9 August 2017

MSICHANA/MWANAMKE AMBAYE HAUJAOLEWA, KUWA KIROHO ISIWE SABABU YA KUTO-JICHANGANYA NA WATU NA KUJENGA MAHUSIANO

 WOKOVU SIYO KUWA  "ANTI SOCIAL" (KUTO KUJICHANGANYA NA WATU)
 Mara nyingi, mahusiano yanayopelekea uchumba hadi ndoa, huanzia katika hutua ya URAFIKI. urafiki hujengwa kwa watu kuwa pamoja, kubadilishana mawazo, kula pamoja, kucheza na kufanya mambo mengi pamoja.



Kotoka kwa Pastor Zakayo Nzogere
WARAKA WA PILI WA ZAKAYO KWA "BACHELORETTES" (Wanawake/Wasichana ambao hawajaingia kwenye ndoa na walio katika mchakato wa kupata wenzi wa maisha).


Utafiti unaonyesha kwamba wadada wengi “WAPENDWA” wanashindwa katika kipengele cha URAFIKI. Wapo wanaodhania kuwa KIROHO ni kuwa full-time kwenye maombi; yani hakuna muda wa kucheka na kufurahi, hakuna michezo, wala kuzoeana na WANAUME. Huu ni msimamo potofu. Yani unakuta MDADA yeye full-time anongelea maombi, mkesha, ushuhudiaji, na ibada. Hana muda wa kuzungumza mambo ya kawaida yanayohusu maisha na mahusiano hata na vijana wa kanisani.
Ni kweli ni vizuri kuwa KIROHO; lakini kuwa kiroho isiwe sababu ya kuto-jichanganya na watu na kujenga mahusiano. Kuna baadhi WADADA WAPENDWA wanawaona WANAUME wote ni watenda dhambi. Yani mtu akitaka kuanza nae mahusiano ya kujuana/urafiki, yeye tayari anakuwa kwenye ALARM ya DANGER… yani anachokiona kwa kijana ni kwamba lazima atakuwa ana nia mbaya.
Ushauri wangu kwa WADADA ni kwamba ni muhimu tujenge mahusiano ya kirafiki na vijana makanisani mwetu. Urafiki ni hatua muhimu ya kufanya maamuzi yanayopelekea uchumba hadi ndoa. Tusivae SURA YA MAOMBI kila saa….!!
Kwa upande mwingine, VIONGOZI WA MAKANISA, tusiwawekee vijana wetu (KIKE/KIUME) vikwazo vingi ambavyo vinasababisha wasiweze kujenga mahusiano. Ni kweli lazima TUSISITIZIE UTAKATIFU lakini tusifanye WOKOVU UGEUKE GEREZA. Tusiporuhusu wajenge mahusiano, je, wataoanaje?? Tuwafundishe vijana wetu wawe na nidhamu ya kuweza kujisimamia na kujua MIPAKA ya urafiki na mahusiano kati yao. Vijana wetu wakibanwa sana wataanza mahusiano kwa siri ambayo mara nyingi huishia vibaya; pia wanaweza kutafuta marafiki nje ya kanisa ambayo pia matokeo yake siyo mazuri sana.
MITHALI 17:17 (BHN); "Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote, ndugu huzaliwa asaidie wakati wa taabu."

 

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP