JOHN SHABANI - NEW ALBUM



KALE NILITEMBEA

Kale nilitembea, nikilemewa dhambi, nilikosa msaada kuniponya mateso.
Hata nilipofika mahali pa msalaba, palinifaha sana, sitasahau kamwe.
Hicho ndicho chanzo, chakufurahi kwangu, hapo ndipo mzigo, ulipo nituliwa
Panapo msalaba, kinatolewa cheti, cha kuingia Mbinguni, kisicho cha kanisa


Usifiwe msalaba! Lisifiwe kaburi! Linalozidi yote, asifiwe Mwokozi

Yule bwana mjinga, alikwenda bila cheti, akitumai kuingia, kama walionacho.
Alipofika langoni, akaulizwa cheti cha kumwonyesha Bwana, akakutwa hanacho
Lituhuzunishalo, ni ninyi msio nacho, kuwa kama mjinga, kwa siku ya arusi

Ubavuni mwa Yesu, mlitokea damu, chemchemi ya uzima, itakasayo roho.
Jitaidi uingie, damuni mwa Mwokozi, utafutiwa dhambi, toka rohoni mwako

Asifiwe mwokozi, asifiwe mwokozi, asifiwe mwokozi, asifiwe mwokozi

MUNGU YU MWEMA

Eeeh  Eeeeeh  Eeeeeh
Mungu yu mwema, Mungu yu mwema,
Mungu yu mwema, Mungu yu mwema.

Mungu wetu, Mungu wetu, Mungu yu mwema
Mungu wetu, Mungu wetu, Mungu yu mwema

Yesu yu mwema, Yesu yu mwema
Yesu yu mwema, Yesu yu mwema

Yesu wetu, Yesu wetu, Yesu yu mwema
Yesu wetu, Yesu wetu, Yesu yu mwema

Mungu yu mwema kwa wajane Mungu yu mwema, Mungu yu mwema kwa yatima Mungu yu mwema. Mungu ni mwema kwa wale walio vunjwa moyo, Mungu wetu ni mwema kwa walio katishwa tama, Mungu wetu hana upendeleo, anawapenda watu wote, anawapenda wtu wote

Kweli Yesu ni mwema sana eeh, hata kwangu ni mwema sana. Ametukumbuka katika unyonge wetu eeh,ameyafuta machozi ya wanaolia Mungu wetu.
Tanzania (yu mwema), Kwa waganda (yu mwema), kwa wakenya (yu mwema), kwa wakongo (yu mwema), burudi Rwanda (yu mwema), Malawi Angola (yu mwema), afrika nzima (yu mwema), Mungu yu mwema hata marekani, ulaya na duniani kote.
Kwa wanyakyusa (yu mwema), wabena (yu mwema), wachaga (yu mwema),

Mungu yu mwema kwa makabila yote, Mungu yu mwema kwa watanzania, yu mwema Africa, tushangilie tupige vigelegele

Nasema Mungu yu mwema sana, nasema Mungu yu mwema sana, asante yehova, Mungu yu mwema wakati wowote, wakati wowote Mungu yu mwema, Bwana Yesu, Mungu wangu, Mungu yu mwema

Hatuna maneno mengi ya kusema hebu sote tusimame, tumwambie Mungu wetu yu mwema haleluya! Yu mwema kwako mama yangu, (yu mwema),  kwako baba yagu (yu mwema), kwako kaka yangu (yu mwema), kwako dada yangu(yu mwema), kazini kwako (yu mwema), nyumbani kwako (yu mwema), katika biashara yako (yu mwema), ulalapo(yu mwema),  , uamkapo(yu mwema),  unaposafiri (yu mwema), Yeye ni mwema Baba Baba Baba

KWA YESU KUNA RAHA

Hii siyo ngonjera, ni mbunge wa serikali ya Mbinguni anayeishi katka dunia hii ambayo watu wake wametaharuki, John Shabani na Chidumule.

Sasa nimetambua ya kwamba kwa Yesu kuna raha

Raha yake siyo ya mwisho wa mwezi wala sikukuu bali ni ya siku zote
Najuwa umejaribu mambo mengi yakupe raha, hebu jaribu kwa Yesu
Unajuwa alikokutoa Yesu, hebu sasa imba, simama sema kwa Yesu kuna raha raha
Yesu ni mwaminifu, tena ana huruma, mimi na ndugu yangu chidumule tunaimba Yesu ametupa raha, raha ooh sasa.

Nilikunywa sana nililewa sana nikalala kwenye mitaro (lakini sikutosheka), kila mganga mpya niliyesikia jina lake nilimtafuta (lakini sikutosheka), wewe na mimi tuliponea chupuchupu kufungwa jela (lakini sikutosheka)

Eeh ndugu yangu, maneno haya ninayo kuambia, si kwa msomi wala mbumbumbu, si kwa kijana wala mzee. Hebu tutafakari hii raha, je iko kweye sigara? Hapana), ugoro? Hapana, pombe? Hapana, umalaya? Uzinzi, hakika huko kote hakuna raha maana hayo yote yatakutenga na upendo wa Mugu. Na Mungu ninaye msema mimi si mungu  wa kwenye kikombe na kwenye vibuyu wala yule mungu wa kwenye mapango na miti mikubwa, bali Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo

Nilibadilisha waganga wa bagamoyo na sumbawanga mimi (lakini sikutosheka), kumbe yoye ilikuwa ni hasara kwangu (lakini sikutosheka), kama dhambi zote nilifanya nilifanya (lakini sikutosheka)

(Kuna raha) kwa Yesu (Kuna raha) ametupa raha (Kuna raha), amenipa raha (Kuna raha) ndiyo maana tunaimba (Kuna raha), ndiyo maana tunaruka (Kuna raha)
Hebu watu wote pigeni vigelegele na nderemo
Raha iliyoko kwa Yesu haifananishwi na chochote, raha iliyoko kwa Yesu hailinganishwi na chochote

Nasikia raha kuwa na Yesu, nasikia raha kuwa na Yesu
 Raha! Raha! Raha! Raha! Raha!)
Kama kweli umeokoka sema raha raha
Raha! Raha! Raha! Raha! Raha!)
Tele tele, siyo nusu, ya milele, kina dada semeni raha, watumishi semeni raha

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP