21 October 2016

PESA HAILETI MAPENZI YA KWELI

 
Pesa haileti mapenzi ya kweli, 
bali mapenzi ya kweli huleta pesa!
Palipo na mapenzi ya kweli pana utulivu na nafasi, hivyo huchangia kuleta nguvu katika utafutaji.
Rafiki, hakuna ubishi mapenzi yanachukua nafasi kubwa katika maisha yetu. Mimi na wewe tunahitaji kuwa na wapenzi tena wenye mapenzi ya dhati ili maisha yetu yaweze kukamilika.
Bila kuwa na mtu ambaye kuna wakati unammis, ukiwa naye unajiona ni mwenye bahati kwa faraja anayokupa, ni lazima utahisi umepungukiwa kitu muhimu. Lakini wakati ukweli ukiwa hivyo, wapo wanaochukulia mapenzi kama kitu rahisirahisi. 

HEBU jiulize kwa nafasi yako hapo ulipo, unautendea haki moyo wako? Mpenzi uliyenaye unampenda au unajilazimisha Elewa kuwa mapenzi ni sehemu ya maisha yetu na kwa hakika maisha yetu hayawezi kukamilika bila kuwepo mapenzi. Ninapozungumza juu ya mapenzi namaanisha yale yanayotoka moyoni mwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Ikiwa unaye mpenzi, boresha mapenzi yenu. Ikiwa ndio kwanza hatua ya urafiki au uchumba na tayari mwiba unakuchoma, acha kuwa king'ang'anizi, ikiwa ndio bado mchakato unaendelea, ni sala na maombi yangu kwa Mungu, mimi na wewe atuwezeshe kuwapata walio sehemu yetu.
Lakini pia zingatia, huwezi kumpata malaika.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP