23 August 2011

MARUFUKU KUKATA TAMAA (Kitabu cha watanzania) kiko mbioni.


 
                     MARUFUKU KUKATA TAMAA

 Never ever give up



John Stephen Shabani
P. O. BOX 15155
      Dar es salaam, Cell: +255 754 818 767


Kitabu hiki au sehemu yake hairuhusiwi kutolewa kwa namna yoyote nyingine, kuhifandhiwa katika namna yoyote, kutwaliwa tena, au kusambazwa kwa jinsi yoyote au namna yoyote, kwa elektroniki au mashine yoyote au kuchapa nakala au kunakili au vinginevyo bila taarifa ya awali ya kimaandishi ya ruhusa ya mtunzi na mmiliki, isipokuwa kama ilivyoidhinishwa na sheria ya hakimiliki ya Tanzania.
Copyright © 2009 na John S. Shaban

Haki zote zimehifadhiwa







YALIYOMO                                                                 

·         DIBAJI……………………………………………………
·         UTANGULIZI…………………………………………....
·         SHUKRANI………………………………………………
·         HITIMISHO…………………………………………......


Kukata tamaa
Dalili za mtu aliyekata tamaa
Athari za kukata tamaa
Mambo yanayokatisha tama
Baadhi ya magonjwa yanayotokana na kukata tamaa
Mtu akikata tamaa huamua chochote maali popote na kwa wakati wowote
Faida za kutokata tamaa
Mifano ya watu waliofanikiwa Kwa kutokata tamaa
Njia za kumsaidia aliyekata tamaa
Siri ya kufanikiwa (Jinsi ya kushinda kukata tamaa)
Baadhi ya jumbe kutoka Kwa watu na watumishi


TAMATI
           Maisha ni malengo……………………………………..




Dibaji

Nimejisikia aliyependelewa Sana Kwa kuwa mtu wa kwanza kukisoma kitabu hiki cha maana sana maishani.

Chaajabu na cha kutia moyo ni kwamba, mwandishi amegusia kwa kina mambo mengi ambayo mimi binafsi nimekuwa nikiyazungumzia katika maeneo mengi na katika semina mbalimbali ndani na nje ya nchi (kwa njia ya Runinga, Redio, magazeti, Midaalo nk.). Ila mvuto na mguso uliomo ndani ya ujumbe huu umebadilisha kabisa baadhi ya mitazamo yangu.

Nina uhakika kwamba wewe hautabaki vile ulivyo wala hutafikiria vile ulivyozoea mara tu utakapofanikiwa kusoma ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho wa kitabu hiki.

Adui namba moja aliyewapeleka wengi katika njia wanayoitegemea na kujuta maishani, adui aliye waingiza maelfu kaburini kabla ya muda wao muafaka, adui aliye wafanya wengi kuonekana wazee kumbe bado vijana, adui aliye wafikisha wengi katika umri walionao wakiwa uchi na mikono mitupu tofauti na ndoto na matumaini yao, adui huyo mara zote amekuwa ni Kukata tamaa.

Vita dhidi ya adui huyo imekuwa ikianzia ndani ya mtu binafsi, na kwa hivyo ukombozi wako haunabudi kupangwa na kutekelezwa ndani ya mtu mwenyewe, yaani wewe mwenyewe binafsi.

Kitabu hiki kitakukomboa katika maeneo yote ya kiuchumi, kiroho, kijamii na kisaikolojia. Kumbuka mabadiliko ya kweli huanzia kwa mtu binafsi, na mara zote nimejifunza kusema chanzo cha mabadiliko yangu ni mimi

Hiki ndicho kitabu ulichokuwa unakiitaji, usikikose.
Ni kitabu pekee kitakachokamilisha ndoto zako “Marufuku kukata tamaa”

Mr. CHRIS MAUKI Bad (ed), MA (Asp) UDSM.
- Assistant lecturer in Psychology and concelling
                      University of Dar es salaam.
-          Radio presenter “ saikolojia na jamii ” Praise power Radio
-          Tv and Radio show Guest speaker ( facilitater )
-          Article writer ( News paper and Magazine )
-          Event planner






Utangulizi


Kwa uzoefu wa miaka niliyowezeshwa na Mungu kuishi hapa duniani, nimejifunza mengi, nimeona mengi na kusikia mengi. Jambo lililonifanya nipate msukumo wa kuandika Kitabu hiki, mimi mwenyewe nikiwa kijana niliyepitia katika misukosuko na mapito ya aina mbalimbali kama vile kukataliwa, kuvunjwa moyo, kuishi maisha ya ufukara, kukosa elimu niliyoitamani, kusengenywa na kuchekwa, kujikuta nikiwa jela bila hatia yoyote
Lakini katika yote hayo adui niliyepambana naye ni kukata tamaa.

Ninapoona matatizo yakiwaandama Vijana (nguvu kazi ya taifa), wajane, yatima, wenye ulemavu, marafiki, wachumba, wanandoa, wafanya kazi n.k najihisi kuna jambo ninalopaswa kufanya kwa jamii hii. Hilo ni jukumu letu sote. Pengine yapo matatizo mengine yanayosababishwa na mawazo na fikra zetu, mitazamo ya watu juu yetu, uelewa wetu katika kupambana na matatizo au hali halisi ya ulimwengu unaotuzunguka. Upo kama ulivyo ni kwamba wewe mwenyewe ulikwishaamini utakuwa hivyo ulivyo leo tangu jana. Na vyovyote vile uwavyo, jinsi utakavyokuwa kesho, itakuwa ni matokeo ya jinsi unavyoamini leo kuhusu hiyo kesho. Ninao uhakika, leo yako ilitegemea jinsi ulivyoishi jana yako na kesho yako itategemea jinsi utakavvyoishi leo. Ukiamua leo kuwa kesho utakuwa na maisha mazuri (mafanikio), utakuwa. Inawezekana! Iliwezekana kwa wengine, na kwako inawezekana.

Wote waliofanikiwa, tajiri na maskini, Mungu aliwaumba wote kama binadamu si kama tajiri au maskini. Hakuna aliyetoka tumboni mwa mama yake akiwa na chochote mkononi. Hali ya kuwa tajiri au masikini ni uamuzi wako. Mazingira ya kuzaliwa na kulelewa yanaweza kutofautiana lakini suala la msingi ni hili: Ni kwa kiasi gani umedhamilia kufanikiwa au kutokuwa masiki? Je! Ni kwa kiasi cha kuwa tayari kutumia mbinu au fursa yoyote halali inayojitokeza mbele yako? Je! Ni kwa kiasi cha kufa au kupona? Ninawafahamu watu wengi ambao walikuwa na mazingira na hali ngumu sana katika familia walikotokea, lakini leo hii ni watu waliofanikiwa sana na wanaoheshimika duniani. Walifika mahali wakaamua na wakadhamria kutokuwa maskini.

Najua wapo ambao tayari wamekata tamaa, lakini pia wapo wanaoelekea kukata tamaa, na wapo ambao hawajakata tamaa kabisa. Hivyo sina jinsi ninavyoweza kumfikia kila mmoja kwa kumtembelea ila kwa njia ya kuwaandikia. Ni imani yangu utasoma kwa makini kitabu hiki na kitakuondoa mahali ulipo na kukupeleka mahali pengine. Wakati mwingine matatizo hutukumba na kutufanya tujiulize kama kweli Mungu katuacha, katuonea au hayupo. Mara nyingi mtu mmoja mmoja ndiye hujiona kuwa ndiye mwenye kuandamwa na matatizo kuliko wote duniani.

Kitabu hiki sio tu kitakutia moyo, bali kitakuelimisha, kukushauri, kukufariji katika mapito unayopitia na kukuondoa katika hali na mzingira uliyokuwa nayo.
Ni maombi yangu mbele za Mungu aliyenipa maono haya na ambaye wote tunamwamini, atakusaidia kupitia kitabu hiki ili usibaki kama ulivyo.

Kuanzia leo jione kuwa mwenye kushinda na sio aliyeshindwa, mzima na sio mgonjwa, jasiri na si dhaifu, tajiri na sio maskini. Marufuku kukata tamaa.





Shukrani
(Acknowledgements)

Natanguliza shukrani zangu za thati kwa Mungu aliyeumba mbingu na nchi, ambaye kwangu amekuwa msaada tosha maishani. Kwangu yeye ni Baba, rafiki, kiongozi, mshauri, mlinzi, msaada nk. Nakiri kuwa hakuna hata moja nililolifanya kwa nguvu zangu mwenyewe. Nashukuru pia familia yangu kwa kunivumilia na kunitia moyo nilipokua nikiandika kitabu hiki, hasa mwanangu Joyce ambaye baada ya msiba wa mama yake amekuwa akinita moyo. Imenichukua miaka kadhaa nikinyenye mbele za Mungu katika kuandika kitabu hiki, tena wakati mwingine niliamka usiku wa manane na wakati mwingine sikulala kabisa. Natambua mchango mkubwa wa wazazi wangu hasa mama yangu mzazi, aliyenilea katika maadili mema na kunishauri jinsi ya kuishi katika dunia, ushauri ambao nimekuwa nikiufanyia kazi siku zote, pamoja na kuwa nimeishi miaka mingi nikiwa mbali na wazazi wangu. Kama leo jamii inaniheshimu na kunihitaji, ni kwa sababu yenu wazazi wangu. Neema na baraka za Mungu ziwe kwenu wazazi wangu wapendwa, nawapenda.

Natoa shurani zangu za pekee kwa wazazi wangu wa kiroho/Mchungaji wangu Bishop Jane Muhegi (Muanzilishi wa huduma ya Dorcus Christian Ministries), pamoja na mumewe, mzee Boniface Muhegi, ambao wamekuwa kwangu wazazi, walezi na washauri wangu wakuu. Mmenitia moyo sana, ninyi ni watu  muhimu kwangu na kwa familia yangu. Mungu wa mbinguni awainue zaidi.

Sitoacha kumshukuru Mchungaji na Dk. Getrude Rwakatare ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shule za St. mary’s na mmiliki wa Kituo cha Redio cha Praise power & Television, Kama alivyo Mama wa Watoto wengi na aliyejaa upendo na huruma, amekuwa pia kwangu Mama, mshauri, mlezi na mtu muhimu katika maisha yangu.

Namshukuru rafiki yangu wa karibu Bishop Charles Jangalason mkurugenzi wa World Hope Trust Fund na mwimbaji wa nyimbo za Injili, ambaye kwangu amekuwa mshauri mzuri. Ushauri wake ndio ulionipa msukumo wa kurekodi  Album yangu ya kwanza inayoitwa “Marufuku kukata tamaa”,  Album iliyogusa mioyo ya watu wengi ndani na nje ya nchi.

Nawashukuru Mchungaji Mulenda Omary, Mch. Wilonja Omary, Askofu Paulo Macha (Jesus Healing Ministries – Arusha) na Rafiki yangu Pastor John Komanya ( Cathedral of joy - Merland – USA) ambao kwa njia moja au nyingine wamekua kwangu washauri na walezi wangu kiroho na kimwili. Pamoja na wengine wengi ambo wamekuwa kwangu watu wa muhimu.

Siwezi kuvisahau vyombo mbalimbali vya Habari kama Praise power Radio, Wapo Radio, Upendo Radio, Radio Tumaini, Redio maria, Safina Radio(Arusha), Radio Sauti ya Injili (Moshi) na nyinginezo nyingi ndani na nje ya nchi. Pamoja na vituo vya Runinga (televisheni) kama vile Trenet chini ya Mtume na Nabii Josephat Mwingira, EATV (East Africa Television), ATN nk. Pamoja na magazeti ya Nyakati, Msema Kweli, Habari Njema, the Guardian, Alasiri, Nipashe, nk, kwa kusaidia kutambulisha huduma na vipaji tulivyonavyo kwa jamii inayo tuzunguka.

Natoa shukrani kwa kampuni ya Msama promotions, ambayo nimekua nikifanya kazi kwa miaka kadhaa, na kunipa uzoefu mwingi, pia kunikutanisha na watu mbalimbali, wakiwemo viongozi mbalimbali wa dini na serekali, waheshimiwa, watu wa rika zote. Pia imenirahisishia kwa kiasi fulani katika uchapaji wa kitabu hiki.


Kukatatamaa                                                    


Kukata tamaa ni hali ya kupoteza matumaini. Hali hii hutokea pale ambapo mtu amepoteza wazo au matumaini ya kufanikiwa katika matarajio yake ya kupata kitu fulani au kufanikiwa kwa jambo lolote alilopanga kulifanya. Pia ni kupoteza tumaini la kufikia malengo katika jambo fulani alilopanga kulifanya au analolifanya, ni hali inayoweza kutokea katika mfumo wa maisha ya kila siku, iwe nyumbani, Kazini, shuleni, kwenye biashara, katika mahusiano au mahali pengine popote katika mfumo wa maisha. Pia ni moja ya matatizo makubwa yanayowafanya watu kutofikia malengo yao au kutopata mafanikio katika maisha yao ya kila siku.
Pia tunaweza kueleza kukata tamaa kama hali ya kufikia kikomo juu ya mafanikio ya jambo halisi. Kufikia kikomo huko hutokana na kujenga taswira na hoja ya kushindwa katika mawazo yako juu ya suala lolote ulilopanga kulifanya au unalolifanya. Pia ni hali ya kuchoshwa au kuvunjwa moyo kunakotokana na mtazamo hasi (Negative) unaoweza kuujenga baada ya  kufikia Ukomo wa ufahamu, ufumbuzi au jawabu la suala lolote linalokukabili, iwe kutokana na mawazo yako binafsi au mawazo ya yatokanayo na watu wengine.



Dalili za mtu aliyekata tamaa                           

Zipo dalili nyingi za mtu aliyekata tamaa ambazo zinaweza zikawa zinatofautiana kutokana na mazingira, sababu, wahusika, matukio n.k. Lakini zipo dalili za msingi na za jumla kwa watu wote. Dalili hizo tunaweza kuzigawa katika sehemu Kuu mbili ambazo ni:

v  Dalili za Ndani
Hizi ni dalili ambazo watu wengine nje ya mhusika hawawezi kuzitambua kiurahisi, ni muhusika tu ndiye anaweza kuzitambua au kuhisi.

v  Dalili za Nje
Hizi ni dalili ambazo watu wengine nje ya mhusika tunaweza kuwa mashahidi kwa kuziona kwa uwazi na kutambua kwamba mwenzetu amekata tamaa. Tunaweza kuziangalia dalili hizi angalau kwa undani zaidi.

1. Dalili za ndani

Kukosa msukumo kimawazo
Kwakua kila jambo linaanzia kwenye mawazo, ili mtu afanikiwe anahitaji msukumo na ushawishi wa mawazo yake. Maana mawazo anayokuwanayo mtu kwa mudamrefu, huwa yanajitokeza ktika maneno yake na hatimaye katika matendo yake. Hivyo basi ukiona msukumo wa mawazo yako ya mwanzo umepungua, basi ujue kuwa hiyo ni dalili mojawapo ya kukata tamaa.

Kuhisi kuchoshwa kimawazo
Ukiona mawazo yako yamechoshwa kwa kuliwazia jambo fulani ambalo mwanzoni ulikuwa umelipanga vizuri, nayo ni dalili ya kukata tamaa.

Mawazo ya kushindwa
Dalili nyingine ni mawazo ya kushindwa au mawazo hasi. Haya ni mawazo ambayo siku zote hayana ushawishi wa kukusaidi kufanya jambo lolote, badala yake huleta woga kufanya jambo kwa kuhofia kushindwa au kukosa uhakika wa kufikia malengo.

Kukosa ubunifu wa njia mbadala
Ukiona jambo linashindikana kwa njia moja na huku unakosa ubunifu wa njia mbadala jinsi ya kulifanikisha jambo hilo, nayo inaweza ikawa ni dalili ya kukata tamaa. Kila mtu ana uwezo mkubwa sana wa ubunifu, tofauti zetu zinajitokeza pale ambapo wengine wanashughulisha sana sehemu ya ubongo zinazo husika na ubunifu, wakati wengine wamezilemaza.

Kupoteza furaha /hamu ya jambo husika
Jambo ambalo ulikuwa unalifurahia na kuliona nzuri, huku ukifikiria kufikia mafanikio, ghafla unaanza kupoteza furaha au hamu ya jambo hilo, nayo ni moja ya dalili ya kukata tamaa.

Kutofurahia ushauri
Ukiona unaanza kuchukia ushauri hasa unaokwenda kinyume cha mawazo yako au ushauri unaokushawishi kuendelea kufanya jambo ambalo umeamua kuliacha.

Kufanya maamuzi ya haraka
Mawazo yako yanapoamua kufanya maamuzi yanayohatarisha maafanikio yako, au kuhatarisha maisha yako kama kujiua, ni dalili tosha ya kukata tamaa.                                                                                                                                                      
Kupoteza taswira ya mafanikio
Taswira ya mafanikio ndio msukumo halisi wa kufikia mafanikio. Kupoteza taswira ya mafanikio akilini mwako, ni dalili ya kukata tamaa.

Kupoteza ujasiri
Akili yako inapopoteza ujasiri juu ya jambo ambalo hapo mwanzo ulikuwa na ujasiri mkubwa wa kulitenda au kukabiliana nalo, hapo moja kwa moja utakuwa umefikia hatua ya kukata tamaa.

Kujihurumia
Hili nalo ni tatizo la ndani ya mtu, unapoanza kuona akili yako inajihurumia nakuona kama watu au jambo lina kukosesha furaha ni dalili ya kukata tamaa.

Kujihisi hufai kabisa
Unahisi maisha yako hayana jambo lolote la maaana la kuchangia na hayafai kabisa.
Huenda ukahisi unahatia nyingi.

Kutamani kufa
Baadhi ya watu hutamani kufa kuliko kuishi kwasababu ya mambo ya hapa duniani yaliyowaumiza mioyo.Wengine hutamani kujiua na wenginehufikia hatua ya kumwomba Mungu awachukue kama vile nabii eliya katika biblia alivyoomba (1wafalme 19:4)

2. Dalili za nje

Dalili za nje kama tulivyotangulia kuziona, ni zile ambazo watu wengine yaani nje ya mhusika tunaweza kuziona au kuzishuhudia, nazo ni:

Maneno yanayoashiria kukata tamaa
Mtu aliyekata tamaa, huwa na maneno yanayoashiria kukata tamaa, maneno yanayokiri kushindwa n.k. Ukimsikia mtu anazungumzia jambo linalohusu kufanikiwa au kutofanikiwa katika maisha, na kama anayasema hayo kwa hiari yake mwenyewe, basi chunguza, utangundua hayo ndiyo mawazo ya moyo wake. Mfano kama wewe ni tajiri, unawaza habari za utajiri, unazungumzia habari za utajiri, unashirikiana na matajiri, na kila unalofanya ni matokeo au ina fanana na mawozo au maneno ya utajiri unayao yatamka mara kwa mara.

Vitendo vinavyoashiria kukata tamaa
Moja ya mambo yanayoongoza kwa kuongeza vitendo vya utovu wa maadili, ni kukata tamaa. Mfano utumiaji wa madawa ya kulevya, ukahaba n.k.

Mabadiliko ya tabia 
Kama sio mara zote basi mara nyingi, mabadiliko ya tabia toka tabia nzuri kwenda tabia mbaya hutokana na kukata tamaa. Tena mara nyingi mabadiliko ya tabia yanaptokea huwa yanatanguliwa na matukio au sababu ya kukata tamaa.


Kujitenga
Mara nyingi mtu huanza tabia ya kujitenga au tabia ya kuwa peke yake, hiyo pia inaweza ikawa moja ya sababu  za kukata tamaa.

Kukosa furaha
Kwa mtu ambaye tunajua kuwa alikuwa na hali ya kawaida ghafla anaanza kukosa furaha na kuwa mnyonge, inawezekana kabisa kuwa hiyo ni dalili ya kukata tamaa.

Kupungua kwa juhudi
Kupungua kwa juhudi au bidii kwa mtu ambaye mwanzoni hakuwa hivyo, inawezekana kabisa kuwa hali ya bidii imetoweshwa na kukata tamaa.

Kupoteza mwelekeo
Kupoteza mwelekeo, kukosa dira kimawazo na hatimaye kiutendaji hutokana na kukata tamaa.

Kuchukua hatua zisizotarajiwa
Hapa tunaweza kuona hatua kama kujiua, au nyingine ambazo ni kawaida kutokea katika jamii.

Kulia machozi
Baadhi ya watu hujikuta wakilia machozi kila wanapokumbuka mambo waliyopitia.
Hii ni dalili ya kukata tamaa. Nimekutana na watu wengi ambao waliumizwa mioyo na watu wengine, mara wanapoelezea juu ya matukio yaliyowaumiza hujikuta wakipiga kelele za kulia. (Usiishi leo kwa mapito yaliyopita jana, yasije yakapita nawe).

Kukunjamana uso
Mtu aliyekata tamaa ni rahisi mara kumuona amekunjamana uso kwasababu ya mawazo na masononeko. Hali hiyo hufanya uso kuchakaa na mtu kuonekana kama mzee hata kama hajafikia umri huo.

Kama vile moyo unapokuwa na furaha hudhihirika usoni kwa mtu, vilevile moyo unapokuwa na matatizo hudhiirika usoni kwa mtu. Kadiri unavyolinda moyo wako ndivyo unavyolinda uso wako na maisha yako kwa ujumla. (Mithali 15:13)


Athari za kukata tamaa

Zipo athari nyingi za kukata tamaa na zimegawanyika kulingana na wanaoguswa na athari hizo; kama ifuatavyo:

(A)  Athari zinazomgusa mhusika

Hizi ni athari ambazo humgusa mtu moja kwa moja aliyekata tamaa (mhusika) nazo zipo nyingi ingawa hutofautiana kulingana na umuhimu wa jambo ulilolikatia tamaa.

Athari zenyewe ni :

Kutofikia malengo uliyojiwekea
(Iwe kibiashara, masom, kazi n.k.)
Lengo zuri lazima litekelezeke (Maana malengo ndio dira, mwelekeo, kipimo au picha ya mafanikio yako au, ya unapotakiwa kuwepo baadaye).Yapo yasiyotekelezeka na ukijiwekea malengo ya jinsi hii yatakupa shida, maana utaishi kukata tamaa siku zote. Moja ya mambo yatakayo kusaidia kujua hilo ni viwezeshaji ulivyonavyo, Mazingira na hali. Ni muhimu kuzingatiwa ili vikusaidie kujua kama lengo hilo linatekelezeka au la. Ninaposema viwezeshaji, hali na mazingira, ninamaanisha uzingatie uwezo uliopo au tegemea kulipia gharama za malengo hayo, uhuru ulio nao katika kuyatekeleza maono yako na pia muda ulio nao wa kuyatendea kazi maono yako (Maana lengo pia lazima liwe linafikika, kwani kuna tofauti ya lengo kutekelezeka na kufikika. Lengo linaweza kuwa linatekelezeka kwa maana ya mikakati lakini halina ukomo, halina mwisho, na hii ni kwa habari ya muda). Kumbuka muda wa kutekeleza lengo hauwekwi kiolela. Sifa nilizo zitaja hapo juu zaweza kusaidia. Na hayo ndiyo yanasababisha malengo kupangiwa muda mrefu au mfupi (Maana malengo yapo ya aina mbili: ya muda mfupi na muda mrefu).                           

Kubaki na hali yeyote ambayo kabla ulihitaji kujikwamua. 
(Mfano umaskini,  maradhi, ujinga n.k)

Kuchanganyikiwa kiakili na uwezo wako kiutendaji.
Unapokata tamaa katika jambo moja unahatarisha hatma ya mambo mengine pia, kwani kukata tamaa husababisha hali ya kuchanyikiwa kiakili na kupunguza uwezo wa utendaji.
Kupoteza mali fedha na hata heshima
mfano unapokata tamaa katika biashara ambayo tayari umeweka nguvu fedha au mali, inamaanisha kuwa kile ulichowekeza kinapotea bure.

Kujengeka kwa tabia ya hofu na kukosa ujasiri.
Kwa vyovyote vile unapopoteza ujasiri juu ya jambo moja unapoteza ujasiri juu ya jambo lingine.

Kupata maradhi yatokanayo na mfadhaiko
Sio rahisi kuepuka maradhi kama shinikizo la damu, madonda ya tumbo na memgine yanayofanana na hayo

Athari nyingine ni matokeo ya dalili tulizoziona 
yaani za nje na ndani zinapotokea. Mfano mdogo ni kukosa furaha na kujitenga na wazazi, kupotezea marafiki wazuri wenye busara na mafanikio

Athari nyingine ni kujiingiza katika vitendo viovu
(kama ulevi uchangudoa, madawa ya kulevya n.k.)

Kuzeeka au kufa mapema (kujiua)


(B) Athari zinazogusa wengine  

man

Hapa tunazumgumzia familia, marafiki, taasisi(kama za dini n.k), mashirika, makampuni, serikali na jamii nzima kwa ujumla wake.

Athari zenyewe ni kama zifuatazo:

kupotea kwa msaada utokao kwa waliokata tamaa
Ni wazi kuwa mtu aliyekata tamaa, kama alikuwa msaada sehemu kati ya hizo ambazo tumezitaja hapo juu na nyinginezo, maana yake msaada wake utakuwa umetoweka.

Kupoteza watu tunaowategemea
Kama ikitokea aliyekata tamaa amechukua hatua ya kujiua, inamaana ataacha pengo lisilozibika.

Kushindwa kuwapata watendaji wazuri
Inawezekana miongoni mwa Watu waliokata tamaa wengine wangekuwa wafanyabiashara wazuri, wasomi, wanasiasa wazuri n.k

Kuongezeka kwa watu wanaohitaji msaada katika jamii
mfano;  Wajane, yatima, watoto wanaoishi katika mazingira magumu n.k. Wengi wao ni wale wanaotoka katika familia za watu waliokata tamaa au wamepoteza maisha yao au wanaishi maisha yasiyoridhisha.

Kukosa maendeleo ya msingi katika Taifa
Kutokana na kukata tamaa, idadi kubwa ya watu waliokata tamaa huongezeka, hivyo umaskini, ujinga n.k, navyo huongezeka, jambo ambalo hulifanya taifa likose maendeleo, hivyo kujengeka kwa jamii isiyo na malengo/mwelekeo mzuri wa maendeleo.

Mambo yanayokatisha tamaa

Kuna mambo mengi sana yanayokatisha tamaa. Tunatofautiana kati ya mmoja na mwingine katika kukata tamaa, kulingana na sababu au mazingira  n.k.

1. Urafiki Uchumba na Ndoa  
Uchumba, urafiki na ndoa ni maneno yanayowagusa watu wengi, mara mnyingi maneno haya kwa imani ya dini zetu hubeba maana sana kama yatafuatana kama urafiki , uchumba na hatimaye ndoa (Hii ni kwa watu wenye jinsia mbili tofauti). Japo katika dini nyingi au kwa ajili ya kulinda maadili, suala la kuwa na urafiki wa jinsia mbili tafauti, halipewi nafasi kabisa. Kinacho tambulika zaidi ni uchumba hadi ndoa.

Urafiki ni neno lenye maana ya kuridhiana, baina ya watu au mtu na mtu mwingine  kwa lengo la  kushirikilana katika kipindi cha shida au raha, iwe kiuchumi kijamii, kisiasa au kitamaduni n.k. Ladha ya maisha haiwezi kukolea sawasawa pasipokuwa na marafiki. Furaha au ustawi wa mwanadamu mara nyangi unamuitaji mtu mwingine. Mara nyingi marafiki huwa wana nia moja.

Uchumba ni maridhiano ya watu wawili walioshibana kitabia wakiwa na tarajio la kuishi kama mume na mke pindi watakapooana. Ni vyema uhusiano wa uchumba uanzishe pale mtu anapokaribia kuoa, pia uchumba unakuwa wa maana zaidi, ikiwa mapatano hayo, yatafanyika mbele ya mashahidi wachache na zaidi sana uthibitishwe na jamii yako, katika dini yako au dhehebu nk. Kwa kufanya hivyo kuarsaidia, ili mchumba asije baadaye akakukana, kukufedhehesha au kukutupulia mbali, huku akijidai kuwa hajawahi kukutamkia wala kuwa na wazo lolote la kukuoa. Pia inasaidia ili kuwafahamisha ndugu, jamaa na marafiki kwamba tokea siku ya kufanya makubaliano hayo, mmefunga mlango kwa wachumba wengine waliotaka kujipenyeza au kujishugulisha au kusumbuasumbua kutaka uchumba kwa mmoja wenu.

Ndoa ni makuballiano/ mapatano au mkataba wa hiari kati ya watu wawilil wenye jinsia tofauti kuishi kama mume na mke. Kama kuna kitu cha kukilinda sana, kukitunza kukiheshimu na kukithamini maishani, ni ndoa. Ndoa ikiharibika, kuna asilimia kubwa ya maisha kuharibikiwa.

Pamoja na tafsiri/ maana nzuri ya maneno haya bado jamii imeshuhudia migongano, vilio, majuto malumbano ambayo yako kinyume na tafsiri halisi. Yapo matatizo yanayo sababishwa na mazingira na yapo yanayosababishwa na watu wenyewe.

(a) Ndani ya ndoa
Kuna matukio mengi ya watu waliojiua au kubadili tabia zao toka tabia njema na kuwa mbaya kwa sababu ya mahusiano yao na ama waume zao au wake zao. Mara nyingi mahusiano huvunjika au kulega lega kwa sababu ya kuvunjika kwa moja ya nguzo muhimu katika  mahusiano ya kimapenzi ambayo ni uaminifu. Kuna visa vingi vya watu waliokufa, kufungwa au kuwa walevi kupindukia, ukahaba n.k, kwa sababu ya kukata tamaa kulikotokana na kuvunjika kwa mhusiano katika ndoa.

(b)  Nje ya Ndoa.
Huko nako mahusiano yamelegalega, watu wanaamua kutooa au kutoolewa, baada ya kuvunjika au kuharibika kwa mahusiano. Wengine wameamua kuwa na tabia ya kukosa uaminifu katika maisha yao wenyewe baada ya tatizo kama hilo. Athari za kuharibika kwa mahusiano ni pamoja na kuwa na idadi kubwa ya watoto ambao hawaangaliwi ipasavyo na wazazi wao, watoto wa mitaani au wasio na makazi maalumu.
Vipi unapoachwa na yule aliyekuahidi atakujengea nyumba hewani na ahadi kemkem? Yule aliyekuwa akikupa maneno matamu kama vile “nitakufa kwa ajili yako, kumbe hawezi hata kuzimia. Usiku silali kwajili yako, kumbe analala hadi anakoroma. Naugua kwajili yako, kumbe hana hata homa nk”.

Je unajihisi ndiyo mwisho wa maisha kwa kuwa eti marafiki wamekutenga, kuugua au kuachwa? Umeachwa na mchumba na unahisi hakuna mwingine tena duniani wa kukupenda? Je una nini? Hakuna uzuri tena? Huoni thamani yako juu ya dunia? Hapana! bado lipo tumaini usivunjike moyo, wewe ni mwenye thamani sana, fanya zoezi hili tafadhali ingia chumbani kwako ukiwa umetulia;

1.  Nenda bafuni fungua bomba lenye maji ya vuguvugu kisha anza kufungulia au mimina maji kuanzia utosini  huku ukifumba macho yako na kutafakari mashairi muhimu  katika maisha yako  ( mambo mema uliyokwisha kufanyiwa duniani)

2. Zoezi la pili, Unaporudi chumbani kwako, chukua kioo jiangallie ulivyo bora na wa pekee  kisha jiambie na kujipongeza ulivyo bora na mzuri mwenye thamani. Kamwe usikatishwe tamaa na mtu vitu au ulimwengu huu. Sawa sawa na imani ya moyo wako kwa unayemwamini, songa mbele kishujaa.


2.      Ugumu wa mambo

Hapa tunaangalia mambo mbalimbali ambayo watu wameshindwa kufikia malengo ya maisha kwa sababu hiyo, wengi wamekata tamaa na kujikuta wakikabiliana na madhara au athari za kukata tamaa. Mfano wa mambo ambayo ni magumu na huwafanya watu wengi kukata tamaa ni
kama yafuatayo:


a)    Maisha
Watu wengi wanakuwa na malengo ya kuwafanikisha katika maisha yao, lakini kwa bahati mbaya wengi pia wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao kwa sababu mbalimbali. Kushindwa kwao kuyafikia malengo waliyojiwekea katika maisha kumewafanya wakate tamaa.

b)     Masomo /Elimu
Wapo waliokata tamaa kwa kuwa masomo ni magumu au upatikanaji wa elimu kuwa mgumu kwa sababu ya kushindwa kulipia gharama za elimu.

c)      Biashara/kazi
Ugumu wa biashara ama upatikanaji wa mtaji au ugumu wa soko la bidhaa unayoiuza au umesomo lakini upatikanaji wa kazi ni mgumu au mshahara unaulipwa haukidhi.

3. Unaweza ukakatishwa tamaa katika mazingira unayoishi (ndugu, jamaa,      majirani n.k), kazini, shuleni, unapofanyia kazi, huduma, biashara n.k.


Baadhi ya  magonjwa yanayotokana na kukata tamaa

Kuna vyanzo mbalimbali vya magonjwa yanayowapata wanadamu. Magonjwa mengine ni ya kibaiologia, mengine ni kisaikologia na mengine ni ya kiroho. Magonjwa ninayozungumzia ni yale ambayo vyanzo vyake vinatokana na kuumizwa moyo.

Watu wengi wamekuwa na maswali mengi ambayo hayana ufumbuzi kwasababu ya kupata magonjwa ambayo hayawezi kutibika katika hospital na mara nyingine hayaonekani katika vipimo vya maabara. Magonjwa hayo ni aleji (allergy) kama maumivu ya miguu, moyo kupanuka,
vidonda vya tumbo, kichwa kisichopona, shinikizo la damu, maumivu ya mifupa, maumivu makali kwenye magoti n.k.

Mithali 4: 23  inasema  Linda sana Moyo wako kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. Kama kwenye chemchemi kukiharibika uzima utatoka wapi?  Moyo ukiharibika ni lazima utasababisha matatizo katika baadhi ya viungo katika mwili.

Moyo ni mojawapo ya viungo vilivyo vya muhimu kuliko vyote katika mwili.
Ni moja kati ya viungo vidogo katika mwili lakini chenye kuitaji kutunzwa au kulindwa zaidi kuliko kiungo kingine chochote. Ukubwa wa moyo ni kama ngumi yako tu, lakini unafanya kazi kubwa mno. Ukiweka mkono wako upande wa kushoto wa kifua chako, utasikia kitu fulani kinadunda.
Kama huwezi kusikia midundo yake kwa urahisi, basi unaweza kukimbia kupanda ngazi za nyumba na kushuka chini kama marambli au tatu hivi, hapo ndipo utakapoisikia midundo yake kwa wazi sana. Je mnalijua jina la mashine hii ya ajabu iliyo ndani ya Mwanadamu, ambayo inadunda daima? Mtasema kwa pamoja kwamba huo ni moyo. Moyo unaweza kuitwa pampu iliyo hai, ambayo inaendelea kufanya kazi yake kwa maisha yote. Kama ungeacha kudunda hata kwa dakika moja au mbili hivi, tungekufa.

Ukiweka mkono wako juu ya moyo na kuyahesabu mapigo yake kwa dakika moja kamili, utaona kwamba unapiga karibu mara sabini na tano au thamanini hivi. Unapokuwa mzee, moyo wako unadunda kwa pole pole zaidi. Ukiyahesabu mapigo wakati umelala chini, utaona yakwamba moyo unadunda kwa pole pole zaidi kuliko wakati unapokaa au kusimama. Tunapokimbia au kuruka, moyo nao unadunda kwa nguvu na kwa haraka zaidi. Moyo wenye Afya na damu safi vinaitaji, Mazoezi, usingizi wa kutosha, hewa safi, Chakula kizuri, Maji safi n.k.

Baadhi ya magonjwa yanayotokana na moyo kuumizwa ni:

Magonjwa ya moyo
Ugonjwa huu ni tatizo kubwa katika jamii. Baadhi ya watu huvimba mioyo au baadhi ya mishipa kupinda n.k. Ukifuatilia maisha yao, utasikia kuwa kumekuwepo na matukio yakusikitisha. Baada ya kufanyiwa mambo ya kusikitisha bila kusamehe kwa muda mrefu huathiri moyo wa mhusika. Wanawake wengi wana matatizo ya moyo kwa sababu ya kukandamizwa na waume zao. Pia kwa asilimia kubwa hasira huchangia ugonjwa wa moyo. Mtu anapokasirika sana, moyo wake huanza kudunda kwa kasi sana na kuleta mfadhaiko wa moyo. Kwa kweli wapo watu wengi waliopata ugonjwa wa moyo kutokana na hasira ya ghafla.

Ugonjwa wa mifupa
Ugonjwa wa mifupa unaweza kuwa wa kurithi kwa wazazi, au kutokana na chakula kilichozidi au kupungua mwilini. Vilevile inaweza kutokana na moyo kuvunjika yaani kuwa na uchungu na kukata tamaa. Moyo wenye uchungu husababisha mwili kutengeneza kemikali ambazo huathiri mifupa na miguu kwa ujumla. Mithali 17:22 inasema “Moyo uliochangamka ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka huikausha mifupa” Ni kweli mtu anaweza kupimwa hospitali na kuambiwa kuwa mafuta ya kwenye viungo yamekauka, lakini ni kwanini yamekauka? Roho iliyopondeka huikausha mifupa.

Vidonda vya tumbo
Kwa kawaida vidonda vya tumbo havinatiba, madawa husaidia kutuliza maumivu tu.
Watu wengi wenye vidonda vya tumbo wana historia ya kuwa na mawazo sana kwa sababu fulani kama ugumu wa maisha, kuumizwa moyo na watu, mausiano nk.

Kwa sababu ya huzuni na uchungu, ni rahisi kukosa hamu ya kula chakula, wakati huo mtu akiwa na uchungu na huzuni sana kitu ambacho hufanya tumbo lizalishe tindikali (acid) nyingi kiasi cha kusababisha vidonda vya tumbo. Kama kutakuwa na chakula tumboni itapunguza uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo. Hivyo hakikisha unakula chakula cha kutosha hata kama unapitia mapito magumu.

Vilevile  Magonjwa yanayosumbua kama vile vidonda vya tumbo, matatizo ya moyo, maumivu ya kichwa na baadhi ya aina za kupooza. Woga husababisha hofu. Hofu humfanya mtu kutotulia na kuvunjika moyo [kukata tama], hali ambazo huathiri neva za tumbo na mabadiliko haya huifanya juisi ya gastric (gastric juice) ya tumbo kuwa isiyo ya kawaida (abnormal ) kutoka katika hali yake ya kawaida (normal) katika utendaji wake wa kazi.
Kutokana na mabadililiko haya vidonda vya tumbo humpata mtu husika. Tatizo la vidonda vya tumbo limekuwa sugu na lenye kuwasumbua watu wengi leo. Pamoja na kuwepo matibabu ambayo naamini katika hali ya kutokuamini kama yanaweza kuisaidia kuleta nafuu! Ufumbuzi wa tatizo hili ni mtu kujifunza kukabiliana na hofu za ziada tunazokumbana nazo katika maisha.
Dk. Joseph F. Mountague katika kitabu chake cha ‘Nervous Stomach Trouble’ anasema “huwezi kupata vidonda vya tumbo kutokana na kile unachokula bali utapata vidonda vya tumbo kutokana na kile kinachoila nafsi yako”. Waweza kuishi ukiwa na vitu vinavyokufanya uliwe kila siku. Woga, hofu, chuki, uchoyo kupindukia na uwezo duni wa kuitazama dunia na mambo yake katika hali halisi. Haya ni baadhi tu ya mambo yanayokula watu. Kwa kiasi kikubwa husababisha udhaifu wa matumbo yao ambao huleta vidonda vya tumbo. Jamani nazidi kupaza sauti – vidonda vya tumbo vinaweza kukuua. Jifunze kushinda hofu ili uwe salama. Plato anasema “Kosa kubwa wafanyalo madaktari ni kujitahidi sana kutibu, ili kuponya miili wakisahau kukabili ili kuponya akili ya mgonjwa. wakati akili na mwili ni kitu kimoja, hivyo haitakiwi kupata matibabu vikiwa vimetengwa” Wazo la Plato limechukua muda mrefu hadi wanasayansi wa tiba kukubaliana na ukweli mkubwa ulio ndani yake. Ndiyo sababu leo kuna jitihada kubwa za kuanzisha tiba mpya iitwayo psychomatic medicine. Tiba itakayotumika kuponya akili na miili kwa pamoja.
Yapo magonjwa mengi yasababishwayo ma vimelea vya magonjwa. Magonjwa kama vile kimeta, kipindupindu, homa ya manjano na mgonjwa mengi hatari yanayowapeleka watu wengi makaburini kila kukicha, lakini vilevile ipo idadi kubwa ya watu wanaoharibu miili yao na hata maisha si kwa vimelea vya magonjwa bali kwa mihemko ya hofu, woga, chuki, aibu kupita kiasi na kukata tamaa. Majanga yasababishwayo na magonjwa ya mihemko yanakua na kusambaa kwa kasi ya ajabu (catastrophic rapidity).

Mtu akikata tamaa huamua chochote mahali popote
na kwa wakati wowote
                                  
Wema alikuwa ni msichana mrembo na mwenye kupendeza sana. Aliwaheshimu wakubwa na wadogo, kamwe hakuwa na roho ya kwa nini wala kumdharau mtu awaye yote. Yawezekana maadili na malezi mazuri toka kwa wazazi wake ndiyo yalimfanya awe hivyo, Hakutamani fedha ya mtu isiyo haki wala mizaha isiyo ya maana. Alikuwa ni binti wakwanza kwenye familia yao. Wema alipenda ibada na kuhudhuria mafundisho ya kidini. Pamoja na uzuri wa kuzaliwa Wema alijipenda na kujitunza sana, Alitamani siku moja awe rubani. Hizi ndizo zilikuwa ndoto zake.
        
Wakati mwingine alisikika akisema “nikiolewa namwomba Mungu anipe watoto  watatu, wakiume mmoja na wawili wa kike wananitosha.” Aliyatamani maisha ya upendo na ya kujali ya wazazi wake. Utampataje mume wakati mwenyewe unawachukia wanaume?  Marafiki zake walimtania . « Duh! Ni kweli washikaji,  tena mmenikumbushia wanaume najisikia kichefuchefu, hebu tubadilishe mazungumzo » Wema alijikuta mnyonge mara alipokumbuka kitendo cha kunusurika kubakwa na kijana wao wa kazi kipindi akiwa darasa la tatu. Kutokana na kitendo hicho kila mwanaume aliye msogelea alitonesha kidonda cha moyo wake. Hivyo Wema akawa hataki kusikia habari za mwanaume zaidi ya baba yake.
                         
Upendo wa Wema na wazazi wake uliendelea hadi siku moja ulipoingia dosari. Siku hiyo akiwa anatoka shuleni alipokuwa akisoma jijini Dar es salaam, alipata lift(msaada wa usafiri) toka kwa kijana mmoja mmliki wa bar jirani na Shule aliyosoma. Kwa kuwa hupita maeneo yale anapokwenda shuleni, ilikuwa rahisi kwa kijana huyu kumtambua. Haikuwa rahisi kwa mtu yeyote kumsemesha habari za mapenzi kwani wengi walifahamu msimamo wake kuwa ni binti asiye na mazoea na wanaume. Wakiwa ndani ya gri, uvumilivu ukamshinda kijana huyo, nakuamua kurusha kete yake kama angefanikiwa. Wema akawa mkali na kutamani kushuka.
                           
Wakiwa bado wana zozana walifika maeneo ya njia panda ya Kawe, kwa bahati mbaya baba yake wema siku hiyo alikuwa yupo kituoni akisubiria usafiri. Kutokana na shida ya usafiri alijaribu naye bahati yake kuomba lifti, ghafla akahamaki kumwona binti yake amekaa, huku kijana yule akimsemesha kwa namna ambayo anaomba penzi kwa mwanadada huyu. Hasira iliwaka juu ya baba yake na kugairi kuomba lifti. Alifanikiwa kufika nyumbani huku akiwa na hasira juu ya binti yake Wema. Mh!Hii ndiyo biashara anafanyaga huku mtaani eh! Atanitambua. Kanajifanya kapole kumbe kahuni kakubwa haka”. Haya yalikuwa mawazo ya mzee juu ya binti yake. Siku hiyo Kijana mwenye bar akatafuta jinsi ya kujiosha kwa kosa alilomfanyia Wema, akamwomba ampeleke hadi maeneo ya nyumbani.

Wema aliendelea kulaani kitendo kile. Mzee kwa mara nyingine tena alipofika maeneo ya nyumbani akakutana na gari hilo likitokea kwake. Jambo hilo likazidi kuupigilia msumari wa mtazamo wake, kuwa  huyu alikuwa hawara wa bintie. Alifanikiwa  kufika nyumbani na kumkuta  mwanae yuko bafuni anaoga, alipiga mlango teke kwa hasira na kumvuta Wema nje na kuanza kumpiga bila huruma. Mama yake ambaye alikuwa jikoni akipika alishtushwa na kelele za mayowe. “Mama niokoe nafaaa! mama njooo mwanao nauwawa mie! Yanini ulinizaaa mama nateseka hivi mamaa!” Yalikuwa mayowe na kilio cha Wema   akipigwa na baba yake. Mama alipofika alimkuta Wema akitokwa na damu amelala chali. Hali hii ilimfanya mama yake Wema kupiga makelele kuomba msaada. Baada ya muda majirani walikusayia. Miongoni mwao alikuwa mama Kosinde na Soza bintiye ambaye pia ni rafiki yake Wema. Baadaye polisi kuchukuwa PF3 kisha akapelekwa hospitalini.
Wema alitibiwa na hatimaye kuruhusiwa kurudi nyumbani asubuhi ya siku iliyofuata.
Alipata jeraha usoni lililosababisha ajute kila alipoliangalia, ukiliganisha na ukweli kwamba wema alijipenda. Hii iliweka chuki ndani ya nafsi yake nakumfanya  amhesabu baba yake kuwa ni miongoni mwa watu waliomjeruhi nafsi. Hakuna kitu kibaya katika maisha ya mtu kama chuki kwani mwenye uwezo wa kuiondoa ni Mungu peke yake. Asubuhi ya siku ya Ijumaa Wema alienda shule huku akiwa na jeraha usoni. Kila aliyemwuliza ilimtonesha kidonda cha nafsi kwani ilimkumbusha uonevu aliotendewa na baba yake. Wanafunzi wenzake wakaanza kumsema na kumcheka. Hii ilitokana na umbea aliouzusha Soza shuleni, kuwa Wema amebakwa na baba yake mzazi. Wengine walisema alibakwa na mwenye bar. “Wanadamu hawana maana, nani aliye waomba wazungumzie hayoyote wakati sivyo! Mbona jamani wanadamu hamna dogo” alijiuliza Wema mara alipopelekewa umbea na Soza.

Suna ndiye kijana ambaye alionekana kuwa karibu na Wema, japo naye alikuwa na lake. Hawakuwa wakipendana na Wema, kwani kunakipindi alikuwa akimtaka Wema kimapenzi, kutokana na msimamo wa Wema juu ya wanaume, akajikuta anakuwa adui yake. Katika kipindi hiki Suna aliona ndio wakati mwafaka wa kutumia udhaiwake kufanikisha azma yake. Alijitahidi sana kuwa karibu na Wema ambaye kipindi hicho alionekana kutengwa na wenzake. Hiyo kila mara Wema alipokumbuka upendo alioukosa kwa Baba yake, aliona Suna ndiye aliyeurudisha kwa jinsi alivyokuwa akimtunza.
Siku moja mvua ilinyesha sana Shuleni, Wema na Suna wakajikuta wamebaki wenyewe pale darasani. Kwa bahati mbaya shetani akafanikiwa kuwajaribu... Kwa mara ya kwanza Wema akajikuta akifanya tendo lile alilokuwa akililaani na kulichukia katika maisha yake. Baada ya kitendo hicho Wema alijuta sana na kutamani ardhi ipasuke. Alikumbuka maneno ya Mama yake aliyokuwa akimwambia “Wema chagua maisha, UKIMWI ama Mimba”. Mawazo yalimsonga Wema alijihisi ana ukimwi au Mimba. Hali hii ilimfanya Wema azidi kukonda siku baada ya siku, maana habari zilizagaa shule nzima juu ya tendo hilo, huku Suna akijigamba kwa marafiki zake. Baada ya muda ikagundulika Wema ni mjamzito. Wazazi wake waliamua kumfukuza. Aliondoka usiku kwenda kumfuata Suna baada ya kufukuzwa. Alipofika kwa Suna alipigwa na kufukuzwa. “Dunia naiona chungu bora nife ili maadui zangu muishi kwa amani kama ndivyo hoja yenu kuu. Hivi kweli Baba na Mama mlishindwa kuchunguza kwa kina kabla ya kuchukua maamuzi hayo dhidi yangu? Mbona hamkunitendea haki japo niliwategemea dhidi ya waonevu wangu!”  Ulisema waraka aliouacha juu ya meza barazani kwao. Kikubwa kilichomfanya achukue maamuzi hayo ni kashfa na machungu ya unyanyasaji wa kijinsia na kupewa jina la Malaya ambalo hakulitegemea maishi na na pia kukukataliwa.
            
Aliondoka usiku wa manane kuelekea asikokujua, akiwa njiani wazo lilimjia kwenda kwa Mchungaji katika Kanisa lililokuwa karibu, lakini kwa bahati mbaya Mchungaji alikuwa amesafiri kikazi. Aliomba anuani ya Mchungaji na baadaye kuendelea na safari yake hadi makaburini. Akiwa makaburini mvua kali iliyoambatana na upepo ilimnyeshea. Akiwa hapo makaburini, alizisikia sauti za watu asiowaona. Kwakua hakuyatamani maisha tena, hivyo hakuogopa chochote, aliona kwake ni afadhali. Aliendelea na safari hadi alipochoka, akalala usingizi hadi asubui ambapo wasamaria Wema walipomuona, walimuokota, wakamchukua hadi kwa wazazi wake. Wazazi walistaajabu kwani walimtafuta kwa muda mrefu. Hivyo Baba na Mama Wema walimkumbatia mwanao na kumwomba radhi. Kama wazazi wenye uchungu na uzazi hawakutamani kumpoteza binti yao kwa njia moja ama nyingine. Wakakumbuka usemi usemao “Mtu akikata tamaa huamua chochote na maali popote wakati wowote”. Hekima ya Baba na Mama ilirejesha furaha ya Wema japo kidogo. Walikubali pia kumtunza mtoto atakayezaliwa punde. Pamoja na hayo ndoto ya shule ikafa na kujiona mtu asiye na mwelekeo wa maisha, huku majirani wakitoa maneno ya kejeli kwa wazazi wa wema “Haya wee! Tusubiri tuone mtakako mpeleka huyo Malaya wenu mliyemsomesha kwa gharama kubwa, hizo fedha si bora mngejengea nyumba ya wageni (Guest house)”.
Wazazi wa Wema pamoja na Wema mwenyewe waliumizwa sana na maneno hayo. Wema alikosa amani, hivyo wazo la kujinyonga likajirudia tena, ila aliamua kumwandikia Mchungaji barua kabla ya kuchukua uamuzi. Baada ya kupata majibu mazuri na yanayotia moyo kutoka kwa Mchungaji, alitafakaria wema wa Mungu, akakumbuka alivyokuwa pale makaburini, mvua na upepo mkali ulivyokuwa lakini hakudhurika. Akakumbuka alivyolala nje eneo lenye sifa ya vibaka, lakini akaokotwa asubuhi akiwa mzima, akaamua kubadili maamuzi. Alienda ibadani na kuanza maisha mapya. Akawa muumini mzuri, tabia yake ikabadilika na kuendelea kuwastaajabisha wana jamii. Akawa mwalimu mzuri wa kwaya hatimaye mwandishi wa vitabu vya mafundisho akielezea historia yake na changamoto ya maisha. Kwa ufupi Wema alipata mtoto wa kiume, na baadaye akapata wafadhili waliompeleka Ujerumani kuendeleza elimu yake. Akiwa chuoni alichumbiwa na kijana mzuri aliyekuwa mwalimu katika chuo hicho. Waliweza kufunya harusi yao nzuri lakini kwa bahati mbaya mwanaume hakuwa na uwezo wa kuzaa, kutokana na hali hiyo alimpenda sana Wema na mwanaye kwa moyo wote. Ole kwa Wema kama angakitupa kichanga chake leo hii asingeitwa Mama.


Ndugu msomaji,
Kuna sababu ya kila jambo chini ya jua. Mungu hakuahidi mchana bila usiku, hakuahidi milima pasipo mabonde. “When its too dark is when you can see the brigthtening stars” (Unapoona kuna giza nene, ndipo nyota ing’aayo huonekana). Waweza kujiona mwovu, usiye na thamani eti tu kwakuwa fulani uliyemtegeme hayupo au amekuacha na kukuumiza moyo wako. Au umedharauliwa, umetukanwa, umenyanyaswa nk.
Hatuna budi kuelewa ukweli kuwa, hakuna mwanadamu aliye mkamilifu. Kukosea kupo na kutaendelea kuwepo kwa kuwa tunatofautiana katika mitazamo. Usikubali mtazamo wa mtu mwingine dhidi yako ukakukatisha tamaa na kuiona dunia chungu na isiyofaa. Mwenye uwezo wa kukatisha maisha yako au baraka zako ni Mungu peke yake. Mwanadamu anauwezo wa kukuchafulia jina na sifa ili furaha yake itimilike, lakini mwenye kuweza kukufuta machozi  na kubadi mitazamo ya binadamu ni Mungu.
Pateni nafasi ya kukaa peke yenu wewe na rafiki yako wa karibu kuliko wote aitwaye nafsi, maali penye utulivu na kisha tafakarini kwa kina mema yaliyowahi kutendeka kwako, hutakuwa na sababu ya kukata tamaa hata kama yapo mazingira ya kukatisha tamaa. Utagundua wewe ni mtu wa thamani, Mungu hajakuumba kwa bahati mbaya.
Shida dhiki, taabu nk, zisiwe mwisho wa maisha yako bali Mungu mtoa uzima awe ndiye suluhisho la kila swali gumu na jepesi la maisha. “Marufuku kukata tamaa”

                                  
Faida za kutokata tamaa

Zipo faida nyingi za kutokata tamaa katika maisha yetu ya kila siku. Si rahisi sana kuzichambua moja kwa moja na kuzimaliza zote kwa mfano; kinyume cha athari na hasara zote nilizotaja maana yake ni faida;

Tunazoweza kuziangalia moja kwa moja ni kama zifuatazo:

Jamii/Taifa kupata watendaji watakao sukuma maendeleo.
Unaweza kufikiri jinsi ambavyo tumepoteza wafanyabiashara wangapi wazuri, wasomi, wazazi n.k, ambao walishindwa kuendelea kwa sababu ya kukata tamaa.
Lakini kwa kutokata tamaa, tumeweza kupata watendaji wazuri na wengine tumewaona leo hii wamekuwa tegemeo kubwa kwa jamii na Taifa (twaweza kuwaita wngine, wajasiriamali), ni mojawapo ya wao kutokata tamaa.

Kufikia malengo na kukuondoa pale ulipo
Huwezi kupata ufumbuzi wa hali inayokusibu kwa sasa ikiwa utaruhusu hali ya kukata tamaa. Kutokata tamaa ndiyo njia pekee inayoweza kukusaidia ufikie malengo na kuondokana na tatizo linalokukabili kwa sasa.

Kufikia kilele cha mafanikio usiyo yatarajia
Faida nyingine ya kutokata tamaa ni ufikia kilele cha mafanikio usiyoyatarajia.
Kutokata tamaa kunakujengea tabia ya kuwa na juhudi katika kila kitu unachokifanya kitendo ambocho kinakuwezesha kupata njia mbadala ya kufanya mambo yako mengi na hivyo kupata mfanikio mazuri.

Kukujengea heshima katika jamii
Kutokata tamaa hukujengea heshima katika jamii, tangu katika familia yako na nje yake. Pia hukuwezesha kuwa jasiri na hodari, tena wengi hutaka kupata msaada kutoka kwako.


Mifano ya watu waliofanikiwa kwa kutokata tamaa.

Wapo watu wengi mno ulimwenguni (katika agano la kale, jipya na katika kizazi chetu hasa katika bara la Afrika) ambao tunaweza kujifunza kupitia historia za maisha yao na jinsi ambavyo hawakukata tamaa na hatimaye walifanikiwa.

Baadhi ya mifano katika kizazi chetu:

Nelson Mandela

Siyo raisi kukubali kukaa gerezani kwa miaka isiyopungua ishirini na saba (27) kwa ajili ya watu wengi, hiyo ni kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai, mwaka 1918. Ni Rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga ubaguzi. Alifungwa katika kisiwa cha Robben. Baada ya kuachiwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano. Mwaka wa 1993, alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel (ya Amani). Chini ya utawala dhalimu wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini, mzee Mandela aliendelea kuamini kuwa siku moja nchi hiyo ingeondokana na ubaguzi wa rangi, bila kujali kuwa yeye yuko huru au  gerezani hatimaye walifanikiwa kuondoa utawala huo.
Julius K. Nyerere
Tunayo mengi ya kujifunza na kujivunia kwa mwalimu nyerere,
Mwasisi na Baba wa taifa la Tanzania.

Kuzaliwa na Malezi
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa April 12/1922 katika ardhi ya Tanganyika, na alifariki 14/10/1999 mjini wa London Uingereza. Alizaliwa katika kijiji cha Butiama, karibu na pwani ya mashariki ya Ziwa la Victoria. Nyerere alikuwa mmoja wa watoto ishirini na sita wa baba yake, Nyerere Burito. Baba yake alikuwa kiongozi wa kabila la Zanaki. Pia baba yake alikuva na fedha nyingi lakini hakuwa na elimu kubwa.

Wakati wa utoto wake, Julius Nyerere alichunga mifugo na alikuwa na maisha ya kawaida. Nyerere alikuwa mfuasi wa dini ya Katholiki, alihudhuria misa mara kwa mara. Watu wanasema alipenda sana kucheza na kufanya mizaha. Pia alichonga meno yake ya mbele na msumeno kuonyesha utamaduni wa kabila lake.
Elimu
Julius Nyerere alijiunga na Shule ya Msingi ya Serikali katika mji wa Musoma wakati alipokuwa na miaka kumi na mbili. Alimaliza masomo ya miaka minne katika miaka mitatu kwa sababu alikuwa na akili sana, alienda kusoma Shule ya Upili ya Serikali ya Tabora. Huko, alipata udhamini wa kwenda Chuo Kikuu cha Makerere. Ni muhimu kujua wakati alipopata udhamini huo, Makerere kilikuwa Chuo Kikuu cha pekee katika Afrika ya Mashariki.  Wakati alipomaliza kusoma, alipata shahada.


Baada ya chuo kikuu, Nyerere alirudi Tanganyika na alifanya kazi katika Shule ya Upili ya St. Mary katika mji wa Tabora. Shule ya St. Mary, ilikuwa shule ya katoliki. Huko, alifundisha masomo ya biolojia na Kiingereza. katika mwaka 1949, alipata udhamini wa kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Edinburgh, hivyo akawa  mtanzania wa kwanza kusoma chuo kikuu cha nchi ya Wingereza na mtanzania wa pili kupata digrii nje ya Afrika. Katika chuo kikuu cha Edinburgh, Nyerere alipata Shahada ya juu ya Sanaa katika Historia na Uchumi, mwaka 1952. Akiwa Edinburgh, alisoma mkondo wa kufikiri unaoitwa “Fabian.” Mkondo wa “Fabian”, ulijumuisha kundi la wataalamu wa Ujamaa wa Uingereza. Azimio la “Fabian” ni kuendeleza mawazo ya kijamaa. kwa sababu alijifunza mawazo ya “Fabian,” alianza kufikiri mabadiliko mazuri sana yangepatikana ikiwa angeweza kuunganisha ujamaa na maisha ya Afrika. Wakati wa maisha yake, Nyerere aliitwa “mwalimu” kwa sababu ya kazi zake za elimu.

Ndoa na Familia
Kabla ya maisha yake ya kuwa mwanasiasa, alioa mwanamke aliyeitwa Maria Magige. Maria alitoka kabila tofauti. Wanahistoria walisema alioa mwanamke wa kabila lingine kuonyesha dunia, ilikuwa muhimu sana kusahau tofauti baina ya makabila na kuwa wamoja.

Mchango Katika Jamii
Mchango mkuu wa Nyerere katika jamii ni kazi aliyofanyia serikali. Lakini kwanza tusisahau kwamba, Nyerere alikuwa mwalimu wa historia, Kiingereza, na Kiswahili. Huko, alianza shughuli za ki-siasa alipokianza chama cha TANU (TAnganyika African NAtional Union) kupigania uhuru kwa nchi za Tanganyika. Ndani ya  mwaka mmoja tu, TANU ilikuwa na watu wengi wapya na ilikuwa kiongozi wa miradi ya siasa katika Tanganyika. Kwa sababu Nyerere alianza kujihusisha na siasa, hivyo alihitaji kuamua baina ya maisha ya mwalimu au ya mwanasiasa. Alijiuzulu kutoka kufundisha, na kuwa mwanasiasa kwa maisha yake.

Alisafiri ndani ya Tanganyika kuzungumza na watu wengi na viongozi tofauti, kujaribu kupata msaada katika harakati za uhuru wa Tanganyika. Katika mwaka 1954, alifaulu kuunganisha jamii mbalimbali kitaifa pamoja kusaidia harakati za uhuru. Nyerere alikuwa na ujasiri wakuzungumza, ujasiri uliomsaidia alipozungumza na UN (Umoja wa Mataifa) kuhusu uhuru wa Tanganyika. Katika mwaka 1958, aljiunga na Colonial Legislative na alishinda uchaguzi wa Waziri Mkuu katika mwaka 1960.

9/12/1961, Nyerere alikuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Tanganyika. Baada ya mwaka mmoja yaani mwaka 1962, Nyerere alishinda uchaguzi na kuwa rais wa Tanganyika.  Pia, ni muhimu kujua kwamba Nyerere alifaulu kuunganisha kisiwa cha Zanzibar na Tanganyika bara pamoja kuunda nchi ya Tanzania katika mwaka 1964, baada ya mapigano huko Zanzibar yaliyomaliza utawala wa Jamshid bin Abdullah, kiongozi wa Zanzibar. 


Nyerere aliendelea kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mpaka mwaka1985. Akiwa Rais, Nyerere alikuwa na matatizo mengi kwa sababu mwaka 1960, Tanzania ilikuwa nchi maskini sana ukilinganisha na nchi zingine duniani, hivyo kuwa na deni kubwa sana na pia kulikuwepo na mfumuko mkubwa wa bei. Katika kusaidia nchi yake, Nyerere aliamua kujaribu ujamaa na maisha ya pamoja vijijini, na utaifishaji. Aliandika dhana zake katika Azimio la Arusha la Mwaka 1967. Watu walihimizwa kuishi na kufanya kazi pamoja katika vijiji vilivyokusudiwa kusambaza desturi ya utamaduni wa Tanzania na kuunda umoja.


Baada ya shughuli zake za urais, Nyerere aliendelea kusaidia jamii yake. Alikuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Na baada ya miaka michache, aliacha shughuli za kisiasa kwa sababu ya umri wake. Alipumzika katika kijiji chake huko Butiama alipozaliwa. Katika mwaka 1990, lakini hata hivyo, aliendelea kufanya kazi za haki za kibinadamu. Kwa mfano, katika mwaka 1996, alikuwa mwamuzi mkuu wakati wa mgogoro katika nchi ya Burundi. Kwa bahati mbaya, Tar 14/10/1999, alifariki mjini London alipokuwa amelazwa. (Nimezipata habari hizi kutoka katika mtandao wa wikipedia)

 

Ellen Johnson Sirleaf


Huyu ni mwanamama ambaye ameweka rekodi ya kihistoria barani Afrika na nchini kwake Libieria, kwa kuwa Rais wa kwanza mwanamke huko Liberia na Afrika kwa ujumla. Unapotaja nchi kama Liberia, hasa katika miongo kadhaa iliyopita, picha inayoweza kukuingia akilini mara moja ni vita, ubabe, visasi, unyama na kila aina ya maovu. Akijitokeza kwa mara ya kwanza miaka iliyopita ni Ellen katikati ya (kundi) idadi kubwa ya wagombea wa kiume alishindwa katia kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu. Hata hivyo hakukata tamaa, kwani miaka mitano baadaye alifanikiwa kugombea tena na kuwaangusha wagombea wengi, hatimaye kuweka rekodi yake ya kihistoria katika bara la Afrika ambako wanawake bado wanapigania uhuru wa kijinsia, haikuwa rahisi kuamini kama Bi Ellen hatimaye angekuwa rais.
Johnson amekuwa Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika. Hata hivyo yeye sio mwanamke wa kwanza kuongoza nchi barani Afrika. Malikia Zauditu wa Ethiopia aliongoza nchi yake kwa miaka 13 toka mwaka 1917 hadi 1930. Ruth Perry ni mwanamke wa kwanza Afrika kuwa mkuu wa nchi pale alipokuwa mwenyekiti wa urais wa pamoja wa jamhuri ya Liberia toka mwaka 1996 hadi 1997.
Johnson-Sirleaf alihukumiwa kifungo cha miaka kumi jela mwaka 1985 baada ya kushutumu utawala wa kijeshi nchini humo katika kampeni zake za kugombea ubunge. Alitumia kifungo hicho kwa muda mfupi kabla ya kuachiliwa na baadaye kukimbilia uhamishoni hadi aliporudi mwaka 1997 akiwa anafanyia kazi Benki ya Dunia na Citibank.
Johnson-Sirleaf alimuunga mkono Charles Taylor wakati wa mapinduzi yake dhidi ya Jenerali Samuel Doe lakini baadaye alikuja kuwa mpinzani wake mkubwa na hata kugombea urais dhidi yake mwaka 1997. Taylor alimwandama na hata kumpeleka mahakamani kwa madai ya kuhusika na hujma za kihaini.
Uchaguzi wa urais mwaka 2005 ulirudiwa baada wagombea urais kutopata kura zinazoridhisha. Katika raundi ya kwanza Johnson-Sirleaf alikuwa wa pili, wa kwanza alikuwa ni mpinzani wake mkubwa George Weah. Ndipo Katika raundi ya pili ya, Johnson-Sirleaf alitangazwa kuwa mshindi.

Wapigania uhuru

Tunayo mengi ya kujifunza  toka kwa wapigania uhuru hasa wa bara la Afrika kama Julius Nyerere, Kenyatta, Kwame Nkuruma, Keneth Kaunda, Samora machelle, Patice Lumumba na wengineo wengi ambao kwa nyakati tofauti walipitia mateso na manyanyaso mbalimbali na hasa kutoka kwa wakoloni, lakini kwasababu ya kutokukata tamaa, nyimbo za kusherehekea uhuru zilisikiwa barani Afrika.

Baadhi ya mifano ya watu katika agano la kale katika  Biblia:

Tunayo mifano ya watu wengi katika biblia ambao
Kwa njia moja au nyingine, wamepitia katika majaribu, shida, misukosuko nk, lakini kwasababu ya kutokukata tamaa hatimaye walifanikiwa.

Esta
Esta ni binti aliyekuwa yatima (aliyefiwa na Baba na mama)
Na kulelewa na mjomba wake mordekai aliyekuwa mtumwa, aliyechukuliwa mateka kutoka yerusalem. (Esta 2:5-17)

Ilitangazwa mbiu ya mfalme Ahsuero (aliyemiliki nchi kubwa yenye majimbo 127) kwamba atafutwe mwanamwali atakayevishwa taji na kuwa malkia au mke wa mfalme.
Walikusanyika mabinti(warembo) wazuri kutoka katika majimbo yote 127 na kupelekwa maali walipokuwa wakiandaliwa kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya kupitisha mbele ya mfalme. Esta aliposikia mbiu ya mfalme, hakujali kwamba yeye ni yatima tena aliyeishi utumwani na mjomba wake aliyekuwa akifanya kazi ya kulinda mlangoni katika jumba la kifalme. Esta hakuona sababu ya kukata tamaa, bali alijitosa kuwania  nafasi hiyo.

Jambo la kujifunza kwa Esta, hakuona sababu ya kidhiirisha kabila lake wala jamaa lake na hatimaye katikati ya wanawali(warembo) wengi,  Esta akapata kibali machoni pa mfalme.

Ndugu msomaji, Huna haja ya kujiona wewe ni mtu wa chini na kuitangaza hali yako kila maali. Esta hakuona sababu ya kutaja ukoo wake wala kutishwa na wingi wa warembo. Usikatishwe tamaa na mazingira yanayokuzunguka, bali jione kuwa mtu wa maana na wa thamani. Badili mtazamo, siyo lazima wanadamu wakufahamu zaidi kuliko Mungu wako. (filipi 4:6)

Yusufu
Huyu ni kijana wa kiyaudi aliyepitia katika misukosuko na mapito mbalimbali, yakiwemo yakuchukiwa na ndugu zake, huku wakipanga njama za kumuua. Hata hivyo waliamua kumuuza huko misri. Yusufu alimcha Mungu kwa kiwango cha hali ya juu. Uaminifu wake ulimsababisha kufungwa gerezani naye Mungu akampa kibali hapohapo gerezani. Yusufu aliendelea kuwa mwaminifu kwa Mungu hata kwa Wanadamu, pia katika mambo yote hakukata tamaa, hakujali ile hali ya kuwa mfungwa, jambo lililosababisha jina lake kubadilika kutoka gerezani hadi kuwa Waziri Mkuu wa nchi (Mwanzo 37:26-28,36, 39:1-14,20-23).

Ayubu
Tunayo mengi ya kujifunza kwa Ayubu, Mtu aliyekuwa mkamilifu aliyemcha Mungu na kuepukana na uovu. Ayubu alikuwa mtu mkuu kuliko wate katika eneo la Mashariki. Utajiri wake ulikua wa hali ya juu sana. Pamoja na kuwa mwenye haki bado Ayubu alipita katika Majaribu mazito ambayo sirahisi Mwanadamu kuyaimili. Alifiwa na wanaye wote, mali zake zote zilifilisika na zaidi ya yote yeye mwenyewe akaugua kiasi cha kufa. Ndugu jamaa na marafiki walimkejeli, kumdhihaki na kujitenga naye. Chakusikitisha hata mke wake akawa kinyume naye na kumtaka amtukane Mungu. Lakini katika yote hayo Ayubu hakukata tamaa, aliendelea kuwa mwaminifu. Kwasaba-
babu hiyo, Mungu alimlipa ayubu maradufu (Ayubu 42:10-11). Usikate tamaa.       

Njia za kumsaidia aliyekata tamaa

Kimsingi hakuna njia moja ya kumsaidia aliyekata tamaa, tena zilizopo zinatofautiana toka jinsi ya kumsaidia mtu mmja hadi mwingine.

Baadhi ya njia zilizopo ni kama zifuatazo:

Gundua tatizo kisha mshauri
Kumshauri mtu aliyekata tamaa unatakiwa kwanza kujua chanzo cha kukata tamaa kwake. Mshauri kwa kumwonyesha tumaini la kufanikiwa katika lile alilolikatia tamaa.

Usitumie mifano ya walioshindwa katika mazungumzo yenu.
Jitahidi sana kutumia mifano ya Watu walioshida tena waliopitia vipingamizi vingi na vigumu zaidi ili kumtia moyo.

Usionyeshe ugumu wa tatizo kana kwamba halina ufafanuzi au ufafanuzi wa kutisha juu ya tatizo linalomkabili
Rahisisha mazungumzo yako, hata kama ugumu upo lakini usionyeshe kuwa hakuna ufumbuzi. Siku zote tunaamini kuwa chini ya jua hakuna lisilowezekana.Unapomsaidia hakikisha kuwa unafahamu vizuri juu ya lile unalomsaidia.

Uwe mtulivu wa Akili na muelewa ili kugundua tatizo,
ili upatekujua jinsi ya kumsaidia.

 Epuka maneno ya kulaumu juu ya tatizo alilonalo.
Ikibidi yatumie kwa umakini huku ukionyesha matarajio ya mafanikio.

SIRI YA MAFANIKIO
(Jinsi ya kushinda kutokata tamaa)

Halipo jambo moja pekee unaloweza kulifanya sikuzote kwa sababu kama tulivyokwisha kuona, sababu za kukata tamaa hazifanani. Lakini zifuatazo ni baadhi ya hatua unazoweza kuchukua ili uweze kuishi duniani kwa raha kama mototo wa mfalme.
Kufanikiwa au kutofanikiwa ni uchaguzi wako
Mungu amekubariki kuwa na uhuru wa maamuzi, kama vile kuchagua aina ya  maisha unayotaka kuishi. Kama hivyo sivyo, huwezi kuwa na uwezo wa kutumia vipaji vyako ulivyonavyo. Fahamu kuwa, akili uliyonayo ni nyenzo muhimu ya kukufanya ufanikiwe, kwa kufikiri na kutumia vipaji ulivyo navyo kisha kuvifanyia kazi.

Kwa kuwa mafanikio yako yanatokana na akili yako uliyonayo. Endapo utatumia akili, hisia na imani yako kwa busara na kufanyia kazi, ni lazima maisha yako yatakuwa na mabadiliko makubwa ya mafanikio.
Una uhuru wa kuchagua namna unavyofikiri, unavyohisi na unavyoamini ili uweze kusonga mbele, kamwe usikubali kuwa na fikra mgando ambazo hazitakusogeza hapo ulipo.Mafanikio au kushindwa kwako inategemea jinsi unavyofikiri.Kwani afya isiyo njema, hali ya kutokuwa na furaha na umaskini, hizo ni dalili za kushindwa katika maisha ambazo zimesababishwa na kuwaza mawazo hasi. Vile vile akili yenye afya bora na mawazo ya matumaini yanakufanya uwe na afya bora na maendeleo mazuri.


Safisha akili yako kwa mawazo mazuri. Siri ya kushinda katika maisha ni kusafisha akili kwa kuondoa tabia zinazokufanya uharibikiwe, kama vile imani potofu, mawazo hasi na badala yake uwe na tabia zenye kukufanya usonge mbele, kuwa na imani na mawazo ya kujenga na si kukubomoa.
Mara zote kuwa na mawazo ya kukujenga kwa mfano iambie nafsi yako kwamba, utafanikiwa katika mambo yote uliyopanga kufanikiwa.
Mara zote jione upo imara katika kufanikisha mipango yako mbalimbali, uwe mtu unayependa kuwajali wengine, uwe mwaminifu katika shughuli zako pamoja na familia yako.
Ukweli, ushindi na ujasiri ni silaha kubwa ya mafanikio katika maisha yako.
Kamwe usiruhusu mawazo ambayo hayana tija ya maendeleo kwako.
Jifunze kuwa jasiri, usikate tamaa, kuwa mtu mwenye msimamo, penda kwenda na wakati, usilewe na usiwachukie washirika wako katika biashara.
Njia yoyote ya kubadili hali yako ya kushindwa katika maisha ni kubadili mawazo hasi unayofikiria, utakapofanya hivyo utabadili tabia ya kufikiri, kuhisi na kuamini. Utakapobadili tabia yako ya ndani, hata tabia yako ya nje itajibadili. Mawazo yana nguvu. Mawazo ya hofu na wasiwasi ni njia ya kushindwa. Utakaposhinda hali ya kutokuwaza kushindwa, kuwa na hofu au wasiwasi utaweza kukabiliana na hali ya ushindi. Kuna kanuni moja inayotawala mawazo. Huwezi kufikiri kitu hiki na kuzalisha kingine. Mara kwa mara, hali ya kushindwa inaweza kukujia ili kukujaribu. Ni wakati wako wa kutumia akili kwa vitendo ili uishinde hali hiyo. Madhara ya kushindwa katika maisha yanaweza kukuletea hali ya uharibifu, imani potofu na mawazo hasi pamoja na hisia za maisha yako. Kwa maelezo mengine, hali hiyo inakufanya ukose furaha, uwe mpweke, kukosa adabu, kuwa na uamuzi mbaya, magonjwa ya mara kwa mara yasiyoeleweka, kuchanganyikiwa na hali ya kushindwa. Hali ya kufanikiwa inakufanya uwe na furaha, maendeleo mazuri, kujiamini, matumaini, amani katika moyo, umoja katika familia, mafanikio kibiashara, busara, ukweli na upendo.
Mwanadamu anaweza kufanikiwa mara nyingi kadiri anavyoielekeza akili yake kufikia mafanikio hayo.
Kila kazi au uzoefu wa mtu anaoupata ni somo muhimu katika maisha yake, kama atautumia vizuri, ataweza kukamilisha malengo yake.
Mwanzoni katika kufikia mafanikio yako, unaweza kufanikiwa mara moja na kushindwa mara nyingi. Hivyo ni vema kuitumia akili yako vizuri katika kufikia mafanikio. Elekeza umakini wako wote katika kukamilisha malengo uliyojiwekea. Hiyo ni moja, mengine yatafuata.
Kama ulifanikiwa mara moja, unaweza kufanikiwa mara ya pili, ya tatu na ya nne au mara nyingi kadiri unavyojipanga katika akili yako. Jambo la muhimu ni kuelewa wewe ninani na zaidi kila unachokifanya hakikisha kinadumu, kinaimarika, si kuanzisha biashara ya duka leo, kesho ukaanza mradi mwingine kabla ya ule wa kwanza kuimarika. Kama ni biashara, kama ni huduma n.k hakikisha imeimarika na kukuwekea historia.
Ili uwe na mafanikio maishani mwako ni vema kuwa na nidhamu katika hisia zako. Kwa kuwa, kupitia hisia zako mbalimbali unajifunza vitu vingi.
Hivyo basi, endapo hisia zako zitalenga kwenye mafanikio utafanikiwa, kama zitakuwa kinyume cha hapo, matokeo yake utakuwa huna furaha, huna afya njema, utahisi upweke, kuchanganyikiwa, hofu na vitu vifananavyo na hivyo.
Ili ufanikiwe unatakiwa kuwa na digrii ya uvumilivu. “Kujua jinsi ya kusubiri ni siri kubwa ya mafanikio,” anasema Joe Main.
Kila jambo haliji kwa wakati mmoja, kupanda milima kunahitaji ujasiri, ustahimilivu, nidhamu, imani na subira. Hivyo utafanikiwa. Ukosefu wa uvumilivu inaonyesha ni ukosefu wa nidhamu ya kufikia mafanikio yako.
Kwa wote wanaotaka mafanikio, wasipokuwa wavumilivu watasababisha vikwazo na kuchelewesha mahitaji yao.
Hivyo kama mambo yako hayatakwenda kama ulivyotarajia, yakupasa uwe mvumilivu. Mambo yako hayawezi kwenda kama unavyotarajia bila kuwa na subira, kwani kila hatua mbele, hata kama ni ndogo, ni hatua moja ya kusonga mbele.
Jifunze fani ya uvumilivu, hiyo ni pamoja na kuwa na nidhamu katika mawazo yako , kipindi kile unapopatwa na hali ya wasiwasi ili kufikia malengo uliyojiwekea. Kwani, hali ya kutokuwa na uvumilivu inakuletea hofu, wasiwasi, kuvunjika moyo na kushindwa katika malengo yako. Uvumilivu unakujengea hali ya kujiamini, ushindi na matokeo mazuri. Kila mmoja anapata mafanikio anapokuwa na tunda la uvumilivu.
Kila mmoja anapenda kufanikiwa, hata katika maisha yetu ya kawaida kuna mambo ambayo ni madogo madogo lakini ukiyazingatia yatakufikisha kwenye mafanikio yako. Mambo hayo ni pamoja na kuwathamini wengine na kuwafanya nao wakuthamini katika kufikia malengo yako ya maisha. Pia kuwaonyesha wengine kuwa unawapenda. Anza na mke wako, familia yako pamoja na rafiki zako. Vile vile wafanye wengine wajisikie ni wa muhimu kwako. Kamwe usikosoe pasipo ulazima wa kufanya hivyo. Hakuna mtu anayependa kukosolewa pasipo na sababu, kosoa kwa kumjenga yule unayezungumza naye na kisha msifu unapomaliza kuzungumza naye.
Mara zote heshimu kila mtu, Salimia watu kwa tabasamu na pale unapokuwa na marafiki zako, kamwe usisengenye wala kuwa na tabia tofauti na wenzako.
Jitahidi kukumbuka majina ya watu, kwa kuyataja kwa usahihi na mara zote mpe heshima yake kama ni bwana, bibi, dada, profesa, daktari au bosi. Kunapokuwa na mazungumzo kamwe usiingilie kati, kwani mazungumzo mazuri ni kupeana nafasi na kuzungumza kwa mpangilio. Penda kusikiliza wengine na changia pale inapokubidi kufanya hivyo.
Mara zote penda kuwasaidia wengine, katika kutoa ushauri wa mafanikio na kuwaelekeza njia sahihi kwa wakati muafaka. Vile vile unapokuwa na wenzako usijione wewe ni bora kuliko wengine, kwa kuwa hakuna mtu hata mmoja aliyekamilika. Kwa kufanya hivyo utajikuta upo kwenye kundi la watu waliokuwa na mafanikio. Kwa sababu unaweza kuwa na bidii katika maisha yako na kufanikiwa lakini ukawa hauchangamani na wengine, hivyo kuona mafaniko yako ni bure mbele ya jamii inayokuzunguka
MAFANIKIO hutokana na jitihada katika maisha tunayoyaishi. Watu wengi wanaopenda kufanikiwa mara zote hutafuta mbinu mbalimbali ili kutimiza ndoto zao. Hivyo basi unatakiwa kuota ndoto ya mafanikio yenye malengo makubwa.
Binafsi ninaamini katika malengo hayo kuwa kuna mafanikio endapo utamaanisha. Wakati mtu anapoanza kuwa na malengo makubwa, anaanza kwa kufikiri jinsi Mungu alivyomwezesha katika jambo hata kufikia hatua na kufanikiwa. Ndoto hiyo ya mafanikio haina gharama, ni jinsi ya unavyoweza kujipangia muda na ratiba zako. Kumbuka ukiwa na malengo ya mafanikio haitakugharimu chochote.
Unaweza ukawa na malengo ya kuanzisha mradi mkubwa pasipokuwa na fedha, inabakia kuwa ni ndoto tu. Mungu alianza kuumba dunia ikiwa haina kitu. Tunaweza kuwa na malengo makubwa ya mafanikio katika maisha yetu, haijalishi ni ya aina gani.
Unapokuwa na ndoto hiyo ya kutaka kufanikiwa, kamwe usiruhusu moyo wako kuvunjika au kuwa katika hali ya kukata tamaa na wasiwasi. Kwani hali hiyo itakudhoofisha na kukufanya usisonge mbele, bali urudi nyuma.
Unapohitaji jambo kubwa kutokea katika maisha yako unatakiwa kuwa na maono mapya. Kumbuka hata wewe unaweza ukawa na maono makubwa ya ajabu. Haijalishi ni mtu wa aina gani, umetoka wapi au umepatwa na jambo gani, katika hali uliyonayo unaweza kuwa na maono mapya. Kumbuka malengo makubwa hayawi kwa watu waliofanikiwa, bali ni kwa wale wanaotaka kufanikiwa.
Vyovyote uwazavyo, ndoto inainua na kuweka kitu kipya katika maisha yetu, inatutengeneza na kutusogeza mbele, inatuwezesha kufikia malengo makubwa tofauti na ilivyokuwa awali. Inatuwezesha kufanya kitu kikubwa ambacho hatujawahi kukifanya tena kabla ya hapo.
Je, wataka kuwa fulani? Kusimama nje ya kusanyiko kubwa? Kukumbukwa? Hali hiyo inakuwepo ndani ya mioyo yetu inayodunda na kutaka kupata siri ya mafanikio.
Tunataka kuwa fulani. Inawezekana, ndiyo inawezekana. Mungu ametoa kwa kila mtu uwezo na vipaji mbalimbali. Wakati Mungu anakuumba alikupa kipaji na akasema kama utatumia kipaji ulichonacho atakiongeza, na kama hutatumia kipaji ulichonacho utakipoteza. Kukitumia kipaji chako au kukiachia ni juu yako wewe!
Dunia yetu imejaa vipaji vingi na uwezo ambao hautumiwi. Unatakiwa kulima kwa bidii, na kupalilia ili upate mavuno bora. Tumia kipaji chako kabla hujakipoteza.
Unaweza kudhani kuwa hauna kipaji chochote, si kweli, labda inawezekana haujagundua kipaji chako. Inawezekana umekiweka kipaji chako kabatini. Amini kuwa kila mmoja anacho kipaji chake alichopewa na Mungu.
Waweza kutumia kipaji ulichonacho au kukipoteza. Maisha yetu yamejengwa katika kanuni hiyo. Kuna mifano mingi ya kupoteza au kupata, hiyo ni kanuni ya kawaida.
Chukua hatua ambazo zitaifanya ndoto yako kuwa kweli. Ota ndoto yenye thamani katika maisha yako. Kama hauna malengo, haitawezekana matarajio yako kutimia. Ndoto inaanza unapokuwa na wazo. Kumbuka watu huvutiwa na wenye maono makubwa. Chagua maono yenye matarajio. Baadhi ya watu wanapoteza muda wao kwa kuwa na malengo ambayo hayatawasaidia. Mfano, kuna kijana katika miaka iliyopita alisaidiwa kupewa ushauri baada ya kupoteza muda wake mwingi akifikiria ni jinsi gani ataweza kumpata mke wa jirani yake na kumfanya awe wake. Ndoto yake hiyo haikuwa ya thamani ya muda mrefu.
Wakati wazo linapokujia katika ufahamu wako, iulize nafsi yako maswali matatu. Je, jambo hilo litampendeza Mungu? Litawasaidia watu wanaoteseka? Kwa maneno mengine litakuwa msaada kwa watu? Litaleta mafanikio mazuri kwako? Kama jibu lako ni ndiyo katika maswali yote, utakuwa na maono yenye mafanikio.
Unapoamua kufanya jambo fulani, usijiulize ulize kuwa hii ni njia nyepesi ya mafanikio? Au ni njia rahisi? Inaweza kuwa na usalama? Haitakuwa na vikwazo? Hakuna utakachoshindwa utakapofanya bidii. Hakuna mwenye nguvu ya kuua ndoto yako, isipokuwa wewe mwenyewe.
Panga mipango vizuri kwa kuwa huwezi kujenga bila ramani. Huwezi kufanikiwa matarajio yako pasipokuwa na malengo makubwa. Ninamfahamu mtu aliyekuwa na maono makubwa lakini yalikuwa hayafiki mbali. Ni kwa sababu alikuwa hana ramani ya maono yake.
Hakikisha unatimiza ndoto uliyojiwekea. Malengo yako hayawezi kufanikiwa kama hujajitoa kufanya hivyo. Ili kufanikiwa katika mipango yako unahitaji juhudi na kufanya kazi kwa bidii ili upate mafanikio.
Amua pa kuanzia. Fanya uamuzi sahihi. Panga muda wa kuanza. Usitafute sababu ya kuacha kufanya malengo yako kwa muda ulioupanga. Katika dunia yetu kuna watu wengi wenye mipango mingi lakini hawaifanikishi. Jiondoe katika kundi hilo. Fanya kitu. Andika barua, piga simu. Anza hatua ya mafanikio.
Jiamini waweza kutimiza ndoto zako. Wakati unajaribu kupata mafanikio utaona kuwa ni kipindi kigumu kwako. Hali ya kukata tamaa inakuwepo katika moyo wako, ikisema jiondoe katika hatua ambayo unataka kuianza ya kupata mafanikio katika maisha yako, kataa.
Kama unakutana na kipindi cha majaribio katika biashara, ndoa, mambo yako binafsi, kwenye wingi wa watu au hali ya maisha uliyoizoea na uko tayari kukabiliana nayo, songa mbele usikate tamaa.
Unachofanya ni kujaribu kupata mafanikio, tena mafanikio makubwa. Katika kila mafanikio unayoyapata, kuna gharama ya kulipa. Kumbuka huwezi kupata ushindi bila kulipa gharama.
Lucy Ngowi
www.ngowil.blogspot.com
lcyngowi@yahoo.com

MAMBO YAFUATAYO YATAKUFANYA UFANIKIWE MAISHANI

  • Jinasue katika mikono ya watu wabaya au mazingira mabaya
yanayoweza kukukatisha tamaa

Utafiti unaonyesha asilimia 80 ya kufanikiwa kwa Mwanadamu kunategemeana na marafiki wanaokuzunguka au unaoambatana nao muda mrefu.
Hunabudi kuugawa ulimwengu katika sehemu mbili (you’ve to divide the world into two parts). wanaokupenda na wasiokupenda na kutofautisha kati ya wanaokusifu na wanaokuponda. Wajapokuwa wapo wanaokununia ila si wote wanaokuchukia. Hivyo jaribukuongeza marafiki pale panapostaili na kupunguza maadui pale inapobidi. Hunahaja ya kujiona kuwa umefika ukingoni mwa maisha kisa watu, vitu, mazingira au maisha yamekuendea visivyo. Yupo Mungu anayekupenda, acha kunung’unika, kulaumu na kulialia, use the stumbling stones to be your stepping stones (tumia mawe uyaonayo kwayo unajikwaa kuwa mawe ya kukanyagia)

Hivyo jiondoe kwenye makundi yasiyokuwa na mwelekeo.
Mfano, kama ulikuwa mvuta bangi, kahaba, kibaka, jambazi au watu wenye mwazo ya kushindwa n.k, usijihusishe tena na makundi hayo. Kumbuka ukipanda basi la wauza samaki, hata kama umejipulizia marashi yanayonukia, utajikuta unanukia harufu ya samaki. Hivyo ukitaka kuwa mfanya biashara kaa au ambatana na wafanya biashara, ukitaka kuwa mwimbaji kaa au ambatana na waimbaji.

  • Hofu ni adui wa mafanikio (kataa hofu)

Najua yapo matatizo yaliyoikumba dunia, na mengine bado yanaendelea kuisumbua siku baada ya siku. Matatizo hayo ni kama vile njaa, vita, magonjwa na majanga mengineyo. Matatizo hayo yote serikali za dunia ikiwamo serikali yetu ya Tanzania huchukua hatua za dhati pamojakutahadharisha raia wake. Pamoja na hayoyote lipo tatizo sugu tena linasumbua na kuumiza dunia katika kiwango cha kutisha nalo si jingine ni hofu! Kama vile mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali yanavyotahadharisha watu dhidi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi nami natoa tahadhari dhidi ya hofu.
Sisi kama binadamu tuliokamilika hatuwezi kukosa kuwa na vihofu vidogo vidogo katika maisha. Hofu inakuwa tatizo pale maisha yetu yanapotawaliwa na hofu za ziada. Hofu ambazo hutufanya tuishi duniani kwa dharura. Kila kitu kwetu kinakuwa ni dharura, matokeo ya dharura hii mara zote yanakuwa machungu kwetu.
Mshindi wa nishani ya Nobel katika dawa za binadamu, Dk. Alexis Carrel, alisema “Wafanyabiashara na wafanyakazi ambao hawana maarifa ya kupambana na hofu hufa wangali vijana”. Naye Dk. O.F. Gorben alieleza juu ya athari za hofu anasema “Asilimia sabini ya wagonjwa wanaokwenda kuwaona waganga na madaktari, wangeweza kuponya nafsi zao kutokana na magonjwa kama wakifanikiwa kuondokana na woga na hofu.”
Anaendelea kusema “Usidhani kwamba ninamaanisha kwamba magonjwa yao ni ya kufikirika” magonjwa yao ni halisi kama vile maumivu ya kichwa na meno na mengine ambayo ni hatari sana . Magonjwa yanayosumbua kama vile vidonda vya tumbo, matatizo ya moyo, maumivu ya kichwa na baadhi ya aina za kupooza.
Woga husababisha hofu. Hofu humfanya mtu kutotulia na kuvunjika moyo (kukata tamaa), hali ambazo huathiri neva za tumbo na mabadiliko haya huifanya juisi ya gastric (gastric juice) ya tumbo kuwa isiyo ya kawaida (abnormal ) kutoka katika hali yake ya kawaida (normal) katika utendaji wake wa kazi. Kutokana na mabadililiko haya vidonda vya tumbo humpata mtu husika. Tatizo la vidonda vya tumbo limekuwa sugu na lenye kuwasumbua watu wengi leo. Pamoja na kuwepo matibabu ambayo naamini katika hali ya kutokuamini kama yanaweza kuisaidia kuleta nafuu! Ufumbuzi wa tatizo hili ni mtu kujifunza kukabiliana na hofu za ziada tunazokumbana nazo.
Dk. Joseph F. Mountague katika kitabu chake cha ‘Nervous Stomach Trouble’ anasema “huwezi kupata vidonda vya tumbo kutokana na kile unachokula bali utapata vidonda vya tumbo kutokana na kile kinachoila nafsi yako”. Waweza kuishi ukiwa na vitu vinavyokufanya uliwe kila siku. Woga, hofu, chuki, uchoyo kupindukia na uwezo duni wa kuitazama dunia na mambo yake katika hali halisi. Haya ni baadhi tu ya mambo yanayokula watu. Kwa kiasi kikubwa husababisha udhaifu wa matumbo yao ambao huleta vidonda vya tumbo. Jamani nazidi kupaza sauti – vidonda vya tumbo vinaweza kukuua. Jifunze kushinda hofu ili uwe salama.
Plato anasema “Kosa kubwa wafanyalo madaktari ni kujitahidi sana kutibu, ili kuponya miili wakisahau kukabili ili kuponya akili ya mgonjwa. wakati akili na mwili ni kitu kimoja, hivyo haitakiwi kupata matibabu vikiwa vimetengwa”
Wazo la Plato limechukua muda mrefu hadi wanasayansi wa tiba kukubaliana na ukweli mkubwa ulio ndani yake. Ndiyo sababu leo kuna jitihada kubwa za kuanzisha tiba mpya iitwayo psychomatic medicine. Tiba itakayotumika kuponya akili na miili kwa pamoja.
Yapo magonjwa mengi yasababishwayo ma vimelea vya magonjwa. Magonjwa kama vile kimeta, kipindupindu, homa ya manjano na mgonjwa mengi hatari yanayowapeleka watu wengi makaburini kila kukicha, lakini vilevile ipo idadi kubwa ya watu wanaoharibu miili yao na hata maisha si kwa vimelea vya magonjwa bali kwa mihemko ya hofu, woga, chuki, aibu kupita kiasi na kukata tamaa. Majanga yasababishwayo na magonjwa ya mihemko yanakua na kusambaa kwa kasi ya ajabu (catastrophic rapidity).
Hofu yaweza kumzeesha mtu kabla ya siku zake. Huweza kuharibu sura na kuifanya ichakae haraka. Hofu yaweza kubadili rangi ya nywele kutoka katika hali yake ya kawaida na wakati mwingine zaweza kunyonyoka kabisa, na kucha upara! Si wote wenye vipara wana hofu za ziada.
Kama ukitaka kuangalia athari za hofu, huna haja ya kwenda mbali hapo usomapo makala haya, jirani yako yawezekana kuna nyumba ambayo wamiliki wake wameathiriwa na kuvunjika moyo. Na hapo jirani kuna mtu anahangaika na kisukari, wakati wengine wanahangaika hawana sukari, yeye imezidi katika damu na mkojo wake.
Hofu yaweza kusababisha meno kuoza. Dk. William I.L. McGonigle anasema “Mihemko yenye kuumiza kama hofu, woga hasira, chuki, uadui, uchoyo, wivu huweza kuharibu uwiano sahihi wa madini ya kalsham mwilini. Uwiano sahihi wa madini haya hufanya meno na mifupa kwa imara. Uwiano wa madini haya unapovurugwa meno huoza na mifupa kutokuwa imara. Wakati mwinge huweza kuleta matatizo ya ngozi, miwasho na hata malengelenge katika ngozi.
Kubwa zaidi ni ugonjwa wa moyo. Huyu amekuwa ni muuaji hatari namba moja duniani kwa sasa. Huyu ni muuaji mkimya anayetesa watu. Sababu kubwa ni watu kuishi kwa hofu na kuishi maisha yasiyo na utulivu wa ndani. Kutokana na hali hii Dk. Carrel alisema ‘wafanyabiashara ambao hawajui jinsi ya kukabiliana na hofu hufa mapema’. Mungu anaweza kusamehe dhambi zetu, lakini mfumo wa fahamu haujui kusamehe. Mara utendapo kinyume na matarajio yake matokeo hupatikana bila ajizi, yawe ni mazuri au mabaya. Ndiyo sababu vilio vya watu kujiua kwa sumu au kujinyonga kunasikika kila kona. Kisa nini? Hofu.
Ndugu msomaji, unapenda maisha? Unapenda kuishi maisha marefu na kufaidi afya njema? Yajaribu haya machache uone matokeo yake. Tunza amani ya ndani kabisa ya moyo wako hata kama unazungukwa na vurugu za kutisha nje yako. Jitahidi kuishi kama wewe katika miji iliyojaa machafuko na maisha ya kukogana. Kwa kufanya hivyo waweza kupata kinga dhidi ya kuvunjika moyo. Unapopitia nyakati ngumu katika maisha apa kutoka ndani! Kwamba hutahofu! Hutaogopa! Hutaomboleza na kumwaga machozi! Jiambie, kama kuna jambo la kukumbuka na kulifanyia kazi ni kuamini katika ushindi! Epuka dhana za kushindwa na maanguko maishani.
Jitahidi kuitafuta tabasamu yako iliyopotea. Tumia gharama zote ili utabasamu. Ni jambo la kushangaza kwamba tabasamu la dhati lisilo lakinafiki huweza kuponya kansa. Huu waweza kuwa muujiza kwako. Kumbuka, hali ya akili yenye uchangamfu, utulivu, amani na furaha husaidia mwili kupambana na magonjwa. Jifunze kukabiliana na changamoto za maisha kwa utulivu, kimbia kutoka katika kujihofia na kuhofu. Jiulize kuna ubaya gani kukabiliana na tatizo kwa utulivu. Jiandae kukabiliana na mambo mabaya na magumu wewe mwenyewe inapobidi. Chagua kuishi na epuka zawadi chungu za hofu. (From Mr Marwa Magori )


  • Ambatana na rafiki bora na sio bora rafiki
                (sio wote marafiki, wengine wanafiki)

Methali 18:24, 13:20
Hunabudi kujiongezea marafiki wazuri pale inapostaili
na kujipunguzia maadui pale inapobidi. Inawezekana kabisa katika mazingira fulani, rafiki yako uliyemtegemea sana na kumweleza shida zako akawa adui, na yule uliyemuona kama adui yako akawa rafiki. Swali huja, unafanyaje pale uliyemtegemea na kumweleza siri zako ukidhani atakusaidi, anapokugeuka na kuwa nyundo ya kukuponda na kukutangaza !

Methali moja ya kingereza inasema “keep company with those who make you batter” yaani ambatana na wale wanaokufanya uwe bora zaidi.

Rafiki mwema ni yule:
-          Anayekuhamasisha upate matokeo bora katika maisha yako, sawasawa ama zaidi yake, ni yule anayekuchochea ufanye vizuri zaidi.
-          Ambaye kwa wema wake wote, amejitoa kuwatumikia watu wengine
-          Ambaye anakusaidia kwenda mbali zaidi
-          Anayetamani siku zote uishi maisha yanayompendeza Mungu na wanadamu
-          Anayetunza siri za wengine na muaminifu.

Hakuna sababu ya kuendelea kuambatana au kung’ang’ana kutumia muda wako mwingi na marafiki wasioweza kukufanya kuwa mtu bora zaidi, badala yake wana kupumbaza, wanakudumaza, wanakurudisha nyuma na kukupotezea wakati wako na rasilimali zako.
Achana kabisa na vijiwe au watu wenye tabia ya majungu, fitina, chuki, uzushi na masengenyo, wenye tabia ya ulevi, utapeli, uongo, uzinzi au washerati nk. Hawawezi kukusaidia  kufika maali popote pa maana katika maisha yako. unapokua na mtu mwenye tabia ya kusengenya wengine, basi jua kwamba siku moja atakugeuzia kibao na kukusengenya akiwa na watu wengine. Jitafutie marafiki  wachache ikibidi, lakini waaminifu, waadilifu na ambao kila mtu ametenga wakati kwa mambo yake. Keep away from people who try to belittle your ambition  Yaani jitenge na wenye dharau, wanaoyafanya malengo yako ya siku za baadaye yaonekane kuwa ni madogo. Ambatana na watu watakao kutia moyo, watakaokushika mkono kwa hali na mali na kukuinua juu.

Inawezekana kabisa urafiki ukavinjika, hata hivyo hauvunjiki hovyohovyo, lazima ziwepo sababu za msingi zilizosababisha kuvunja urafiki. Hivyo ni jambo la busara kuvunja urafiki wa aina yoyote ambao unaonekana haufai. Pia marafiki hawabadilishwi kama nguo. Ukiwa na tabia ya kuachana na marafiki mara kwa mara na kujiunga na wengine, hatimaye utajikuta huna hata rafiki mmoja.

·         Kuwa na shauku ya kufanikiwa

Mafanikio yoyote ya mwanadamu yanategemea na shauku uliyonayo.
Ukiwa na shauku kubwa na mafanikio yako yatakuwa makubwa, ukiwa na shauku ndogo na mafanikio yako yatakuwa madago.

Shauku itakupa njia, akili, au mbinu za kufanikisha mambo yako.
 Tatizo kubwa katika jamii yetu, watu wamekaa mkao wakutokuwa na wazo au ndoto la kutoka hapo walipo. Tangu ulipoanza kulipwa mshahara wa laki moja tangu miaka kadhaa iliyoita basi akili zako zimekwamia hapohapo n a huku maisha yanapanda. Watu hawana akili ya kuwa na vyanzo vingi vya mapato. Watu wa kizazi hiki wamekaa mkao wa kuonewa huruma, kulalamika au kulahumu.

    • Anza na kidogo ulichonacho huku ukiwa na mawazo ya kufanya makubwa zaidi

Inashangaza kouna mtu anweka pesa yake ndogo Benki huku akisubiri iongezeke ndipo aanze biashara. Kumbuka pale benki pesa haiwezi kujizalisha yenyewe.

Inawezekana unampango wa kujejenga nyumba yenye gorofa  nyingi huku uwezo wako ukiwa bado hautoshi, wewe anza tu, maana yawezekana unapoanza msingi tu tayari watu wakaanza kuzuiya vyumba vya biashara tena kwa pesa.

Mungu wetu anaweza mambo yote, lakini bado hutumia vitu au mambo madogo ili kufanya makubwa zaidi. Alimwambia Musa unanini mkononi, kwa mtazamo wa kibinadamu, Musa asingewaza hata siku moja kwamba kwa kutumia fimbo au kijiti tu bahari ya shamu ingegawanyika na taifa la Israeli wakavuka.Usidharau hicho ulichonacho maana ndicho kitakachokuvusha na kukupeleka maala pengine. (Methali 13:11)

Kuanzia leo usidharau kile kidogo ulichonacho, kiwe kipaji, karama, mtaji mdogo au hata wazo fulani, washirikishe hata watu wengine utakaoona wanafaa.

  • Jifunze kwa Watu waliofanikiwa (Waliokuwa na hali ngumu kama yako au zaidi)


Hii ni hatua muhimu sana ili ikusaidie kuamini kwamba hata wewe unaweza kufanikiwa kama wao. Ni muhimu ufahamu kuwa, hujazaliwa peke yaku duniani na kilema ulichonacho, si wewe peke yako duniani mwenye mazingira ya kukatisha tamaa. Wapo waliokutangulia na wameishinda hali hiyo. Wala si wewe peke yako binti aliye haribiwa maisha na kutelekezwa na wanaume ukaachwa peke yako, wapo wenzako lakini pamoja na hali hiyo wamefanikiwa katika maisha hata kujijingea hashima kubwa. Kumbuka si wewe mume au mke pekee uliyeachwa na mwenzio na watoto.  wapo wenzako waliowahi kupitia hali hiyo na bado wakafanikiwa kufanya yanayotama- nisha kuiga. Hata leo tunazo shuhuda nyingi za watu waliougua Magonjwa ya kutisha ka vile UKIMWI, lakini hawakukata tamaa, waliigeuza hali hiyo wakaitumikia jamii kwa namna ambayo haifai kusahaulika. Naamini  hata wewe hutakata tamaa na maisha.

Wapo watu wengi katika jamii inayokuzunguka ambao unawafahamu, juzi walikuwa watu wa kawaida lakini leo hii wamefanikiwa. Jifunze kwa watu hao, taka sana kujua njia halali walizotumia hata wakafanikiwa.

Kumbuka kufanikiwa haimaanishi kuwa na pesa tu, watu waliyoweza kuishi kwa kuifaidi jamii ndio watu waliyofanikiwa, na ujifunze kutoka kwao. Jifunze ni nini kilichowawezesha kufikia malengo yao. Jifunze kutokana na mafanikio yao na kutokana na makosa yao ili wewe usiyafanye.

Hebu  andika malengo yako unayotaka kuyafikia baada ya muda fulani, chukua lengo mojawapo; Jiulize ni nani katika jamii yako au nchi yako ambaye unaweza kumuona au kuwasiliana naye aliyetimiza lengo kama hilo. Ni vizuri akawa ni mtu ambaye walau una uhuru wa kuhojiana naye! Labda amefanikiwa katika biashara fulani,  huduma fulani, kampuni fulani, labda ni sanaa fulani n.k. Wasiliana naye na umueleze nia yako ya kutaka kujifunza kutoka kwake na umuombe akupe muda wa kuongea na wewe.

Akikubali, jiandae vema kabla hamjaonana. Hakikisha una karatasi na kalamu ya kuandi mambo ya msingi atakayokueleza au utakayojifunza mwenyewe. wakati wa kuzungumza naye waweza kuwa na mengi ya kumuuliza ila yapo yamsingi kama:
-          Ni nini kilikuwezesha kufika hapa ulipo sasa?
-          Ni ni watu gani waliokuwa msaada kwakosana?
-          Ni watu gani au nini hasa kilichokuwa pingamizi kwako ?
-          Ni nini umewahi kufanya (kukosea) ambacho kwa sasa unatamani laiti usingekifanya ?
Kumbuka  kuwa wewe ni mtu wa thamani, siku moja unaweza kuwa kama wao na zaidi. Tunajifunza kwao kwa kukubali ukweli kuwa wametutangulia tu kufanikiwa na sio kwamba wao ni tofauti na sisi.

Nina uhakika kuwa wapo watu waliopata mafanikio kwa njia ya haki. Hivyo ukimaliza kwa mmoja, waweza kwenda kwa mwingine na kwa mwingine. Usika- tishwe tamaa na wabinafsi wachache utakaokutana nao, maana nao wapo! unapo jifunza kwa wengi, ndipo unapozidi kupunguza uwezekano wa wewe kuyarudia makosa yao na kuongeza fursa za wewe kufanikiwa zaidi. Bila shaka utakutana na watu waliokuwa na hali ngumu kimaisha kuliko wewe na wamefanikiwa.

Hebu jiulize fukara aliye mkasirikia Mungu na kumnunia eti kwasababu amemuomba ampe viatu vizuri vya kuvaa na hajampa, alafu anapita njiani na kukutana na kiwete ambaye asiye  hata na hivyo vifundo vya miguu vya kuvalia hata hivyo viatu ! unadhani huyo fukara hatarudia kumshukuru Mungu kwamba heri yeye? Nakuhakikishia pamoja na hali yako, unaweza kubadili mtazamo wako, mawazo yako, kunena kwako hatimaye ukawa na mafanikio. Usikate tamaa.


  • Soma vitabu na vyanzo vingine vya habari vinavyokupa mitazamo ya mafanikio maishani

Ninalo ombi kwa watanzania na watu wote, wawe na tabia ya kujisomea vitabu. Kuna hekima na busara nyingi sana katika vitabu, kumbuka, kwa njia ya kusoma vitabu, tunakutana na mawazo ya watu ambao wala tusingetarajia kukutana nao kamwe. Ni watu ambao hatuna hadhi ya kuketi nao meza moja tuzungumze. Ni watu wakuu na wa kuheshi- mika sana duniani. Au na watu ambao tungetamani kupata mawazo yao yatusaidie maishani lakini wameshakufa. Kwa bahati nzuri, waliyaweka mawazo yao na uzoefu wao katika maandishi. Tunayapata huko. Wanazuoni na waandishi wengi wa Kitanzania husema Watanzania wengi hawana tabia ya kusoma vitabu, kuna ukweli katika hilo, lakini tubadilike. Maana kupitia vitabu, tunafurahia ushirika na akili zilizobarikiwa, katika vitabu , watu wakuu uongea nasi, hutupa mawazo yao ya thamani sana, na kutumiminia mioyo yao bila hiana. Mungu na ashukuriwe kwa vitabu. Vitabu ni sauti ya walio mbali na waliokufa, hutufanya sisi warithi wa maisha yao kwa busara zao.

Ninakushauri, soma vitabu vya hadithi uwezavyo. Si lazima uwe na pesa za kununua, zipo mbinu nyingi za kupata vitabu. Unaweza kuwa mwanachama wa maktaba zenye vitabu vizuri kwa gharama kidogo sana. Pia tafuta marafiki, wapendao kusoma vitabu, wafanye marafiki zako. Tabia kubwa ya watu kama hao, huwa wana vitabu vingi vizuri au wanajua vinapopatikana. Unaweza kuazima vitabu vya marafiki, pia jadiliana nao kuhusu mawazo uliyoyapata kwa kusoma. Tafakarini pamoja. Peaneni mbinu za kuyakabili maisha kwa kutumia mawazo mliyoyapata vitabuni.
Chagua vitabu vizuri vya kusoma. Ni vizuri kusoma kila kitabu kipitacho mbele yako na kila habari upatayo kuwa ina faida – lakini sirahisi kuwa na muda wa kusoma kila kitabu. Hivyo kwa nia njema, ni vyema uwe na lengo unaposoma vitabu ili uwezekucha- gua vitabu vinavyofaa kwa wakati huo. Kwa kuwa tunazungumzia nama ya kusaidia akili yako kuamini kuwa hata wewe unaweza kufanikiwa kama walivyifanikiwa wengine. basi, tafuta vitabu vinavyoelezea maisha ya watu waliofanikiwa  maishani; vinavyoelezea walikotoka na jinsi walivyofanikiwa (Autobiography).

Kwa sababu watanzania wengi si wasomaji wa vitabu – hata wasomi! – sio wengi pia walioandika vitabu vya aina hii, lakini vipo. Nenda maktaba waeleze aina ya vitabu unavyotaka kusoma watakusaidia au waulize wasomaji wa vitabu. Na kama wewe unafahamu kusoma kiingereza, hivi viko vingi sana.

Kipo kitabu ambacho mimi binafsi nimekipenda kuliko vitabu vyote! Kina hekima na busara zote unazohitaji – kibiashara, kimausiano, kiroho na kwa maisha ya kawaida kabisa ya kila siku! Kitabu hiki ni BIBLIA. Nimugundua hekima zote zipo ndani yake. Kwa wanaofahamu historia ya Mfalme Sulemani kwa mfano, amefanya makosa mengi sana maishani na matokeo yake akaandika kitabu chenye hekima, ambacho hukisoma na kujifunza hicho, hautafanya makosa aliyofanya yeye. kitabu hicho ni moja ya vitabu vilivyopo ndani ya Biblia. kinaitwa kitabu cha Mithali: Nakisoma na kutafakari na kutumia hekima zake kila siku!

Tusione kama sisi tuliandikiwa kuwa masikini tu bali tuamini inawezekana tukawa na mafanikio pamoja na kwamba tumezaliwa, tunalelewa na tunaishi katika hali duni zisizo na matumaini kiuchumi.Ili kubadili mtazamo huo tuliona kuwa;

  1. Ni lazima kufika hatua na kufanya uamuzi kwamba, pamoja na sababu zote za kukatisha tamaa, sitakufa masikini, nitafanya lolote lililo haki, kufa na kupona mpaka nibadili hali yangu kiuchumi.
  2. Ni lazima tujifunze kutokana na mafanikio na makosa ya waliotutangulia.
  3. Tuamini kuwa hata sisi tunaweza kufanikiwa kwa kuwa Mungu hakuwapangia wateule wachache tu kufanikiwa duniani. Mungu anatupenda sote.
  4. Tuwe na tabia ya kujisomea vitabu, tutumie chanzo chochote cha habari cha kutuelimisha.


·         Taka sana kusikiliza/kutazama vipindi vinavyofundisha mafanikio, au kuhudhuria kwanye kongamano, semina au mikutano inayofundisha mafanikio

Watu wenye wako tayari kusikiliza au kuangalia burudani, muziki au mambo ambayo hayawasaidii chochote katika maisha. Wengine hupenda kuhudhuria matamasha, soka, vikao mbalimbali nk. Sio vibaya kuhudhuria, lakini mambo hayo yapo siku zote na yanakugharimu. 


  • Ondoa utegemezi kwa Watu.

(Usitegemee kutiwa moyo na kusifiwa na watu (usiishi kwa kura za wanadamu)

Mwanadamu ni mwanadamu tu na msaada wake ni wa muda fulani, tena maisha ya mwanadamu yako mikononi mwa Mungu. Unaweza ukaweka tegemeo lako kwake na kesho akatoweka au akapatwa na tatizo la ghafla kama ajali mbaya n.k. Ndio maana Biblia inasema amtegemeaye mwanadamu amelaaniwa.

Pia usitegemee kusifiwa na watu, maana mtu anweza kukusifu leo na kesho akakupondo. Kusifiwa, kutiwa moyo au kupongezwa ikiwa umefanya vizuri ni jambo jema kabisa. Ila pia kutosifiwa au kutokutiwa moyo ni vizuri zaidi, maana kwa mtu anayetaka kufika mbali, hizo ndizo changamoto za kukufanya ufanye vizuri zaidi. Ndio maana ili ufanikiwe unahitaji mtu au rafiki bora, lakini ili ufanikiwe zaidi unahitaji maadui.

Hakuna hata mmoja kati yetu anayeweza kusema kuwa alikuwa amekamilika katika eneo fulani ndipo Mungu akavutiwa, akamuokoa au akaamua kumbariki.

Inawezekana kabisa katika maisha yako umepungua, unao udhaifu fulani kama Mefiboshethi (2Samweli 9:1-13), usikate tamaa. Acha kujidharau na kudumu ukiutazama ukubwa wa udhaifu wako au tatizo lako. Acha kujihurumia na kujiona mbwa mfu kama mefiposhethi, acha kuitazama na kuisikiliza hali ya nje wala usiishi kwa kura ya mazingira au kura ya wanadamu bali ishi kwa kura ya Mungu inayokuambia siku zote  “usiogope maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako wewe u wangu”  (Isaya 43:1-2). Maneno hayo ya Mungu ni zaidi ya kura ya ndugu zako, ni zaidi ya kura za wanadamu wote na shetani.

  • Usijilinganishe au kujifananisha na wengine

Hebu ichunguze pua yako au hata sura yako, utagundua hufanani na mtu yeyote duniani. Hata kama wakiwepo akina John wengi duniani, lakini hawawezi kuwa kama mimi, wala kufanana na mimi. Wewe ni wa kipekee kutokana na jinsi ulivyo, huhitaji kujilinganisha na mtu mwingine. Unapoanza kujilinganisha au kulinganisha kazi yako au huduma yako na watu wengine, matokeo yake utaanza kujidharau, kujihukumu, kujiona hufai au kujiona huwezi kufanya jambo lolote la maana katika maisha yako na duniani. kilamtu aliumbwa afanye kitu kilicho tofauti na mwingine. Jiheshimu na kujithamini. thamini kile unachokifanya huku, ukiongeza juudi ili kufanya vizuri zaidi.

  • Kuwa mbunifu kwa kila unalofanya

Mwanadamu anayo akili yenye uwezo wa ajabu sana, mara nyingi hatuitumii ipasavyo. Ubongo wa mwanadamu umeumbiwa na Mungu zaidi ya seli (chembechembe) billion 14! Kuna sehemu maalum katika ubongo kwa ajili ya kila jambo mwanadamu analo- taka kufanya au kujifunza kama vile kucheza, kuimba, muziki, sayansi, n.k.


Ukweli ni huu, ubongo wa  mwanadamu hauwezi hata siku moja kuzidiwa na majukumu. Na hii nayo ni falsafa (Responsibilities are always proportional to ability). Ukiona mtu anasema kazidiwa na majukumu hajatambua bado uwezo wa akili aliyopewa na Mungu! Tatizo, wengi wetu tunalemaza akili zetu kwa kutozishughulisha Matokeo yake, baada ya muda, sehemu za ubongo zinazohusika na majukumu fulani fulani zinadumaa kikazi (dormant). Akili zetu zina tabia moja muhimu, kadri unavyo- jishughulisha, uwezo wako unaongezeka. Lakini kwa usivyo itumia, inalemaa.

Kila mtu anao uwezo mkubwa sana wa ubunifu! Hata wewe. Kila atakayeshughulisha ubongo wake, na uwezo wake wa ubunifu unaongezeka. Wengine wanaonekana  hawana uwezo wa kubuni mambo mapya lakini sivyo ilivyo. Wanao uwezo. Ni kwamba  tu hawajishughulishi.
Ili uweze kufanikiwa maishani, ni lazima uwe mbunifu. Ni muhimu, na kusema kweli, ni lazima. Ubunifu ni kama silaha madhubuti inayotuwezesha tusipoteze nguvu zetu bure tunapotia bidii katika kazi. Tutatumia jasho letu kupata mapato lakini linaweza kuwa bure kama hatuna ubunifu. Ni lazima tuwe wabunifu katika kila tunalofanya, ili mafanikio yetu yawe dhahiri.
Anzia ubunifu wako kwenye kazi, huduma au chochote unachokifanya kwa sasa. Inawezekana ni kinyozi, biashara ndogondogo za kutembeza  au ajira zingine. Ili uweze kuwa mbunifu ni lazima uipende kazi yako. Ipende maana ndiyo inayo kutunza, ndiyo inayokupa kuishi. Ukishaipenda, tunaanzia ubunifu hapo kwa kufikiria mbele.

Jizoeze kupanga mipango ya mbele mapema, uwe na maamuzi yako binafsi kwamba baada ya muda unataka uwe nani. Hiyo ndiyo itakayokuwa dira yako na kipimo cha mafanikio yako. Hukusaidia usitumie pesa ulizopata  ovyo bali kwa malengo. Pia tabia ya kujiwekea malengo ya mbele itakusaidia kuwa na nidhamu juu ya mapato yako mwenyewe. Itakusaidia pia kuwa na ubunifu na bidii ili uweze kufikia lengo lako.

Katika dunia tunayoishi leo, waajiri hawatafuti watu wenye vyeti lukuki, bali wabunifu na wenye mtazamo chanya kuipatia kampuni heshima kwa ubunifu wao katika medani ya ushindani. Si vyeti!

Kwa hiyo, wakati wengine wanatafuta ajira na kuridhika na mishahara wapewayo na hivyo, wanafanya kazi wanazo pangiwa tu, wewe uwe na mtazamo tofauti na wao. Nenda katika kampuni au shirika au mahali popote unapojishughulusha, kwa lengo la kufanya zaidi ya majukumu ya kawaida. Uwe na mtazamo wa kutafuta tatizo linalowasumbua pale kazini, kwenye taasisi ile, ili ulipatie ufumbuzi. Usiseme halipo, ofisi yoyote, taasisi yoyote(iwe ya kidini au serekali) ina matatizo! Yapo, yatafute utayapata. Ukiyapata tumia ubunifu wako kuyatafutia ufumbuzi.
Wakati wengine wanakalia viti na kufanya majukumu ya kawaida, na kupokea mishahara, wewe uwe na malengo ya ziada, kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kiofisi! Au kuiongezea kampuni mafanikio au utambilisho au heshima kwenye medani za ushindani. Suala hili la kujibidisha, unawaza ukalitumia maali popote unapohitajika (katika dhehebu lako au dini yako n.k).

Jitaidi usababishe jambo jipya(alama)kutokea kila uendapo. Jiulize, hivi nikiondoka ofisi hii au maali ninapotoa huduma, watajisikia wamemkosa mtu muhimu? Azimia moyoni mwako mwenyewe kwamba popote utakapofanya kazi, iwe ya nyumbani, ofisini, udereva, kanisani n.k, siku utakapo ondoka, waseme wewe ni mfanyakazi bora. Hivyo itaongeza kiwango cha heshima na kuhitajika kwako. Acha alama.

Unaweza pia ukawa mbunifu katika kazi zako binafsi unazozifanya, hata kama ni kukaanga maandazi. Mfano, labda wewe ni Baba au mama lishe, unafanya biashara ya kuuza bidhaa,unakaanga maandazi n.k, na mnaotoa huduma hizo ni wengi, utafanya nini ili bidhaa yako ivutie zaidi? Nini kitakachofanya mteja aje kwako na si kwa mwingine? Ubunifu na kujitangaza kidogo. Wakati mwingine, tembelea ofisi zinazo kuzunguka, wazungushie bidhaa zako (kama vile nguo, viatu, kanda n.k) kwani wafanya kazi wengi kwasababu ya majukumu, hawana muda wakutembelea masoko au kujua kama kuna aina ya bidhaa mpya ilioingia. Lakini zingatia kuvaa vizuri, uonekane nadhifu ili mtu aweze kukusikiliza. wakati mwingine panga apointment ikiwa ofisi haiingiliki kiraisi. Lakini pia zingatia vigezo vifuatavyo :

-          Ubora wa huduma au bidhaa uwe kivutio
Jitaidi kujitofautisha na wengine, fikiri namna ya kuinua/kuboresha kiwango cha  huduma/bidhaa yako.
-          Bei ya huduma au bidhaa yako imvutie mteja
Pamoja na kuboresha, jitaidi huduma au bidhaa yako isiwe ya ghali, ili uweze kuwashawishi watu kuhiitaji. Usitake faida kubwa au mafanikio ya mara moja.
Inawezekana huduma yako ikahitajika maali fulani, lakini kwasababu umejiweka kuwa mtu hadimu, umetanguliza pesa mbele kuliko utu au huduma yako, hata kama ulikua mtu wa kufanikiwa, huwezi kufika maali ambapo Mungu angetaka ufike, utakuwa umewakatisha watu tamaa kabisa
-          Muonyeshe mteja au mpenzi wa huduma yako kuwa unamjali
Kumbuka, unapoweza kumshawishi mtu mmoja (kwa lugha unayo tumia, tabia yako, hali n.k), utawapata ndugu jamaa na rafiki zake. Wapo watu wengi wasioangalia pesa au mali zao (wanapoamua kutoa), bali lugha au heshima wanayopewa.
-          Usijali muda wako tu, jali na kuthamini muda wa mtu mwingine
-          Tangaza huduma au bidhaa yako
« Biashara ni matangazo na matangazo ni biashara » Najua matangazo ni gharama, lakini tunatumia shilingi kutafuta shilingi. Hivyo watu wengi watakaposikia habari ya huduma zako, watatamani wafike wajionee wenyewe. Lakini, usitangaze huduma ambayo huwezi kuitoa au kwa kiwango hicho, ukifanya hivyo utakuwa umewafukuza na hutawapata tena, wajapo na kuikosa. Kumbuka, ukimpoteza mmoja, umepoteza wengi.

Ukiona mtu anakosa la kufanya au kunung’unikia juu ya umaskini, ni kwamba si mbunifu. Ukiwa mbunifu hata kama huna mtaji, akili yako ni mtaji tayari.
Kumbuka kuna watu wenye pesa yao, wanatafuta wampe nani mwenye uwezo au mawazo mazuri azizungushe ili wote wafaidike. Pia wapo watu wenye mawazo mazuri ya bishara au huduma fulani yenye mafanikio, wanatafuta waongee na nani ili awape mtaji. jipange sawasawa, changamka, kuwa mbunifu nawe utafanikiwa.
 
  • Badili mtazamo wako

Mtazamo ni uwezo wa kuona jambo katika hali ambayo wangine hawajaona, kufikiria
na kuwa sehemu ya jambo husika kwa hali ambayo unapata maana na chanzo cha jambo kisha ukapata jibu au suluhisho la tatizo onekana, bila kuathiri jambo au kitu chenyewe. Mitazamo ni zaidi ya kufungua macho na kuona, ni zaidi ya uwezo wa kutofautisha mambo. Mtu mwenye mtazamo mzuri hugundua tatizo la mwenzake na kumsaidia aondokane na tatizo hilo bila kuathiri hali njema ya mwenzake.

katika pilikapilika za kila siku, tunakumbana na mambo mengi. Kati ya mambo hayo zipo habari na taarifa nzuri na nyingine mbaya ambazo maskio yetu hayataki kusikia. Yapo mambo ambayo ni mapya hujawahi kuyaona wala kuyasikia. Mengine ni ya kale ambayo umeyasikia lakini hukuwahi kuyaona, ila yapo na yanaendelea. Yapo pia mambo tanayoyaona kila siku kukicha.

Ipo mitazamo mizuri na mibaya. Lakini mara nyingi wanadamu wamekuwa na mitazamo mibaya zidi ya wengine. Mitazamo mibaya (wrong perception) hutokea pale mtu anapo mhukumu mtu mwingine, kumouna ana hatia kutokana na yeye mwenyewe anavyojiona au kutokana na mlinganisho alionao dhidi ya mwingine kwa kabila, taifa lake, mwonekano wa sura, rangi, jinsia, umri, umbile n.k. kutokana na hilo tumesikia jamii ya kale na baadhi yao hata sasa kuwa mwanamke hana haki katika familia na jamii, mtazamo huo umesababisha jamii iwaone wanyonge, dhaifu, wasioweza kuamua, kutawala na hata kupambanua mambo. Hali hiyihiyo ipo hata kwa watoto, kwamba hawana uwezo wa kushiriki katika kutoa mawazo, kushauri au kukosoa mambo yanapokwenda kombo. wakati mwingine tumewanyima haki zao za kimsingi za kisheria. hiyo sio mitazamo sahihi.

Mitazamo mibaya imetenganisha ndoa nyingi, imeachisha wengi kazi zao nzuri, imesababisha magonjwa na pia imeleta hata vifo. Je, Unapokua kazini, ofisini, sokoni, safarini, sehemu za ibada au popote pale, unawatazamaje wenzako? Labda wewe ni mzazi, mtoto, kiongozi katika chama, shirika, taasisi, serekali au katika dini au dhehebu fulani, Je kila aliyekosea (au kukukosea) ulishawahi kujifunza kwanini au kisababisho gani kilichomfanya atende hivyo? Unapambana na mambo mema na mabaya, unayahukumu vipi na kwa vigezo gani? Ni vema usihukumu mtu au jambo  kwa mtazamo wa nje bali pata nafasi ya kuchunguza kama itakulazimu, ili usijejuta au kusababisha madhara makubwa au kusababisha wengine kujuta kwasababu yako. Lakini pia wakati mwingine ikiwa jambo halikuhusu, halikunufaishi wala kunufaisha wengine au halileti  madhara yoyote, achana nalo, usipoteze muda wako, fanya yaliyo muhimu nawe utafanikiwa na kuwa heri.

Sitegemei kama utakuwa na mtazamo kuwa mwenzako ni mjinga au mshamba kwa jinsi ulivyoona wewe juu yake, kisha ukamtangaza na kumcheka kutokana na ujinga wake, kwani siyo suluhisho la matatizo bali kuangalia chanzo cha muhusika kutenda hayo uyaonayo. Mtazamo wako sahihi unaweza kuathiri mwenendo na amani ya wengine.Ukitakakujua maumivu wapatayo wengine, jiweke wewe chini ya viatu vyao(If you want to feel the pain others get, put yourself under others' shoes ).
Mume anaweza kuwa na mtazamo mbaya dhidi ya Mke wake au Mke dhidi ya Mumewe au inawezekana mitazamo mibaya kati ya wachumba au marafiki kisha ikasababisha madhara makubwa katika mahusiano kwa ujumla. Ndoa zinaweza kuvunjika au mahusiano kuharibika kwasababu ya mitazamo mibaya. Bosi anaweza kuwa na mtazamo mbaya dhidi ya mfanyakazi wake kisha ukaaribu ofisi au Maisha ya mmoja wapo. Hali hii yawezekana kwa Mwalimu, Daktari, viongozi wa ngazi mbalimbali, iwe katika dini, Vyama, Serekali nk.
Mtazamo mbaya juu ya jambo au hata mtu binafsi akiwa na mtazamo mbaya juu yake mwenyewe, unaweza kukufanya usisitawi wala kuendelea na kupata mafanikio uliyoyategemea. Wakati mwingine huna haja ya kugombana na ndugu au rafiki eti kwa vile hakupendi au hafanyi unavyotaka wewe. Badili mtazamo sasa,  jione kuwa wewe ni mtu wa thamani na Mungu haja kuumba kwa bahati mbaya.

  • Badilisha unavyowaza juu ya hali yako
(Jione kuwa mtu muhimu na wa maana chini ya jua)

Mambo yote, ikiwepo hali aliyo nayo mtu kiuchumi, iwe utajiri au umasikini, huwa ni matokeo ya yale ayawazayo mtu moyoni mwake. Mawazo ni asili ya hali aliyo nayo mtu. Mawazo ni kama mbegu; ikioteshwa hukua nakuzaa matunda. Inapokuwa mbegu, huonekana ndogo lakini, ikiishaota na kukua, punde tu, huwa mti mkubwa sana!
Katika maisha ya mwanadamu, siku zote kufanikiwa hutokana na ukubwa wa mawazo ambayo mtu mwenyewe anajiwazia. Ndio maana ili mtu aweze kuishi maisha bora na kuyafurahiya, bila shaka, hanabudi kujiwazia mawazo bora na makubwa. Ikiwa mawazo ajiwaziayo mtu ni duni na manyonge, kamwe mtu huyo hawezi kuishi maisha bora na yenye furaha (wafilipi 4:8).

Hebu tafakari wale wapelelezi kumi kati ya kumi na mbili waliotumwa na Musa kuipeleleza nchi ya kanaani walivyojiwazia na kujiona kuwa wao ni kama mapanzi (Hesabu 13:33). Mawazo yao yalilingana kama panzi wanavyofikiri na kutenda. Hivyo kuna uhusiano mkubwa sana kati ya mawazo ya mtu na maneno mtu ayanenayo (zaburi 19:14). Ayazungumzayo mtu ndio yaujazayo moyo wake.   Kwa kawaida mtu anapoona, anaposikia au jambo linapomtokea yeye mwenyewe, akili au ufahamu wake humpa tafsiri mbalimbali juu ya jambo hilo. Fikra anazokuwa nazo juu ya jambo  hilo, zinampa mtazamo fulani {waweza kuwa chanya au hasi} katika maisha yake. Hayo yanakuwa mawazo au mtazamo wake juu ya jambo hilo katika maisha yake. Mawazo anayokuwa nayo mtu kwa muda mrefu huwa yanajitokeza katika maneno yake na hatimaye katika matendo yake. Mtu anayewaza mafanikio katika maisha yake kwa mfano, ni kawaida kumkuta akizungumza juu ya mafanikio na hata matendo yake yatathibitisha hilo pia.

Kwa hiyo, mawazo aliyo nayo mtu juu ya maisha ambayo pia husababishwa na yale ayasikiayo, ayaonayo na yanayomtokea hudhihirika katika maneno. ‘‘Mahuburi’’ hayo husababisha mtu kuwa na imani yenye muelekeo wa mawazo na maneno yake. Matokeo yake ni matendo yenye muelekeo huo huo. Hivyo basi, ukiona mtu amekata tamaa  kimaisha, chanzo au asili yake ni mawazo. Pia, ukitaka kumsaidia mtu au kujisaidia mwenyewe kutoka katika hali ya kimasikini, eneo la kuanza kushughulikia  ni la MAWAZO!

Na hapa nitakupa mfano. Jitazame mwenyewe hali uliyonayo.  Hali yako kiuchumi iko hivyo ilivyo kwa sababu, baada ya kujikuta katika mazingira duni kimaisha, kuanzia kwenye familia ya wazazi wako, au baada ya kujikuta hupati msaada wa ndugu na marafiki uliowategemea, au ulipoona una kilema mwilini mwako, kilichofuata ni mawazo ya kujiona huwezi kuiepuka hali hiyo na hivyo utaendelea kuwa masikini. Ulipowaza hivyo kwa muda, moyo wako ukaamini hivyo. Unajua nini kilifuata? Lolote unalofanya unaona tu kama halitafanikiwa, hata ukifanya kwa bidii namna gani.

Mtu mmoja Justice Cardozo wa ‘‘The United States Supreme Court’’ {Mahakama Kuu ya Marekani} alikuwa Mmarekani aliyeheshimiwa sana duniani kwa utetezi wake wa haki za binadamu wakati ule wa ubaguzi wa rangi Marekani na aliwahi kusema ‘‘Tupo kama tulivyoamini kwamba tupo’’ kwa kauli hiyo alimaanisha kwamba kama unaamini wewe ni tajiri, basi wewe ni tajiri, kama unaamini wewe ni masikini basi wewe ni masikini, kama unaamini wewe huwezi kufanya jambo ni kweli huwezi; na ukiamini unaweza, utaweza. Ni kweli kabisa! Na hii ni kwa sababu kuna nguvu ya kuweza katika kuamini.

Inawezekana uliwahi kusikia habari za ubaguzi wa rangi uliokuwepo Marekani miaka ya 1920. Halikuwa jambo la kawaida kumuona Mmarekani mweusi akiwa na kazi nzuri, gari nzuri, nyumba nzuri au hata akisoma shule nzuri! kuwa tu mweusi kulitosha kumbagua na kumwaminisha kuwa atakufa masikini, hataweza kufanikiwa katika jambo lolota! Ilifika mahali ambapo, wengi wao kwa kuwa walinyanyasika sana, wakaamini wao ni wanyuma siku zote hata wao wenyewe wakajibagua.

Katika kipindi kama hicho ambacho, kama ilivyo kwa mazingira na hali yako leo,  ARTHUR GASTONE, akiwa Mmarekani mweusi,alizikataa fikra za umasikini na akaamua kutumia ubunifu  wake kuinua kipato chake kwa muda mfupi sana,  Gaston akawa bilionea Mmarekani mweusi! Halikuwa jambo rahisi na la kawaida, hata ukiwauliza Wamarekani wenyewe watakwambia. Lakini aliamua kutokuwa masikini hata hivyo! Nataka ujue ni suala tu la uamuzi!

Gaston, akiwa kijana mdogo, asiye na elimu sana, miaka ya 1920, baada ya kugundua kuwa ana kipaji cha biashara, aliamua kupambana na umasikini kwa kutumia kipaji chake. Aliona jinsi weusi walivyokuwa hawatendewi haki pale wao wenyewe au ndugu zao wanapokufa. Akajua hilo ni tatizo, linahitaji ufumbuzi. Hakua na senti mkononi lakini, aliyathamini mawazo yake, hakuangalia kuwa hana elimu, yeye ni Mmarekani mweusi, yeye ni kijana tu masikini bali aliamua kutumia akili aliyopewa na Mungu. Kwanza kuwasaidia wanajamii wenzake pili, katika kuwasaidia huko, kuinua kiwango cha uchumi wake.
Alianza kwa kuwaahidi wamarekani weusi kuwa, kama wangesaini mkataba naye na kumlipa kiasi kidogo tu cha senti ishirini na tano kwa juma pesa za Kimarekani, hakika angeyashughulikia maziko yao pindi wanapokufa kwa hadhi ile ile wanayo zikwa weupe. Ama kwa hakika senti 25 kwa juma ilikuwa kidogo sana, na kama ilivyotegemewa, wengine walikufa mapema kabla hawajalipa hata kiasi cha kutosha kugharamia mazishi yao. Arthur, alitumia malipo ya wengine kugharamia maziko yao. Na kama ilivyotarajiwa kuwa wengine walichelewa kufa na hivyo kulipa zaidi! Kwa sababu ya uaminifu wa kampuni ya Arthur Gaston, wengi sana walijiunga na kulipa pesa nyingi. Gaston akaanza kumiliki kampuni tajiri sana.

Inawezekana umekaa chini huku ukiwaza  kwamba huwezi kufanya lolote kwa kuwa huna mtaji. Silikiza ! Hakuna mtu yeyote popote anayeanza kutafuta mtaji bila maono! Sharti maono (au mawazo ya ubunifu) yawepo ndipo utafute mtaji.Wazo ndio la msingi, si mtaji! Umeshindwa kufanikiwa kwa kuwa unatafuta pesa ndio ujue utafanya nini uzizalishe. Wewe unawaza kinyume nyume! Kutokana na kusoma vitabu na kuwa na tafakari nyingi, nimejifunza mengi katika maisha ya watu wengine. Hayo yamenifanya kujikusanyia ‘‘kweli’’ au ‘‘kanuni’’auwaweza kuziita falsafa ukipenda, zinazonisaidia katika maisha yangu.Mojawapo ni hii; ‘‘Siku zote, vyanzo vya fedha hufuata maono na si vinginevyo’’ (usually resources follow vision and no vice versa).

Kumbuka Hilo unaloliona wewe ni tatizo ndio njia unayoiweza kutumia kuinua kipato chako! Tatizo lililopo kwenye  jamii yako ndio mtaji wako, kuwa tu mbunifu na changamka!

Christopher Mwakasege, mwalimu na mhubiri wa neno la Mungu alisema hivi siku moja, ‘‘kumbuka hili siku zote, chanzo chako cha matumizi ni chanzo cha mapato cha mwingine ! Kwa mfano, bomba lako likiharibika, kwako ni chanzo cha matumizi lakini kwa fundi bomba na chanzo cha mapato. Vivyo hivyo kwa gari lako, nyumba yako n.k.’’

Huo ndio ukweli, tatizo lako ni neema kwa mwingine! Unaweza kushangaa lakini ni kweli kwamba watu wasipougua madawa hayauzwi na madaktari hawatakuwa na kazi. Tatizo la jamii ni neema kwa wabunifu! Kwa nini isiwe hivyo kwako ?

Usibaki kunung’unikia hali yako tangu asubuhi mpaka jioni, usiku utaingia na utajikuta upo kama ulivyokuwa asubuhi, hujafanya lolote. Tumia nafasi na fursa zinazojitokeza kwako ujiondoe katika umasikini. Acha kujiwazia mwenyewe kuwa wewe ni masikini na huwezi kufanya lolote. Badilisha kuwaza kwako. Sikushawishi uikatae hali halisi, la ! Huwezi kuikana. hivyo ndivyo ilivyo. Lakini kumbuka; ukweli kuwa umezaliwa na umekulia hali duni ya maisha, haimaanishi ni lazima kufa masikini. Huo nao ni ukweli. Haijalishi sana ulikotoka bali kule uendako. Usiiachie asili ikuamulie mustakabali wako, ni lazima uamue (You don’t leave the nature to decide for your destiny, decide it).

Inawezekana sasa upo tayari kubadili mtazamo wako uwe chanya kuhusu maisha, lakini swali lako ni hili; nimezaliwa katika hali hii, nimekulia na ndio inayonizunguka mpaka sasa, isitoshe, nilishaamini hivyo na hata hivi nimekata tamaa ya maisha, nitabadili vipi mtazomo huo? Nitakuambia ni kwa nini: ni vigumu kumshawishi asiye na kiu kunywa maji. Lakini, mara apatapo kiu, ukichelewa kumpatia maji, uwe na uhakika atayafuata mwenyewe.
Wewe ni mtu wa thamani, umeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu mwenyewe. Hakuna mfano wako popote duniani, hakuna mwenye alama za vidole (finger prints) kama zako katika ulimwengu mzima. kuna mtu mmoja tu mwenye mfano wa sura yako, naye ni Mungu. Upo duniani ukiwa umepewa kazi maalumu (assignment) ambayo Mugu hajampa mtu mwingine. Fanya kitu fulani ili kuifanya dunia yetu kuwa maali bora pa kuishi. Kuanzia leo, Jipende, jikubali, jitengeneze, jizungumzie, jinenee, jitabirie maneno mazuri. Jikubali na wala usijifananishe na mtu mwingine. Wewe ni wa thamani, umebeba sura ya Mungu. Zaburi 8:4-9, Waebrania 2:6-8


  • Usikiri/usiogope kushindwa

Siku zote katika kila ufanyacho au unachotarajia kukifanya, ukitanguliza mawazo ya kushindwa, si rahisi kushinda. Chamsingi, fanya kama wengine walivyofanya na wakafanikiwa
Mungu alimwumba mwanadamu kwa sura na mfano wake. Kama vile ambavyo neno litokalo katika kinywa cha Mungu linavyoweza kuumba, ndivyo maneno yetu pia yanavyoweza kuumba pia. (Methali 18:21” Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi” Kilatutakachokiri ndicho kitakachotokea. Ukikiri magumu kwa kuwa ndiyo yanayoonekana basi utaumba hayo magumu.

Kwa mfano unasikia dalili za ugonjwa fulani katika mwili wako ukikiri neno la Bwana katika kitabu cha Isya 53:4-5 “Hakika ameyachukua maskitiko yetu, amejitwika huzuni zetu. Alijeruhiwa kwa makosa yetu alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona”.

Maneno haya yanaonyesha wazi jinsi ambavyo uzima wetu kiafya na ushindi wetu kwa ujumla siyo kitu cha sasa au kitakachotokea bali tayari tulishafanyiwa hayo zaidi yamiaka elfu mbili iliyopita pale msalabani. SISI TUMEPONA- na siyo tutapona.

Unapokiri kwa imani kama ilivyoandikwa, basi Bwana atatimiza ndani yako. Neno lake uliloliamini na kulikiri, shetani atakimbia, magonjwa yatatoweka maana yanasikia neno la Mungu. Umasikini na ufukara utatoweka na hutakuwa mtu wa kukata tamaa tena, badala yake utakuwa msaada kwa wengine. Lakini fikiri dalili za ugonjwa zinakuja na unaanza kukiri “ule ugonjwa wangu unanirudia, au hizi ni dalili za malaria, ndio kawaida yangu nk. Marko 11:23 “Amini nawaambia, yeye atakayeuambia mlima huu ng’oka ukatupwe baharini wala asione shaka moyoni mwake ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia yatakuwa yake”.

Hii ni kusema kuwa unapokiri (unapotamka) jambo linatokea kama ulivyosema.
Unapokiri uzima bila kuwa na shaka (hofu) uzima huo utakuwa wako. Kadhalika unapokiri ugonjwa, shida, umaskini wako basi unaumba na vitakuwa vyako kwasababu hukuwa na shaka moyoni mwako ulipokua unakiri. Shetani atasimama nyuma ya hayo maneno yako na atayatumia.


Uamuzi unao wewe. Katika hali inayotangaza umaskini wewe kiri kama Ilivoandkwa « kwa umaskni wake sisi tumekuwa matajiri » 2Wakorintho 8:9. Katika mazingira na hali ya upweke/kukataliwa, katika mazingira yanayokutangazia kushindwa, wewe kiri “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” Wafilipi 4:13.


  • Kitumie kipaji au kipawa ulichopewa na Mungu kikufanikishe (kikutajirishe)

Kipaji au kipawa ni uwezo/ujuzi alioweka Mungu ndani ya mtu bila ya yeye kugharimia chochote. Ni uwezo wakufanya mambo maalumu kwa ufanisi wa hali ya juu sana. uwezo au ujuzi huo mtu huzaliwa nao. Hicho ni kipawa, zawadi wakati mwingine huitwa karama n.k.

kuna vipaji ambavyo huanza kujidhihirisha tangu utotoni lakini vingine inabidi vipigwe msasa kidogo ‘training’ Vistuliwe kama gari (starter). Wapo wenye vipaji na wanaweza kuvitumia hata kama hawana elimu. Sasa usinielewe vibaya, si kwamba hawahitaji mafunzo, kufundishwa ni muhimu tu ili kukihamsha na kukiweka kazini. Nazungumzia vipaji, si kila apitiaye darasani au apataye mafunzo atang’ara katika eneo hilo, ni wenye vipaji hasa.

Kila mtu (awe mtoto, mtu mzima, mwanamke, mwanaume, kijana au mzee, msomi na asiye na elimu, mlemavu n.k) anacho kipaji au kipawa alichopewa na Mungu, na wapo wenye vipaji zaidi ya kimoja. Inawezekana hujui kipaji chako au hujajishughulisha, hujibidishi kukijua au umekidharau, ukitamani au kudhani vipaji vya wengine ndio bora zaidi. kipaji kikitumiwa vizuri, huinua, hufanikisha, hutajirisha. Hakuna sababu ya kulialia, kusononeka, kukata tamaa kwasababu ya hali ngumu ya kimaisha ilihali unacho kipaji cha ki-Mungu ndani yako.
Inashangaza sana ukiwauliza watu wengi kipaji chako ni kipi ? utasikia ;

-          Naweza kuimba
-          Naweza kupiga vyombo vya muziki
-          Naweza kuche mpira, dansi au mchezo mwingineo
-          Nakimbia mbio sana.

Wengi tunadhani ni kuimba kama R. kely, kuigiza, kucheza mpira kama Ronaldinho, tunawaza tu kuwa ‘superstars’. Nimara chache kusikia majibu kama (nawapenda watoto, ninakipaji cha kulea, nina kipaji cha kusoma au kuandika vitabu, cha kutafsi au kueleza jambo likaeleweka).

Kipawa (kipaji au zawadi) cha mtu humpatia nafasi, humleta mbele ya watu wakuu (Methali 18 :16)
Hivyo ni kazi ya kipawa (na wala sio kipawa fulani, ni kipawa chochote) endapo kitatumiwa ipasavyo....

Kuna watu wana vipaji vya upishi, akipika chochote hata kama hajaweka utaalamu au hata viungo vya kutosha, lakini kila aonjaye anamsifu. Akikifahamu kipaji chake vizuri na kukitumia kitamtajirisha, kitamketisha na wakuu. Maana kila anayeandaa sherehe atamtafuta, pia wenye hoteli zao watamgombani, mwishowe hata kwenye sherehe za kiserekali. Hivyo ndivyo biblia isemavyo.... « Humleta mbele ya wakuu ». Inawezekana wewe ni mwandishi stadi wa hotuba, ukikitumia kipaji chako vizuri, hatimaye utatafutwa na wakuu kwa ajili ya kuandaa hotuba za wakuu. Unaweza ukajifunza hata kwa waandishi, wengi wana elimu hiyoo lakini hawana kipaji. Wale wenye vipaji Mungu amewainua, wananafasi ya kuojiana na wakuu na hata kusafiri nao, kukaa nao, ili waandike habari zao vizuri. Tafakari fundi stadi wa kushona nguo, akikitumia kipaji chake ipasavyo, jina lake linapata umaarufu kuliko hata kiongozi wa serekali. Watoto hata wake wa wakuu wanamtaka huyohuyo na wakati mwingine wanamhamishia majumbani mwao. Hiyo ni kazi ya kipaji. Wapo wenye vipaji vya kufundisha, yaani kila atakaye fundishwa na mwalimu huyo, atataka kila rafiki yake au ndugu afundishwe naye pia. Wapo pia wenye vipaji vya uchoraji, akikutazama kwa dakika chache, anakuchora kama ulivyo. Pia wapo wenye vipaji vya uchekeshaji (hata kama utakuwa umeudhiwa, akitokea lazima ucheke tu), udereva, utangazaji, kinyozi, ususi, udobi, kuhariri (hata kama utawapelekea wahariri mbalimbali kitabu chako, baadaye ukimpelekea, anagundua makosa madogo madogo ya kiuhariri au ya muundo wa lugha ambao wote hawakuyaona !). 

kwaiyo kwa kadiri kipawa cha mtu kinapotumiwa kwa usahihi na mahali pake, kitamheshimisha na kumuinua. Hivyo thamani inapopanda na kipato chako kinaongezeka. Sasa hebu angalia mazingira yanayo kuzunguka kama yanakuruhusu kutumia moja ya vipaji ulivyonavyo. ukiona kuna uhitaji (chance), changamka, kichomoe kipaji chako na kiweke kazini kabla wengine hawaja changamkia.
Methali 17 :8 - Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho, kila kigeukapo hufanikiwa.

« Kila kigeukapo » (maana yake unapokishughulisha) hufanikiwa.
Kipawa kamwe hakifanikiwi usipokishughulisha. Mafanikio yapo kwa yeyote anayekishughulisha kipawa kwani ni cha ki-Mungu.


  • Usikubali kudumu katika matatizo (kataa hali uliyonayo sasa)

Inawezekana ukapita katika tatizo fulani, lakini usikubali kudumu katika tatizo hilo. Matatizo yanatofautiana, na kila mmoja huona kuwa tatizo lake ni kubwa kuliko ya wengine.

Mtu wa Mungu Eliya, alifika mahali pa kuomba afe (1Wafalme 19:4-8),
lakini kumbe mtazamo wa Mungu ulikuwa tofauti kabisa. Badala ya kufa Mungu akampa chakula na kwa nguvu ya chakula akasonga mbele. Kumbuka malaika wa Bwana alimjia mara ya pili akamwambia, inuka ule maana safari yako bado ndefu.
Inawezekana umepita katika hali fulani iliyo kukatisha tamaa, lakini kuna kujiliwa mara ya pili. Hapo ulipo unapitia tu, hayo yanaitwa mapito tu inamaana yanapita, hayakai. Usikubali kubaki hapo, inuka maana kuna maali Mungu anataka ufike.

Mara nyingi tumeitaji au kuomba mambo manyonge au vitu vya kutuangamiza au kutuua kabisa. Vile tuonavya sivyo Mungu anavyo tutazama. Unajiona maskini, fukara, Mungu anakuona mwenye mafanikio makubwa. Unajiona mdhaifu, mnyonge, usiyefaa, usiyejiweza, hujasoma, yatima au mjane au mtu wa chini kabisa, sivyo Mungu akutazamavyo. Wewe ni mtu wa maana, usikate tamaa, inuka usibaki kubaki hapo ulipo, hilo lilikua pito tu, safari yako bado ni ndefu kuna maali Mungu anataka ufike.

Mbinu za shetani ni kuleta matatizo ili tukwame au tuchelewe  kabisa katika matatizo hayo, katika kutafuta suluhisho ambalo halitapatikana kamwe. Sasa hatupaswi kuyatazama na kuyazingatia sana, ila kuchukua hatua kufanya kile ambacho tumeamuriwa na Bwana kukifanya. Ukitaka kubadili mawazo na mtazamo wako kuhusu umasikini ulio nao. Hatua ya kwanza kabisa ni ya uamuzi, amua sasa kwamba, pamoja na hali uliyonayo, mazingira yaliyokuzunguka na historia yote ya nyuma, hutaki  kwa namna yoyote ile,  kuendelea kuwa masikini. Amua kuukaribisha Utajiri. Sina wazazi wala jamaa ya kuitegemea, sawa! Sina kazi ya kuajiriwa, sawa! Sina mtaji wa biashara, sawa! Lakini hata hivyo, siutaki tena umasikini . Nitafanya lolote lililo haki litakalobadilisha hali yangu kimaisha, Maadamu Mungu amenipa kuishi,

Ninakuhakikishia huo ni uamuzi mzito sana, lakini amini usiamini, umefanya uamuzi ambao utaukumbuka siku zote za maisha yako! Wakati mwingine ukiweza jiwekee kumbukumbu kwa siku hii. Utawaeleza hata wanao watakapo kuuliza ulifanyaje ukawa tajiri? Utawaambia, kwanza niliamua kutokuwa masikini! 

Ni uamuzi mzito kwa sababu, hautaweza tena kufanya kazi ki – ulegevu, uamuzi huo utasumbua wenyewe, hautaweza tena kufanya kazi ilimradi tu, katu hutatulia na kuridhika na kidogo, utafanya bidii. Hii ni kwa sababu kuna kitu unakumbuka kila mara. Umeazimia na hakitakuacha utulie! Na Mungu  atakupa akili njema yanye ubunifu katika utendaji wako, naye ataibariki kazi ya mikono yako. Uamuzi ulioufanya ni agano la nafsi yako mwenyewe, ni deni, na Mungu ni shahidi wako atakupa nguvu na akili kulitimiza.
Sasa kumbuka hilo ni azimio (au uamuzi) la kubadili mawazo au mtazamo wako kuhusu umasikini, lakini hali halisi ipo palepale – bado haijabadilika. huo ni uamuzi wa nafsini mwako. kwa maana hiyo ili ile imani kwamba wewe ni masikini daima iondoke, ni lazima kuzungumza kwako kuanze kubadilrka. Maana yale uyaaminiyo ndiyo utakayosema na ndivyo utakavyoenenda vile vile.

Ili mawazo yako yabadilike, ni lazima uwe makini nayale unayoyasikia, unayoyatazama na kujihusisha nayo katika maisha yako. Huwezi kuwa na mawazo ya matumaini ya maisha, ikiwa kila siku vijiwe vyako ni vile vinavyozungumza habari ya kukata tamaa kimaisha, haiwezekani! Anze sasa kujihusisha na vyanzo vya maneno yenye mtazamo chanya kuhusu maisha yenye malengo ya mafanikio. Wataalam wa Saikolojia wanaamini kwamba, kwa kiasi kikubwa sana, uwezekano wa tabia na mwenendo wa mtu kufanana na watu anaojihusisha nao ni mkubwa sana. Ipo nguvu ya ushawishi (influence) kwa tabia miongoni mwa marafiki. Huu ni ukweli usiopingika.

Ukiambatana na watu waliokata tamaa kimaisha, baada ya muda fulani, utajikuta ndivyo. Ukiambatana na watu wenye mtazamo chanya kuhusu mafanikio maishani, utafanana nao .Hata biblia imesema. ‘‘Enenda na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima: Bali rafiki wapumbavu utaumia; (Mithali 13:20)
Ndio maana ni muhimu sana kufanya uamuzi wa ni aina gani ya marafiki wa kuambatana nao kabla ujawatafuta. Si kila mtu tu ni wa kuambatana naye!

Kwa hiyo, baada ya kuweka uamuzi, sasa ni lazima uachane na propaganda ulizozoea na maneno ya vijiweni yanayouhubiri moyo wako kuwa wewe ni masikini kwa sababu hii na ile. Ukiendelea nayo, utaiumba imani ileile na utashindwa kubadili kunena kwako. Badala yake, tafuta sasa ushirika katika mazungumzo na hata kazi na watu wenye mtazamo wa mafanikio katika maisha. Zungumza nao,  tianeni moyo,  utajikuta ukiamini hata wewe unaweza kubadilika. Utajenga imani na mtazamo wako namna hiyo. Ghafla maneno yako na mwenendo nao vitaanza kubadilika. Utajikuta unaanza kusema inawekana! Ipo siku tu! Utafanya kazi kufa na kupona ukiwa na lengo.


  • Usijihukumu

(Warumi 8:1-2) Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika kristo Yesu….

Wapo watu wengi sana na hasa hao wamchao Mungu wanateseka chini ya mzigo wa hukumu na hii ndio silaa mojawapo ambayo shetani anaitumia  kuwaweka utumwani. Anajua kuwa shida ya hukumu tayari imetatuliwa, na hivyo basi anatumia silaa ya ufahamu wa dhambi. Kwa maneno mengine, anawafanya wa “hisi” kuwa wametenda dhambi ingawa hawajatenda dhambi.
Hisia hizi za kupotosha zinawafanya watu wengi waamini kuwa hawastaili kuyatenda mapenzi ya Mungu au kuzipokea baraka za zake. Pia mara nyingi watu wanajihukumu wao wenyewe kuliko wanavyo hukumiwa na watu wengine. Watu wengine hujikataa na kutokujipenda kwasababu wana makosa madogomadogo wanayofanya. Watu hawa huamini kwamba, watu wengine ni wazuri, ni bora au wana akili nyingi zaidi kuliko wao. Laiti ungejuwa wapo wengine wanaokutamani na kuomba kwamba wangekuwa kama ulivyo. Ukipenda kuwa bora na kuishi maisha bora, basi jiamini,  jikubali na kuyakataa maisha ya kujihukumu.

Hakuna haja hata kidogo kwa wana wa Mungu kuendelea kuvaa vazi nzito la kujihukumu. Hata kama utakuwa umetenda lolote lililo ovu, una haki ya kusamehewa    (1 Yohana 1:9) Huna haja ya kujihukumu tena, na pia usijaribu kuishi kulingana na matarajio ya wengine, ishi kulingana na matarajio ya Neno la Mungu. Hivyo utajiona kuwa mtu huru na siye aliyetawaliwa na matatizo, na pia itakusaidia kuishi kwa imani.

Mfano : Vijana wawili walikua wameajiriwa kufanya kazi katika nyumba ya tajiri mmoja. Mmoja alipangiwa kufanya kazi za ndani na mwingine alipangiwa kazi za nnje. Siku moja yule aliyekuwaakifanya kazi za nnje baada ya kumaliza kazi, alipumzika chini ya mti huku akiwa ameshikilia manati yake aliyokuwa akiitumia mara kwa mara akiwa amemaliza kazi zake.

Hivyo baada ya kupitiwa na usingizi, alijikuta ghafla, kumbe alikua amerusha jiwe na likampiga jogoo wa mwajiri wake. Baada ya kuona jogoo kafa, alishikwa na hofu kuu, akachimba shimo, akamfukia,  kumbe mwenzie akiwa ndani, aliyaona yote yaliokua yakiendelea nnje. Na baadaye akamwambia nimeona yote uliyoyafanya na nitamwambia mzee. Hivyo ilibidi jamaa apige magoti na kuomba msamaha. Mwenzie akamwambia nitakusamehe lakini kwa sharti moja, amka kila siku mapema fanya kazi zako, baadaye fanya kazi zangu pia. Hivyo ikamchukua mda mrefu akifanya kazi zote mbili kwamaumivu, uchovu, mateso n.k, (akawatumikia mabwana wawili kwa muda mrefu).

Siku moja akasema moyani mwake, nitakaa kwenye utumwa huu hadi lini ?
nitamwendea tajiri wangu nimwambie yaliyotokea. Nitaomba msamaha. Niko tayari kwa masharti yoyote atakayonipa, kuliko kuendelea kuishi maisha ya kujihukumu. Ndipo alipomwendea katika hali ya unyenyekevu na kutetemeka huku akilia machozi. Lakini jambo la kushangaza, mwajiri wake akamwambia futa machozi, kwani siku ile alipokufa jogoo hata ukamfukia shimoni, nilikuona kwa macho yangu. Hivyo muda wote huu ulikua umenivunja moyo sana. Sio kwasababu ya kifo cha jogoo, lakini kwasababu ya wewe kuufanya moyo wako kuwa mgumu na kukubali kuishi na hukumu hiyo mda mrefu, lakini nimeku samehe. Alirukaruka huku akitokwa na machozi ya furaha. Hivyo tangu siku hiyo, ikawa ndio mwisho wa kuwatumikia mabwana wawili. Na hata mwenzie kwa hasira alivyomwendea tajiri, akimpelekea mashitaka, alikua amechelewa.

Ndugu msomaji,
Kwanini uishi maisha ya kujihukumu? Hata kama umekosea, hujui ikiwa una haki ya kusamehewa? Kuanzia leo, usiwe na mabwana wawili moyoni mwako. Ikiwa umekosea, tubu mbele za Mungu naye atakusamehe. Hivyo hata shetani, wanadamu au mawazo na hisia zako vikikushitaki, yatakua hayana nguvu tena. Hivyo utaishi maisha ya amani. Kuanzia leo, usijihukumu au kujishutumu kuwa huwezi kufanya chochote chini ya juwa. Jijali, jitengeneze vizuri, vaa vizuri kama mwenye sura na mfano wa Mungu, jithamini bila kujali umri wako, mwonekano wako ama vyovyote vile. Yatambue na kuyathamini hata yale mambo madogo madogo unayoweza kuyafanya au unayo yafanya vizuri, anzia hapo songa mbele.

  • Sahau yaliyopita

(Isaya 43 :18-19). Inawezekana yapo mambo mabaya(au watu wabaya) yanayokatisha tamaa, mapito vikwazo na majaribu mbalimbali. Usisumbuliwe na hayo, yanaitwa mapito na yamepita. « Ruhusu yaliyopita yapite, vinginevyo yatapita pamoja na wewe ». Jikumbushe tu yale mazuri ambayo mungu amewahi kukutendea huko nyuma, hayo yatakujengea hali ya ujasiri na kujiamini. hayo yatakusaidia kukabiliana na mabadiliko yoyote yatakayojitokeza katika maisha.

Jambo au sifa moja kati ya nyingi zinazomtofautisha wanadamu na Mungu ni kusamehe na kusahau. na hili limevunja mausiano mengi(urafiki, uchumba ndoa n.k). Lakini pomoja na hilo, yapo mambo ambayo tusipoyasahau na kuendelea kuyasumbu- kia, yatatuumiza, na kutufanya kuishi maisha ya kukata tamaa siku zote. Narudia tena, acha yaliyopita yapite, yawe mabaya au mazuri, maana adui mkubwa wa kufanikiwa kwako ni mafanikio yaliyopita.

Inawezekana maisha unayoishi leo yanatokana na jinsi ulivyoenenda jana, bado huo sio mwisho wa maisha, hata kama jana uliishi vibaya, sasa ione jana kama darasa ili leo ufaulu mtiani utakao kufanya ufanikiwe kesho.


  • Jijengee mazingira ya amani na furaha

Chanzo cha amani na furaha yako kimo katika moyo wako.
Ukitambua hili huta ruhusu Mtu au kitu chochote kikuondolee amani na furaha yako na kukukatisha tamaa (Mitahali 17:22)

Shina kuu la Moyo kuumia ni kutunza uchungu moyoni.
Uchungu ni hasira ambayo imekaa moyoni bila kushughulikiwa na humfanya Mtu kuishi maisha ya ghadhabu na kukata tamaa siku zote.

Hata kama umeonewa, umeudhiwa, umenenewa vibaya n.k, inakupasa usamehe kwa ajili ya usalama wa maisha yako. Ninajua kwamba wapo watu wasiotaka suluhu kiasi kwamba hata kama wamekosa hawaoni sababu ya kutubu. Lakini unapaswa kumsamehe Mtu wa jinsi hiyo kwa maana ndivyo mapenzi ya Mungu na mafanikio yako kwa ujumla.

  • Jenga tabia ya kujali, kuheshimu, kuthamini na kusaidia watu wengine. (taka wengine wafanikiwe) methali 3 :27

Siri moja ya mafanikio maishani, ni kuwashirikisha watu wengine mafanikio au siri ya mafanikio au baraka zako, jisikie vizuri wengine wakifanikiwe. Usiwe mchoyo wa kuwasaidia au kuwaeleza wengine siri ya ufanisi wako, na ndivyo na wewe kwa kufanya hivyo utakuwa umetoa mchango wa kuiendeleza jamii inayokuzunguka na matokeo yake kwa kufanya hivyo, wewe utaendelea zaidi. Hakuna faida yoyote  ya kuendelea peke yako wakati waliokuzunguka wote ni wajinga, fukara, maskini nk

Mwanadamu yeyote chini ya jua ni wa muhimu tena anafaa. Hivyo usije ukambagua au kumdhara mtu yeyote hata kama ukifanikiwa, maana hujui ninani atakaye kusaidia maishani. Maana wale tunaowaona kuwa ni wadogo, maskini, hawana elimu n.k, hao ndio wanaotufanya tuishi vizuri. Wengine ni wasichana au wafulana wetu wa kazi, wanatupikia, wanatulelea watoto, wengine ni madereva n.k.

  • Usitegemee akili zako mwenyewe, mtegemee na kumtumaini Mungu.
Hata kama imani yako ni ndogo, bado unaweza kumtumaini Mungu na kuamini kwamba Mungu wa amani atamseta Shetani mara chini ya miguu yako (Zab 42:5) (Rum 16:20).
  • Usifanye jambo lililo zaidi ya uwezo wako kwa kujionyesha au kujipendekeza (Ayubu 32:21-22, matendo 12:22-23)
  • Usiahidi zaidi ya uwezo wako (timiza ahadi kwa wakati Muhubiri 5:4-5)
  • Uwe mwaminifu kwa Mungu, kwa Wanadamu na kwa wakati
  • Ondoa kiburi, kuwa mtii na mnyenyekevu siku zote (mithali 29:23)
  • Kumbuka mema yote Mungu aliyokwisha kukutendea (itakusaidia utakapokata tamaa au kukatishwa tamaa)

  • Mche Mungu na kujiepusha na uovu wa kila aina

Kumcha Mungu kunaongeza siku bali miaka ya wasio haki itapunguzwa
(methali 10:27). Kuongezwa siku ni pamoja na kuwa na afya njema pamoja na
Mafanikio katika Mwili na Roho. Uovu ni sawa na uchafu. Kama vile ambavyo mahali pachafu huwavutia Inzi. Methali 3:6-8, 16:17 Katika njia zako zote mkiri yeye naye atayanyosha maapitoyako.

Utajiri na heshima zinapatikana kwa Mungu wetu (mithali 8 :18, 13 :7)
Hivyo inawezekana ukayafurahiya maisha yako ya kila siku, lakini maisha yanakuwa na maana zaidi pale mtu atakapokuwa mwaminifu kwa Mungu – kuishi maisha yanayompendeza Mungu au yenye hofu ya ki-Mungu.

Onyo : Mafanikio au utajiri ambao mtu anaupata kwa wizi, utapeli, rushwa (iwe ya pesa, mwili, vitu n.k), ubadhilifu, kuwaendea waganga wa kienyeji na wachawi au kudiriki kuua binadamu mwenzio n.k, utajiri huo huleta majuto sikuzote, hauleti utoshelevu, hauwezi kudumu na huwezi kuishi maisha ya amani na furaha. Utajiri wa kweli na wenye kudumu hutoka kwa Mungu, Hivyo tuwe na maisha ya uchaji wa Mungu, pamoja na kujishughulisha. Lakini masuala ya Mungu tuyape kipaumbele, hivyo hata tukifanikiwa, hatutaziabudu mali zetu wala kuzitanguliza bali tutamuabudu na kumtanguliza Mungu (mathayo 6 :33)
-          Baraka za Mungu(mafanikio yatokayo kwa Mungu) hutajirisha wala hazichangamani na huzuni (mithali 10 :22)
-          Baraka za Bwana hazimfanyi mtu kukosa muda wa kupumzika au kutulia na familia yake ndugu jamaa na marafiki
-          Baraka zilizotoka kwa Mungu, hazimfanyi mtu kukosa nafasi ya kumuabudu Mungu wake.

  • Usilipe tatizo heshima na hadhi, muone Mungu kuwa mkubwa kuliko tatizo lolote.

Tatizo la kuwa na macho mawili  yaani  kuutazama ukuu wa Mungu na ukubwa wa matatizo kwa wakati mmoja, liliwapelekea wana wa Israeli hali ya kushindwa walipopanga vita na wafilisti (1 Samweli 17). Baada ya Israeli kutoka kwenda kupigana wakiwa na imani kabisa kwa Mungu, walipomtazama Goliati mwenye jumla ya vidole ishirini na nne mikononi na miguuni mwake, imani yao ikawa kama moto uliomwagiwa maji, na ghafla kukiri kwao kwamba yuko Mungu wa Israeli kukageuka kuwa wimbo kama wengi wanavyoimba leo lakini katu hawako tayari kupigana vita.
Kumbuka tatizo siyo tatizo kabla hujaanza kuliheshimu kuwa ni tatizo; siku unapoanza kulihesabu na kulipatia heshima ndani yako ya kuwa tatizo, ndipo litakapoanza kuwa tatizo na litaanza kukusumbua maishani, hata kukufanya uishi maisha ya kukata tamaa siku zote.

Njia nzuri ya kuyashinda siyo kuyapatia heshima au hadhi ya kuwa tatizo, bali anza kuyatazama kama Paulo (2 Wakorinto 12:8-10) kwa imani kama njia ambayo Mungu ataitumia kukuongezea neema yake na siyo kukata tamaa.
Si ajabu kusema kwamba Mungu anaweza kuruhusu  udhaifu au hali fulani katika maisha yetu ili anapotuongeza, anapotuinua, anapotubariki kwa neema yake,  hali au udhaifu huo utukumbushe kwamba tunamuhitaji yeye siku zote. Ili tunyenyekee badala ya kuwa na kiburi na kujiinua katika maisha yetu na kujiona bora kuliko wengine.

  • Usisahau mema yote Mungu aliyokutendea 

Wakati watu wengine wanahesabu idadi ya matatizo yaliyopo au yaliwatokea maishani, wewe hesabu baraka zako(mema yoteMungu amewahi kukutendea) huku ukiyatazama malengo au maono yako, hapo ndipo utaona kwamba idadi ya baraka ni kubwa kuliko idadi ya matatizo. Kumbuka jinsi Mungu alivyokulinda tangu tumboni mwa mama yako, aliyekulinda tangu utotoni mpaka hapo ulipo

  • Jizoeze, jiumbie tabia ya kucheka  (Badala ya kununa)
       (Zaburi 2:4)Yeye aketiye Mbinguni anacheka…..

Mara nyingi watu ambao hawacheki, wana dhulumiwa na mawazo na fikra zao. Hivyo wanaonekana kana kwamba ni wazee kuliko umri wao halisi. Wanadhani kuwa maisha ni “biashara isiyotaka mchezo” hivyo basi , hawapati au kuwa na sababu ya kutabasamu, achilia mbali kucheka. Lakini kumbuka kicheko ni dawa hata ya kiroho. Hii ndio maana Biblia inasema kuwa “ moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa” (Mithali 17:22)

  • Usikubali hali ya maisha iamue furaha yako.

Wakati inapokuwepo hali ngumu, huo ndio wakati wa kucheka. Ndio maana maali pengine Biblia inasema, hesabuni kuwa ni furaha tupu, mkiangukia  katika majaribu mbalimbali (Yakobo 1:2)

Inawezekana umekuwa ukupitia wakati fulani mgumu au majaribu fulani, na mda wote huo umeonekana kama mzee kwa ajili ya kununa/kukata tamaa; na hakuna faida uliyoipata. Hebu badili mtazamo, irudishe furaha yako, tabasamu na uwe mtu wa kucheka daima huku ukimtegemea Mungu badala ya kuyatazama matatizo, uone jinsi Mungu atakavyo kutokea na utukufu wake.

Ukizoea kumcheka ibilisi katikati ya majaribu, ni mojawapo wa uamuzi wa mtu anayetaka kuishi maisha ya ushindi. Unapopatwa na jaribu au ugumu wowote, jitenge maali penye utulivu na uanze kutafakari nyakati amabazo Mungu amekutendea mema na uanze kucheka. Baada ya muda kicheko chako kitatoweka, kitabaki kicheko cha ki Mungu na mara moja hali uliyokuwa unaona ngumu itatokomea, utajikuta ukinena au kukiri neno la Mungu litakalo badilisha mtazamo wa maisha yako.

Kumbuka furaha ya Mungu ni nguvu yako (Nehemia 8:10)
Hivyo jiumbie moyo wa furaha daima.

  • Simama Kwenye Ahadi Ya Mungu

Petro anatuasa kuwa wanyenyekevu chini ya mkono wa Mungu, kumtwika Yeye fadhaa zetu, kuwa na kiasi, kumpinga Shetani na kuwasaidia wengine wanaoteseka (1Pet 5:6-11). Zipo ahadi nyingi nyingi katika kitabu kitakatifu (Biblia) kwa ajili ya wote wamchao Mungu. Kisome kitabu hicho kwa bidii, nawe utaziona, nazo zitakuwa msaada kwako.

  • Jifunze kumshukuru Mungu (Usinung’unike)

Neno la Mungu linasema shukuruni kwa kila jambo. Kushukuru ni kimyume cha kunung’unika. Unapomshukuru Mungu kwa imani katika maombi yako au kwa hali yoyote ile utakayosikia ndani yako nguvu ya manung’uniko na malalamiko inakosa nafasi au upenyo katika nafsi yako. Na neema ya Mungu kukupa nguvu ya kupita au kuyashinda mambo ambayo kibinadamu hayawezekani kabisa. Utajikuta ukijiuliza yaliwezekanaje au nilivukaje nilishindaje, hiyo ndiyo kazi ya Neema ya Mungu. Inaweka akili, nafsi na roho yako katika hali ya kuhifadhiwa salama bila mahangaiko katika hali ambayo siyo rahisi mwanadamu timamu kuhisi usalama kama siyo Neema hiyo kuingilia kati.
Katika Wafilipi 5:6,7 “Msijisumbue kwa neno lolote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mung ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu”
Kumbuka kuwa tuko vitani na uwanja mkubwa wa vita vya kiroho uko katika akili zetu. Shetani anapotaka kupigana vita na wewe ili kukushinda na kuuharibu uhusiano mzuri ulioko baina yako na wazazi wako au na kiongozi wako au kuondoa amani na upendo katika ndoa yako, atarusha wazo katika akili yako. Atakuonyesha kwamba hujafanikiwa kwa sababu hao wazazi wako hawakukujengea msingi mzuri wa maisha. Ataleta wazo katika akili yako kwamba huyo kiongozi wako hakutambui, anakubagua nk. Unaona? Biblia inasema shetani ni muongo na baba wa wale wanauamini huo uongo wake katika fikra zao.
Atarusha wazo katika akili yako kukuonyesha jinsi ulivyokosea kuingia katika ndoa na mwanaume au mwanamke huyo asiye na kipato cha kutosha au kazi maalumu ya heshima. Hayoyote ni kwajili ya kukukatisha tamaa ili usiendelee. Mawazo haya ndiyo yanayoitwa vita vya kiroho (Spirtual war fare) Neno linasema “Maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome; tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijinuacho juu ya elimu ya Mungu; tukiteka nyaraka kila fikra ipate kumtii Kristo” 2Wakorintho 10:4,5.

Kwa upande mwingine mawazo hayo yanaitwa ‘Mishale yenye moto ya yule adui’ Paulo akasema “Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu” Waefeso 6:16. Kabla shetani hajakushinda huitikisa kwanza akili yako (mawazo). Anarusha kwanza mishale yenye moto juu ya kuta za misimamo yako ya Kiroho.
Katika historia ya Biblia walikuwa wanatumia upanga kama silaha na pia walitumia mishale ya kawaida na mingine iliyopakwa lami. Hivyo kama wangefika katika mji uliozungukwa na ukuta mrefu na mpana mishale hiyo iliyopakwa lami na kuwashwa moto kurusha katika ukuta huo na ukuta wote ungewaka moto na hatimaye utabomoka na walioko ndana watashambulia bila kupingwa na kitu chochote. Hivyo hayo mawazo (mishale yenye moto ya shetani) unaporuhusu katika akili yako
utajikuta yameshuka mpaka moyoni mwako na ndipo utaanza kushuhudia kuta za misimamo yako mizuri inaanza kushambuliwa na kubomolewa kabisa na mashambulizi ya kiroho yatakuwa makubwa na utajikuta umeshindwa kabisa.
Mtume Paulo anaposema amani ya Kristo (Neema ya Kristo) ipitayo akili zote itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu, ana maana kuwa unaposhukuru kwa imani badala ya kujisumnbua na kunung’unika kwa ajili ya hilo ambalo wazo baya limekuja juu yako kwa ajili yake. Neema (Amani ya Kristo) itaachiliwa katika akili yako ambayo itakusaidia kuendelea kubaki ukiwa na moyo safi na nia safi (maamuzi sahihi juu ya wazazi wako, mke au mumeo, marafiki na viongozi wako). Hivyo huwezi kuishi maisha ya kukata tamaa au kukatishwa tamaa.

Kwa njia hiyo, Utawapenda na kuwaheshimu wazazi wako, viongozi wako na hata wale wasiyokutakia mema, wanao kunenea vibaya nk. maana nia yako imefichwa ndani ya Yesu Kristo. Na hapo unakuwa mshindi dhidi ya mishale hiyo ya adui na kuta za misimamo ya imani yako itabaki imara daima.
Isaya 40:31, Neno linasema “Bali wao wamgonjeao Bwana watapata nguvu mpya watapanda juu kwa mbawa kama tai”
Badala ya kunung’unika katika mambo yenye utata katika maisha yako, msubiri Bwana kwa imani katika maombi na kumshukuru yeye. Kumbuka manung’uniko ndiyo yaliyowaua wana Israeli jangwani. Unaponung’unikia, utashindwa kuchukua hatua ya ya kusonga mbele, huwezikuona nuru ya mafanikio ndani yako kwani kilichoujaza moyo wako ni manung’uniko. Inakubidi umshukuru Mungu katika kila jambo ili Neema yake iendelee kuwa juu yako. Ni afadhali kupoteza kila kitu lakini siyo neema, ndiyo nguvu yako. Manung’uniko siyo ishara ya mtu anayeishi kwa imani bali  kinyume chake. Maana anayeishi kwa imani atatiwa nguvu kwa imani akimshukuru Mungu maana anaiona ahadi ya Mungu. Ibrahimu mtu wa Imani alitiwa nguvu kwa imani hiyo akamtukuza Mungu katika mazingira yaliyokuwa na utata.
Warumi 4:20 “Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini bali alitiwa nguvu kwa imani huku akimtukuza Mungu” Ibrahimu hakulemewa katika uwanja wa vita vya kiroho (Akili), bali alipomtukuza na kumshukuru Mungu kwa imani Neema ya Mungu iwezeshayo ilimsaidia kudumu katika mpango wa Mungu mpaka alipotenda mambo makuu katika maisha yake. “Bado unanafasi ya kutenda mambo makuu ndani yako, usikate tamaa”.

  • Tembea katika Nguvu ya Mungu

Neno la Mungu ndiyo mwisho wa matatizo yote. Unapoliamini na kulikiri linatenda. Neno la Mungu pekee ndilo linaweza kugeuza laana kuwa baraka, kushindwa kuwa ushindi, ugonjwa kuwa uzima, umasikini kuwa utele. Linaweza kuumba na kufanya kisichokuwepo kikawepo. Tatizo ni pale wengine wetu hawalijui au hawaliamini neno. Watu wanapolijua neno la  Mungu na kuliamini kwa asilimia zote na kulikiri, watatembea kama wafalme na siyo kama watumwa. Lakini kwa kutokuliamini neno wengi wanaishi chini ya kiwango kilichokusudiwa na Mungu juu yao.

Sulemani kwa kujua nguvu na baraka za neno la Mungu ilimshangaza kuwaona watumwa (wasiomjua Mungu) wamepanda farasi huku wafalme (waliomjua Mungu) wanatembea kwa miguu – wanaishi chini ya alama zilizokusudiwa. Sulemani akasema katika Mhubiri 10:5-7 “Liko baa (janga) nililoliona chini ya jua, ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi (matajiri) hukaa maali pa chini. Mimi nimeona watumwa wapanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.”

Shetani amewafunga wengi wasilipende neno la Mungu, wasiwe hatari kwake. Ebu tafakari, wanaomiliki biashara kubwa, magari ya kifahari, wanaosomesha watoto shule nzuri wengi ni watu wasiomjua Mungu kabisa. Si vibaya wao kumiliki vitu na vimewekwa kwa utukufu wa Mungu na sote tu watu wake. Ukitazama sana utakuta idadi ya kubwa ya watu wasioweza kujimudu kimaisha ni wale wanaomjua Mungu (Ingawa si wote) shida ni nini? Kwa kutokulijua neon, watumwa wamepanda farasi na wafalme wanachapa mwendo kwa miguu (wanasota wanaishi chini ya kiwango). Hii ni kwa sababu wanalidharau neno au hawaliamini. Unapotangaza semina za Neno la Mungu au vipindi vya mafundisho (Bible study) hawaji, lakini wanapotangaziwa mikutano ya miujiza watakuja wote. Wanapenda miujiza kuliko neno la Mungu. Sina maana miujuza ya kimungu ni mibaya ila nataka ieleweke tu kwamba msingi wa miujiza tunayofanya ni neno la Mungu pekee. Ndiyo maana magonjwa mengi na matatizo bado yako ndani ya watu wanaojiita kuwa wanamwamini Mungu. Wengine bado wanaogopa wachawi, mapepo, laana na hofu ya magonjwa kwamba yanaweza kuwavamia wakati wowote.

Kwanini uendelee kuishi kama mtumwa wakati neno la Mungu liko. Usikubali kuwa mtumwa wakati umeshawekwa huru. Usishindwe wakati tayari ushindi upo. Usiendelee kulipa gharama ngumu kwa ajili ya  afya yako na maisha yako wakati Yesu ameshalipa gharama zote msalabani. Je utakufa njaa wakati chakula kiko mezani tayari? Kwanini uwe mfungwa katika gereza la magonjwa, laana mapepo, umasikini na mateso wakati unazo fungua mikononi mwako? Unaweza kutoka na kuwekwa huru. Neno la Mungu ndiyo ukombozi. Kuanzia leo, kataa maisha ya kukata tama.

  • Tabiri nguvu ya uumbaji juu ya mifupa mikavu.

Kuna tafauti kubwa kati ya bonde na shimo. Shimo huchimbwa kwasababu fulani, hivyo huwa ni kitu kidogo. Na hata likijitokeza lenyewe, hufukiwa mara moja. Bonde si rahisi kulifukia na kama itabidi, basi itagharimu pesa yingi, nguvu na mambo mengi. Maana yapo mabonde yaliyokuwepo tangu misingi ya ulimwengu kuwepo. Hivyo takataka zote za uchafu wa mvua au zinazozolewa katika miji mikubwa, hutupwa kwenye bonde. Mungu akamwambia Ezekiel tabiri katika lile bonde lililojaa mifupa mikavu ya watu waliokufa siku nyingi ili wawe hai tena. Alipotabiri kwa neno la Bwana ile mifupa ikawa hai tena.
Ezekiel 37:1-10 mistari 4,7,10 inasema “Akamwambia tena toa unabii juu ya mifupa hii, uiambia tena unabii juu ya neno la Bwana nikatoa unabii kama nilivyoamriwa hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama tetemeko la nchi na ile mifupa ikasogeleana mfupa kwa mfupa mweziwe. Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikamwingia, wakaishi wakasimama kwa miguu yao jeshi kubwa mno”.

Fikiri jeshi la watu wengi waliokufa miaka mingi na mifupa yao iko katika bonde moja. Nani angejua mguu wa huyu ndio ule au mkono wa yule uko pale au kidole cha yule au fuvu la huyu na jino lake liko wapi. Hata Ezekiel ilimshinda akasema ‘Bwana wewe wajua’. Lakini mara tu alipoanza kutabiri katika bonde lile la mifupa ghafla mifupa ilianza kusogeleana (kutafutana) na kuungana. Kila mfupa ulimtafuta mwenzake. Kila mfupa ulimfuata mwenyewe na hatimaye likasimama jeshi kubwa la watu likiwa hai tena.

Katika maisha, kuna wakati mbao umesongwa na magumu, shida, matatizo, huzini au hali inayokatisha tamaa kwa kiwango ambacho akili zako, elimu yako, nguvu zako, haziwezi. Lakini neno la Mungu lina nguvu ya kuumba upya. Neno ndiyo Mungu mwenyewe. Neno limebeba upako wa kuumba ma kuhuisha vilivyo kufa. Unahitaji upako huu wa uumbaji ndana yako ili uweze kuumba na kufufua vilivyo kufa kwa kutabiria maisha yako au ya mtu mwingine kwa neno la Bwana huku ukiwa na imani yenye nguvu. Nguvu hii kubwa kuliko nguvu yoyote ya umeme inayoweza kutengenezwa na mwanadamu (This power is greater than any electric company could ever produce) ndiyo iliyomfufua Lazaro, ndiyo iliyoshusha moto kutoka mbinguni, ndiyo inayokausha magonjwa yote.
Tabiri sasa juu ya mifupa mikavu ipate kuishi tena. Pengine mwili wako umekuwa mifupa kila wakati magonjwa yanakuandamana na unapoteza fedha nyingi kwa ajili ya matibabu na pengine umekosa msaada. Au pengine ni ndoa, uchumba, elimu, kazi nk.
Lazima kili jambo, kila kitu kirudi kirudi tena upya. Ni marufuku kukata tamaa, ni wakati wako kwa kutabiria maisha yako, familia yako, ukoo wako, nugu, jamaa au mwili wako uwe na afya njema  kwa kuamini na kukiri neno la Mungu. Isaya 53:4-5.

  • Ijue thamani yako

Yohana 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe
wa pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.

Unapoingia katika duka kununua  kitu, kuna alama au nembo ya bei zinazotambulisha “thamani” ya kile unachotaka kukinunua. Hivyo utalipia pesa yenye thamani ya kitu ulichonunua peke yake.

Mungu alionyesha wazi na dhahiri thamani yako, alipomtuma Yesu aje akufie msalabani. Ebu fikiria, hakumtuma malaika mwenye cheo zaidi mbinguni au malaika yeyote au wote kwa pamoja waje wakufie, alimtuma mwanaye wa pekee. Kwa Mungu hiyo ilikuwa alama ya bei ghali. Kama ingekuwa wewe peke yako ndiye unayeitaji wokovu duniani, Yesu bado angekuja. Hivyo kulingana na Mungu, thamani yako ni maisha na damu ya mwanaye Yesu Kristo(warumi 5:8).

Mtu akikuuliza ni kwanini unadhani kuwa wewe ni mtu wa thamani au maalumu (special) Mwambie kilicholipwa ili upate wokovu. Simama leo, ishi maisha ambayo Mungu amekuitia kuishi. Kama vile alivyo Yesu, nawewe ni wa thamani mbele za Mungu.

  • Taka sana/tamani sana kuongozwa na roho wa Mungu

Ikiwa wewe ni mcha Mungu, na zaidi sana, mwana wa Mungu, Basi, unamuhitaji Roho wa Mungu. Yale tusiyoweza, Roho wa Mungu anaweza, yale tusiyoyajua, hata maisha yetu ya baadaye, yeye anayajua. Anazijua hata sari za mbinguni. Tuna muhitaji huyo, maana ndiye pekee awezaye kutusaidia katika dunia hii iliyojawa matukio ya kutisha, shida, dhiki, misukosuko na maasi ya kila namna. Ni roho wa Mungu awezaye kutusaidia katika udhaifu wetu na kutuombea (Warumi 8:26-27)


BAADHI YA JUMBE KUTOKA KWA WATUMISHI NA WATU MBALIMBALI

KUKATA TAMAA
Christopher na Diana Mwakasege

Salamu katika Jina la Yesu,
Kukata tamaa ni kutokuamini. Kutokuamini ni kutokuwa na uhakika. Kutokuwa na uhakika kunazaa hofu na wasiwasi. Hofu na wasiwasi vinazaa kusita sita. Kusita sita ni jamii ya mashaka. Mwenye hali ya namna hii asitegemee kupokea kitu toka kwa Mungu (Yakobo 1:6-8).
Ukiomba utapewa, uwe na uhakika na jambo hili, kwa kuwa ndivyo Baba alivyotuahidi.
Ibrahimu aliomba kwa ajili ya watakatifu wa Sodoma na Gomora, Mungu alimjibu (Mwanzo 18:16-33)
Musa aliwaombea msamaha wana wa Israeli, Mungu akamjibu na akawasamehe (Kutoka 32:9-14).
Eliya aliomba Mungu ajidhihirishe kwa wapinzani wake, akasikiwa na moto ukashuka toka mbinguni (1Wafalme 18:30-40)
Eliya aliomba mvua isinyeshe juu ya nchi kwa muda wa miaka mitatu na nusu, akasikiwa na Mungu, na mbingu zikafungwa (Yakobo 5:17). Pia, baada ya miaka hiyo mitatu na nusu aliomba kwa bidii mvua inyeshe, - na Mungu akajibu na mvua ikanyesha.
Yesu Kristo alituombea msamaha Mungu akatusamehe, na hadi leo bado tunaendelea kuupokea msamaha huo, kwa njia ya msalaba – kila tunapotubu dhambi zetu.
Kanisa liliomba kwa juhudi, wakati wa Mtume Petro, alipokabiliwa na hukumu ya kifo, na Mungu akajibu kwa kumtuma malaika kumfungua (Matendo ya Mitume 12:5-19). Elizabeth na Zakaria waliomba wapewe mtoto katika ndoa yao, Mungu akawajibu kwa kuwapa Yohana (Luka 1:5-48).
Omba, nawe utapewa. Usiwe mwepesi kukata tamaa. Mungu si mwanadamu hata aseme uongo. Ni tabia yake kujibu maombi ya watu wake.
Tunamwabudu Mungu yule yule wa Ibrahimu, wa Musa, wa Eliya, wa Yoshua, wa Yesu, wa Mitume. Wala hana kigeu-geu. Aliloahidi analifanya. Ameahidi kujibu maombi, kwa hiyo uwe na utayari wa kupokea.
Si tabia ya Mungu kutokujibu maombi ya watoto wake. “Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema , je! si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?” (Mathayo 7:9-11).
Ni furaha ilioje kwa mtoto kujua kuwa atapewa na Baba yake kile alichomwomba? Je! si zaidi sana sisi tulio wana wa Mungu katika Kristo, kwa kuwa Baba ameahidi kutufurahisha kwa kutupa tuombayo?
Kama ulikuwa umefika hali ya kukata tamaa, na kuona Mungu hajasikia kilio chako, tunakuambia ujipe moyo mkuu, kwa kuwa Mungu ameahidi kukupa ulichoomba sawa sawa na mapenzi yake juu yako.
Je! unaweza kwenda kuomba kitu kwa mtu ambaye unajua ni mnyimi ambaye hatakupa kile utakachomwomba hata kama anacho?
Je! unaweza kuomba kwa Mungu ambaye hajali wala hajibu maombi ya watu wake? Iko faida gani ya kumwamini na kumtumikia Mungu wa namna hiyo?
Lakini tunaye Mungu anayejibu kwa jina la Yesu Kristo! Huyu ndiye tunayemwamini. Watu wa kale waliijua siri hii. Hata mfalme Yehoshefati alipokuwa amezungukwa na majeshi ya adui, aliomba kwa Mungu ajibuye, na Mungu akampigania na kuwaangamiza maadui (2 Mambo ya Nyakati 20:1-30) – Ukiwa na matatizo mwombe Mungu naye atakusaidia.
Weka hili katika roho yako. Ni tabia ya Mungu katika Yesu Kristo kujibu maombi ya watu wake.
Na usidhani ya kuwa ahadi za Mungu ni kwa Wakristo fulani tu. La hasha, bali ni kwa kila mkristo. Kwa kuwa imeandikwa ‘kila’ aombaye hupokea (Mathayo 7:8). Neno ‘kila’ lina kujumlisha na wewe! Nafasi yako uliyopewa usimpe mtu mwingine. Simama katika nafasi yako ndani ya Kristo, kwa kuwa ukiomba utapewa!
Kiini cha furaha ya Mkristo, ni mawasiliano yasiyokatika kati yake na Mungu wake. Bila kujibiwa maombi, wokovu unakosa ladha inayotamanika na kutumainisha. Furaha ya wokovu ni pamoja na kujibiwa maombi. Kwa hiyo hakikisha unajifunza na kufahamu kuomba maombi yanayojibiwa.
Tatizo la kukata tamaa
Rafiki yetu mmoja alituambia maneno ambayo tunaona yanaelezea sababu ya sehemu kubwa ya watu kurudi nyuma kiroho.
Alisema hivi, “Nimegundua siku hizi ya kwamba wakristo wengi wamerudi nyuma kiroho, kwa kuwa hawajapata majibu ya maombi yao!”
Tukamwambia, “Hiyo ni kweli kabisa!”
Akaendelea kusema, “Kuna mtu mmoja, ambaye alikuwa ameokoka siku nyingi, na ni mhubiri wa injili, ambaye ameamua kuacha wokovu, kwa kuwa alimwomba Mungu apate mtoto kwenye ndoa yake, lakini alikuwa bado hajapata, wakati umekwisha kupita miaka kumi.
“Pia aliomba kwa Mungu ajazwe Roho Mtakatifu ili anene kwa lugha mpya, lakini miaka mingi imepita bado hajanena kwa Lugha Mpya. Kwa ajili hiyo siku hizi ni mpinzani mkubwa wa wokovu. Na anaona hata kunena kwa Lugha Mpya si jambo la kweli”.
Tulitafakari habari hii, na tuliona ya kuwa ndugu yetu huyu alikuwa amepatwa na tatizo la kukata tamaa.
Na wakati mwingine tulikutana na Mzee mmoja ambaye alitueleza matatizo ya magonjwa yaliyoikumba nyumba yake. Akatuambia mke na watoto wake wawili wana ugonjwa ambao hospitali zimeshindwa kuutibu.
Tukamwuliza, “Wewe ni Mkristo”? Akajibu, “ndiyo”
Tukasema, “Unafahamu ya kuwa ukiomba lolote kwa Mungu utapewa, kama yasemavyo maandiko?” Akasema “Niliwapeleka wagonjwa hawa kwa kiongozi wetu wa kanisa, na aliwaombea mara nyingi lakini hawakupona!” Tukamwuliza tena, “Ulipoona hawajapona ulichukua hatua gani?”
Akajibu akasema, “Niliamua kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji, na hadi sasa nimekwisha zunguka kwa waganga wasiopungua arobaini”
Tukamwuliza “Na je! Hali ya wagonjwa ikoje sasa? Akasema, “Bado hawajapona, ingawa nimekwisha tumia fedha nyingi sana, bila mafanikio …..!!
Kwa kukosa majibu ya uponyaji wa familia yake, ndugu huyu aliamua kuvuka mipaka ya ukristo wake, na kutafuta njia nyingine ili apate msaada.
Pia, huyo alikuwa amekata tamaa, na kuona ya kuwa Mungu hatajibu maombi yake.
Hali ya namna hii imewasonga wakristo wengi sana, ambao kwa kutopata majibu yao kwa muda wanaotaka na kwa njia wanazotaka, wanaamua kutumia njia nyingine, ambazo ni kinyume na ukristo wao, ili wapate mahitaji yao.
Je! Sikio la Mungu ni zito kiasi cha kwamba hawezi kusikia maombi ya watu wake?
Lakini Biblia inasema,
“Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka hata usiweze kuokoa, wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia” (Isaya 59:1).
Na, vile vile kwa kujua hali ya wakristo ya kutokuwa na uvumilivu, imeandikwa ya kuwa
“Imewapasa kumwomba Mungu siku zote, wala wasikate tamaa” (Luka 18:1)
Inawezekana ya kuwa hata wewe unayesoma haya umo katika hali ya kukata tamaa-au unamfahamu mtu ambaye yumo katika hali kama hii ya kukata tamaa. Inawezekana umemwomba Mungu juu ya hitaji lako, lakini hujapokea majibu. Na kwa sababu hiyo umeamua, au unajitayarisha kutumia njia nyingine iliyo kinyume na maadili ya Kikristo, ili kupata hitaji lako.
Sasa! Kabla ya kuchukua hatua hiyo, tulia kwanza na usome ujumbe huu, na uyatafakari yaliyomo, na uyatendee kazi; Kwa kuwa Roho wa Mungu, ameuweka ujumbe huu mikononi mwako, kwa makusudi kamili ya kuinua maisha yako ya maombi.
Na utakapozidi kuyatafakari yaliyomo utaona ya kuwa ni tabia ya Mungu kujibu maombi ya watu wake. Na ukijua hili, utaona ya kuwa si busara mtu kukata tamaa ya kujibiwa, unapomwomba Mungu kitu.
Wengi hawana furaha ya kweli katika maisha yao kwa kuwa wameomba, lakini hawajapata walichokiomba. Kwa kuwa bado hujapata ulichokiomba, haimaanishi ya kwamba Mungu hajibu maombi. Mistari hiyo tuliyosoma ni baadhi tu ya ile inayotuonyesha tabia ya Mungu ya kujibu maombi.
Maombi ni kuzungumza na Mungu, na Mungu aseme na wewe, Watu wengi wameifahamu siri hii kwa muda mrefu, kama tunavyosoma katika agano la kale.
Unapoomba uwe na utayari wa kupokea na siyo utayari wa kutokupokea. Ni tabia yake Mungu kukujibu maombi yako.

Kumbuka yafuatayo
1. Kwa kuwa Yesu Kristo hajabadilika, Ni yeye yule, jana, na leo, na hata milele; na ya kuwa hana upendeleo, ukikata tamaa ina maana imani yako kwake imeyumba. Kwa sababu kukata tamaa ni kinyume cha imani. Imani ni kuwa na uhakika (Waebrania 11:1), na kukata tamaa ni kutokuwa na uhakika. Palipo na imani hakuna kukata tamaa. Ukikata tamaa maana yake imani yako imeondoka juu ya kitu hicho ulichokikatia tamaa.
Inawezekana ni jambo ulilokuwa unaliombea au kulitafuta kwa muda sasa. Na kwa sababu hiyo au umeacha kuomba au unakaribia kuacha kuliombea, au tayari umeingiwa na mawazo ya kuwa si mapenzi ya Mungu upate unachokiombea kwa sababu tu hujajibiwa. Je! ni kazini? Ndoa yako? Wazazi wako? Mume wako? Mke wako? Watoto wako? Mwenzi wa maisha? Fedha? Masomo? Madeni? Huduma? Kanisani kwako? Biashara? Nyumba ya kuishi?
2. Kuna vyanzo mbalimbali vinavyoweza kumfanya mtu akate tamaa hata kama anasema ameokoka. Biblia imetupa mifano ya namna ya kukabiliana na hali hizo. Mifano ya vyanzo vinavyoweza kukukatisha tamaa ni hii:
(i) Chanzo cha Kwanza ni Mungu kuchelewa kujibu maombi yako. Yesu alisema imetupasa kumwomba Mungu siku zote, wala tusikate tamaa. Habari hii imo katika Luka 18:1-8. Pamoja na kwamba inawezekana Mungu anakuvumilia tu kwa sababu kuna jambo unalofanya ambalo halimfurahishi, hategemei uache kuomba kwa kuwa amechelewa kukujibu katika wakati uliotaka. Endelea kuomba. Kuacha kuomba na kukata tamaa, ni kuonyesha ya kuwa imani yako ina shida.
· Katika Luka 11:5-13 Yesu Kristo pia ametoa mfano mwingine wa mtu na rafiki yake. Jambo alilokuwa anasisitiza ni lile lile la “kutokuacha kuomba”. Akitaka tuombe hadi tupewe, tubishe au tupige hodi hadi tufunguliwe; na tutafute hadi tuone.
· Katika Mathayo 15:21-28 tunaona mfano wa mama mkananayo ambavyo imani yake kwa Yesu haikumpa nafasi kukata tamaa au kukatishwa tamaa. Mara ya kwanza Yesu hakumjibu Neno. Ungeweza kutafsiri ya kuwa Mungu alikaa kimya! Je! umewahi kuwa na hali ya namna hii? Kuona kama Mungu amekunyamazia au hakujibu kitu? Je! umeamua nini? Je! hali ya kutojibiwa imekukatisha tamaa? Yule mama Mkananayo hakukata tamaa hata baada ya wanafunzi wa Yesu kutoona uzito wa tatizo lake. Yesu aliendelea kujitetea ili asimsaidie yule mama mara mbili zaidi, kabla ya kumponya binti yake. Huko kung’ang’ania kwa mama huyo katika kumwomba msaada – Yesu aliita hali hiyo “Imani Kubwa”
(ii) Chanzo cha pili kinachoweza kukukatisha tamaa ni maneno ya watu
· Mfano wa kipofu Bartimayo katika Marko 10:46-52 unatupa picha nzuri ya hali hiyo. Usifikiri kila mtu aliye na Yesu au ameokoka atataka upate msaada toka kwa Yesu kabla yake. Wakati huyo kipofu alipopaza sauti yake kumwita Yesu ili amsaidie; Waliomzunguka Yesu walimkemea ili anyamaze! Biblia inasema; “….lakini alizidi kupaza sauti”. Na Yesu akasimama, akasikiliza shida yake na kumponya. Fikiria kama angekatishwa tamaa na kule kukemewa na wale waliokuwa karibu na Yesu – ni wazi kwamba asingepata uponyaji wa macho yake! Je! kuna maneno yaliyosemwa juu yako na wale ‘walio karibu na Yesu’ na yamekukatisha tamaa katika maisha yako ya wokovu na ukristo wako? Je! ni katika huduma yako? Tunataka tukutie moyo ya kwamba endelea kumwita Yesu na kumtumikia. Maana katikati ya maneno mabaya na kukukatisha tamaa namna hiyo, Yesu bado atakusikiliza usipokata tamaa!
(iii) Chanzo cha tatu kinachoweza kukukatisha tamaa ni mapokeo na mipaka ya dini yako. Tunafundisha hili tukitumia mfano wa mwanamke mwenye kutoka damu katika Marko 5:25-34. Huyu mama hakukubali vizuizi vya dini ya kiyahudi kwa akina mama “wenye kutokwa damu,” vimzuie kutafuta uponyaji kwa Yesu. Na wewe usikubali dini yako na mapokeo yake vikuzuie kutafuta msaada kwa Yesu.
(iv) Chanzo cha nne kinachoweza kukukatisha tamaa ni mazingira yanayokuzunguka unapotaka msaada kwa Yesu. Mfano mmojawapo ni watu waliobomoa dari ili kumpitisha mgonjwa wao afike mbele ya Yesu. Soma habari hii katika Marko 2:1-12. Hawa watu wangeweza kukatishwa tamaa na umati wa watu, na kutokuingilika kwa Bwana Yesu. Lakini imani waliyokuwa nayo iliwapa kutafuta njia ya kumfikia Bwana Yesu. Wangekata tamaa wangerudi nyumbani na rafiki yao bado mgonjwa. Yesu aliona ‘imani yao’ katika ‘njia’ waliyotumia kumfikisha mgonjwa mbele yake bila kukatishwa tamaa na mazingira magumu waliyoyakuta mahali Yesu alipokuwa.
Nia yetu ni kuona maisha yako yanafanikiwa na pia unajibiwa maombi yako unapoomba kwa Mungu, hasa unapojua ya kuwa ni tabia ya Mungu kujibu maombi ya watoto wake, usikate tamaa.
Tuzidi kuombeana.


PAMBANA HADI KUPATA USHINDI

Na Askofu Rodrick Mbwambo

Moja wapo ya maonyo yaliyotolewa na Yesu kwa wanafunzi wake wakati alipokuwa pamoja nao, ni onyo juu ya kutokukata tamaa. Yesu alisema hivyo kwa kutumia mfano wa hitaji la mwanamke maskini lililokuwa likishughulikiwa na kadhi dhalimu. Kila mara mama huyo alipolipeleka hitaji lake, kadhi huyo alionyesha kutokuwa tayari kulishughulikia. Hata hivyo pamoja na ugumu wa moyo wa kadhi huyu, bado aliendelea kumgongea yule kadhi, hadi pale alipopewa haki yake. Luka 18:2-5. Kwa kuwa kukata tamaa ni moja ya mambo yanayowazuia watoto wa Mungu kuvifikia vilele vya mapenzi ya Mungu katika maisha yao, uko umuhimu mkubwa kwa watoto wa Mungu kuelewa jinsi ya kupambana na vyote vinavyoinuka mbele zao, hadi pale ushindi unapopatikana.

Moja ya picha za watu waliopambana na hatimaye wakapata ushindi katika maisha yao, ni yule mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu katika Israeli, kwa miaka kumi na mbili. Katika kuteseka kwake, mwanamke huyu alipambana na magumu mengi, ila kamwe hakukata tamaa. Adui alimzingira pande zote, ila alipambana hadi pale alipokutana na mapenzi ya Mungu katika maisha yake. Mambo yaliyomwezesha kupenya na kupata ushindi, yanayoweza kukusaidia hata wewe, ni pamoja na haya yafuatayo:-

KUWA NA UTAYARI WA KUPAMBANA
“Na mwanamke mwenye kutokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuwepo katikati ya mkusanyiko uliomfuata Yesu.” Marko 5:25
Kila mara wakati wa kuuendea mji wa mafanikio, viko vikwazo vitakavyoinuka ili kumzuia mwamini kukutana na yale yaliyokusudiwa na Mungu kuwepo katika barabara ya maisha yake. Mwamini atakutana na ushindi katika maisha yake, pale tu atakapoamua kupambana na vikwazo hivyo na kuvishinda. Kile ninachotaka ukione hapa ni kuwa, mafanikio yoyote yatakayomjia mtu katika maisha yake, kwa sehemu yanategemea maamuzi anayoyafanya katika maisha yake ya kila siku na aina ya maamuzi hayo. Kama maamuzi yatakuwa mabaya, maisha yake yatadidimia badala ya kwenda juu.
Hivi ndivyo ilivyotokea kwa mwanamke huyu, usugu wa tatizo lake ulitengeneza vikwazo kadha wa kadha vilivyotakiwa kuvukwa kabla ya ushindi kupatikana. Ukiiangalia hali ya mwanamke huyu muda mfupi kabla ya kumwendea Yesu, unaweza kukubaliana nami kuwa, alikuwa na kila sababu ya kutoendelea na safari yake ya kutafuta uponyaji. Hata hivyo ingawa vikwazo vilionekana kuwa vikubwa kuliko uwezo wake wa kupambana navyo, yeye aliamua kupambana navyo. Kama tunahitaji kuuona ushindi katika maisha yetu ya kiroho au yale ya kimwili, ni lazima tuanze na mhimili huu wa kufanya uamuzi mzuri.
Vikwazo ambavyo mwanamke huyu aliamua kupambana navyo, ni pamoja na hivi  vifuatavyo:-

KUPAMBANA NA VIKWAZO VYA KIDINI
“Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo ni katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatokwa na damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutokwa na damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa  katika siku za kutengwa kwake; yeye ni najisi. Kila kitanda akilaliacho katika siku zote za kutoka damu, kitakuwa kama kitanda cha kutengwa kwake; na kila kitu atakachokilalia kitakuwa najisi, kama unajisi wa kutengwa kwake. Na mtu yeyote atakayevigusa vitu vile atakuwa najisi, naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.” Lawi 15:25-27
Mara nyingi katika maisha tunaweza kugundua kuwa vikwazo vinavyoongoza katika kuwazuia watu kukutana na mapenzi ya Mungu, ni vikwazo vinavyotokana na dini. Jimmy Swagart wakati fulani katika mahubiri yake alitamka kuwa, umati mkubwa wa watu watakaoingia Jehanamu, utaenda huko kutokana na vikwazo vya kidini na kitamaduni. Hivi ndivyo ilivyotukia kwa mwanamke huyu, baada ya tatizo lake kugeuka kuwa sugu, alikutana na kikwazo cha kidini kilichohitaji kuvukwa kabla ya muujiza kutokea. Mwanamke huyu  kama mwenyeji wa Mashariki ya kati na mwamini wa dini ya Kiyahudi, alijikuta katika karantini iliyotokana na andiko letu hapo juu la kutochangamana na watu kutokana na ugonjwa aliokuwa nao wa kutokwa na damu.
Mwanamke huyu angelisikia habari ya matendo makuu yaliyokuwa yakitendeka katika misafara ya Yesu ila kikwazo hiki cha kidini kilimwambia,”huruhusiwi kwenda!” Hiki ndicho kinachowatokea watu wengi katika miaka tuliyo nayo. Wanawaona wengine wakiokolewa na kupokea baraka mbalimbali za kiroho na kimwili, ila wao wanaishia kusema, “KWETU hatuokoki, hatuneni kwa lugha, hatuombei wagonjwa, na kadhalika.” Ili ukutane na mapenzi ya Mungu katika maisha yako, cha msingi ni kile kinachozungumzwa katika biblia na wala sio taratibu zinazopatikana katika tamaduni za mahali au dini. Hivi ndivyo mwanamke huyu alivyofanya, dini na utamaduni vilimwekea mipaka ila yeye akaweka juhudi za makusudi  kukivuka kikwazo hiki.

KUPAMBANA NA KUTOKUWA NA NGUVU KIFEDHA
“Amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya.” Marko 5:26
Kikwazo cha pili kilichomkabili mwanamke huyu katika kuuendea muujiza wake, kilikuwa ni kikwazo cha kutokuwa na nguvu kifedha. Ingawa huduma zilizokuwa zikitolewa na Yesu zilikuwa ni bure, bado kulikuwa na gharama ambazo wahitaji walipaswa kuzigharimia. Kwa mfano, kama mhitaji alikuwa mbali na eneo alipokuwa Yesu, ilimbidi yeye, ndugu au rafiki zake kugharimia zoezi la kumpeleka kule Yesu alipokuwa. Uhalisi wa ukweli huu, tunauona katika mojawapo ya huduma za Yesu, alizozifanya katika mji wa Kapernaumu. Baada ya habari za ujio wake kuenea kila mahali, kalamu ya Marko ilikuwa na haya ya kuandika. “Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake. Wakaja watu wakimleta mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.” Marko 2:1-2.
Kutokana na andiko hili, unaweza kuona kuwa, kulikuwa na gharama zilizotakiwa kulipwa ili kumfikisha mhitaji pale Masihi wa Mungu alipokuwa. Mbali na kugharimia usafiri, wakati mwingine kulikuwa kulipia gharama za chakula na malazi wakati wa kushiriki huduma zilizokuwa zikitolewa na Yesu. Marko akielezea mojawapo ya gharama hizi, aliandika yafuatayo:-  “hata zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa; uwaage watu hawa, ili waende zao mashambani na vijijini kando kando, wakajinunulie chakula.” Marko 6: 35-36. Kupitia mifano hii miwili, tunaweza kuona kuwa, ingawa Yesu aliwahudumia watu bure, bado kulikuwa na gharama za kibinafsi, zilizotakiwa kubewa na mhitaji. Kutokana na gharama hizi zilizotakiwa kubebwa na mhitaji, ni wazi zilitengeneza kikwazo kingine kwa mwanamke huyu aliyekuwa katika hitaji la kukutana na muujiza wake. Alitambua mahali ulipo muujiza wake, ila hali ya uchumi wake ilimwambia, huwezi kwenda huko.
Kutokuwa na nguvu za kifedha, kumewazuia watoto wengi wa Mungu kupanda ngazi za kiroho na kimwili zilizowekwa na Mungu mbele ya maisha yao. Roho Mtakatifu anaweza kuweka maono au dukuduku fulani ndani ya mtu, ila badala ya mtu huyo kuanza kuzitendea kazi dukuduku hizo, utamsikia akisema, “Sina pesa!” Waamini hawa wanashindwa kuelewa kuwa, katika mazingira ya kawaida, Mungu anapomtaka mtoto wake afanye kitu fulani kinachohitaji nguvu ya pesa, huwa haanzi kwa kumpatia mtu huyo pesa. Mungu huweka maono ndani ya mtu, na mhusika anatakiwa kuwa na utayari utakaoigeuza sifuri kuwa tarakimu iliyo na thamani. Katika hili mwamini anatakiwa akumbuke kuwa, hata ulimwengu tulio nao, ulitokana na vitu visivyoonekana.
Tukirudi katika habari inayomhusu huyu mwanamke aliyekuwa na tatizo la kutokwa na damu, tunaona kuwa alikuwa anataka kufanya mradi wa kutafuta uponyaji, ila nguvu yake ya kiuchumi ilikuwa sifuri. Ingawa hali yake ya kifedha ilikuwa mbaya kiasi hicho, bado hakukiruhusu kikwazo hicho kimzuie kufanya mradi aliokusudia kuufanya. Badala yake, aliamua kufanya yale yaliyokuwa katika uwezo wake ili kufika pale muujiza wake ulipokuwa. Ni baada ya kukishinda kikwazo hiki, ndipo alipofaulu kuwa miongoni mwa umati uliokuwa ukimfuata Yesu.
Kama unahitaji kutumiwa na Mungu na kuishi kama alivyokukusudia uishi, ni lazima uhakikishe kuwa, unakishinda kikwazo hiki kinachotokana na kutokuwa na nguvu za kifedha. Kile unachotakiwa kuanza nacho katika kupambana na kikwazo hiki, ni kujitamkia kuwa, “Pamoja na kutokuwa na nguvu za kiuchumi, hakuna kitakachonizuia kuishi maisha niliyokusudiwa na Mungu, niyaishi.”

KUPAMBANA NA  MADHAIFU YA KIMWILI
“…amegharimiwa vitu vyote alivyo nayo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake, ilizidi kuwa mbaya.” Marko 5:26
Udhaifu wa kimwili ni kikwazo kingine kinachotumiwa na Shetani, kuwafanya waamini waishi maisha yanayotofautiana na vile Mungu alivyowakusudia waishi. Katika miaka tuliyo nayo, watu wengi wamemruhusu Ibilisi kutumia udhaifu wa kimwili walio nao, kuwatenganisha na mapenzi ya Mungu katika maisha yao. Kuwa na udhaifu fulani katika mwili, kamwe hakutakiwi kuwa kigezo cha kumfanya mwamini asipige hatua kwenda mbele.
Katika hili nina mfano ulio wazi wa mtu, aliyemkatalia shetani kuutumia udhaifu wa mwili wake kumtenganisha na kusudi la Mungu katika maisha yake. Mtu huyu alizaliwa bila mikono na miguu, ila bado anaweza kucheza mpira kwa kutumia kichwa, anaweza kuogelea, pamoja na amefanikiwa kupata ujuzi unaompatia riziki yake ya kila siku. Hivi ndivyo ilivyotukia kwa mwanamke huyu aliyekuwa katika harakati za kukutana na muujiza wake, ingawa ugonjwa ulimfanya kuwa nusu mfu, bado alifanikiwa kupenyeza katikati ya umati mkubwa wa watu na kugusa vazi la Yesu.
Ni kweli udhaifu wa mwili, unaweza kumzuia mtu kuwa na kasi ya  mtu asiye na tatizo katika mwili wake, ila hauwezi kumzuia kwenda kwa kasi iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili yake. Katika hili, ninaamini kuwa, ‘Mungu ameandaa vilele vya  baraka kwa kila mtu na umbali wa kuvifikia vilele hivyo, unategemea vile uwezo wa mtu ulivyo.’ Kama unataka bendera ya maisha yako ya kiroho na kimwili ipepee, fanya kile kilichofanywa na mwanamke huyu. Yeye aliuangalia udhaifu aliokuwa nao kimwili na kusema, “Muda wote Yesu aishipo, bado lingaliko tumaini.”

KUPAMBANA KIKWAZO CHA UPWEKE
“Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo ni katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatokwa na damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutokwa na damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa  katika siku za kutengwa kwake; yeye ni najisi. Kila kitanda akilaliacho katika siku zote za kutoka damu, kitakuwa kama kitanda cha kutengwa kwake; na kila kitu atakachokilalia kitakuwa najisi, kama unajisi wa kutengwa kwake. Na mtu yeyote atakayevigusa vitu vile atakuwa najisi, naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni.” Lawi 15:25-27
Mara zote tatizo la mtu linapokuwa sugu, huwa ni rahisi mno kwake kukumbwa na roho ya upweke. Kwa mfano, kulingana na sheria ya Musa, mtu aliyekuwa na ugonjwa wa kutokwa na damu muda mrefu, huyo hakuruhusiwa kuchangamana na watu wengine waliokuwa wazima. Kwa maneno mengine, ugonjwa uliomkabili mwanamke huyu, ulimweka katika kifungo kibaya mno cha upweke. Mfano mwingine unaoonyesha vile matatizo sugu yanavyotengeneza upweke kwa mtu, tunaupata katika andiko lifuatalo; “Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima? Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani..” Yohana 5:6-7.
Kutokana na upweke huu unaozaliwa pale tatizo la mtu linapokuwa sugu, waamini wengi wameshindwa kumzalia Bwana matunda. Kama hili halitoshi, waamini wengi wachanga wamerudi nyuma kiroho, kutokana na roho hii ya upweke. Hata waamini wengi wachanga wanashindwa kuendelea na maisha ya wokovu, kutokana na upweke. Wako pia kinamama waliofikia hatua ya kujinyonga baada ya kufiwa na waume zao pale waliposhindwa kupambana na roho hii ya upweke.  Roho ya upweke iko kwa baadhi ya vijana waliopoteza wachumba wao, kwa ushirika uliopoteza mchungaji wake, mume aliyepoteza mke wake na kwa wanafunzi walio mbali na wazazi wao. Pamoja na kikwazo hiki cha upweke, ushindi uko katika kupambana nacho hadi kukishinda.
Hivi ndivyo alivyofanya mwanamke huyu, tunayejifunza kupitia maisha yake katika injili ya Marko. Ukiangalia mazingira ya tatizo lake kama yanavyoonekana katika andiko letu hapo juu, unaweza kuona kuwa, ni mwanamke aliyekuwa katika upweke usiopimika kwa mizani wala kwa shubiri. Kama tulivyoona katika vipengele vilivyopita, utamaduni na dini yake vilikuwa havimruhusu kuchangamana na watu, pili, alimwendea Yesu Kristo bila kuwa na mtu wa kumsindikiza. Ingawa alikosa mtu wa kumshika mkono wala kumtia moyo, yeye hakukubali hali hii imkatishe tamaa. Mwanamke huyu aliitumia imani yake kama mkongojo na kusema, “kwa ‘mkongojo’ huu, nitakutana na mapenzi ya Mungu katika maisha yangu.”
Ndugu yangu, kama unakabiliwa na tatizo sugu, na tatizo hilo limekufanya uwe mpweke, napenda kukutia moyo kuwa, kwa msaada wa Mungu, unaweza kuushinda upweke unaokukabili. Jambo la kwanza ushindi utakujia kwa kutambua kuwa, upweke ni moja ya silaha zinazotumiwa na Ibilisi kuwazuia watoto wa Mungu kula mema ya nchi. Ukiujua ukweli huu, utapambana na kikwazo hiki, badala ya kukaa mkao wa kulegea kana kwamba huna la kufanya. Ukweli wa tatu unaotakiwa kuutambua ni kuwa, mara zote upweke kwa watoto wa Mungu sio kitu kilicho halisi. Kamwe haitatokea mtu aliyeokoka na kuishi sawasawa na mapenzi ya Mungu, kuwa katika hali ya upweke. Hili nalisema kutokana na sababu kubwa mbili. Sababu ya kwanza, Mungu katika neno lake, tayari ameshatamka kuwa, “Yuko pamoja nasi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” Mathayo 28:20. Pili, sambamba na Mungu kuwa pamoja na mwamini nyakati zote, mwamini ni sehemu ya familia ya Mungu.
Familia hii iko katika makundi makubwa mawili. Kwanza, ni ile familia ya waamini wanaoishi katika eneo moja la kijiografia naye, inayojulikana kama kanisa la Mungu la mahali (local church). Kundi la pili, ni la waamini wanaoishi katika maeneo mengine ya kijiografia yaliyo mbali na mwamini, wanaojulikana kama kanisa la Kristo la kiulimwengu (universal church). Kwa vile waamini wote ni viungo vya mwili wa Kristo, ni uongo pale Shetani anapompandikizia mwamini roho ya upweke na kumtaka kuuamini uongo huo. Katika hali zote mwamini anatakiwa atambue kuwa, wako waamini wanaomjua na wasiomjua wanaomwombea kwa mzigo. Kupitia ufahamu na ukweli huu, ukatae uongo huu wa Shetani na utamke kwa ujasiri kuwa, kama mwanamke huyu ambaye hakuwa mwamini aliweza kuushinda upweke na kupokea muujiza wake, mimi kama mtoto wa Mungu, nitashinda pia kile kinachoonekana kuwa upweke katika maisha yangu.


KUPAMBANA NA VIZUIZI VINAVYOLETWA NA WATU
“Na mwanamke mwenye kutokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuwepo katikati ya mkusanyiko uliomfuata Yesu.” Marko 5:25
Kikwazo kingine kilichomkabili mwanamke huyu, ni umati mkubwa uliokuwa umemzunguka Yesu, katika safari yake ya kwenda kumponya binti Yairo. Kupitia miujiza miwili iliyofanywa na Yesu ya kuwalisha watu, yawezekana kwa uchache umati uliokuwa ukimfuata Yesu, ulikuwa haupungui watu 10,000. Kutokana na umati huu, ilikuwa ni vigumu mno kwa wagonjwa waliozidiwa kumfikia Yesu na kukutana naye uso kwa uso. Wakati mwingine ilimbidi mhitaji au ndugu zake watumie nguvu za ziada, ili kuifikia mikono ya Yesu. Mfano mzuri katika hili, ni ule unaomhusu mwenye kupooza, aliyepelekwa kwa Yesu na watu wanne katika injili ya Marko. Kutokana na umati uliokuwa unamsonga Yesu, iliwabidi wale waliomchukua wavunje dari ili wapate nafasi ya kumtelemsha mgonjwa wao pale Bwana wa uponyaji alipokuwa. Marko 2:4.
Mfano wa pili, ni huu wa huyu mwanamke aliyekuwa akitokwa na damu kwa miaka 12 mfululuzo. Kutokana na  udhaifu katika mwili wake, ni wazi ilikuwa vigumu mno kwake kupenya katikati ya umati wa watu, hadi kufika pale Yesu alipokuwa. Kitu cha kutia moyo ni kuwa, pamoja na ugumu huu, bado aliweza kupenya na kushika vazi la Yesu. Tunachojifunza katika mifano hii miwili ni kuwa, watu wanaweza kumsaidia mwamini kupata ushindi, na wakati mwingine  wanaweza kuwa kikwazo cha kumzuia mtu kukutana muujiza wake. Kwa mfano, mwenye kupooza katika mlango wa kondoo katika injili ya Yohana, alishindwa kufunguliwa mapema, kutokana na kukosa mtu wa kumwingiza birikani. Yohana 5:2-7. Tukija kwa Bartimayo yule kipofu, mambo yalikuwa kinyume, yeye watu ndio waliojaribu kuuzuia muujiza wake!
Kwa yeyote yule anayetaka kupata upenyo na kumliza yule aliyekuwa akimliliza, anatakiwa afanye uamuzi wa kupambana na Shetani mpaka pale ushindi atakapopata majibu ya maswali yake. Hivi ndivyo huyu mwanamke alivyofanya, umati ulikuwa kikwazo kikubwa kwake, ila aliweka bidii ili kukishinda kikwazo hiki kwa lengo la kuutwaa muujiza wake.

KUWEKA BIDII YOTE KATIKA KUPAMBANA
“Na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu WENGI…” Marko 5:26
Jambo lingine lililochangia kumletea mwanamke huyu ushindi, ni ile bidii aliyokuwa nayo katika kupambana na tatizo alilokuwa nalo. Tatizo lilipompata, alihakikisha kuwa anawaendea madaktari wote aliokuwa anawafahamu, kwa lengo la kutafuta uponyaji. Tunapozama ndani katika kipengele hiki, ninataka utambue kuwa, katika ulimwengu tulio nao, kamwe hakuna mtu aliyeandikiwa na Mungu kuishi maisha mabaya. Mungu kama Muumbaji mwenye upendo,  ametengeneza barabara nzuri za maisha kwa kila mtu, ila mtu mwenyewe, ndiye anayeweza kuamua kutembea ndani au nje ya barabara hiyo.
Kwa mfano, mtu anapoukataa wokovu, hamkatai tu Kristo, bali, anayakataa pia mapenzi ya Mungu katika maisha yake. Hali kadhalika, mtu aliyemwamini Kristo na hatimaye akalegea katika kupambana na vikwazo vinavoinuka katika maisha yake, huyo naye atakuwa mbali na mpango wa Mungu wa neema, ulikusudiwa kuwa katika maisha yake. Ulegevu tunaouongelea hapa, ni ule wa kutotumia NGUVU zote, MOYO wote na ROHO yote katika kumwishia na kumtumikia Mungu. Roho hii ya kufanya mambo nusu nusu, ndiyo iliyomfanya mfalme wa Israeli, ashindwe kuangamiza majeshi ya mfalme wa Shamu. Nabii alimwambia kupiga mshale chini, yeye akapiga mara tatu na kuacha. Alipoacha Elisha alimwambia maneno yafuatayo; “Ingelikupasa kupiga mara tano au mara sita; ndipo ungaliipiga Shamu hata kuiangamiza; bali sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.” 2 Wafalme 13:19.
Tukiingia ndani ya kanisa la siku hizi za mwisho, tunaweza pia kuona kuwa roho hii ya kufanya mambo kwa kutumia nguvu kidogo, ndiyo inayoifanya idadi ya wafuasi wa imani ya Kikristo, kukaribia ile ya Waislamu wakati ambapo Uislamu, ulianza karine tano baada ya Ukristo kuanza. Kiongozi wa kanisa la mahali, anaweza kuhamasisha waamini kwenda kushuhudia, ila  baadaye, utawakuta waamini hao wakirudi mikono mitupu bila mavuno. Kama atatokea wa kuuliza kulikoni, mara zote jibu linakuwa rahisi, “hatukupata mtu leo!” Hata hivyo ukiliangalia zoezi zima la huo ushuhudiaji, utagundua kuwa, waamini hao hawakutumia nguvu zao zote katika kulifanya zoezi hili. Udhaifu huu, uko pia katika maeneo ya ufuatiliaji, utoaji, uimbaji na kadhalika; ndio watu wanafanya, ila sio kwa kutumia nguvu zao zote.
Kwa mwanamke huyu tunayemzungumzia katika habari yetu, hakuridhishwa na madaktari wawili au watatu, wakati wa kutafuta muujiza wake. Yeye alitumia nguvu yote ya fedha aliyokuwa nayo, kutafuta tiba ya tatizo lake. Hata tunapoangalia Biblia, tunaona kuwa, watu waliotumiwa kwa namna ya kipekee na Mungu, ni wale walioweka bidii ya kutosha katika shughuli za kiroho na zile za kimwili. Mfano mzuri wa watu hawa, ni wanafunzi wa Yesu. Wao hawakumfuata Yesu nusu nusu, bali walimfuata kwa mioyo yao yote na kujitoa kwao ndiko kulikomfanya Petro atamke kuwa, “Sisi tumeacha vyote tukakufuata.” Marko 10:28.
Kama waamini wa siku za mwisho wanataka kuuona mkono wa Mungu, katika maisha yao ya kiroho na kimwili, ni lazima watumie bidii yao yote kutafuta mambo ya rohoni nay ale ya kimwili. Kwa maneno mengine, kama nguvu za wanadamu zingelikuwa sawa na mipira ya manati, wanatakiwa wajivute mpaka ifikie kikomo cha kuvutika kwake.

KUTOKUBALI KUKATA TAMAA
“Na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya; aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyumba, akaligusa vazi lake.” Marko 5:26
Kitu kingine kilichomsaidia mwanamke huyu kusonga mbele hadi kuufikia muujiza wake, ni ile roho aliyokuwa nayo ya kutokukata tamaa. Andiko letu hapo juu, linaonyesha vile kibinadamu, mwanamke huyu alivyokuwa na kila sababu ya kukata tamaa. Katika kupambana na tatizo alilokuwa nalo, alipitia waganga wengi, pochi yake ilikuwa tupu, ila kulingana na andiko letu hapo juu, bado aliendelea kutafuta waganga. Ni katika kutafuta huku, ndipo alipokutana na Mganga wa waganga, aliyeweza kumwondolea mzigo uliokuwa ukimlemea. Kama angelikata tamaa, angelibakia nyumbani na hapo angelikufa kile kifo Waswahili wanachokiita, ‘kifo cha kiofsa.’
Kuifungulia roho ya kukata tamaa, kumechangia mno kuzorotesha maendeleo ya kiroho na ya kimwili ya watoto wa Mungu. Mtu anaweza kumpokea Yesu leo na kesho tu anataka kuwa mhubiri kama Billy Graham au Reinhard Bonke. Hali kadhalika, kama ni mafanikio ya kimwili, nayo wanataka yaje mithili ya kumulika kwa radi. Yale wanayoyatarajia yasipokuja kwa wakati wanaoutaka, wanaamua ‘kuozea’ katika mkeka wa kukata tamaa. Wakati umefika kwa waamini kujifunza kutokata tamaa kutoka kwa watu maarufu kama vile Thomas Edson. Mskotishi huyu, alijaribu kutengeneza balbu za umeme zaidi ya mara 2,000 bila mafanikio na hapo, wakatokea watu wengi walimtembelea kwa lengo la kumkatisha tamaa. Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa Ayubu mbele za wataabishaji wake, mtu huyu alikataa kabisa kuifungulia mlango roho ya kukata tamaa  na leo bulbu za umeme zimeenea dunia nzima.
Kama watoto wa Mungu wa kanisa la siku za mwisho wanataka kuishi maisha ya ushindi, wanatakiwa kukataa kwa gharama yoyote ile, roho hii ya kukata tamaa.

KUUONA USHINDI KABLA HAUJATOKEA
“Maana alisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.” Marko 5:28
Andiko hili linatuonyesha kiwango cha imani kilichokuwa ndani ya mwanamke huyu. Kama vile Yona alivyomtukuza Mungu akiwa ndani ya tumbo la samaki, ndivyo alivyofanya. Imani ya kupokea aliyokuwa nayo, ilimpelekea kuamini kuwa, pale tu atakapolishika vazi la Yesu, atapona msiba aliokuwa nao. Tunachokiona kwa mwanamke huyu ni kuwa, aliamini shuhuda zote alizozisikia kuhusiana na matendo makuu yaliyofanywa na Yesu na akazigeuza shuhuda hizo kuwa pumzi ya mapafu yake. Kwa maneno mengine, tunaweza kusema kuwa, ujazo wa shuhuda za matendo makuu ya Yesu, ulijaa ndani yake kiasi cha kutobakia nafasi ya mashaka ndani ya roho na ufahamu wake. Imani hii ya kupokea, ndiyo iliyomfanya auone ushindi dhidi ya tatizo alilokuwa nalo, hata kabla ya kukutana na Yesu.
Kama wewe ni mmoja wa wale wanaotaka kula mema ya nchi, itakulazimu, uruhusu aina hii ya imani kuumbika ndani yako. Mambo yote yaliyoletwa na Mungu duniani kupitia kwa Yesu Kristo, yanapatikana kwa imani. Kama vile milango mitano ya ufahamu inavyomwezesha mtu, kuwa na uhakika wa mambo yaliyopo katika ulimwengu wa kimwili, kwa imani mwamini anakuwa na uhakika wa kile kinachofanyika katika ulimwengu wa kiroho kuhusiana na maisha yake. Kupitia jicho la imani, Yusufu aliuona ukombozi wa wana wa Israeli kutoka Misri na kuwaagiza akisema, “Bila shaka Mungu atawajia ninyi, nanyi mtaipandisha huko mifupa yangu.” Mwanzo 50:25. AMENI!


Tamati

Maisha ni malengo

“Inawezekana kutoka kwenye ufukara na kuwa mtu fulani”
(Haijalishi huna Elimu, Maskini, Mlemavu, Mjane, Yatima nk.)

Lengo ni picha ya hatua iliyoko mbele yako ambayo bado hujafikia lakini unataka ufikie. Unaweza pia ukayaita maono. Watu wasipokuwa na malengo, hawawezi kuwa na mwelekeo wa utendaji. Hawawezi kujipima nidhamu ya utendaji maana hawana/hawajui wanapokwenda.

Malengo ndiyo dira, mwelekeo, kichocheo, kipimo na picha ya unapotakiwa kuwepo baada ya muda fulani. Hivyo huwezi kulala wala kupumzika, utafanya kila jitihada ili ufanikishe malengo yako. Kwasababu ni maono au picha uionayo ya mambo yanayotakiwa kuwa lakini bado hayajawa hivyo, sasa ili yatimizwe, ni lazima ziwepo mbinu au mikakati.

Malengo bila mikakati, ni sawa na mtu anayejua anatakiwa kwenda mahali lakini hajui njia. Atafikaje asipoanza safari ? Ataanzaje safari bila kuijua njia ?

Kijana mmoja masikini asiyekuwa na elimu, asiye na thamani kwa jamii. Aliamka asubuhi kutafuta vilipo vibao vyenye maneno”kuna kazi”. Alitafuta kazi mwaka mzimzsiku bila mafaniko. Mungu sio Athumani siku moja akafanikiwa kusikia tangazo kuwa kuna kazi mahali fulani. Furaha yake ikawa kuu akijionea mwenyewe katika mtazamo wake kama alivyodhani ni sahihi kumbe ni tofauti. Alipofika maali hapo, baada ya kumpokea asiye na adhi walimuonea huruma kwa jinsi alivyochakaa lakini hawakuweza kuamua bila kufanya usaili. Alijieleza vyema ila tatizo likabaki kuwa ili aweze kuajiriwa lazima awe na anuani ya barua pepe (email- address). Maskini hakuwa nayo. Kwa huzuni aliondoka ili akatafute fedha za kufungua email address ili apate ajiri. Haikuwa rahisi kwa asiye na kipato kupata pesa ndogo alizotakiwa kulipia internet ili afungue anuani ya barua pepe (e-mail) kusudi apate kazi ya mesenja aliyoitegemea kuinua maisha yake. Mungu alimfungua macho bila ya yeye kujua, kamavile wengi wanavyodhani ni jitihada zao wenyewe. Usiku aliota ndoto kuwa anamilliki bustani ya pilipili kwa miche aliyoipata jalalani.

kuna maneno yasemwayo kwamba « ukiota ndoto iandike » inamaanisha unapopata ufunuo wa jambo usiliache hewani, liandike kusudi liwe msaada pindi ushauri utakapokosekana au utakapoitaji jambo la kufanya liweze kuwa msaada usivyodhani. Kamwe usiyadharau mawazo au ndoto yako. Kwa hiyo kijana alianza kutafuta miche ya pilipili Kwa sababu hapakuwa na miche wala uwezo wa kununua miche sokoni aliamua kwenda jalalani kutafuta miche kama angepata. Wakati huo, hakujali maneno ya watu, wala kujali wanavyomwona ; bali alifahamu kuwa umasikini wake unamuhusu yeye na sio mtu mwingine. Kutokana na hali hiyo alichukua miche ile michache aliyoipata na kuanzisha bustani.
Tofauti na wengi ambavyo wangedhani, kijana huyu alifanya jambo moja lenye kufurahisha, kwa mapato au mazao ya kwanza toka bustanini, aliwapa wahitaji wa kijiji kile bila kutarajia faida. Alifahamu kuwa yupo aliyempa maono hayo hivyo hakuwa na jinsi ya kumfikia kumpa asante kama sio kupitia watu wake. Kwa kuwa alimtegeme Mungu alizidi kupata maarifa zaidi, naye akazidi kubarikiwa katika kidogo alichokithamini. Wengi walitamani kujifunza kwake, pia kununua bidhaa hii na hatimaye kuendelea kuongeza ukubwa wa bustani kutokana na uhitaji, kadiri siku zillivyozidi akawa amebobea na kusahau kuwa alitakiwa aende kufungua e- mail address ili apate ajira.
Wateja walizidi kuongezeka kila kukicha. Hatimaye ndoto ya kufungua anwani ya barua pepe kusudi aajiriwe ikafa, ikawa email kwajili yake binafsi kwa wakati ule. Baada ya muda wateja wenye kuhitaji kusafirisha pilipili nje ya nchi, walihitaji awape anuani yake ya barua pepe kusudi wawasiliane kwa biashara. Ndoto ya kuwa mesenja ikazidi kutoweka. Alipanua shamba hatimaye kuanzisha kiwanda cha kusindika pilipili, hivyo kufungua ajira kwa mamia ya wenyeji wa nchi ile na kufahamika ulimwengu mzima kwa ubora wa pilipili.

Ndugu msomaji,
unafanyaje nini ili utumie uwezo wako kuishi katika dunia ya walio hai? Je unatazamaje umaskini wako?  Bado unasubiri e- mail address ili uajiriwe kama mesenja au unaona miche minne ya pilipilli jalalani itakayokusahaulisha umesenja unaouhitaji? Je ndivyo kweli ulivyo jinsi unavyojitazama? Rejea falsafa hii Jinsi uonavyo mambo ni kipimo tosha cha mafanikio au kushindwa kwako.

Ni imani yangu kuwa unayo mahitaji muhimu katika kuendelea kuishi pasipo shida ya chakula malazi na mavazi. Naelewa kuwa yako matarajio uliyonayo umejiwekea au unayolenga kuyafikia. Yawezekana hayapo tena kutokana na vikwazo mballimbali kama vile kufukuzwa kazi, kushindwa mitihani, kukosa mtaji, kunyanganywa mali na haki zako au vyovyote vile hivyo umepoteza dira na matumaini. Haijalishi ni leo kesho au lini ila ipo njia kurudisha furaha yako, marufuku kukata tamaa.

Hivyo hivyo ulivyo wewe ni mtaji jitizame kwa jicho la tofauti leo. wewe ni nani na unataka kuwa nani? Kumbuka siku zote ("Development comes to those who dare to dream") maendeleo huja kwa wale wanao thubutu kuota.  Usikate tamaa, andika ndoto yako ili ufanikiwe wala usidharau hisia zako.

Mungu hakuumba wachache waneemeke na wachache wabaki kuwa watumwa katika nchi yao wenyewe, Kama ndivyo angetutenganisha katika sayari mbalimballi ili kuwa na mgawanyo sawa na haki. Sina shaka kuwa hajakosea na mpango wake ni kuwa tutaishi dunia moja nakugawana rasilimali zote sawa bila kujali dini, jinsia au umri (vijana na wazee) au walemavu sina pingamizi kuwa kuna baadhi ya majukumu hayawezi kugawanywa bila kuzingatia uwezo jinsia na maumbilie.
                    
Ukilinganisha na idadi ya vijana ninaokutana nao vijiweni bado ni asilimia ndogo sana ndio wameajiriwa serikalini na katika taasisi za umma na mashirika ya watu binafsi. Pamoja na hayo wana hali ngumu na baadhi hawana haki kisheria katika sehemu zao za kazi. Kutokana na ukosefu wa ajira vijana wengi wamejikuta wakijiingiza katika mambo yasiyo na maadili kwa kisingizio cha hali ngumu ya maisha kama wizi, uvutaji wa bangi, ulevi wa kupindukia, uzinzi n.k. Matokeo ya haya yote ni kuwa na uchumi mbaya kwani nguvu kazi hii haitumiki katika sekta kwa usahihi upasavyo, hatimaye Kuenea kwa magonjwa ya zinaa kama UKIMWI mwisho wake misiba ambayo nayo bila huruma hutumia fedha ndogo tunazozipata katika uchumi wetu mdogo.

Ninafahamu kwa hali halisi wanoathirika kutokana na UKIMWI ni wazazi (au walemavu na watoto wasio na uwezo wa  kuzalisha) hivyo hulazimika kutumia hazina zillizowekwa katika kuuguza vijana ambao ni muhimu kwa taifa na jamii ili kuinua uchumi wetu. Safari ya kuendele kudidimiza  uchumi haishii hapo kwani baada ya kuondoka duniani nguvu-kazi  hii, wapo wanoacha wajane ambao nao bila huruma hunyanyaswa na kunyimwa haki zao  za msingi, kama kumiliki rasilimali na uhalali wao kushiriki katika gurudumu la maendeleo, kama kuwa na kauli katika jamii, kisiasa, kiuchumi na kielimu. Hawa bado bila huruma wanategemewa na watoto wanaoachwa na marehemu baba/mama zao.
Uchumi mbaya wa vijana na kukosa sauti katika jamii huwafanya washindwe kumudu gharama za elimu na kuendelea kuongeza idadi ya vijana wasiokuwa na elimu, ujuzi na nyenzo za shughuli wanazofanya ili kuinua uchumi wa nchi yetu changa. Katika uumbaji Mungu alimpa kila mtu kipawa na karama ili aweze kuishe maisha bora na kukabiliana na hali ngumu ya maisha. “Man was created to make earth paradise, a place to enjoy life.” Kutokana na ukosefu wa elimu na mwangaza wa maisha, wengi hushindwa kuelewa vipawa vyao na umuhimu wao katika dunia waliyoumbiwa yenye rasililmali maridhawa kwa maendeleo yao wenyewe.

Kwa kutambua hilo ipo haja ya vijana, kina Mama, kina Baba kujitambua na kufahamu umuhimu wao na kutafuta kwa bidii kupata taarifa na ujuzi wa kujikomboa kimaisha. Haitoshi kusema au kulalamikia serikali, kwa mashairi yaliyozoeleka kuwa, hali ni ngumu, serikali hitujali, itupatie ajira. Bado zipo fursa nyingi kama vijana watajiunga, pia Wasanii au wenye ujuzi mbalimbali ili kuanzisha vikundi vya kujikwamua kimaisha, kwa njia ya kubadillishana na kushirikishana vipawa.

Kama vikundi vya jamii  vitapata nafasi ya kukutana na kupeana uzoefu, wanaweza kuhamasika na hatimaye kuwa na watu wenye mwelekeo  sahihi  katika kuungana na sera za nchi katika kupambana  na umasikini, maradhi na ujinga hivyo kuwa chachu ya maendeleo  katika taifa nzima na dunia.
Hakuna malengo yanayotimizwa au mikakati inayotekelezwa bila kujiwekea nidhamu. Tatizo la wengi wetu wanaoshindwa kutimiza malengo yao ni kutojiwekea nidhamu au kutoheshimu mikakati waliyoiweka wenyewe. Mfano, kwa kuwa tumezoea kufika ofisi tulizoajiriwa kwa muda tuliopangiwa, tunaona huo kama utumwa na tunapokuwa na miradi yetu wenyewe, tunaona kama tumekombolewa na hivyo tunakwenda katika kazi zetu kwa muda tunaojisikia! Hivyo hukuna nidhamu ya kazi kabisa! eti kwa sababu ni duka lako au saluni yako mwenyewe, unafungua kwa muda unaojisikia! huwezi kamwe kuyatimiza malengo.

Ikibidi wakati mwingine, unahitaji elimu fulani ya utaalamu wa sera na mipango ili kuzijua na kuishi maisha ya kujiwekea malengo. “if you think education is expensive, try ignonce” (kama unadhani elimu ni ghali basi, jaribu ujinga). Yanini kuujaribu ujinga ilihali unagharimu zaidi kuliko elimu? Ukweli ni kwamba gharama ya ujinga ni kubwa kuliko gharama ya elimu au kujielimisha. Kujielimisha ni kupona.
“Marufuku kukata tamaa”


Mwisho

Najua Kitabu hiki kwa njia moja au nyingine kimekusaidia na ungependa kuwa rafiki wa karibu wa maono haya. Ikiwa unataka kuchangia ao kupanda mbegu kwa ajili ya maono haya, andika jina lako, sahihi na anwani yako na namba yako ya simu ikiwezekana, kisha tuma kwa

JOHN STEPHEN SHABANI
P.O.Box 15155, Dar es salaam Tanzania.
Mob: +255 754 818 767
neverevergiveup2008@yahoo.com

Na ikiwa unamchango wowote wa mawazo, ushauri au umeamua kuombea maono haya,  Kwa mawasiliano tumia anwani hiyo. Kama ni pesa kwa ajili ya kuchangia, kuinua maono haya, tuma kwa njia ya western union ukitumia anwani hiyo au nitumie kwa njia ya Bank.
                                  Jina: JOHN SHABANI & DEBORA SHABANI
                                    Bank: CRDB Bank (Kijitonyama Branch)
                                    Acc no. 01j2013291800
Au waweza kutumia njia yoyote utakayoona inafaa, ukitumia anwani hiyo hapo juu.

Tafadhali usiache kukinunua kitabu hiki. Lakini pia nakushauri nunua nakala zingine uwapatie ndugu, jamaa au rafiki unaopenda wabarikiwe kama wewe. Ukiona vema wanunulie wengine wengi hata wasio wakaribu nawe, au ukishavilipia na ungependa tukusaidie kuvipeleka kwa wahitaji Mungu atakaotuongoza, basi wasiliana nasi, nasi tukotayari kukusaidia. kwa kufanya hayoyote, utakua umenisadia kuwafikishia ujumbe huu wenye mafanikio. Utakuwa umewasaidia wao binafsi, lakini pia pesa yako itakua haijapotea, umeipeleka maali salama.  Itahesabika kuwa sadaka kwa Mungu, zaidi ya hayo, siku zote watadumu kumshukuru Mungu kwa ajili yako, na utabarikiwa hakika! (Tafadhali, soma 2kor 9:10-15) 

 

Asante sana na Mungu wangu akubariki.


ASILIMIA KUMI 10% YA MAUZO YA KITABU HIKI YATASAIDA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU, WAJANE, YATIMA NA WALIOATHIRIKA NA GONJWA LA UKIMWI



Historia fupi ya mwandishi

John S. Shabani ni mzaliwa wa kijiji cha Kirando katika kitongoji cha Nyankima, kata ya sunuka, Wilaya ya Kigoma Vijijini, Nchini Tanzania. Ukoo wake ni waumini wazuri wa dini ya kiislam (Islamic Religion).

Baada ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi kirando, alijiunga na elimu ya sekondari, lakini kutokana na itikadi za kidini, alijikuta akiwa katika wakati mgumu wa kupigwa vita na wazazi, ni baada ya uamuzi wake wa kujiunga na Dini ya kikristo. Hivyo John ameishi miaka mingi akiwa mbali na wazazi wake, lakini hata hivyo hakukata tamaa.

Mwaka 1992, John akiwa kijana mdogo, alipata ufadhili wa kwenda nchni Kongo (Zamani Zaire), ambako huko alijifunza muziki na kusoma Chuo cha Biblia (Bible knowledge), na huko kipaji chake cha kutunga nyimbo na kuimba kilijitokeza kwa kasi, hata akatokea kupendwa sana.

John hakutaka kuona mtu yeyote akiwa katika hali ya kukata tamaa, maana alifahamu madhara yake. Kwasababu hiyo, alianzisha vikundi mbalimbali vya vijana akiwa na lengo la kuwaelimisha ili kujikwamua katika hali ya kukata tamaa na kutokujihusisha na vitendo viovu kama madawa ya kulevya, Ukahaba na anasa za kila aina, mambo ambavyo aliyapiga vita sana.

John ameishi miaka mingi kama yatima, lakini hali hiyo imemsaidia kujifunza mengi na kuwa na tabia njema, kumheshimu na kumthamini kila mtu, mambo yaliyompelekea kupata kibali machoni pa wengi hata kuwa mfano wa kuigwa. Amekuwa msaada kwa Vijana wengi (Ndani na nnje ya nchi) na kuwakwamua wengi waliokuwa wamekata tamaa na kujihusisha na vitendo viovu. Pia kutokana na ujuzi wa muziki alioupata na pia kipaji kikubwa alichonacho cha kutunga, kuandika nyimbo na kuimba, John amekuwa msaada kwa waimbaji mbalimbali binafsi na vikundi ndani na nje ya nchi, hasa nyimbo za Injili. Ni mwalimu bora na mshauri kwa waimbaji. Wengi waliopitia kwake sasa ni waimbaji wazuri na maarufu.

Mwaka 2001 John alifunga pingu za maisha na binti aitwaye Debora Shabani na mwaka 2002 walipata mtoto wa kike. Alimwita mwanaye Joyce, akiwa na maana ya kuyasahau maisha ya huzuni na shida na kujitabiria maisha ya furaha.

Mwaka 2004, John aliajiriwa katika kampuni ya Msama promotions ya jijini Dare es salaam, kampuni inayojihusisha na kuinua vipaji na pia kuwainua vijana na watu wa rika na jinsia zote waliokata tamaa ya maisha n.k, na hasa wale walioko vijiweni wakijihusisha na madawa ya kulevya, ukahaba n.k. Kampuni hiyo imewasaidia Vijana wengi na Jamii kwa ujumla, na wengi wamejikomboa kimaisha

Tarehe 19/03/04, John alirekodi Album yake aliyoiita “Marufuku kukata tamaa
Album ambayo imewasaidia wengi waliokata tamaa na kuwapa matumaini mapya. Album hiyo na nyingine alioirekodi mwaka 2009 inayoitwa “Huu ni wakati wangu”, zimekuwa msaada mkubwa kwa kila aliye au anayezinunua, zimegusa na kuinua mioyo ya watu wengi. Kwani amepokea shuhuda nyingi ndani na nnje, hata za wale waliodiriki kujiua, lakini baada ya kusikiliza nyimbo hizo waliahirisha. “Nakusii nunua kanda hizo, naamini zitakusaidia”. Pia utakuwa mchango wako kwa kutimiza ndoto na malengo ya John.

John ametembelea nchi mbalimbali, akijifunza maisha ya watu. Amegundua kwamba karibu asilimia kubwa ya wanadamu, awe maskini, tajiri, msomi au asiye na elimu, wenye vyeo au waajiriwa, watoto kwa wakubwa, wanaume kwa wanawake, awe mzungu au mweusi n.k, wote kwa njia moja au nyingine wamepitia katika hali ya kukata tamaa au kukatishwa tamaa na jambo fulani, mtu, watu, hali au mazingira fulani. Ndipo mwaka 2006, alipata maono na msukumo mkubwa wa kuandika Kitabu ambacho kitakuwa msaada kwa njia moja au nyingine kwa kila atakayekipata.

Tarehehe 11/7/08 ni siku ambayo John hawezi kuisahau. Siku ya huzuni na majonzi, siku ya kilio na kuomboleza. Ni siku alipofariki mke wake mpendwa na mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili, Debora Shabani, mwimbaji aliyegusa mioyo ya watu wengi ndani na nnje ya nchi, mwimbaji ambaye msiba na mazishi yake yalihudhuriwa na maelfu ya watu, wakiwepo Maaskofu, Wachungaji, Waimbaji binafsi, Kwaya pamoja na viongozi mbalimbali wa serekali. Hata hivyo, John hakukata tamaa.

Tarehe 26.04. 2009, John alitunukiwa tuzo ya heshima pamoja na cheti (certicate of appreciation) kwa kutambua mchango wake kwa ajili ya kuinua vipaji na pia kuchangia kuinua muziki wa Injili Afrika mashariki na kati. Pamoja na hayo amekua akianzisha makundi mbalimbali kwa ajili ya kuwaelimisha kuhusu maisha ya kujitegemea, kujishughulisha na kuhepukana na vitendo viovu kama wizi, ujambazi, utumiaji madaswa ya kulevya, ukahaba n.k. Tuzo hiyo ilitolewa na kampuni moja maarufu Tanzania yenye makao makuu jijini Dar es salaam (Christian promoters Ltd).

John ameanzisha huduma inayoitwa Never give up “Usikate tamaa” Ambayo anategemea kuisajili wakati wowote. Huduma hii, inalenga kuinua vipaji, mipango na mbinu za kuwakwamua vijana au watu kujihusisha na madawa ya kulevya, ukahaba, utapeli wizi, ujambazi nk, mambo yanayosabisha magonjwa kama vile ukimwi, kufungwa jela au kufa kabla ya wakati, matokeo yake kuacha wototo wengi yatima na wajane nk. Pia kutafuta ufadhili kwa ajili ya kuaendeleza vijana ki-elimu pamoja na kuwawezesha pale inapobidi. Kwa sasa anayo program inayoitwa Touching voice program (Darasa la uhimbaji)
Ni kwa ajili ya kwaya, Band/vikundi na waimbaji binafsi.
Lengo ni:

  • Kufundisha kuimba au kunyoosha (Singing training)
-          Jinsi ya kuitumia sauti kuitunza na kuitawala
-          Historia ya muziki na maadhi ya muziki
-          Sifa na mbinu za kuwa mwimbaji bora kama vile: (Performance, personality, stage presence, self confidance, body language, pronuaciation, vocal range etc)
-          Matumizi ya kipaza sauti (How to use microphone)
  • Kuwatungia nyimbo au kurekebisha nyimbo zilizotungwa tayari (Song writing/composing)
  • Kutoa ushauri kwa wanaotatarajia kuingia studio
  • Kushauri mbinu za kuitangaza album au nyimbo zako zikubalike
  • Kutengeneza muziki wenye viwango (Music arrangement)
  • Kutengeneza cover za kanda za kawaida (Audio cassette), cd, vhs (Cover designing)
  • kuzalisha CD na DVD (CD & DVD burning)

Naamini kwamba Kitabu hiki sio tu kitakufurahisha au kukufariji, lakini kitakutoa mahali ulipo na kukupeleka mahali fulani.Kitakuondoa kwenye Umaskini na kuwa tajiri, kwenye Ujinga na kuwa Mwerevu, kwenye magonjwa na kuwa mzima, kwenye huzuni na kuwa mwenye furaha, kwenye taabu na shida na kuwa mwenye mafanikio, kwenye ufukara aibu na kuchekwa na kuitwa mheshimiwa fulani.

HIKI NDICHO KITABU ULICHOKUWA UNAKIHITAJI, USIKIKOSE. NDICHO KITABU PEKEE KITAKACHOKAMILISHA NDOTO ZAKO. MARUFUKU KUKATA TAMAA


JUMBE ZA KINGEREZA ZINAZOTIA MOYO

1. Never think of the past coz it brings tears and don’t think much of the future coz it brings fears. Life is where you are, commitment and self determination are the mirrors of your precious up coming future, look forward with confidanceand backward with gratitude and where you are with hope.
2. Many of life's failures are people who did not realize how close they were to success when they gave up
3. Do not count what you have lost… just see what you have now… because past never comes back, but sometimes future gives back what you”ve lost.
Life ends when you stop dreaming, hope ends when you stop believing
4.Dont take life too seriously, Always find time to laugh... Remember that laughter not only adds years to ur life, ButaddsmoreLifetourYears....


PAGE YA NYUMA

Hiki ndicho kitabu pekee ulichokua unakiitaji, ndicho kitakachobadili hali mazingira na mtazamo wa maisha yako, Kitakuondoa kwenye umaskini, ufukara, kuchekwa na kuwa tajiri (Tajiri wa rohoni na mwilini), kuitwa mheshishimiwa au kuwa mtu mwingine kabisa. Kitakutoa kwenye ugonjwa na kuwa mzima. Ni kitabu kilichojaa mifano na hadithi za kusisimua, zinazogusa moyo. Ni hadithi za kweli tena zitakazoinua imani yako. Ukidiriki kuanza kukisoma kitabu hiki, kitakubadilisha. Hakika kitabu hiki kitakubadilisha kwa kiasi kikubwa ki-mawazo na kimatendo.

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP