27 February 2012

GLORIOUS CELEBRATION BAND



 Band nzuri inayovuma kwa sasa nchini Tanzania, kwa uchezaji wao wa staha na sauti zenye kusikika vyema. Kiongozi wa  Glorious Celebration Band Emmanuel Mabisa, aliongea nasi machache kuhusu kazi yao na malengo waliyonayo katika kuujenga mwili wa Kristo.

“Maono yetu ni kufanya huduma mashuleni na vyuoni kwa ajili ya kuwahubiria Vijana Habari njema za Kristo, na pia kufanya matamasha makubwa mbali mbali”
Alkadhalika kundi hili linaundwa na waimbaji mahiri wanaosikika kwenye soko la muziki wa injili na wengine chipukizi wanasikika. Band hii inalelewa na msimamizi mkuu Bishop Mwakang’ata wa Full victory Gospel Church ya Chang’ombe Temeke, Dar es salaam.
Waimbaji wengine wanaounda kundi hilo ni Angel Bernard ambaye ndiye mweka hazima, Chaka Mtunguja Katibu wao, Jesca Honore, Nice Marandu, Davina, Risper, Ima Malisa, Emmanuel Materu, Emmanuel Gripa, Daniel Kibambe, Arone Botto, David Silomba, Ester Peter, Paul Mwakanyamale na Mercy Denis.
Kwa sasa wanajiandaa kurekodi Live Dvd mapema mwezi wa sita mwaka 2012! Hapo awali wamerekodi video ya album yao ya kwanza NIGUSE, unaweza kufarijika kwa kusikia wimbo huu wa NIGUSE,
Mpaka sasa wametimiza mwaka mmoja tangu wameanzisha bendi yao na wametoka na album ya NIGUSE….hata hivyo kama watu walivyozoea kila Ijumaa kuwaona THE ATRIUMS HOTEL, kwa sasa itakuwa wanamtukuza Mungu kila ijumaa ya mwisho wa mwezi, viwanja vile vile.
Tanzania tunajivunia kuwa na waimbaji kama hawa!

1 comments:

Anonymous said...

Napenda kumba sana! na kumtukuza mungu wangu sana, je niktaka kujiunga nao nitapaswa nimuone nani katika kundi lao?!

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP