29 September 2014

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI ALIYEVAA MADHABAHUNI VAZI LA UFUKWENI AKERA WENGI



Huyu ni muimbaji wa kike wa nyimbo za injili ambae yuko nchini Marekani. Na katika mkesha mmoja nchini humo alipanda kuhudumu akiwa amevaa mavazi haya, jambo ambalo liliwashangaza hata baadhi ya wamarekani.
Naamini kabisa hata kufikia maamuzi ya kuvaa hivi ana sababu zake binafsi na pia hata maandiko ya kujitetea anayo, na andiko ambalo wanapenda kulitumia hata watumishi wa type ya huyu mama ni Mungu anaangalia moyo haangalii mavazi, lakini wanasahau kabisa lile andiko linalosema makwazo hayana budi kuja, na ole wake yule ayaletae.
Andiko lingine wanalopenda kujifichia ni lile ambalo Paulo anasema kwa Warumi alikuwa kama Mrumi ili awapate warumi. Huku wakisahau kuwa kanisani sio kwa Warumi hivyo unatakiwa uwe kama mtumishi ili injili yako isipate kikwazo. Maana huwezi kuvaa vazi la kikahaba na kuanza kutabiri alafu watu wakaupokea ujumbe wako kwa amani, lazima watazaa maswali wmbayo majibu yao yatafanya wakukatae wewe na ujumbe wako hata kama ni mzuri kiasi gani.
Ushauri wangu kwenu ndugu zangu dada zangu wa type hii, msibebe biashara ile na kuinadi kwa njia ya bible alafu mkazuga kuwa mmechanganywa na utamu wa Yesu.
Huo ni ushauri wangu kwenu na pia ni mawazo yangu.
Ewe Mtume, Nabii, Mchungaji, Muinjilisti, Mwalimu, Askofu,Mzee, Shemasi, hata muumini wa kawaida kemea tabia na uvaaji kama huu maana hizi ni hila za shetani ndani ya kanisa. Maana kitendo cha mtu kuvaa kihuni alafu ukampa madhabahu, hata wanaokutazama watahisi na wewe una hitirafu kichwani ndio maana unakubaliana na uhuni.


Habari kutoka Mr Bashando

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP