22 August 2011

CATHERINE KYAMBIKI (MKONGWE WA NYIMBO ZA INJILI AFRIKA MASHARIKI) AFUNGA PINGU ZA MAISHA


Hatimaye mwana mama Catherine kyambiki, aliyejulikana hapo awali kwa jina la Catherine njogu, amefunga pingu za maisha na Mr Samuel raiya wa Angola. Mwimbaji huyo mkongwe, alifunga pingu hizo katika kanisa la Dorcus Christian Ministries lililopo kunduchi mtongani - Dar es saaam. Sasa, usimwite Catherine nzogu au catherine kyambiki, anaitwa Catherine Samuel. Mwana mama huyo aliyezaliwa miaka ya sabini, amejitwalia umaarufu katika Nchi kadhaa za ki Afrika. Alijulikana sana kwa kibao chake kiitwacho Yesu anaweza yote. Pia ni miongoni mwa waimbaji wa injili wanao ongea lugha mbalimbali za ki Afrika, pia anao ujuzi wa kupiga vyombo kadhaa vya muziki. Hivi sasa Catherine na mumewe, wameweka makazi yao huko Angola.

                                         Siku alipotangaza uchumba

                                           Vazi la Kitchen Part
 Baadhi ya waimbaji wa nyimbo za Injili wakiongozwa na Rais wa Chama cha muziki wa Injili (Chamuita) Mr Addo november, Makamu wake Mchungaji Malumbu, Mc wa sherehe hiyo Mr John Shabani, Jane Miso, Christina Matai, Mwana mapinduzi, Joshua Makondeko na wengine wengi kutoka ndani na nje ya nchi, pamoja na kwaya mbalimbali, ikiwemo ya Joybringers kutoka mikocheni B na Lulu kwaya kutoka mtoni.

                          Catherine Akiwa katika poz na kipenzi chake Mr Sam, raia wa Angola

                                               Mambo ya keki
                                     Jane Miso aka Omoyo, akipokea keki kwa niaba ya wanamuziki wa Injili


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP