21 December 2011

BELLA KOMBO AMRUDIA BWANA


Christabella Kombo kwa jina maaarufu Bella Kombo, hivi karibuni ameamua kuachana na muziki wa dunia na kuanza kumwimbia Bwana. Mwanadada huyo aliyeonekana kuvutia sana kwenye mashindano ya Bongo Star Seach BSS ya 2010 na 2011, hivi sasa amerekodi album yake ya nyimbo za injili. Kabla hajajiunga na Bss, Bella alikua mwimbaji mzuri kanisani na pia sauti ya Bella imesikika sana ktika baadhi ya nyimbo mbalimbali za mwalimu John Shabani.

Akiongea na mwandishi wa blog hii, bella amekiri kumrudia Bwana maana yeye siku zote alikua ni mwimbaji kanisani. Kilichotokea ni kwamba, baada ya watu na wadau mbalimbali kugundua kipaji chake, walimshauri na kumshawishi ajiunge na Bss kwamba huko kipaji chake kitajulikana zaidi pamoja na kujitangaza kwasababu kazi ya Bss ni kuinua vipaji haijalishi unaimba maadhi gani ya muziki. Baada ya kipaji chake kujulikana zaidi, alishawishiwa kujiunga na kundi la Machozi Band, hata hivyo moyo wake umekuwa ni wa kumwimbia mwenyezi Mungu. Baada ya kushauriwa na watu pamoja na watumishi mbalimbali hasa zaidi mwalimu wake bwana John Shabani ambaye hapo awali amekuwa akiimba pamoja na bella, ndipo alipoamua kurudi kundini na kuanza tena kumwimbia Bwana.

Hivi sasa Bella anategemea kujiunga na kundi la Glorious Celebration la jijini Dar es salaam.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP