6 November 2012

JOHN SHABANI KUZURU UBELJIJI (BELGIUM) - ULAYA, NI MWALIKO WA KUSHIRIKI ALBUM YA INJILI




                                     John akiwa na Josiane

 Kundi la Destiny Sister
 
Baada ya kumshirikisha katika album yake mpya mwanadada wa kitanzania Josiane na kundi lake la Destiny sisters, mwanadada huyo anayeishi huko Ubeljiji kwa sasa, ameguswa na huduma ya John, na kuamua kumshirikisha katika baadhi ya nyimbo zake. Josiane amepata shavu ya kurekodi nyimbo zake baada ya promota mmoja kuridhika na kiwango kizuri cha uimbaji cha mwanadada huyu.. Josiane aliguswa sana na wimbo alioshirikishwa na John Shabani na pia baada ya John kutumia gharama kubwa kumleta mwanadada huyo 

kutoka ulaya ili kuja kushiriki katika mkanda wa video.
Albam hiyo mpya ya John Shabani inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu. Kuchelewa kutoka kwa video hiyo ya mwalimu wa muziki wa injili afrika mashariki, ni kutokana albam hiyo kushirikishwa waimbaji wengi hivyo kugharimu pesa nyingi na wakati mwingine imekuwa ni vigumu kuwapata waimbaji hao kiurahisi. Inakisiwa takribani shilingi miliono saba (Tsh 7000.000) kutumika katika kugharimia nyimbo hizo kwa maana ya audio na video.

Baadhi ya waimbaji walioshiriki katika album hiyo mpya ya John Shabani ni:
Mzee Cosmas Chidumule, Upendo Kilahiro, Faraja Ntaboba, Destiny Sisters, Bella kombo, Jane Misso, Christina mwang’onda, John Komanya, Children of praise na wengine kibao.

Baadhi ya picha katika maandalizi ya mkanda wa video


 John na Christina Mwang'onda
 John, John Komanya bna Upendo Kilahiro
 John na Comas Chidumule
 John na Faraja Ntaboba

 John na Childern of praise
 John na Destiny Sisters

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP