3 December 2012

MWIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI KUTOKA SWEDEN KUFAYA KWELI MKUTANO WA BIAFRA.

                                          Rachel akiwa kazini
                                                




Kwa wale wapenzi wa nyimbo za injili, jina la la Rachel Scharp (Rachael Scharp) si ngeni, kwani nyimbo zake zimetokea kupendwa sana hasa nchi za ulaya. Kati ya waimbaji watakao hudumu kwenye mkutano mkubwa wa injili Bafra Dar es salaam, ni pamoja na mwimbaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheza na kuimba mbele za Bwana.

Akihojiwa na John Shabani (mmiliki wa blogu hii), Rachael sambamba na kundi lake ameahidi kufanya kweli katika mkutano huo. Mkutano huo wa kimataifa, utahubiriwa na muhubiri wa kimataifa Dr. Godfrey Kamese anayezunguka duniani kote akihubiri neno la Mungu, kuponya na kufungua maelfu ya watu kwa jina la Yesu.
Tayari jukwaa la kisasa limefungwa katika uwanja huo. Jukwaa hilo la kisasa  lina taa za kisasa na vyombo vya muziki vya kisasa ,

Hii ni neema kwa watanzania kutembelewa na mtumishi huyo ambaye Mungu amekuwa akimtumia kwa viwango vikubwa. Hebu tazama baadhi ya matukio katika mikutano yake mikubwa duniani. Kwa habari zaidi: 0716560094, 0754818767


0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP