4 November 2018

KUNA VYA KULAZIMISHA VYA KUFORCE LAKINI SIO NDOA

Usilazimishe kuolewa au kuoa, usimnyenyekee mtu ili akuoe au muoane, usijidhalilishe, usijikondeshe, usitokwe na mchozi kwaajili ya kutaka mume/mke.
Utavaa nguo na kumech viatu na mkoba lakini kama MUNGU hajaruhusu uolewe na huyo huto olewa nae. Utajitaidi kumlinda, kumwezesha, kumrembesha, kama ni mkaka unajitaidi kumfanya awe mtanashati, aendane na fashion lakini kama hajaandaliwa kwaajili yako mtapotezeana muda tu.
Usijibebishe My Dear tulia Tulizana Yupo wakukunawisha Uso na Kukushika Mkono Atatoka kwa MUNGU


USITUMIE AKILI YAKO KUYALAZIMISHA MATATIZO YAKUZOEE...
Na Ukimlazimisha Mtu muoane tarajia Matusi na Dharau katika Ndoa yenu. Badala ya kujikomba, kujifanya mtu fulani wa matawi, mdada fulani hivi, badala ya kuongeza kiwango cha kurembua, kiwango cha makeup, wewe badili lifestyle yako na kuanza kuongeza kiwango cha utii kwa Mungu kisha kuomba Mungu akusaidie.

Ndoa ni kitu kizuri sana pale panapokuwapo na utayari wa mioyo ya pande zote mbili, nikimaanisha utayari wa mwanamke na mwanaume wote kuridhia kwa moyo mmoja pasipo kusukumwa kwa namna yeyote ile. Naelewa kuna nature ya Inertia (law of inertia) katika kila maisha ya mwanadamu kwamba smtms hawezi kumove kwenda hatua/sehemu ingine bila external force kuwa applied.

Ila sasa hii haiapply kwenye ishu ya ndoa. Wapo wanawake ambao mara kwa mara wamekuwa wakiforce wanaume wawaoe ili hali wao bado hawako tayari kuoa.

Wangine wanadiriki kuwashikia bango kwamba bwana usiponioa hadi mwezi fulani mimi na wewe basi, unamuimbia mwanaume wimbo wa ndoa ndoa kila kukicha kwamba utanioa lini?, hadi kufia hatua ya kuwapangia kabisa siku ya kwenda kulipa mahari.

Wengine mnatumia mbinu au makakati wa kushika mimba au kujibebesha mimba kisha kuwashinikiza kuolewa kisa mimba. Hii ni hatari sana. Unataka uolewe wewe au hiyo mimba?

Na ndio inapelekea mtu uko kwenye ndoa miezi michache tu unaanza kuichoka ndoa yako mwanaume haeleweki, kwanini? Kwa vile ulimlazimisha kukuoa wakati yeye hakuwa tayari so inamuwia vigumu kubehave like a husband.

Acha kabisa kulazimisha kupendwa, kuolewa, ukiona muda wako unaenda ni vyema ukajiondokea then ukamlingana Mungu ili akupe aliye tayari kuoa na sio kumforce akuoe. Mwanaume siku akiwa tayari kuoa utamwona anaanza yeye mwenyewe kusema sasa nataka nikuoe, siku fulani twende nikalipe mahari kwenu.

Labda huko nyuma ulikosea ukazaa na mwanaume, Kuzaa na mwanaume haimaanishi akuoe. Mwanamke hata siku moja usilazimishe ndoa. Labda kama unataka kuja kujilipua mwenyewe.

Ni ushauri wa bure kutoka kwa Brother John Shabani

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP