THE OFFICIAL JOHN SHABANI AND GOSPEL IN AFRICA BLOG

Welcome to the official blog of the the gospel singer, songwriter and teacher John Shabani. If you are one of the fans among the millions, feel free to get connected with John Shabani and stay updated on this blog.To learn more about John Shaban and his Ministry, please click the about button above.

GET THE LATEST FROM JOHN SHABAN AND THE GOSPEL NEWS COMMUNITY

You will be able to read and review the latest news on John Shabani's tour and other specials. You will also come across the best articles of news on Gospel from all across Africa and the International Community.Please do feel free to review our categories of news and events.

FEEL FREE TO LEARN MORE ABOUT JOHN SHABANI AND HIS MINISTRY

If you wish to learn more about John Shabani and his ministry, please feel free to connect with John Shabani on the social networks. You can keep up with John Shabani and the Gospel in Africa community on both twitter, facebook, google plus and many other more.

STAY UPDATED WITH INTERNATIONAL AND LOCAL GOSPEL NEWS

Gospel in Africa Blog is a comprehensive gathering place for African Gospel music fans. Offering the latest news and information about Local and International Gospel music and news, Gospel in Africa Blog also shares the spotlight with other genres of Christian music that more than ever, seemingly overlap musical genre lines, such as Bluegrass Gospel, Christian Country and others. Singing News, the leading African Gospel and International music Blog, features African and international Gospel lyrics, radio, news, Christian concerts, songs, artists, and more.

GET IN TOUCH AND STAY CONNECTED WITH JOHN SHABANI

If you are interested in contacting and staying in touch with John Shabani then here are the contacts. E- mail: touchingvoice@yahoo.com or , princejohntz@yahoo.com, Mob: +255 754 818 767 or +255 716 560 094, www.facebook.com/john.shabani.

26 November 2014

WAJANE WAANZA KUNUFAIKA NA CHAMA CHAO



 Wajane wakiwa wametulia nje ya ofisi za chama, huku wakimsikila mwenyekiti
 Mwenyekiti akisaidia kubeba viti
 Wajane wakigonganisha vinywaji vyao na mwenyekiti kwa kutakiana afya njema



Ni mkutano mwingine wa wajane, wakijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja 
na kuimarisha umoja huo.
Akionekana mwenye uso wa furaha, mwenyekiti wa chama hicho ambaye kabla ya kikao kuanza alijitolea kubeba viti na kuvipanga, amewapongeza wajane kwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiunga na chama. Pia kwa juhudi zake mbalimbali, zipo shule  pamoja na wafadhili mbalimbali wamekubali kuwasomesha watoto wa wajane. Wito wa Mwenyekiti ni kuziomba shule mbalimbli kukukubali kuwasomesha watoto wa wajane.
Katika mkutano huo uliofanyika nje ya ofisi za Chama cha Wajane Tanzania , maeneo ya kinyerezi Dar es salaam, wajane pia wamenufaika na misaada kutoka kwa wadhili mbalimbali ikiwa ni pamoja na mavazi, chakula, sukari, mchele pamoja na sabuni.
Mkakati mkubwa sasa ni kuhakikisha kila mjane anasaidiwa kupata mtaji ili kuwa na shughuli binafsi ya kumwingizia kipato, ili kujikimu kimaisha. Maana lengo kuu la chama ni 
kurejesha matumaini ya wajane.
Wito ni kwa wajane wote Tanzania kujitokeza kujiunga na chama hicho kilichosajiliwa kihalali. Pia mlango uko wazi kwa wafadhili wa ndani na nje, taasisi mbalimbali, matajiri na wakereketwa kujitokeza kusimama na wajane na kuwasaidia kwa hali na mali.
Mkakati sasa ni kukieneza chama nchi nzima.

20 November 2014

CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI TANZANIA NA MKAKATI WA KUPANDA MITI NA MICHE YA MATUNDA NA MAUA NCHI NZIMA



Hii ni ziara ya kihistoria iliyoandaliwa na chama cha Muziki wa Injili Tanzania.

Mungu alipoumba Dunia, aliifanya yenye kupendeza na kuvutia sana, lakini kwasababu ya matumizi mabaya ya wanadamu, sasa maeneo mengi duniani yanaonekana kama jangwa, kwasababu ya matumizi mabaya ya ardhi, kumekuwa na ukame uliokithiri, ardhi sasa haina rutba ya asili, joto linasumbua duniani kote, majira ya upatikanaji mvua yamebadilika sana; wanaoathirika ni viumbe hai akiwemo mwanadamu.
Kwakulitambua hilo, waimbaji wa nyimbo za injili, tumeamua kujitolea kufanya kampeni nchi nzima ya upandaji miti pamoja na miche ya maua na matunda ili kurejesha uoto wa asili katika nchi yetu.
Pamoja na hayo pia ziara hiyo inaandaa matamasha ya uimbaji ikiwa ni pamoja na kuwahubiri watu waache uovu na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Jambo linguine la msingi ni pamoja na kuwa na kuiombea nchi  amani, utulivu, umoja na mshikano wetu.
Baada ya ziara ya umisheni mkoani singida, waimbaji walipata fursa ya kuhudhuria kikao cha bunge na baadaye kupata picha ya pamoja na  Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, Naibu Waziri wa Fedha Mh. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razaro Nyarandu, Mbunge wa CCM Viti Maalum – Singida Mh. Martha Mlata, Mbunge wa Viti Maalum CCM – Mbeya Mh. Marry Mwanjelwa, Mh. Magreth Sitta na wengine wengi.
Ziara ilihitimishwa kwa kupata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Mh. Nyarando ndani ya Dodoma Hotel. Mh. Nyarando aliweza kuwashukuru waimbaji kwa ushiriakiano wao na jinsi walivyoweza kujitolea kufika vijijini kufanya kazi ya Mungu.
Pia aliweza kuwaahidi waimbaji kutembelea Ngorongoro Crater mapema iwezekanavyo, ili kujifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kutangaza vivutio vya utalii.

Kwa msaada wa Mungu tunaweza!

 waimbaji wakiwa wamejipanga tayari kuelekea kupanda miti


 Msafara wa waimbaji wakishirikiana na wanakijiji wa tarafa ya Ndago mkoani Singida pamoja na viongozi wa dini, wakielekea kupanda miti
 Mheshimiwa Martha Mlata akipanda mti
  Stela Joell akipanda mti
  Madam Ruti akishirikiana na mtangazaji wa Star Tv, bi Sauda  kupanda mti
 John shabani na Jane Misso, wakipanda mti
 Edson Mwasabwite akipanda mti
Mch. Vaileth na Bupe kingu wakishirikiana na watumishi wengine kupanda mti

4 November 2014

Mafundisho ya Askofu Kakobe Kuhusu Pete – asema pete ya ndoa si mpango wa Mungu!



Ni maelezo mbalimbali kuhusu maisha ya Akofu. Baada ya kuulizwa maswali mbalimbali kuhusu maisha yake na huduma, hapa Askofu Zakaria anaendelea kumjibu mwandishi:

Naendelea kuwaletea maelezo kuhusu maisha ya Askofu Kakobe baada ya kuokoka na kuanzisha kanisa.

Mwandishi: Kuna waliosema kuwa ulianzisha kanisa nchini Marekani na ulikuwa na mpango wa kuhamia huko, je ni kweli?

Askofu Kakobe: Kuhama nchi siwezi lakini ni kweli baada ya maombi ya muda mrefu Aprili 16, 2012 nilifungua kanisa Marekani, hii ni nia ileile ya kuokoa mataifa na kuinua jina la Yesu.

Mwandishi: Tunaona watu wakifunga ndoa wanavaa pete lakini katika kanisa lako hilo halipo, unazungumziaje hilo?

Askofu Kakobe: Pete kwenye ndoa siyo agizo la Bwana na ndiyo maana tunaona Mungu mwenyewe akichukizwa na watu waliovaa pete, vikuku na mapambo mengineyo. Soma maandiko haya Isaya 3:21, 16-24; Hosea 2:13;  Mwanzo35:1-5; Kutoka 33:4-6; Yeremia 4:30; 1Timotheo 2:9-10; 1Petro 3:3-5. Mapambo ni mavazi ya waabudu miungu, yanahusishwa na ibada ya miungu (mashetani).

Mwandishi: Lakini wanaotumia pete katika ndoa wanasema eti pete ni mfano wa upendo usio na mwanzo na mwisho, unasemaje kuhusu madai hayo?
Askofu Kakobe: Hiyo siyo kweli, mwanzo wa upendo ni pale walipokutana na wakapendana na mwisho wa upendo ni pale mmoja  anapofariki na kumfanya mwenzake kuwa huru kuolewa au kuoa. Yesu alisema mbinguni hakuna kuoa wala kuolewa.

Hutapewa mke wako au mume wako uishi naye huko mbinguni. Yote hii ni janjajanja ya shetani anayekuja kwa mfano wa malaika wa nuru ili kutufanya tuingize mapambo katika nyumba ya Mungu na kujenga ngome za mashetani kwa visingizio  kwamba mimi nimevaa pete sasa ni mke wa mtu au mume wa mtu. Mbona nyumba za wageni (guest houses) zimejaa watu wenye pete za ndoa? Kama pete hizo zingekuwa zinawafanya watu wasiwe makahaba, tusingekuwa na matatizo tuliyonayo leo.

Habari kutoka: www.kigoma24hours.blogspot.com


HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP