29 November 2011

Martha Mwaipaja avishwa pete ya uchumba


Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Martha Esau Mwaipaja (pichani)  amechumbiwa na Mchungaji, John Said anayehudumia Kanisa la Udhihirisho wa Injili lililopo Ukonga jijini Dar es Salaam, Risasi Jumamosi linakupa habari kamili.

Habari zisizo na chenga zilizotua kwenye meza ya ya blog hii zilisema, Martha alivishwa pete ya uchumba na mchungaji huyo  katika Kanisa la Victoria lililopo Ubungo External jijini Dar na baada ya zoezi hilo kulikuwa na sherehe ndogo kanisani hapo kwa ajili ya kumpongeza kwa kufikia hatua hiyo,”
Mwana dada huyo anayetamba na vibao kama vile Usikate tama, wewe ni baba n.k amekiri kuchumbiwa na mchungaji huyo na kuongeza shughuli ya kesho ilinogeshwa na waimbaji wenzake kama vile Bahati Bukuku, Sarah Mvungi, Ambwene Mwasongwe na Christina Matai.
Wengine ni David Robert, Debora John, Josephine Mwasulama, Ado November, Jennifer Mgendi, Lianga George, Stella Swai na wengineo.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP