14 February 2017

JIAMBATANISHE NA WATU WATAKAO KUFANYA UWE BORA ZAIDI



Kuna watu wanaweza kuwa sababu ya mafanikio yako au kushindwa kwako, kuinuka kwako au kushuka kwako, kufanya vizuri au kufanya vibaya, kwenda mbali au kubaki hapo hapo!

Chunguza kwa makini watu unao ambatana nao na ikiwezekana, achana na wale wasiokufaa. Sijasema uwadharau, nimesema ujitenge nao. Wengine ni nyoka kwako wanatema sumu, wengine ni kinyonga, wanabadilika badilika, wengine ni konokono, wengine ni Mbweha, kazi yao kuharibu mizabibu, wengine ni Kuku, maisha yao ni ya chini, hivyo wewe kama Tai unahitaji kwenda juu…

Lakini pia zingatia haya;
KUWA NA HESHIMA KWA WATU WENYE MAMLAKA YA KIROHO.
Kuna maeneo 3 yenye mamlaka ya kiroho. Serikali [Taifa], Kanisa na Familia.

Heshimu maeneo haya. Kuna watu wanajikosesha baraka kwa kukosana na maeneo haya 3. Yule ambaye unadhani ni adui ktk maeneo haya matatu mpendwa wangu yamkini ndo amebeba muujiza wa kuinuliwa kwako. Daudi hakumdharau Sauli pamoja na kwamba Mungu alikuwa tayari ameshamkataa. Yusufu hakumdharau Farao au Potifa. Daniel hakuudharau uongozi wa Babeli. Maadui zako ndio waliobeba baraka zako na miujiza yako. Kwenye maeneo haya matatu usigombane nao kama wanakuchukia. Waombee na kuwatakia baraka siku zote nawe utashangaa namna utakavyokuwa ukitembea ktk kibali na neema ya Mungu.

Nakuhakikishia hebu chukua nafasi ya kuombea viongozi wako eneo lako la kazi kila siku uone mabadiliko ktk ofisi yako. Chukua nafasi ya kuombea viongozi wako wa kanisa hata kama wanakuchukia. Chukua nafasi kuwaombea wazazi wako na mwenzi wako hata kama hajaokoka na hata kama anakuchukia. Hao ndio waliobeba ushuhuda na muujiza na baraka zako mwana wa Mungu. Usiwachukie. Maandiko yanasema ‘Wala haikanushiki kabisa kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa’ #WAEBRANIA 7:7. Wakubwa wako hawa wamebeba muujiza wako. Waombee sasa.

Nasema asante kwa Bishop Kitonga, Mtume Fernandos, Dr. Livingstone Banjagala, Dr. Lakhan wa UK, Rose Sarwatt (Mwenyekiti wa TAWIA), Dr. Getrude Rwakatare, Askofu Jangalason, Dr. Migiro (balozi wa Tanzania Wingereza), Mh. Jakaya, Rev. Alex (Mkufunzi wangu pale ISOM na Christian Leadership University), Rev. Wilson Waidhaka (Rafiki yangu sana hapo Nairobi), Rev. Benjamin Bukuku  na wengine kibao. Hekima yenu, ushauri wenu, mafundisho yenu na maisha yenu yamefanyika msaada kwangu na kwa watu wengi.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP