6 October 2011

WAIMBAJI WA INJILI WAMTUNUKU MKURUGENZI WA KAMPUNI YA MSAMA PROMOTION CHETI CHA HESHIMA



                                Alex Msama akiwashukuru waimbaji wa injili



                          Waimbaji wa nyimbo za Injili wakiongozwa na mwalimu John shabani, 
        wakiutambulisha wimbo wa miaka 50 ya uhuru wa tanzania mbele ya waandishi wa habari.
        Kulia ni mwimbaji mheshimiwa Martha Mlata, sambamba na Rais wa chama cha muziki wa Injili
        Tanzania (Chamuita) bwana Addo November, Katibu wa Chama Jane Misso, Makatibu wenezi Stella
         Joel na John Shabani, Meneja Wa Praise Power Radio Mr George Mpela na wengine wengi.

Chama cha muziki wa injili Tanzania (Chamuita) kikishirikiana na waimbaji wa injili, wamemtunuku cheti cha heshima (Certificate of appreciation) bwana Alex Msama ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Msama promotions. Amekabithiwa cheti hicho mbele ya waandishi mbalimbali wa habari, ni kwa ajili ya kumpongeza kwa moyo wake wa kupigania haki za wanamuziki kwa kupigana na maharamia wa kazi za wanamuziki.

Pia waimbaji hao kwa pamoja mbele ya waandishi wa habari, wameutambulisha wimbo wa miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Wakiongozwa na mwalimu John Shabani wameimba kwa umahiri mkubwa kiitikio cha wimbo huo. Sehemu ya wimbo huo ni: {Haaa tumethubutu, tumeweza, tunasonga mbele kwa uwez wa Mungu Tanzania. Sehemu nyingine ni: Tuitunze amani yetu watanzania, tudumishi umoja wetu watanzania} Hii ni kwa mara ya kwanzaktika historia ya Tanzania, waimbaji zaidi ya 50 wa nyimbo za injili kuwa maali pamoja na kurekodi wimbo wa kumshuku Mwenyezi Mungu kwa ajili ya uhuru wa Tanzania. Baadhi ya waimbaji walioshiriki kurekodi wimbo huo ni:

1. Gloria kilahiro                                            18. Mzee Makassy
2. Amon Kilahiro                                            19. Mzungu Four
3. Masanja Mkandamizaji                                20  Jane Misso
4. Upendo kilahiro                                            21 Addo November
5. Stella Joel                                                  22. Martha Mlata
6. Nely Nyamanga                                         23. Ambwene mwasongwe
7. Joyce Ombeni                                                                                                                       
8.  Bony Mwaitege                                          24. Douglas Pius
9. John Shabani                                              25. Mchumu Maximillian
10. Rose Manoza                                              26. Charles Thobias Malya
11. Yona Abiud                                                  27. Joshua makondeko
12. Miriam Lukindo Mauki                                  28. Daniel Safari
13. Robert Bukelebe                                          29. Naomy Mbwambo
14. Nicholaus Misuzi                                          30. Joseph kasigala
15. Christina Matai                                             31. Debora Said
 16. Tina Marego                                               32. Stara Thomas  
17. Martha Mwaipaja                                        33. Victor Ahron
Na wengine wengi.

Wengine kwasababu mbalimbali, wameahidi kushiriki kwenye video inayotegemea kuandaliwa mapema iwezekanavyo. Kazi hii kubwa ya kuwakutanisha  waimbaji wa injili na kurekodi wimbo, imefanyika katika studio za PRO ARTS STUDIOS iliopo mbezi africana Dar es salaam, chini ya Producer TC (Timothy Chilula) Ambaye pia ni miongoni mwa waanzilishi wa wazo hili


                    Waandishi wakimuhoji mmoja wa wakongwe wa muziki
                           wa injili Mchungaji Mzungu Four

                              Rais wa Chamuita akiongea na waandishi


                                   Mheshimiwa Martha Mlata ambaye pia ni mmoja wa walezi wa Chamuita
                              akimpongeza Msama pamoja na  kutoa wito kwa serikali kuliangalia suala la wanamuziki
                              kwa jicho la tofauti.
                           Waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari Nchini Tanzania

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP