20 December 2012

KONGAMANO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI l LATIKISA DAR ES SALAAM, PIA CHAMUITA WAIOMBA SERIKALI KUWABANA MAHARAMIA WA KAZI ZA MUZIKI




          Waimbaji mbalimbali na wadau wa muziki wa injili ndani ya ukumbi wa wanyama hotel sinza





                                                                           Mchungaji Abel
 Kongamano kubwa la waimbaji wa Muziki wa Injili lililo andaliwa na chama cha Muziki wa Injili Tanzania "CHAMUITA" limefanyika likiwa na lengo la kutambulisha viongozi wapya wa chama cha muziki wa Injili Tanzania pamoja na kutaja malengo ya chama.
Katika kongamano hilo CHAMA cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA), kimeiomba serikali kuhakikisha inasimamia vema kazi zao ili zisihujumiwe, na wao waweze kupata faida kupitia kazi hizo za Mungu.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa semina ya kutoa elimu kwa wadau mbalimbali juu ya kazi zao jijini Dar es Salaam jana, Rais wa chama hicho, Addo Mwasongwe Mwl John Shabani, Bahati bukuku pamoja na waimbaji mbali mbali kwa nyakati tofauti, wametoa ombi hilo kutokana na serikali kuwa na mamlaka makubwa hapa nchini ya kulisimamia suala hilo.
“Serikali ina uwezo mkubwa wa kuhakikisha sisi wasanii tunanufaika na kazi zetu, kwa kuwa wao wakianza kuwakamata ambao wanatuhujumu na kuwachukulia hatua, nina imani mambo haya yataisha na sisi tutazidi kujivunia kazi zetu ambazo zinaleta ajira hapa nchini,” alisema Mwasongwe.
Aidha, Mwasongwe alisema wanachukizwa na kitendo cha Wakristo kufanya wizi wa kazi za Mungu, wakati kila Jumapili huenda kwenye ibada na kumtukuza.
“Tunasikitishwa sana kwa kuwa miongoni mwa wezi wa kazi zetu na Wakristo nao wamo, inauma sana, mtu anakwenda kwa wale ‘wanaobani’ CD na kumuomba nichanganyie nyimbo ya Bukuku, Mkone na wengine, wakati yeye kama Mkristo anatakiwa kuwa mstari wa mbele kuacha kufanya hivyo. Hivyo basi tuna imani serikali itatusaidia,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, CHAMUITA kiliwatambulisha viongozi wapya ambao ni Addo Mwasongwe (Mwenyekiti), Mchungaji Joseph Malumbu (Makamu Mwenyekiti), David Mwamsojo (Katibu), Stella Joel (Katibu Msaidizi), John Shabani (Naibu Mwenezi), na Upendo Kilahiro (Mweka Hazina), huku wajumbe wa Kamati Kuu wakiwa zaidi ya 60, wakiongozwa na Mbunge Martha Mlata, Christina Shusho na Bahati Bukuku.pamoja mh. Martha mlata (Mbunge wa singida viti maalum CCM na Mr Alex Msama ambao ni walezi wa chama hicho.


Miongoni mwa madhumuni ya semina hiyo ni kulinda utamaduni wa Tanzania na heshima ya muziki huo, kuhamasisha maendeleo ya muziki huo na nyanja zake nyingine, kuwa na chombo cha kuwezesha mawasiliano kati ya watu na vikundi katika kupeana taarifa mbalimbali na mengine mengi ambapo iliudhuriwa na wanamuziki wengi wa injili hapa nchini.
        Lulyalya Sayi Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki akieleza umuhimu wa mfuko wa LAPF               
 
                                          Abubakari Ndwaka Meneja Mafao wa LAPF.  

Katika kongamano hilo liliudhuriwa na viongozi wa mfuko wa pensheni wa LAPF ambao ndio waliokuwa wadhamini wakuu wa kungamano hilo. Mfuko huu ulizungumzia umuhimu kwa waimbaji wa muziki wa injili kujiunga nao kama sehemu mojawapo ya wao kuwekeza katika maisha ya baadae, pia kutoa fursa kwao kujipatia mikopo ya nyumba na kuwekeza katika akiba yao ya baadae.



Pia kampuni ya Grace products ltd inayojihusisha na kutengeneza mafuta ya ngozi, shampoo, sabuni na bidhaa mbalimbali zisizokuwa na kemikali, walikuwepo katika kongamano hilo wakiwaelimisha waimbaji na watumishi wa Mungu kutumia bidhaa nzuri kwaajili ya kulinda miili yao. Pia afisa kutoka TRA alifafanua jinsi serikali ilivyojipanga kuwasaidia wasanii nchini. Kongamano hilo limehudhuriwa pia na wachungaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi akiwemo Nabii Machibya kutoka wingereza.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP