafunzi wenzake wa sauti

John Shabani akisimamia waimbaji katika kuandaa wimbo wa miaka 50 ya uhuru wa Tanzania


                                                                                                                          



0716 560094



Haya ni masomo machache sana niliyoyachagua kati ya mengi ili kukupa hamasa kujiunga na darasa la uimbaji linaloendelea katika kituo chetu cha mafunzo, Kamara Dar es salaam chini ya mwalimu John Shabani na timu yake

 Karibu ujifunze.

Lakini pia kwa wale wanaotaka kurekodi nyimbo zenye ubora na kufanya video zenye ubora, nimefungua studio yenye vifaa vya kisasa, unaweza ukatazama baadhi ya video zangu kama; 
- Mtoto wa mfalme by John shabani
- Futa machozi by John Shabani
- Nakupenda by John Shabani
Karibu sana. 





Utangulizi:
Nianze kwa kusema kwamba , kwa wale wanaofahamu maana ya bora ktika muziki, ni kwamba ni kosa kubwa sana na hairuhusiwa kuingia kwenye music recording studio bila kupitia vocal studio. Kwa wenzetu unapotaka kuingia studio lazima uwe na voice coacher, vikundi mbalimbali vya uimbaji lazima view na voice coache.

Kazi kuu ya voice coacher ni;
-      Kufundisha ( training)
-      Kukushauri (councel)
-      Na kulea kipaji hadi mtu atoke (mental)
MALENGO/MAONO
1.                 Kuvipata/kuviendeleza na kuviwezesha vipaji vya uimba
2.                 Kuwa ni program ya uimbaji itakayoongoza kimafanikio Tanzania

MAWASILIANO
Mob: 0716560094, 0754818767


Mambo ya msingi yanayofunzishwa katika program hii:
Ø  Historia ya uimbaji
Ø  Tofauti ya mwimbaji na mwanamuziki
Ø  Kuwa na sauti bora au afya ya sauti (vocal health)
Ø  Vyakula na vinywaji vinavyofaa na visivyofaa
Ø  Sifa na mbinu za kuwa mwimbaji bora au uimbaji kitaalam
Ø  Jinsi ya kuitunza na kuiponya sauti yako
Ø  Amri 10 za mwimbaji (za sauti)
Ø  Matumizi ya kipaza sauti (Microphone technique)
Ø  Utunzi au uandishi wa nyimbo
Ø  Mazoezi ya viungo yanayofaa kwa mwimbaji na faida zake
Ø  Ushauri kwa wanaotaka kurekodi nyimbo

Kumbuka moja ya vitu vya msingi katika uimbaji ni nguvu (energy) “As you sing higher, you must need more energy, as you sing lower, you must useless”. Zipo nguvu za kiroho na za kimwili. Ili kuwa na nguvu za kimwili unahitaji maji ya kutosha, chakula kizuri pamoja na  mazoezi ya viungo. 


KUIMBA

Kuimba ni mpangilio wa maneno na sauti unaoleta ladha fulani inayopendeza kwenye sikio la mwanadamu, ni kutamka maneno katika hali ya ki-muziki au pia twaweza kusema ni kutamka maneno moja baada ya jingine kwa sauti yenye lahani (sauti ya ala ya muziki, tuni) au ghani (Singing is the act of producing musical sounds with the voice)

Mwimbaji ni mtu yeyote mwenye uwezo wa kuimba au bila vyombo vya muziki (be sung a cappella) au kwa kutumia vyombo. Mwimbaji huyo kwa lugha ya ki-muziki anaitwa vocalist. Ikumbukwe kuwa pia katika vikundi vya uimbaji wapo wale wanaoongoza wengine katika uimbaji (A lead singer) na wengine kazi yao ni kuitikia (backing singers)


N.B Mwanadamu yeyote mwenye uwezo wa kuongea, anao uwezo wa kuimba pia.

Kama vile tulivyo na ala za aina mbalimbali, mwimbaji naye pia anazo ala mbili muhimu:
         Mdomo wenye uwezo wa kutoa sauti ya uimbaji
         Mwili
Kumbuka moja ya vitu vya msingi katika uimbaji ni nguvu (energy)
Mckinney alisema: “As you sing higher, you must need more energy, as you sing lower, you must useless; as  you sing higher, you must use more space; asa you sing lower, youmust need use less””. Inamaanisha kadri unavyotumia sana sauti hasa kwa sauti ya juu sana, ndipo unapohitaji pia nguvu kubwa, japo wapo watu kwasababu ya uzoefu wa kuimba kwa muda mrefu au kupitia madarasa kama yale yanayofundishwa na mwalimu John Shabani, kwao kuimba sauti ya juu au ya chini ni jambo la kawaida.

 Zipo nguvu za kiroho na za kimwili. Ili kuwa na nguvu za kimwili unahitaji maji ya kutosha, chakula kizuri, hewa pamoja na  mazoezi ya viungo  maalum kwaajili ya uimbaji au ya pumzi.
Mwimbaji pia anahitaji Pumzi ya kutosha (Breathing support), chakula kizuri na maji ya kutosha.

UIMBAJI KITAALUMA
Mwimbaji asiyejua kuimba hawezi kuwa huru kuhudumu ni muhimu afahamu uimbaji ili aimbe kwa uhuru na kwa ufanisi. Ufanisi unahitaji muda wa mazoezi yakutosha pamoja na mwalimu mwenye uwezo wakukuelekeza jinsi ya kuimba Muziki (uimbaji), mambo hayo upo katika mafungu makuu mawili :
I. Vocal
II. Instrumentals

VOCAL: Ni sauti ya wanadamu. Sauti isiyochanganywa kitu chochote. Sauti asilia ya mtu (Natural voice)
INSTRUMENTALS:
Ni sauti zitokanazo na vyombo. Sauti pasipokuchanganywa na kitu chochote yaani ala za muziki. Sehemu hizi mbili zikichanganywa pamoja hufanya kitu kinachoitwa muziki (uimbaji) na kukamilisha maana ya NENO MUZIKI.

SAUTI. Ni hisia inayonaswa na masikio na hutokana (hutengenezwa) na msuguano wa hewa katika mzunguko, mgongano wa vitu au mkwaruzo kiasi cha kutoa mlio (sauti).
SAUTI –MLIO (AUDIBLE, SOUND)

1. Kitaalamu Sauti ina misingi au kanuni .
Misingi hiyo ni Miwili. Ni kwa misingi ya sehemu hizo mbili kuu- Sauti hujengwa/huumbika, tutaelewa misingi hiyo vizuri kwa kuziangalia tabia za sauti (Characteristics of Musical Sound) Au tabia za milio.

Msingi wa kwanza:
Sehemu hii ya kwanza nazungumzia nadharia ya tabia za sauti, tabia hizi huwezi kuziona wala kuzihisi, ila unaweza kuzifikiria katika mawazo.
a) Sauti ina tabia ya – Melody – Yaani kwa Kiswahili – Ghani
Melody – Ghani – (Mpangilio wa nota na maneno kimuziki). Ni mistari ya sauti ya muziki inayotambulisha chanzo (tone) cha wimbo ni sauti yenye kuelekeza ubora wa mtiririko wa ghani (melody) unaokupa hisia ya mlio unaohusika au unaousikia.
b) Rhythm – Ni utaratibu au mfumo wa aina ya mwendo wa sauti katika wakati au mfululizo wa sauti katika muda, mwendo, pigo, mdundo au msisimko. Uwezo wa sauti wa kutembea katika wakati usiobadilika.
c) Harmony – Mkusanyiko wa sauti unaopendeza, utaratibu au mfumo wa ulinganifu wa sauti, usawa, muafaka, kusikilizana pasipokuachana kwa sauti au kuwa nje ya tune hasa wakati kuna watu wengi wanaimba, katika ngazi tofauti yaani sauti ya msitari wa 1, 2, 3 na 4 pamoja.
d) Unison—Ni sauti ya aina moja inayoimbwa na watu wengi bila ya kutofautisha ngazi za sauti ya kwanza, pili,tatu na nne. Na kwa kawaida sauti ya unison hutumia sauti ya kwanza.
e) Form – Ni mwonekano wa kipekee, utaratibu au mfumo wa kuweka uimbaji katika aina ya mfumo unaojitambulisha katika mtindo wake wenyewe kama vile mtindo wa kizungu, wa kiafrika, kigogo, kihaya nakadhalika.
f) Tone Color – Aina mbalimbali za sauti kufuatana na chombo au mtu anayeimba – kwa mwanadamu sauti hutegemea mapafu yake na mishipa ya fahamu ya kichwani. Yaani sauti kavu, sauti laini, yenye mikwaruzo, yenye mawimbi nakadhalika, kusikika kwa sauti kipekee, kivyake kwa kadri ya mtu anavyotoa sauti au chombo kinavyo toa sauti kwa namna ya mlio wake.
3. Msingi wa Pili:
Sehemu ya kwanza Nimetaja nadharia ya tabia za sauti, tabia hizi huwezi kuziona wala kuzihisi, ama kuzisikia, ila unaweza kuzifikiria katika mawazo. Kuimba sio nadharia wala mawazo ni matendo halisi. Nadharia hiyo lazima itafsiriwa katika vitendo tunavyoweza kuviona, kuhisi, kusikia tabia za sauti au milio hiyo. Haya yanawezekana kwa kutumia nyenzo , njia za muziki za kiufundi zinazotuwesha kutenda. (Musical Skills Performance Methods)
Katika msingi huu wa pili tunafika katika kukamilisha muziki na ndiyo uimbaji. Muziki ni sayansi lakini kila mmoja wetu anayo na anaweza kuitendea kazi kwa kujifunza na kujizoeza.
Nyenzo au njia hizo ni:
a) Kuimba – (Singing – Melody) Unapoimba ndipo Ghani itajitokeza katika mpangilio wa sauti kwa njia inayopendeza na kwa utaratibu, hapo Tone Color itasikika yaani kwa kuimba wimbo, ghani na aina za sauti katika ubora wake utasikika.
b) Kupiga vyombo vya muziki – Accompanyments – vikolezo. Melody ambayo ni Ghani itasikika – Tone color pia itasikika.
c) Form, Kutenda vitendo – (Moving – Movement –Steps) Rhythm na Form itaonekana yaani kucheza kwa mwendo wa mapigo. Yaani sauti na maneno unayoimba yataenda kwa kufuata mapigo na midundo ya wimbo na kuwa na muonekano wa kipekee.
d) Harmony. Kusikiliza ndiko kutakuwezesha kuleta ulinganifu katika mkusanyiko wa sauti za kupendeza na kukuwezesha uimbe sawasawa na sauti nyingine bila kuhitilafiana wala kuachana au kuwa nje ya ghani.
e) Kuunda au Ubunifu (Creation – Form, Rhythm na melody) Wimbo utakamilishwa kwa kuunganisha nyenzo hizo nakuwa halisi yaani wimbo halisi wenye kusikika vizuri.






SIFA ZAKUWA MWIMBAJI BORA

Mambo  muhimu yatakayokufanya uwe muimbaji bora; Haya ni mafunzo ya msingi na ya kwanza kwa mtu anayetaka kujifunza kuimba au kuwa mwimbaji bora. Sisi tunaita mafunzo ya chekechea kwa mwimbaji.



1.                  Breath au breathing (pumzi au kupumua). Jambo la kuzingatia na la kuelewa ni kwamba; msingi wa uimbaji (the foundation of singing) ni pumzi. pumzi huhitajika sana  wakati wa uimbaji  muimbaji mzuri ni yule anaye jua kutumia pumzi yake vizuri, muimbaji asipokuwa na uwezo wa kutumia vizuri pumzi  katika maeneo yasio takiwa itasababisha sentensi ya wimbo kukatika katika .vile vile muimbaji  usipokuwa na pumzi utashindwa kuimba noti za juu na katika noti ambazo unatakiwa uimbe na uzivute kwa muda hautaweza na itakusababishia uimbe na kutoifikia pitch kama hauna pumza anza sasa kufanya mazoezi  ya pumzi. Hivyo katika eneo hili tunajifunza mazoezi ya kujenga uwezo wako wa kupumua. Zipo mbinu nyingi (teknics), moja wapo ni;
-          Hissing sound (z, s, v)
-          Ballon teknics (mbinu ya pulizo)
-          Book method
-          Birthday cake
-          Three methode (mbinu ya mti). Hii tunaita ni aina ya juu sana ya mafunzo ya sauti (a deep breathing method) n.k.
2.                  Pitch –pitch (Ear training) – yaani kufundisha sikio lako kujisikia mwenyewe kama uko sahihi au la au kuwasikia watu wengine.  Pitch ni uwiano wa sauti yako mwimbaji pamoja na vyombo au waimbaji wenzio kutegemea na (key) ufunguo unaoimbia au mnaoimba. mwimbaji asipoimba katika pitch humpelekea muimbaji huyo kuimba nje ya ufunguo (out  of key) kwa sababu  ule uwiano wa sauti yake na ya vyombo katika (key) ufunguo unaoimba unakuwa haupo kama unatatizo katika eneo hili  unahitajika sana kufanya mazoezi ya pitch
3.                  Rhythm-ni mapigo ya mziki kwenda  katika mwendo usio badilika na kuwa  na idadi sawa ya mapigo katika kipimo(measure), mwimbaji lazima awe na uwezo wa kuimba na kufuata  beat (mdundo),vile vile na uwezo wa kuimba akifuata  ridhimu  ya wimbo.
4.                  Voice (sauti) – Tone -  Range (ukomo wa sauti kwenda juu na chini) mwimbaji ni vizuri uimbe katika sauti yako ya asili lakini sauti yako inabidi iwe inatoka au kuimbwa kwa kufuata misingi ya kimuziki unatakiwa kufanya mazoezi ya sauti(voice training) ili kuiboresha sauti yako pia fanya mazoezi ya kuimba scale mbali mbali za muziki kama moja scale  chromatic scale arpeggios…
5.                  Diction (lafudhi au matamshi) kujifunza sauti  peke yake haitoshi bado unatakiwa kujifunza kuimba na kutamka maneno vizuri ili wasikilizaji waweze  kukuelewa  unachokiimba hivyo kuumba matamshi ni kitu muhimu sana katika uimbaji. Baadhi ya mafunzo ya matamshi ni kama;
-          Zima switch, washa switch
-          Masachusets
-          Entusiasm

Zingatia pia:  Kusimama kwenye ufunguo (Key), mwonekano, (appearance), Uwezo wa kuitumia sauti na kuitawala (Manage your vocal), kuua lafunzi ya asili kulingana na aina ya uimbaji, mwanekano jukwaani(Stage presence), kuwa na sikio la muziki eitha ukiwa peke yako au katikati ya wengine, kujiamini, kujitambua, lugha ya mwili (body language) kujithamini (Self Cofidance), kuwa mbunifu na kujitengenezea swaga zako binafsi huku zinazoendana na muonekano wako usoni na mwili mzima (facial expression). Kujituma, kujiachia lakini usipitilize, mawasiliano na watu wengine ikiwa ni pamoja na wapigaji na madhabau n.k.

HATUA 4 ZA KUREKODI AU KUWA NA ALBAM BORA
(Mwimbaji kuwa bora, tungo au ujumbe bora, muziki bora, Studio bora)

NGUZO 4 ZA MUZIKI  
Kusikiliza muziki/uimbaji (Listening), Kuhifadhi muziki/uimbaji (Copying), Kuiga au kukariri (imitate), Kuzalisha muziki (producing)


Mazoezi kwa mwimbaji
Yapo mazoezi maalum kwaajili ya kuboresha uimbaji na pia kumfanya mwimbaji awe na nguvu ya kutosha na kuepukana na baadhi ya magonjwa. Kwa ushauri zaidi wasiliana na mwalimu John Shabani.

Pamoja na faida nyingi za mazoezi lakini pia mazoezi huchangamsha mwili, hulainisha koo, husaidia kuwa na pumzi ya kutosha, hukuhepusha au kupunguza baadhi ya magonjwa kama kisukari, presha n.k, hung’arisha ngozi, na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu, mazoezi husaidia katika mfumo wa usagaji chakula kuwa mzuri , kukupa nguvu na kuweza kufanya kazi kwa nguvu zako bila kujiskia umechoka na mwisho wa siku hupunguza mafuta mwilini,  hupunguza uzito, kunyoosha na kuimarisha misuli ya mwili, husaidia mapigo mazuri ya moyo kwa kuongeza kasi ya mapigo yake wakati wa mazoezi, hupunguza mrundiko wa damu kwenye mishipa, hii ni muhimu kwa sababu mgando wa damu husababisha magonjwa ya moyo pamoja na kupoteza fahamu, mazoezi huimarisha mifupa ya mwili, huboresha usingizi ambao unafaida sana kwa mwimbaji.

Fikiria mwenyewe kama mwanamichezo au mtu wa fani fulani na jifunze kuwa mtu wa kula na kunywa kulingana na fani yako: Aina ya chakula na kinywaji na muda  wa kutumia ni jambo la kuzingatia sana. Kula na kunywa ni muhimu lakini Jiepushe na ulafi kwani huleta uchovu, mfumo wa kupumua kuathirika na wakati mwingine kusababisha magonjwa.
Kuna misimu fulani kama msimu wa vumbi au baridi kali au alegi au matatizo mengine kibao, wakati mwingine aina fulani ya dawa kwa ajili ya ugonjwa fulani, Wakati mwingine husababisha mafua au kutokwa na kamasi mara kwa mara au kukausha koo kabisa, hivyo husumbua sana na kuathiri mfumo wako wa kuimba. Wakati mwingine mazingira ya shughuli au kazi tuzifanyazo au pia mazingira ya makazi huweza kuathiri sauti zetu. Hivyo masomo ya utunzaji wa sauti ni ya muhimu sana.

VYAKULA NA VINYWAJI KATIKA UIMBAJI

1.0 Utangulizi
Uimbaji ni taaluma kama zilivyo taaaluma zingine za sheria, elimu, uhandisi, usimamizi wa fedha, biashara na kadhalika. Taaluma hizo na zingine zinautaratibu uliowekwa ili kumfanya mtu asiyejua kujua na hatimaye kuitwa mwanasheria, mwalimu/mwezeshaji, muhandisi au msimamizi wa fedha. Hivyo basi, uimbaji nao una taratibu zake hata mtu akafikia kiwango cha kuthibitika kuwa ni muimbaji ama kwa kupewa cheti au kuonesha uwezo wake mbele ya wengine; kanisani, kwenye majukwaa ya matamasha ya uimbaji na kadhalika.
Kwahiyo, makala hii imelenga kumsaidia muimbaji kumpa sheria na taratibu za uimbaji hususani katika suala zima la chakula gani muimbaji ale au asile na vinywaji gani muimbaji anywe au asinywe ili awe na uwezo wa kuimba vizuri mahali popote.

2.0 Nafasi ya Vyakula na Vinywaji katika uimbaji.
Katika suala la kula na kunywa muimbaji yeyote anaweza kufananishwa na mkimbiaji. Mkimbiaji hawezi kujishindilia chakula kingi au kunywa maji mengi wakati akijua anakwenda kwenye mazoezi au mashindano ya kukimbia umbali wa maili fulani. Hii ni kwa sababu, atashindwa kukimbia vizuri. Hata muimbaji; hawezi kula au kunywa kwa kupitiliza halafu asipate shida wakati wa zoezi la kuimba. Hii ni kwa sababu, kushiba sana kunazuia zoezi la upumuaji wakati wa uimbaji na kusababisha muimbaji kushindwa kutengeneza sauti nzuri za uimbaji.
Pia, mkimbiaji hatokuwa na nguvu za kukimbia kama hatokula chakula cha kutosha au kunywa maji ya kutosha. Muimbaji halikadhalika, anahitaji kula chakula na kunywa maji kwa kuwa uimbaji ni kazi ngumu ambayo inahitaji virutubisho vya kutia nguvu mwili ambavyo vinapatikana katika vyakula na vinywaji tunavyotumia katika maisha yetu ya kila siku. Hivyo, kula na kunywa ni jambo la muhimu sana kwa muimbaji katika zoezi la uimbaji lakini kwa tahadhali. Kama nilivyotangulia kusema, kuimba ni kama riadha, inahitajika nguvu kwa ajili ya utendaji wako. Hata hivyo, ni muhimu pia kuepuka kuimba tumbo likiwa limeshiba sana. Yapo madhara mengi yanayotokana na shibe. Unaweza ukawasiliana na mwalimu wa sauti ili kujua madhara hayo

2.1 Tahadhari ya vyakula na vinywaji katika uimbaji (nini muimbaji hapaswi kula au kunywa katika siku ya uimbaji na wakati wa uimbaji)
Muimbaji asishinde na njaa au kutokunywa maji kabisa siku ya uimbaji. Hii ni kwa sababu, kutokula kutanyong’onyesha mwili wake hivyo atashindwa kuimba kwa ufanisi. Zingatia: kama muimbaji amefunga; atumie maji (anywe kidogokidogo) ili kulainisha na kulifanya koo lake lisiwe kavu. Pia, maji yatampa muimbaji nguvu ya kusimama na kuwahudumia watu kwa muda uliopangwa.

Muimbaji asinywe kinywaji chochote chenye kafeni. Hii hujumuisha vinywaji kama vile; kahawa, cola (soda), chai ya rangi nyeusi (black tea) na vinywaji vyote ambavyo vina cafeni ndani yake. Vinywaji hivi ni kichochezi cha mkojo na hufanya mwili wa muimbaji kushindwa kufyonza maji kunakosababisha mwili kukauka au kuishiwa maji ambayo ni muhimu sana katika kumpa muimbaji nguvu ya kuimba. Pia, vinywaji hivi husababisha; kuzalishwa kwa kitu kama uteute (kamasi) kwenye kinywa na koo, ukavu na maumivu kwenye koo, huleta kiungulia na kusababisha kucheua mara kwa mara wakati wa uimbaji.
Zingatia: Kama muimbaji anashindwa kuacha vinywaji hivyo, inashauriwa kusukutua koo kwa maji mara baada ya kunywa kinywaji cha namna hiyo kwa siku nzima ili kusafisha koo na kuepuka athali zisababishwazo na vinywaji hivyo katika uimbaji. Pamoja na hilo, muimbaji anywe maji mengi; zaidi ya glasi nane kwa siku. Au, Muimbaji atumie chai nyeusi (black tea) ambayo inaelezwa kuwa na kiwango kidogo sana cha kafeni. Ila matumizi ya chai ya kienyeji ni bora zaidi (mchaichai).

Muimbaji asile vyakula au kunywa vinywaji vinavyoongeza au kuacha uteute kwenye kinywa na katika koromeo kabla na wakati wa uimbaji. Mfano wa vyakula hivyo ni mayai, maziwa, ‘ice cream’ na bidhaa zingine za maziwa kama pipi, ‘chocolate’, biskuti, keki, siagi, samri, koni na kadhalika. Uteute unaosababishwa na vyakula na vinywaji hivyo huzuia utokaji mzuri wa sauti ya uimbaji wakati wa kuimba. Ndio maana utakuta waimbaji wengine wanahama funguo za muziki au kushindwa kuimba sauti za funguo za juu au kupata tatizo la kushindwa kupanda na kushuka vema kwa sauti wakati wa uimbaji.

Muimbaji asitumie vyakula au vinywaji vinavyokausha koo. Mfano wa vinywaji hivyo ni kama vile; pombe, matunda jamii ya ndimu kama chungwa, limao, chenza, daransi, embe bichi, na kadhalika. Kukauka kwa koo kutasababisha sauti ya muimbaji kutotoka vema kwasababu koo lake ni kavu.

Muimbaji asitumie soda na vinywaji vyovyote vinavyotoa povu wakati vinapofunguliwa. Vinywaji hivi huweka gesi/hewa tumboni na kumfanya muimbaji kubeu na/au kucheua hovyo na kusababisha muimbaji kupata shida wakati wa kuimba na kutoa sauti mbaya.

Muimbaji asile vyakula ambavyo vitaacha vitu kama makapi kwenye koo lake. Vyakula hivyo ni kama vile; bisi, mahindi, karanga, tambi kavu, chama, na kadhalika. Ulaji wa vyakula hivi kabla na wakati wa kuimba husababisha ugumu wa utoaji wa sauti za kuimbwa. Pia, makapi hayo wakati mwingine hurukia katika koo la chakula na kusababisha muimbaji kupaliwa na hatimae muimbaji kushindwa kupumua vema, kukohoa na kuimba vibaya.

Muimbaji asile vyakula vya mafuta sana;
kama vile nyama zilizonona na kadhalika. Pia, sukari nyingi haifai kwa muimbaji.
Muimbaji asile vyakula au vinywaji vinavyoleta mwasho au kukera koo (throat irritants), vinavyochangamsha, kusisimua au kulewesha (Overly spicy foods) kama vile; kahawa na pilipili, vinywaji baridi sana, sukari iliyosafishwa, chocolate na kadhalika.

Muimbaji asitumie Jamii ya vitu vyenye alkoholi, Sigara, tumbako, bangi, ugoro na aina yoyote ya madawa ya kulevya kwakuwa vinaathali kubwa kwenye koo na mapafu ambavyo ni viungo muhimu sana katika utengenezaji wa sauti bora za uimbaji.

Muimbaji asitumie vyakula vyenye madhara kwa mwili wake (mzio; allege). Kwa mfano, baadhi ya waimbaji hupata shida baada ya kula matunda jamii ya machungwa, ngano, karanga, samakigamba, soya na kadhalika.

Muimbaji asitumie vyakula vyenye mafuta mengi, na nyama nyekundu kama ya ng’ombe, mbuzi na kadhalika.

2.2 Vyakula na vinywaji vitakavyofanya muimbaji aimbe vizuri (vyakula na vinywaji ambavyo muimbaji anashauriwa kuvitumia kabla na /au wakati wa uimbaji)
Muimbaji ale chakula cha wastani (kiwango cha kutosheka) masaa mawili kabla ya uimbaji. Hii itasaidia chakula kumengenywa vema na kumpatia muimbaji nguvu wakati wa kuimba. Kushiba sana (kuvimbiwa) husababisha tumbo kushindwa kumeng’enya chakula kwa haraka na hivyo kutamfanya muimbaji ashindwe kutoa sauti vema. Hii ni kwa sababu, tumbo litashindwa kusukuma hewa kutoka nje ili kutengeneza sauti nzuri za uimbaji. Pia, muimbaji atakuwa anabeua na kucheua hovyo wakati wa kuimba hali ambayo humfanya kutoa sauti mbaya au kushindwa kuimba kabisa.
Muimbaji anywe maji ya kawaida (room temperature water) yaani yasiwe ya moto wala ya baridi au barafu. Maji hayo yanywewe masaa mawili kabla ya uimbaji. Maji haya yatampa nguvu muimbaji, yatafanya koo la muimbaji kuwa bichi (sio kavu) na mwili kutokuwa mkavu. Muimbaji hanabudi kutambua kuwa matumizi ya maji ya moto hutanua na maji ya baridi (au barafu) husinyaza/hubana koromeo hivyo kusababisha kiboksi cha sauti kushindwa kutengeneza sauti za kuimba vizuri na muimbaji ataimba vibaya. Zingatia: Unaweza kunywa maji ya moto au ya baridi baada ya uimbaji na sio kabla au wakati wa uimbaji.
Muimbaji ale matunda yenye maji mengi kwa ajiri ya kuufanya mwili wake kufyonza maji na kupata nguvu. Mfano wa matunda hayo ni pamoja na tikiti maji, tango na kadhalika.
Muimbaji ale mboga za majani zenye maji mengi kwa ajiri ya kuufanya mwili kupata maji, chumvichumvi na madini ambavyo vyote ni virutubisho vitakavyompa muimbaji nguvu ya kuimba na kutoa sauti yake vizuri wakati wa kuimba. Mfano wa mboga hizo ni pamoja na mchicha, tembele, ‘spinach’, ‘chinise’, na kadhalika.
Muimbaji anaweza kutumia asali, na chumvi kidogo ni nzuri kwa koo la lake katika siku ya uimbaji.

NB. Matumizi ya chai ya mitishamba (mchaichai) ni bora zaidi kwa afya ya koo na tumbo lako ili kusaidia utengenezaji wa sauti nzuri za uimbaji.

3.0 Hitimisho na mapendekezo.
Koo hupendezwa, hutulizwa, huburudishwa, hutengenezwa na aina fulani ya pipi, asali, mvuke, chai ya mitishamba (mchaichai), kusafisha koo kwa maji chumvi, baadhi ya dawa kwa ushauri wa daktari, unywaji wa maji, na kadhalika. Pia, kinyume chake koo laweza kuharibiwa na matumizi ya vyakula au vinywaji kama vile; pombe, kahawa, soda, maziwa, chokoleti, pipi, ubuyu, matunda jamii ya ndimu, mayai, karanga, mahindi, bisi na kadhalika. Hivyo, muimbaji awe na taadhali katika matumizi ya vyakula na vinywaji ili kufanya sauti yake kuwa bora na kupendeza mbele za watu na Mungu tunayemtukuza kupitia sauti zetu.

Mathalani, mwanafunzi mzuri ni yule anayetafuta zaidi maarifa mara baada ya kujifunza jambo fulani. Hivyo, ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatakuwa msingi bora kwa muimbaji kutafuta zaidi kwa habari ya vyakula na vinywaji katika uimbaji. Haya yalioelezwa hapa ni machache sana. Pamoja na hayo, mabadiliko chanya ya uimbaji yatategemea uzingativu na utekelezaji kwa vitendo wa mambo hayo na sio kusikiliza tu. Pia, mabadiliko hasi yatatokea kwa wasiozingatia na kutekeleza kwa vitendo mambo hayo. Yuko mshairi anasema,
“Mshumaa tuliwasha, ili nuru kumulika, Giza kulitokomesha, na nuru kuenezeka,
Mshumaa unawaka, giza mbona linazidi?” Pia, mshairi mwingine anasema,
“Mnazi walioukwea, Shinani wameanzia, Si kama mejirukia, Kileleni taka tua, Jikazie yako kwego, mnazi upate kwea.” Hivyo, huu ni mwanzo wa kujifunza uimbaji; huna budi kuifuata nuru (mafunzo) unayoangaziwa (kupewa) ili ufanikiwe katika uimbaji. Hii ni kwa sababu, wote waliofanikiwa katika aina yoyote ile ya huduma, walianzia chini na kwa kuwa walisikiliza na kutekeleza waliyoelekezwa na viongozi wao wakaweza kupanda na leo hii ni watu wakuu katia huduma.

Ili kuwa na afya nzuri katika mwili na katika uimbaji wako zingatia :
1.                  Punguza  matumizi mengi ya sukari, ongeza matumizi ya matunda
2.                  Punguza kula nyama nyekundu, ongeza matumizi ya mbogamboga
3.                  Punguza matumizi ya soda, ongeza matumizi ya maji
4.                  Punguza kuendesha, ongeza kutembea kwa miguu
5.                  Punguza kupoteza muda wa kulala, Zingatia kulala kwa wakati
6.                  Punguza msongo wa mawazo, ongeza kupumzika


UMUHIMU WA MAJI NA ASALI MWILINI
Maji
Tunaambiwa kuwa maji ni muhimu sana ndani ya miili yetu. Maji yana faida nyingi sana na wengi tunazijua, lakini tutajikumbusha baadhi.
1.                 Moja maji husaidia kupunguza calories mwilini, yaani badala ya kunywa vimiminika vingine kama soda, bia na juisi ambavyo vina calories, maji hayana calories. hivyo utakua umekunywa maji ambayo ni salama mbadala na vinywaji vingine ambavyo vina calories.Kumbuka pia maji hayana sukari, mafuta na viungo vingine vinavyotengeneza vimiminika vingine
2.                   Unywaji wa maji mengi hutupunguzia uwezekano wa kupata magonjwa kama ya moyo, hivyo inashauriwa kwa siku tunywe zaidi ya bilauri mbili za maji na kuendelea.
3.                   Maji huongeza nguvu mwilini kwani unapokua na upungufu wa maji, unaanza na kusikia kiu ambayo huenda kupelekea kujisikia uchovu, misuli kuchoka, kizunguzungu na ishara nyingine za kunyongonyeza mwili.
4.                   Maji ni dawa ya maumivu ya kichwa. Mara kwa mara tuumwapo kichwa pengine ni upungufu wa maji ndio uliopelekea maumivu haya, lakini tunywapo maji basi maumivu huoondoka. Kuna sababu nyingine zinazopelekea vichwa vyetu kuuma lakini, ukosefu wa maji mwilini ni sababu inayojulikana zaidi.

5.                   unywaji maji hupelekea kusafisha ngozi yako, na mara kwa mara Rafiqs wengi wamejivunia kuwa na ngozi bora baada ya unywaji wa maji wa kutosha. Haiwezi tokea mara moja ila baada ya wiki moja utaanza kuona mabadiliko ya ngozi yako na itaanza kung’ara.
6.                   mfumo wa kuchanganya chakula ndani ya miili yetu (digestive system) unahitaji maji mengi ili kufanikisha kazi yake kifasaha, hivyo yatupasa kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi yake vyema katika muda sahihi kwa kunywa maji ya kutosha. Pia maji husaidia kuponesha maumivu ya vichomi vya tumbo, na pia hutupa urahisi pale tuendapo haja kubwa, kwani tunakua hatuna ukosefu wa maji mwilini. Maji husaidia pia kuondosha uchafu ndani ya miili yetu na kuacha mwili ukiwa msafi.
7.                   Kwa unywaji mwingi wakati wa mfumo wa kuchanganya chakula unaendelea, imeonekana kuwa maji husaidia kupunguza uwezekani wa kupata saratani ya colon kwa asilimia 45, asilimia 50 ya saratani ya kibofu cha mkojo na pia hupunguza uwezakano wa kupata saratani ya matiti kwa kina mama.
8.                   Kuwa na ukosefu wa maji mwilini husababisha kukurudisha nyuma katika swala zima la mazoezi na kukufanya iwe ngumu kunyanyua vyuma vya mazoezi, pamoja naa kufanya mazoezi mengine, hivyo basi inashauriwa kunywa maji kabla, wakati na baada ya mazoezi ili uweze kuyafanya vyema na katika hali salama.
                                                                                           
Tunaweza anza jiuliza, kiasi gani cha maji twatakikana kunywa?
 Inashauriwa ni glass nane kwa siku,??? Labda inawezakana sio sahihi sana…… kwasababu kiasi hicho kinahusisha maji safi ya kunywa tunayoyanywa, pia maji yanayopatikana kwenye vyakula tunavyokula na vinywaji vingine mbali na maji ya kunywa. Pia kiasi hicho hakikuangalia uzito wa miili yetu kitu ambacho ni muhimu sana tunapoongelea kiasi cha maji cha kunywa, na pia kiasi cha maji hutofautiana pale ambapo tunaumwa, au kwa wale tunaofanya mazoezi kila siku.
Jambo lingine, unaposikia kiu, kumbuka kwamba tayari una upungufu wa maji kwa hiyo kunywa pale hakutimizi  zile glass nane za kunywa maji.
Cha kufanya basi, ni kujenga mazoea:

2.                  Kunywa glass moja ya maji pale uamkapo, glass moja kila baada ya mlo, glass moja katikati ya milo yako ya siku, na kumbuka kunywa maji kabla, wakati wa na baada ya mazoezi. Jaribu kuepuka kupata kiu ya maji.
3.                   Beba chupa ya maji: Wengi wenye shughuli za kutembea hapa na pale itawapasa kubeba chupa ya maji mkononi na kunywa mara kwa mara, inapoisha ongeza nyingine. Na kwa wale wanaokaa maofisini, weka glass ya maji pembeni yako na uwe unakunywa mara kwa mara na kuongeza pale inapokwisha. Njia nyingine, ni kuegesha mlio kwenye saa ya mkononi au ya kwenye simu, au kwenye Computer yako, iwe inalia kila lisaa kamili linapotimu, ili uweze kukumbuka pale unaposikia kengele au alarm.
Iwapo unajisikia hamu ya kunywa soda au kimiminika chenye kilevi au cha aina nyingine yeyote, badala ya kukifuata hicho, badili na fuata glass ya maji na unywe. Jaribisha maji yenye ladha pale unapokua katika sherehe au makutanoni na marafiki.

Anza mazoezi, kwani mazoezi hukufanya uwe na hamu ya kunywa maji maana si utasikia kiu. Si lazima kunywa vinywaji vya kuongeza nguvu, ila kama unafanya mazoezi zaidi ya lisaa limoja na kuendelea waweza kuvinywa. Kunywa maji mapema iwapo wajua utaenda kufanya mazoezi, kwani itasaidia maji kufika kwenye system ya mwili wako vyema pale unapoanza mazoezi, kunywa maji wakati wa mazoezi na baada ya mazoezi.
Fuatilia mwenendo wako wa unywaji maji kwa kuandika pahala kwa ajili ya kumbukumbu. Hii itakusaidia kukuonesha na kukukumbusha kwamba yakupasa kunywa maji katika muda ule ule kila ufikapo na kiasi ambacho umejipangia. Andika muda upande wa kwanza na wapili unaweka alama ya vema kila mara unywapo maji .

Asali
Nyuki anauwezo wa kutembea mile elfu tatu akikusanya maua ya aina mbalimbali toka miti mbalimbali milioni kumi na tano kwa ajili ya kutengeza asali kilo moja ndani ya miezi mitatu. Kutokana na mchanganyiko huu unaotengenezwa na mdudu nyuki ASALI ina uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya mia moja. Bado utaendelea kutumia sukari yenye 'chemicals' zinazopunguza uwezo wa kuona na kuleta madhara mengine!. Unashauriwa na wataalamu wa afya kwamba kila siku uamkapo ramba asali ujazo wa kifuniko cha soda kimoja pia tumia asali kama kiungo cha chai, uji,maziwa na kadharika. Pia asali inatumika kama mboga kwa kulia ugali uliopoa. Ukila na ugali wa moto unaweza kupata maumivu ya tumbo. Tumia asali kwa wingi kwani ni 'antibiotics' pia. Kumbuka asali Mbichi ambayo haijachemshwa motoni ndiyo inayofaa. Hakikisha umejiridhisha kuw asali uliyonunua ni mbichi.


Pia mazoezi mengine rahisi kwa mwimbaji ni ku Harmony (Harmonize) =
“Huuuuu, haaaa, hoooo”. Mwimbaji lazima uwe mjanja na personal swagga na lazima ziendane na facial expression pamoja na kukaa kwenye ufunguo (key) na mapigo ya wimbo. Pia add lips (kuchombeza) huleta ubora wa uimbaji.

NB. Inawezekana lugha niliyoitumia hujaielewa sana, na wakati mwingine nimechanganya na kingereza au lugha ya muziki. Ikumbukwe kuwa muziki una lugha yake, na pia nimejaribu kutafsi kutoka kwenye notisi zangu ambazo mimi mwenyewe najifunza kwa lugha ya kingereza. Lakini kwa ushauri zaidi tuwasiliane.

Kumbuka muziki au uimbaji ni kama bahari, kila mtu anaogelea pale anaweza kufika, mimi naweza nikakutoa hapa nikakupeleka pale, na mwingine akakutoa pale na kukupeleka kwingine. Hakuna aliyefika kikomo cha kujua muziki au uimbaji, sote ni wanafunzi, na pia katika kufundishana sote tunajifunza. Ikiwa unataka kuwa mwimbaji bora, na unahisi bado unatatizo fulani tuwasiliane.

MAFUNZO BINAFSI YA KUWA MUIMBAJI BORA

Yafuatayo  ni  baadhi  maelekezo muhimu yatakayo kufanya kuwa muimbaji bora, kwako wewe mwenye uwezo wa kuimba au usiye jua kabisa na umekuwa na ndoto ya kuja kuwa muimbaji lakini hujui namna ya kujifunza.

1.Anza  kufanya mazoezi ya uimbaji pamoja na waimbaji katika CD’s, hakikisha unaendana na mianguko yote. Sauti za juu, sauti za chini na kati  kwa kiingereza hufamika kama(pitch).vile utajifunza jinsi ya kuhama ufunguo(key)kutoka ufunguo mmoja  na kwenda ufunguo mwingine na jinsi ya redio, zoezi hili litakuwezesha kufahamu mbinu nyingi wanazotumia waimbaji wakati  mwingine bila hata wewe kujijua yaani automatic,mambo unayoweza kujifunza kutumia  pumzi wakati wa uimbaji  nk.

2. Jaribu  kuanza kuimba mbele ya watu wa karibu na yako mfano marafiki zako, familia yako, mpenzi wako  na kuwaomba  wakusikilize ikiwezekana wakukosoe au kukuponda. Hapa ukipata msikilizaji anayejua muziki, itakuwa ni vizuri zaidi kwani anaweza kukurekebisha maeneo utakayo kuwa umekosea wakati unapoimba,kama kuchanganya sauti, kutofuata mwendo wa mapigo wakati unapoimba, kuimba nje ya ufunguo nk.

3. Jirekodi na jisikilize mwenyewe kama unaona kuna dosari yoyote kinyume na ulivyotarajia katika uimbaji wako rudia tena kuimba na kujirekodi,ukizingatia kutorudia tena makosa uliyoyaona mwanzoni. Aidha kama unaona  umefaulu kwa kiwango ulichokitaka, jaribu kuwapa wengine  wasikilize  rekodi ya wimbo wako na kutoa maoni yao.

4. Nunua vitabu au video  vitakavyokupa maelekezo na mbiu  tofauti kuhusu uimbaji, hii ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi ya sauti voice training, itakupa uwezo zaidi katika kuimba nyimbo za aina tofauti

5.Jiunge na vikundi vya uimbaji na kuanza kuimba nao ilikupata uzoefu zaidi kwani kuna utofauti mkubwa kati ya kujiimbia mwenyewe na kuimba mbele za watu kenye umati.

Pamoja na kufahamu  mambo hayo lakini kuna vidokezo muhimu vya kwako wewe unaweza kujifunza kuimba navyo ni:
1.                  Fanya mazoezi ya kuimba mara kwa mara hata wakati unapokuwa peke yako.
2.                  Jiamini  wewe binafasi  na usijinganishe na waimbaji wengine,wenye majina kwani kila mtu anauwezo na kipaji chake hata wewe unaweza kuwa juu siku moja.
3.                  Hakikisha  una sauti  nzuri japo si lazima sana na unakipaji na kuipenda kwa dhati kazi ya uimbaji ili hata utakapokabiliana na vikwazo haita kuwa tatizo kwako, bali itakupa changamoto ya kujifunza zaidi na kujisahihisha maeneo yenye udhaifu..
4.                  Inawezekana katika uimbaji wako kuna eneo unaliwezea sana na linakuongezea wapenzi au mashabiki wengi (kucheza, kutawala jukwaa, kutetemesha sauti n.k) basi boresha zaidi.
5.                  Kuwa na ukaribu na mwalimu wa muziki/uimbaji au mtu mzoefu,aliye mwaminifu ili aweze kukupa mawaidha kadhaa uweze kufikia kiwango kinachoridhisha hata kwa wasikilizaji watakao kusikia.
6.                  Ukifanikiwa katika mambo hayo anza sasa kujifunza ala za muziki, kama guitar, kinanda pia unaweza kujifunza hata kucheza hii itakusaidia kukupa uzoefu wa kuimba na vyombo live performance’'katika matamasha ya wazi na kanisani.
Vile vile kitu kingine muhimu ni kuomba msaada kutoka kwa mwalimu wa muziki/ uimbaji au  mtu  yeyote  mtaalam  wa muziki uanze kufanya mazoezi ya kuimba scale kama major scale,chromatic scale na scale nyinginezo labda nikupe mfano wa major na chromatic scale na unaweza kumuomba mpiga kinanda  akakipigia ili uzisikie jinsi zinavyosikika na uzifanyie mazoezi ya kuimba mara kwa mara.
Mfano wa major scale katika ufunguo wa C(key C).C,D,E,F,G,A,B,C

Mfano  wa chromatic scale katika  ufunguo wa  C(keyC)
C,C#,D,D#,E,F,F#,G,G#,A,A# B,C
Endapo utasoma nadharia ya muziki  unaweza kujifunza aina za scale.pia mwalimu akupe mazoezi ya kujenga uwezo wa sikio lako kimuziki uwe na sikio la muziki itakusaidia kuimba bila kutoka nje ya key, kuijua sauti yako na kujua kama ala za muziki hazijarekebishwa vizuri,mpigaji ukiwa na sikio la muziki ni muhimu

pia utabaini vitu hivyo kama muimbaji  anaimba na kutoka nje ya key pia utaweza kutyuni ala zako. Lakini kama sikio la muziki hauna si rahisi kutyuni ala kama gitaa. Ni vizuri waimbaji na wapigaji kujifunza nadharia ya muziki (music theory) itasaidia sana katika kukuza uelewa. Pamoja na hayo vilevile jifunze kufanya mazoezi mbalimbali kama major,minor na zinavyosikika na kuziimba.

N.B. Sio kila mwimbaji mwenye jina anafaa kuwa mwalimu wa kukuelekeza au kukufundisha. Pia sio lazima uweze kila kitu kwenye uimbaji au muziki ndipo uwe mwimbaji bora.
Sio waimbaji wote ni wanamuziki na sio wana muziki wote ni waimbaji. Sio kila mwimbaji ni mtunzi, lakini pia inawezekana mtu akawa mtunzi na asiwe mwimbaji.

Zingatia nguzo nne za muziki pamoja na mazoezi ya pumzi yanayofaa kwa mwimbaji.




UBORA WA SAUTI
Nianze kwa kusema, nimekuwa mmoja kati ya waalimu wa sauti na uimbaji, niliyewezesha watu wengi, vikundi vingi, na kwaya nyingi kuimba vizuri.
Lakini pia nashangaa wapo watu wengi wanaokimbilia studio, wanatengenezewa studio lakini ukweli ni kwamba hawajawa waimbaji wazuri, ni waimbaji wa kuimbia CD. Jamani kuimba vizuri kuna gharama zake.
Ikumbukwe kuwa, ili uimbaji wetu au muziki wetu uwe wa viwango vya kimataifa yapo mambo yanayotakiwa kufanyika:
Kwanza  ni uandishi mzuri, ubunifu zaidi, studio bora (quality of studio), kuandaa video yenye viwango (quality of video).
Nimekua nikifundisha kwa kina kuhusu hatua nne za kuelekea kuwa na albam bora ya audio, ikiwa ni pamoja na: mwimbaji kuwa bora, tungo bora, muziki bora na studio bora.
Nikualike tena kuhudhuria mafunzo yetu ya sauti yanayoendelea maeneo ya Ukonga. Kwa kuchangia kidogo tu nitakufundisha mbinu za kuwa mwimbaji bora. Tuwasiliane.

Tuendelee na somo:
Unahitaji kufanya nini?
Unahitaji kuboresha sauti yako kwa kupumua vizuri na kutuliza misuli yako badala ya kuiga mtu mwingine.
Kwa Nini Ni Muhimu?
Sauti nzuri hufanya wengine watulie na kufurahia kusikiliza. Sauti mbaya huaribu mawasiliano, na inaweza kumfadhaisha mwimbaji/msemaji na wasikilizaji.
KWA KAWAIDA watu hawavutiwi tu na mambo yanayosemwa, bali wanavutiwa pia na jinsi yanavyosemwa. Ikiwa mtu anayezungumza nawe au anayeimba mbele yako ana sauti nzuri, changamfu, ya kirafiki, na yenye fadhili, utafurahia kumsikiliza kuliko kama ana sauti kali isiyo ya kirafiki, sivyo? Kukuza sifa hizo nzuri hakutegemei tu kuboresha sauti. Kunaweza kuhusu utu wa mtu pia.

Nyakati nyingine sauti isiyofaa inaweza kusababishwa na kasoro fulani ambayo mtu amezaliwa nayo au ugonjwa uliodhuru zoloto. Huenda kasoro hizo zisiweze kurekebishwa katika mfumo huu wa mambo. Lakini, unaweza kuboresha sauti yako ukijifunza kutumia vizuri viungo vya usemi. Kwanza, tufahamu kwamba sauti za watu hutofautiana. Kwa hiyo, usijaribu kuiga sauti ya mtu mwingine. Badala yake, boresha sauti yako mwenyewe pamoja na hali zake. Unawezaje kufaulu?

Kuna mambo mawili makuu;
-          Pumua Vizuri. Ili sauti yako iwe nzuri, unahitaji hewa ya kutosha na unahitaji kupumua vizuri. Bila kufanya hivyo, sauti yako inaweza kuwa dhaifu mno na unaweza kukata-kata maneno katika hotuba yako au uimbaji wako.

Sehemu kubwa za mapafu haziko juu kifuani; sehemu hizo huonekana kubwa kwa sababu tu ya mifupa ya mabega. Lakini, sehemu za mapafu zilizo pana zaidi ziko chini, juu tu ya kiwambo. Kiwambo kinashikana na mbavu za chini na kinatenganisha kifua na tumbo.
Ukivuta pumzi na kujaza tu sehemu za juu za mapafu, utakosa pumzi haraka. Sauti yako itakosa nguvu na utachoka haraka. Ili uvute pumzi vizuri, unahitaji kuketi au kusimama vizuri na kurejesha mabega nyuma. Jaribu sana usipanue sehemu ya juu pekee ya kifua unapovuta pumzi. Kwanza vuta pumzi kabisa. Sehemu za chini za mapafu zikijaa hewa, mbavu zako za chini zitapanuka. Kwa wakati huohuo, kiwambo kitasonga chini, kikisukuma chini kwa utaratibu sehemu za tumbo hivi kwamba utasikia mkazo kwenye mshipi wako au kwenye vazi katika eneo la tumbo. Lakini mapafu hayako kwenye eneo la tumbo; yamefunikwa na mbavu. Unaweza kuthibitisha jambo hilo kwa kuweka mkono mmoja kila upande wa mbavu za chini. Kisha vuta pumzi kabisa. Kama unavuta pumzi vizuri, utaona kwamba huingizi hewa tumboni na kuinua mabega. La, badala yake, utasikia mbavu zikisonga juu kidogo na kupanuka.
Kisha, jaribu kushusha pumzi. Usishushe pumzi kwa ghafula. Ishushe polepole. Usijaribu kuzuia pumzi kwa kukaza koo kwa sababu sauti itajikaza au itakuwa nyembamba sana. Mkazo wa misuli ya tumbo na mkazo wa misuli iliyo kati ya mbavu huondosha pumzi, lakini kiwambo hudhibiti mwendo wa pumzi hiyo.

Msemaji au mwimbaji anaweza kudhibiti jinsi anavyopumua kwa kujizoeza kama vile tu mwanariadha anavyofanya mazoezi ya mbio. Simama vizuri kama umerejesha nyuma mabega, vuta pumzi kabisa ili sehemu za chini za mapafu zijae hewa, kisha shusha pumzi polepole na kwa utaratibu ukihesabu kwa kadiri uwezavyo kabla ya kuvuta tena pumzi. Kisha jizoeze kusoma kwa sauti ukipumua kwa njia hiyo.

-          Tuliza Mkazo wa Misuli. Jambo jingine muhimu linalotokeza sauti nzuri ni utulivu! Unaweza kuboresha sana sauti yako ukijifunza kutulia unapozungumza. Ni lazima akili na mwili zitulie, kwa kuwa mkazo wa akili husababisha mkazo wa misuli.

Ifikirie misuli ya koo na kujaribu kuituliza. Kumbuka kwamba nyuzi zako za sauti hutikisika zinapopitisha hewa. Sauti hubadilika misuli hiyo ikikazika au ikitulia kama tu vile uzi wa gitaa hubadili sauti ukikazwa au ukilegezwa. Sauti hurudi chini nyuzi za sauti zinapotulia. Kutuliza misuli ya koo pia hufanya mianzi ya pua ibaki wazi, na hiyo huboresha sauti.
Tuliza mwili wako mzima—magoti, mikono, mabega, na shingo. Ukifanya hivyo, utaweza kuvumisha sauti vizuri ili isikike wazi. Sauti huvumishwa wakati mwili wote unapohusika kuitokeza, lakini mkazo huizuia. Sauti hutokezwa kwenye zoloto nayo huvumishwa katika mianzi ya pua, kwenye mifupa ya kifua, meno, na kaakaa ya mdomo na mianya iliyo katika mifupa ya pua. Sehemu hizo zote zinaweza kuchangia ubora wa sauti. Ukiweka kitu kwenye kibao cha gitaa cha kupaazia sauti, sauti itafifia; ni lazima kibao hicho kisiwe na kitu ili kitikisike na kutoa sauti vizuri. Ndivyo ilivyo pia na mifupa ya mwili wetu ambayo imeshikiliwa na misuli. Uvumishaji mzuri wa sauti unakuwezesha kuwa na ubadilifu wa sauti na kuweza kuonyesha hisia mbalimbali unapoimba au kuzungumza. Pia utaweza kuimbia au kuhutubia watu wengi zaidi bila kukaza sauti.

JINSI YA KUFAULU
Fanya mazoezi ya kuvuta pumzi, ukijaza sehemu za chini za mapafu kwa hewa.
Unapoimba au kuzungumza, tuliza misuli yako ya koo, shingo, mabega, na mwili wote mzima.

MAZOEZI: (1) Kwa dakika chache kila siku katika juma, fanya mazoezi ya kuvuta pumzi kabisa mpaka uzijaze sehemu za chini za mapafu yako. (2) Jaribu kutuliza misuli ya koo unapoimba au unapoongea, angalau mara moja kwa siku.

SAUTI HUTOKEZWAJE?
Sauti zote hutokezwa na hewa inayotoka mapafuni. Mapafu hupiga hewa kama pampu kupitia koo na kuingia ndani ya zoloto ambayo iko katikati ya koo. Ndani ya zoloto mna misuli miwili midogo inayoitwa nyuzi za sauti, msuli mmoja uko upande mmoja na msuli mwingine upande mwingine. Nyuzi hizo za sauti ndizo vitokezaji vikuu vya sauti. Misuli hiyo hufungua na kufunga njia ya hewa katika zoloto ili kuingiza hewa na kuitoa na vilevile kuzuia vitu visivyotakikana visiingie kwenye mapafu. Tunapopumua kwa njia ya kawaida nyuzi za sauti hazitokezi sauti wakati hewa inapopita. Lakini mtu akitaka kuimba au kuzungumza, misuli hufinya nyuzi za sauti, na nyuzi hizo hutikisika wakati hewa inayotoka mapafuni inaposukumwa kuzipitia. Utaratibu huo hutokeza sauti.

Kadiri nyuzi za sauti zinavyokazika, ndivyo zinavyotikisika kwa kasi zaidi na ndivyo sauti inavyoinuka. Na kadiri nyuzi hizo zinavyolegea, ndivyo sauti inavyopungua. Mawimbi ya sauti yanayotoka kwenye zoloto huingia sehemu ya juu ya koo inayoitwa koromeo. Kisha mawimbi hayo hupitia mdomo na pua. Hapo sauti nyinginezo huongezwa ili kurekebisha, kukuza, na kuimarisha sauti ya awali. Kaakaa la mdomo, ulimi, meno, utaya, na midomo huungana pamoja ili kutawanya mawimbi ya sauti, na kutokeza usemi unaoeleweka.
Sauti ya mwanadamu ni ajabu sana, na haina kifani ikilinganishwa na chombo chochote kile ambacho binadamu ametengeneza. Ina uwezo wa kuonyesha hisia mbalimbali kama vile upendo na chuki kali. Sauti ikikuzwa na kuzoezwa vizuri, inaweza kubadilikana sana na kutokeza nyimbo tamutamu na semi zinazogusa mioyo.

KUSHINDA MATATIZO FULANI HUSUSA
Sauti dhaifu.
Sauti ndogo huenda isiwe dhaifu. Ikiwa nzuri na yenye kuvutia, wengine wanaweza kufurahi kuisikiliza. Lakini ni lazima sauti iwe yenye kiasi kinachofaa ili iweze kufaidi wengine.
Ili uboreshe ukubwa wa sauti yako, unahitaji kuivumisha zaidi. Unahitaji kutuliza mwili wote mzima, kama ilivyoonyeshwa katika somo hili. Pamoja na kutuliza mwili, fanya mazoezi ya kuimba hali umefunga midomo. Midomo inapaswa kugusana kidogo, isishikane sana. Unapoimba kwa njia hiyo, sikia mitikisiko ya wimbo huo akilini na kifuani. Nyakati nyingine sauti husikika kuwa dhaifu au kukazika kwa sababu ya ugonjwa au kukosa usingizi. Bila shaka, hali hiyo ikiboreka, sauti itaboreka.

Sauti inayoinuka juu sana.
Mkazo kwenye nyuzi za sauti hufanya sauti iinuke. Sauti yenye mkazo hufanya wasikilizaji wawe na mkazo. Unaweza kupunguza sauti nyembamba kwa kutuliza misuli ya koo ili kupunguza mkazo kwenye nyuzi za sauti. Jaribu kufanya hivyo, ukifanya mazoezi kila siku unapozungumza. Pia ni vizuri kuvuta pumzi kabisa.

Sauti ya kubana pua.
Nyakati nyingine pua iliyofungika hutokeza tatizo hilo, lakini mara nyingi hali hiyo husababishwa na jambo jingine. Nyakati nyingine kwa kukaza misuli ya koo na mdomo, mtu hufunga mianya ya pua na kuzuia hewa isipite vizuri. Jambo hilo hutokeza sauti inayobana pua. Unahitaji kutulia ili kuepuka jambo hilo.

Sauti nzito na kali.
Sauti kama hiyo haileti mazungumzo ya kirafiki uimbaji wa kirafiki. Inaweza kutisha wengine.
Katika hali fulani, jambo muhimu ni kuendelea kujitahidi kubadili utu wako. Ikiwa tayari umefanya hivyo, kujaribu kutumia kanuni za kurekebisha sauti kunaweza kusaidia. Tuliza koo na taya. Kufanya hivyo kutafanya sauti yako ipendeze zaidi na kufanya maneno mengine yasitokee vibaya kwa kuyalazimisha kupitia meno.

VIUNGO VYA MATAMSHI
Kaakaa, Ulimi, Meno, Midomo, Taya, pua…
Kumbuka kwamba kila mtu duniani ana tone yake na hii hutokana na hivyo viungo nilivyotaja hapo juu. Maana rahisi ya tone ni sauti ya mtu inapotoka au kusikika. Hivyo awe mwimbaji, muhubiri, mwalimu, mtangazaji, public speakers… ana tone yake. Wapo wengi sana wametokea kupendwa au kupata ajira nzuri kwasababu tu ya tone. Kumbuka haya yote yanafanyika kupitia kitu kinaitwa DIAPHRAM; Mfano halisi ni kwamba, mwimbaji anaimba kupitia diaphragm singing, muhubiri anatumia diaphragm speaking …

MKONDO WA HEWA MWILINI
Tundu la pua, Kinywa, Koo, Nyuzi za sauti, Njia ya chakula, Mapafu, Kiwambo
Nyuzi za Sauti (zikitazamwa kutoka juu)
Unapozungumza
Unapovuta pumzi
Unapovuta pumzi kabisa.





AFYA YA SAUTI (VOCAL HEALTH); UNAPENDA KUIMBA VIZURI? BASI HII NI KWA AJILI YAKO

You are the instruments – Learn to sing like a pro!
Wewe ndie chombo halisi, jifunze kuimba kama pro!

Ieleweke kwamba, Kuwa na utimamu wa kimwili (fitness) sio kuwa bora kuliko mtu flani, bali ni kuwa bora kuliko ulivyokua awali. Watu wengi sana hutumia muda wao mwingi tu katika majumba ya mazoezi (Gym) wakifanya mazoezi mbalimbali ya kimwili na wana nidhamu sana katika hili, ni jambo zuri sana kiukweli. Lakini tunasahau kitu kimoja; Koo lako ni sehemu ya mwili wako pia! na kama ukitenga muda kwa ajili ya mazoezi, na utunzaji mzuri wa Sauti yako, utawashsangaza wengi sana na ubora wa sauti yako! Ungependa kuelewa nini cha kufanya??

AFYA YA SAUTI:
Sauti yako ndiye balozi wako kwa ulimwengu, umewahi kuona mtu hata awe mpole kiasi gani, lakini kama akiwa na sauti ya kutisha (hasahasa wazee) hata watoto humuogopa?? au hata ukifatwa na mtu ambae humjui na ana sauti ya ajabu ajabu we mwenyewe lazima uogope!
Sauti unayoitumia kuongea ndiyo hiyo hiyo unayoitumia kuimba, hivyo basi, ukiitumia sauti yako hovyo katika maongezi utaathiri pia uimbaji wako! Zingatia hili; kama vile mwanamuziki kitendea kazi chake ni kile chombo cha muziki, vilevile mwimbaji kifaa chake ni lake. Sasa guitar likikatika nyuzi unaweza ukatafuta uzi mwingine, lakini koo halina spare, litunze. Unyevu, Mazoezi ya misuli ya shingo na mapumziko, ndiyo viungo muhimu katika kuipika afya ya sauti yako. Vinafanyaje kazi? ENDELEA…

UNYEVU;



Msingi wa sauti ni maji mengi

Tumia Maji ya Kunywa kwa wingi sana ili kuzifanya Ala zako za Sauti (Vocal Chords) ziwe na unyevu, zisikauke. Maji hulainisha na kuyaondoa makohozi katika koo na kuyafanya yasigandamane kwenye ala za sauti.
Usitumie “spray” ya aina yoyote kunyevusha koo lako. Kumbuka kubadili mazingira yenye hali za hewa tofauti tofauti huathiri ala za sauti. Cha kufanya, kunywa maji ya kutosha na kula matunda yenye maji mengi kama matikiti maji na matango, achana na matunda yenye tindikali nyingi kama “citrus fruits” mfano machungwa, malimao, na ndimu kwani yatazisugua ala za sauti na kuziachia mikwaruzo.
MAZOEZI;

“Mazoezi ya sauti yanachekesha, yafanye ukiwa peke yako, hasa bafuni unapooga”
Fanya mazoezi ya sauti na mwili kwa ujumla na kwa bidii. Fanya mazoezi ya ulimi kama “tongue trill” (yafanye ukiwa mwenyewe, hasa bafuni ili usije ukachekesha watu) ili kuruhusu upitaji mzuri wa hewa kwenye koo, na upumuaji mzuri kwa ujumla.
Jifanyie pia masaji maalum za ulimi na maungio ya taya, fanya “humming“, yaani tamka herufi ‘m‘ kwa muendelezo, ukiwa umefumba mdomo, (kama sauti ya nyuki wengi) ukiwa bafuni ili kuipasha sauti yako. Hakikisha unafanya hivi kila siku kwa matokeo mazuri.
Fanya pia mazoezi ya misuli ya shingo, koo taya na mabega, pia legeza misuli ya shingo na koo unapoimba noti za juu sana au za chini sana, ukikakamaza shingo itakusababishia maumivu na sauti itaharibika.

MAPUMZIKO;

Baada ya kuunguruma kwa muda mrefu, pumzika

Hakuna kitu kinachoweza kufanya kazi bila kuchoka, hata iwe mashine ya Mjerumani. Kwahiyo, hakikisha unapata mapumziko ya kuongea baada ya kutoka kwenye maongezi au uimbaji uliokufanya utumie nguvu nyingi ili kuinusuru sauti yako.
Epuka tabia za kupiga kelele hovyo, kubishana kwa sauti na nguvu nyingi, au kuimba kwa nguvu sana kusiko kua na maana yeyote. Epuka sana uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kwani kutakusababishia madhara kwenye sauti.
KWA KUMALIZIA…
  • Acha sauti yako ing’ae, kuwa wewe na usiigize sauti ya mtu
  • Siku zote kunywa maji mengi yasiyochanganywa na kitu, maji tu!
  • Pata muda wa kutosha wa kupumzika, epuka kelele zisizo za msingi
  • Mwisho, Jifunze mbinu bora za uimbaji
(Kwa masomo zaidi yanayohusu mbinu za uimbaji, hudhuria madarasa yetu)




 John Shabani akiongoza sifa



Moja ya huduma za John Shabani





Mwalimu John akiongoza mazoezi yapumzi

Joyce John akijifunza kupiga kinanda


Mwl. John akielekeza matumizi ya asali



MAFUNZO YA SAUTI
VOCAL TRAINING
By John Shabani
Mobile: 0716560094, 0754818767
Facebook: John Shabani




MAZOEZI NA FAIDA ZAKE







 

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP