18 November 2012

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WATOA SEMINA KWA WASANII




 Meneja wa LAPF akiongelea faida za kujiunga na  mfuko huo
 Mfanyakazi wa LAPF akiwamakini kuandika maswali ya wasanii
 Nahibu katibu mwenezi wa chama cha muziki wa injili bwana John Shabani akitoa mchango wake katika kuboresha maisha ya wasanii nchini


 Waandishi wa habari hawakuwa mbali kurekodi matukio
 Mgao wa kalenda za LAPF
 Katibu wa shirikisho la muziki Tanzania akichangia jambo.
 Wasanii wakijaza famu za kujiunga na mfuko huo
Mfuko wa pensheni wa LAPF, watoa semina kwa wasanii ili waweze kujiunga na mfuko huo na kufaidika na pensheni mbalimbali kwa maisha yao yasasa na ya baadaye.

Mafao yanayotolewa na LAPF ni: Pensheni ya uzee, pensheni ya urithi, pensheni ya ulemavu, mafao ya uzazi, mafao ya mazishi, mikopo ya nyumba pamoja na mikopo ya wanachama kupitia saccos.

Kikao hicho cha aina yake kimefanyika katika majengo ya LAPF MILLENIUM TOWER  kijitonyama Dar es salaam, katika ukumbi wa mikutano gorofa ya nane.

Mengi yamezungumzwa na pia viongozi wa vyama mbalimbali vya wasanii wakiwemo wa nyimbi za injili, walipata fursa ya kuuliza maswali na baada ya hapo tukio la kujaza fomu za kujiunga na  mfuko huo liliendelea.

Kikao hicho kimedhuriwa na viongozi na wawakilishi wa vyama hai vinavyounda shirikisho la muziki Tanzania.

Baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na wasanii, ni kuangalia suala suala la matibabu pamoja na kujegewa nyumba za wasanii ili waendelee kulipia taratibu na baadaye kuwa wamiliki halali wa nyumba hizo.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP