26 November 2014

WAJANE WAANZA KUNUFAIKA NA CHAMA CHAO



 Wajane wakiwa wametulia nje ya ofisi za chama, huku wakimsikila mwenyekiti
 Mwenyekiti akisaidia kubeba viti
 Wajane wakigonganisha vinywaji vyao na mwenyekiti kwa kutakiana afya njema



Ni mkutano mwingine wa wajane, wakijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja 
na kuimarisha umoja huo.
Akionekana mwenye uso wa furaha, mwenyekiti wa chama hicho ambaye kabla ya kikao kuanza alijitolea kubeba viti na kuvipanga, amewapongeza wajane kwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiunga na chama. Pia kwa juhudi zake mbalimbali, zipo shule  pamoja na wafadhili mbalimbali wamekubali kuwasomesha watoto wa wajane. Wito wa Mwenyekiti ni kuziomba shule mbalimbli kukukubali kuwasomesha watoto wa wajane.
Katika mkutano huo uliofanyika nje ya ofisi za Chama cha Wajane Tanzania , maeneo ya kinyerezi Dar es salaam, wajane pia wamenufaika na misaada kutoka kwa wadhili mbalimbali ikiwa ni pamoja na mavazi, chakula, sukari, mchele pamoja na sabuni.
Mkakati mkubwa sasa ni kuhakikisha kila mjane anasaidiwa kupata mtaji ili kuwa na shughuli binafsi ya kumwingizia kipato, ili kujikimu kimaisha. Maana lengo kuu la chama ni 
kurejesha matumaini ya wajane.
Wito ni kwa wajane wote Tanzania kujitokeza kujiunga na chama hicho kilichosajiliwa kihalali. Pia mlango uko wazi kwa wafadhili wa ndani na nje, taasisi mbalimbali, matajiri na wakereketwa kujitokeza kusimama na wajane na kuwasaidia kwa hali na mali.
Mkakati sasa ni kukieneza chama nchi nzima.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP