2 January 2015

JOHN SHABANI NA ZIARA YA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII WA TANZANIA PAMOJA NA KUIBUA VIPAJI VYA WATOTO

 Nikiwa na watalii mbalimbali karibu na mto wa ajabu, baada ya kuzunguka kutwa nzima eneo la Ngorongoro Crater, watalii huja mahali hapa penye idadikubwa ya viboko.
 Imekuwa ni ziara ya kipekee kati ya ziara nilizowahi kuzifanya. Kwani nimejionea moja ya maajabu ya dunia, Ngorongoro Crater. Pia nimeweza kuibua vipaji vya watoto pamoja na kurekodi nyimbo kadhaa.
Ngorongoro ("Ngorongoro Conservation Area") ni umbali wa takribani kilomita 180 kutoka Arusha na pia hifadhi ya taifa inayojulikana kote duniani. Eneo hili ni sehemu ya Serengeti.
Kuna jumla la wanyamapori wakubwa takriban 25,000, wakiwa pamoja na vifaru, viboko, nyumbu, pundamilia, nyati, simba, fisi na chui .
Ngorongoro imepokelewa katika orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO.


Je unajua kitu kuhusu Ngorongoro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
NI mahali pekee panapohifadhi wanyamapori na binadamu, mchanga unaohama, palipogunduliwa nyayo za miguu na fuvu la binadamu wa kwanza.
Pia, kuna Ziwa Magadi ndani ya bonde refu na kubwa maarufu kwa jina la ‘Ngorongoro Crater’ lililosababishwa na milipuko ya volcano zaidi ya miaka 2000 iliyopita.
Mahali hapo si pengine popote, ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (Ngorongoro Conservation Area Authority – NCAA) iliyoanzishwa mwaka 1959 na kukabidhiwa majukumu makuu yafuatayo:
Kuhifadhi maliasili (wanyamapori, ndege na mazingira) zilizopo, kuendeleza binadamu wenyeji (Wamaasai) na utalii katika hifadhi hiyo.
Ina eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 8,292, inapakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) upande wa Kaskazini Magharibi na miji ya Arusha, Moshi na Mlima Kilimanjaro upande wa Mashariki. Maelfu ya watalii kila mwaka kutoka pembe nne za dunia hutembelea Ngorongoro.





 Nikiwa na watoto wa Shalom Orphanage center baada ya kukaribishwa kula chakula                  katika hotel ya Sarena

 John Shabani, watoto wa Shalom na rafiki zetu wengine
Nikiwa na kundi kubwa la watoto baada yakupata chakula katika hotel ya Serena

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP