bwana John Shabani akihojiwa na bi Revina Steven mtangazaji
wa Top radio kuhusu chama cha muziki wa injili Tanzania
Mkurugenzi wa Top radio bwana Steven Lukindo akiwa katika picha
na makatibu wenezi wa chamuita.
bwana Magida Timotheo amabaye ni mjumbe wa chamuita
anayewakilisha watu wenye ulemavu, akiwa ameshikilia katiba ya chama
kabla ya kukikabidhi kwenye uongozi wa morogoro
John Shabani akikabidhi fomu za kujiunga na chama
Wawakilishi wa kwaya, bendi na waimbaji binafsi wakionyesha nyuso za
furaha baada ya kuletewa chama cha muziki wa injili morogoro.
Viongozi wa chama wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa
Vatican Lodge bwana Thomas B. Butabile. Hapo ndipo walipofikia viongozi hao.
Maswali mbalimbali yakiulizwa
Chama cha Muziki wa Injili kupitia kamati ya uenezi chini ya makatibu wenezi bwana John Shabani na bi stella Joel, wameanza ziara ya kukieneza chama hicho mikoani, wakianzia na mkoa wa morogoro. Ziara hiyo imetokana na maagizo ya shirikisho la muziki Tanzania (Tanzania music federation) na braza la sanaa la taifa (BASATA), kwamba chama hai ni kile kilichoenea nchi nzima. Wakwa mkoani morogoro, viongozi hao wakiwa wameongozana na mwimbaji bwana Magida Timotheo ambaye ni mjumbe wa chama hicho anayewakilisha watu wenye ulemavu, wamepewa ushirikiano mkubwa na Top Radio chini ya uongozi wa bwana Steven Lukindo. Pia Dada Revina Steven na Dada Bupe kama watangazaji wa redio hiyo, wamefanya kazi kubwa ya kuhamasisha wakaaji wa morogoro na vitongoji vyake, waweze kujiunga na Chama hicho. mamia ya wakaaji wa morogoro wameonyesha kuitikia mwito wa kujiunga na chama hicho na kuomba ziara hiyo isiishie morogoro peke yake bali katika nchi nzima. Viongozi hao wa chama wamekabidhi katiba ya chama na fomu za kujiunga na baada ya muda si mrefu uongozi wa mkoa wa morogoro utaundwa chini ya usimamizi wa makao makuu
0 comments:
Post a Comment