18 April 2019

TULIZA FM - MERU KENYA NA SJ STUDIO - TANZANIA WAKISHIRIKIANA NA UMOJA WA MAKANISA, WAANDAA KONGAMANO KUBWA LA KIROHO MERU KENYA


Tulizoea kualikwa, tulizoea kuandaliwa sasa tumevuka mipaka, tumekua,tunaanza kuandaa wenyewe na kualika.  SJ STUDIO, tumeandaa siku sita za mafundisho ya neno la Mungu, kuibua vipaji, kuwaona wenye shida then kurefresh. Ni huko Meru katikati ya Nchi ya Kenya. Wanenaji kutoka Tanzania, South Africa, kenya na waimbaji mbalimbali watakuwepo. Kongamano litarushwa live Tuliza FM. Menyeji wa kongamano hilo ni Askofu Dennis Mwenda wa Live Gospel Church


Ni wiki ya kudumu hekalu mwa Bwana, kuumega mkate, kusifu na kuabudu pamoja na kuanzisha kituo cha mafunzo ya sauti na kuibua vipaji. Lakini pia tutazungukia vivutio vya utalii pia kujifunza maisha ya watu vijijini. Ni kuanzia tarehe 23 mwezi huu wa nne. Njoo tumtumikie Mungu, njoo tujipe raha wenyewe😀😀 Twenzetu kenya

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP