10 December 2012

HATIMAYE MTANGAZAJI WA CHANNEL TEN, BONIFACE MAGUPA ATANGAZA MSIMAMO, AMVISHA PETE MCHUMBA WAKE JESSICA HONORE

 Biniface Magupa sambamba na mchumba wake Jesca



 
Ilikuwa ni siku ya kihistoria kwa Boniface na Jessica baada ya kufanya uamuzi wa busara wa kuvisha pete mbele za Mchungaji wao Deo Lubala. Ilikuwa furaha sana katika kanisa la Word Alive. Kama unavyojuwa Jessica Honore ni mwimbaji wa nyimbo za Injili hapa Tanzania, na alikuwa katika wazo zito akijiuliza ni lini mzee mzima atamvisha pete.

Watu walikuwa ni wengi sana kuwa-support maharusi hawa watarajiwa. Kulikuwa na Mkurugenzi wa Global Publisher-Shigongo, Mkurugenzi wa Rumafrica-Rulea Sanga, MD wa Glorious Celebration-Emmanuel Mabisa, Mwimbaji nguli-Robert David, Watangazaji wa Wapo Radio-Mbise na Chiwalo, Mchekeshaji Chavala, Mtangazaji wa Praise Power-Kisaka, Mchungaji Deo Lubala wa WordAlive na wengine wengi

Uongozi wa blogu hii tunawapongeza sana.

Endelea kuwaombea wapendwa hawa.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP