13 December 2011

WIMBO ULIOIMBWA NA TANZANIA GOSPEL ALL STARS WAPATA HESHIMA YA KUWA WIMBO MAALUM KATKA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA

                                   Umati wa maelfu ya watu

                                        Upendo kilahiro akiwa na mwalimu John Shabani
                                    G stars wakiimba mbele ya marais na waheshimiwa mbalimbali
                                       Mwalimu maarufu wa nyimbo za injili Afrika mashariki
                                      (John shabani), akiimba kwa hisia kali mbele ya rais



                          Mzee makasy (Mwimbaji mkongwe), Akiimba mbele ya rais



                             Mheshimiwa martha mlata akiimba kwa hisia

                                Mtoto wa miaka 6 Gloria kilahiro akiimba kwa hisia kali mbele ya waheshimiwa



                              



Wimbo wa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania ulioimbwa na Tanzania Gospel All stars (Waimbaji nyota wa muziki wa injili Tanzania), umepata hadhi na heshima ya kuwa wimbo maalumu katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara.

Chini ya mwalimu John shabani na usimamizi wa chama cha muziki wa injili Tanzania(Chamuita), Waimbaji hao walipewa nafasi maalum ya kuimba wimbo huo mbele ya Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete na mbele ya marais wa nchi mbalimbali, mawaziri, wabunge, mabalozi,  pomoja na maelfu ya watu waliohudhuria katika maadhimisho hayo. Viongozi na watu mbalimbali wamewapongeza waimbaji hao wa injili kwa umoja na mshikamano wao, pia wameupongeza wimbo huo, hivyo kuwaomba kuusambaza wimbo huo kwa watanzania ili kila mtu abarikiwe na wimbo huo

Hii ni mara ya kwanza kwa waimbaji wa injili kuungana pamoja na kurekodi wimbo wa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya uhuru wa Tanzania.
Video ya wimbo huo inategemea kusambazwa kwa watanzania kwa gharama ndogo.

Waimbaji walioshiriki kurekodi wimbo huo ni:

1. Gloria kilahiro                                            18. Mzee Makassy
2. Amon Kilahiro                                            19. Mzungu Four
3. Masanja Mkandamizaji                                20  Jane Misso
4. Upendo kilahiro                                            21 Addo November
5. Stella Joel                                                  22. Mheshimiwa Martha Mlata
6. Nely Nyamanga                                         23. Ambwene mwasongwe
7. Joyce Ombeni                                                                                                                    
8.  Bony Mwaitege                                          24. Douglas Pius
9. John Shabani                                              25. Mchumu Maximillian
10. Rose Manoza                                              26. Charles Thobias Malya
11. Yona Abiud                                                  27. Joshua makondeko
12. Miriam Lukindo Mauki                                  28. Daniel Safari
13. Robert Bukelebe                                          29. Naomy Mbwambo
14. Nicholaus Misuzi                                          30. Joseph kasigala
15. Christina Matai                                             31. Debora Said
 16. Tina Marego                                               32. Stara Thomas  
17. Martha Mwaipaja                                        33. Victor Ahron
Na wengine wengi.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP