5 March 2012

HATIMAYE MARTHA MWAIPAJA AMEOLEWA



Staa wa muziki wa Gospel Tanzania Martha Mwaipaja hatimae ameolewa, pembeni yake ni mumewe Pastor John Said. Martha Mwaipaja ambae ni miongoni mwa mastaa wachache wa Gospel wanaouza sana kwa sasa, ana historia iliyondefu kidogo kutoka kuwa mfanyakazi wa ndani mpaka kuwa staa wa gospel, amepitia mengi lakini ashukuriwe Mungu asiyekuwa na upendeleo amamfanikisha mwana dada huyu. Hakika ilikuwa ni Furaha ya Ajabu kwa Wanandoa hawa Wawili baada ya kufunga Ndoa katika Kanisa la Udhihirisho wa Injili, lililopo maeneo ya Kipunguni B Ukonga, jijini Dar es salaam, na kufuatiwa na Shughuli ya Kuwapongeza wanandoa hao iliyofanyika na Katika Ukumbi wa Delux, ulioko maeneo ya Sinza jijini Dar es saalam.


Kabla ya ndoa hiyo ilifanyika Kitchen Party ya nguvu Siku ya J/pili ya Tare 26/2/2012  iliyo fanyika Ukumbi wa Bwende ulioko Kiwalani jijini Dar es salaam.

Tare 1/3/2012 ilikuwa Send off yake iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP.

Marha Mwaipaja Mungu amempatia Mume ambae ni Mchungaji wa Kanisa la {Udhiirisho wa Injili} Pastor John Said.Kwa mujibu wa Pastor John amesema kuwa, Ndoa itafungwa katika kanisa la Ukonga Mombasa shughuli itafanyika Ukumbi wa Sinza Delux kuanzia Saa moja usiku na kuendelea.

Mwanamuziki wa injili Martha Mwaipaja akiwa na Mumewe mtarajiwa Mch John Said jana siku ya send off party.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP