4 June 2015

LEON MAC'S NA ANNA MAC'S WANANDOA WANAOFANYA VIZURI KATIKA KUMWIMBIA BWANA


Huu ndio muonekano wa ujio wa Leon na Anna. Hakika ni mfano wa kuigwa, lakini pia nyimbo zao zina mguso wa pekee. Jiandae kubarikiwa na nyimbo za zao.



Hivi ndivyo wanavyosema Leon Mac’s na Anna Kihwili Mac’s ambao ni mume na mke: 

Tumemtolea Bwana Yesu maisha yetu miaka 12 iliyopita na tulifunga ndoa miaka sita iliyopita. Wote tumepewa neema ya utunzi na   tumemtumkia Mungu katika makanisa mbalimbali,  kwa hivi sasa Mungu ametupa kibali cha kufanya album yetu ya kusifu na kuabudu tunayotarajia kuimaliza hivi karibuni, inaitwa Roho Mtakatifu (Njoni) na ni jina la nyimbo ambayo tunaitambulisha  sasa

Nyimbo hii ilikuja kwetu kama  ufunuo ambao tumeuishi na kuufanyia kazi kwa muda wa miaka mitano sasa, ni maombi yetu kuwa kanisa tutampa Mungu wetu Roho Mtakatifu nafasi ya Kutukusanya na kutuongoza katika kumwabudu BABA siku zote za maisha yetu.


Albam itakuwa na nyimbo 10 kama

Roho Mtakatifu (Njoni) , karibu Mtukufu ,Naomba nafasi, Asante, Sintoacha kukusifu(Neno),, New song, Nakuabudu, Karibu Roho wa Bwana na nyinginezo.

Tunawaomba wadau wa mziki wa injili kutupa support na maombi katika kipindi chote cha maandalizi na hakika hautapoteza muda maana utafanya kitu kikubwa sana katika ufalme.


Pia wako tayari kwa mialiko ya huduma katika huduma mbalimbali kama semina, mikutano, maombezi n.k

Wafuatilie katika mitandao ya kijamii kama facebook na twittwer kwa majina yao au piga simu namba 
0713375588 au 0716421881 
na MUNGU AWABARIKI SANA.


0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP