10 March 2012

BEATRICE WILLIAM WA BONGO STAR SEACH AOKOKA

Mwanadada aliyetengeneza jina kupitia shindano la kufatuta vipaji, Bongo Star Search 2008 na 2009, Beatrice William ameamua kuokoka.  Mwanamuziki huyo aliamua kuokoka siku ya juma tano tarehe 7/3/2012 katika ibada ya matendo makuu ya Mungu, katika kanisa la Mikocheni B Assemblies of God (Mlima wa moto)
Akiongea   siku ya mkesha wa ijumaa ya tarehe 9, Beatrice akiwa Madhabauni alisema kwamba uamuzi wake wa kuokoka ni wa dhati kabisa akiwa na akili zake timamu. Mara nyingi nilipenda sana  kuokoka lakini niliogopa kumbipu Mungu kama wengine wanavyofanya, aliongea Beatrice.
Kabla ya kuokoka msanii huyo kutoka pande za Mwanza amejipatia umaarufu mkubwa na hasa pale alipotoa nyimbo yenye jina la ‘Acha waone’
Hakika ukimtatzama , Siye yule beatrice unayemfahamu, amebadilika kabisa na kuwa mtu mwingine katika Bwana.
Tutaendelea kukujuza kuhusu uamuzi huo wa Beatrice…….

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP