24 October 2011

TANZANIA GOSPEL STARS WAKAMILISHA VIDEO YA WIMBO WA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA

Hatimaye waimbaji wa nyimbo za injili Tanzania  wakiongozwa na mwalimu wa muziki wa injili afrika mashariki bwana John Shabani, chini ya usimamizi wa chama cha muziki wa injili Tanzania (Chamuita) wamekamilisha video ya wimbo ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Pamoja na waimbaji mbalimbali kushiriki katika wimbo huo pia yumo mheshimiwa Martha Mlata ambaye amechangia sana katika kufanikisha kurekodi wimbo huo. Baadhi yam abo aliyo yafanya ni pamoja na kufanikisha kupata sare na bendera kutoka serekalini pamoja na kutoa feha za kufanikisha kurekodi video. Pia studio ya Pro arts studio ya jijini Dar es salaam ilijitolea kurekodi sauti. Wazo la kuwakusanya waimbaji wa injili na kurekodi wimbo wa miaka 50 ya uhuru, lilianzishwa na bwana Tc Timothy  Chelula na kumshirikisha mwalimu John Shabani, ndipo walipo kihusisha chama cha muziki wa injili na vyombo mbalimbali vya habari. Muda si mrefu wimbo huo utasambazwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Baadhi ya waimbaji walioshiriki kurekodi wimbo huo ni:
1. Gloria kilahiro                                            18. Mzee Makassy
2. Amon Kilahiro                                            19. Mzungu Four
3. Masanja Mkandamizaji                                20  Jane Misso
4. Upendo kilahiro                                            21 Addo November
5. Stella Joel                                                  22. Martha Mlata
6. Nely Nyamanga                                         23. Ambwene mwasongwe
7. Joyce Ombeni                                                                                                                       
8.  Bony Mwaitege                                          24. Douglas Pius
9. John Shabani                                              25. Mchumu Maximillian
10. Rose Manoza                                              26. Charles Thobias Malya
11. Yona Abiud                                                  27. Joshua makondeko
12. Miriam Lukindo Mauki                                  28. Daniel Safari
13. Robert Bukelebe                                          29. Naomy Mbwambo
14. Nicholaus Misuzi                                          30. Joseph kasigala
15. Christina Matai                                             31. Debora Said
 16. Tina Marego                                               32. Stara Thomas  
17. Martha Mwaipaja                                        33. Victor Ahron
Na wengine wengi.
                                Mheshimiwa Martha, Mr Masanja na Malimu John wakitabasamu
                  Kampuni ya Pro arts wakiwa kazini
                                  Masanja mkandamizaji akifanya vitu vyake


                            Baadhi ya magari mbalimbali ya waimbaji nnje ya jengo la studio

                     Mwimbaji mkongwe mzee makasi katika pozi
                      Mwalimu John Shabani akiwaongoza waimbaji wa Injili


Pamoja na hayo, viongozi wa chama cha muziki wa injili Tanzania tunatoa wito wa kujiunga na chama hicho, kwani kuna faida nyingi za kujiunga na chama. Fomu sasa zinapatyikana. kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0754818767, 0716560094.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP