25 February 2020

ZIARA YANGU KUMTEMBELEA MZEE WA KIMAASAI MWENYE WAKE 33 NA WATOTO PAMOJA NA WAJUKUU 360


Nikiwa nimetembelea Mkoa wa Arusha wilayani Monduli, Nchini Tanzania ndipo ninapokutana na mzee mwenye umri wa miaka 105. Idadi ya watoto na wajukuu wa mzee huyo ni 360 na wake 33.
Huyu ni Mzee Meshuko Ole Mapi, almaarufu Mzee Laiboni.
 Amelazimika kuwa na shule yake na soko kwa ajili ya jamii yake hiyo na anasema bado ana azma ya kuendelea kuoa. Watu kutoka mataifa mbali mbali hufika kumtembelea mzee huyo kama sehemu ya utalii.
Nilimuuliza idadi ya familia yake na shule aliyoanzisha na kwa sababu mzee huyo hajui lugha ya kiswahili alikuwa na mkalimani wake ambaye alimtafsiria lugha ya kiswahili
Mkalimani wake alisema kuwa
Kuhusu ni vipi mzee angeweza kuhudumia familia yote hiyo licha ya umri wake alisema kwamba,wakati wa kiangazi yeye huuza ngombe na kununua mahindi
Aliongezea kuwa idadi ya ngombe alionao inakaribia 3000.
Mzee laiboni alisema kuwa wazo la ujenzi wa shule,lilijiri kwa sababu watoto wake walikua wanasoma shule ya mbali na kuna wakati walikua wakishindwa kwenda shule kutokana na tembo ambao pia waliwahi kuua mtu.
Baadaye nilionana na mwalimu mkuu wa shule hiyo. Mwalimu huyo alisema kuwa licha ya kuwa mzee Laiboni sio mbaguzi lakini asilimia 90 ya wanafunzi wote ni watoto wake.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP