20 February 2013

MWIMBAJI DAVID ROBERT: AWAKUTANISHA BAADHI YA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI KUTENGENEZA WIMBO MAALUM WA KULIOMBEA TAIFA.





Kushoto ni Upendo Nkone,Upendo Kilahilo,Bahati Bukuku,Rose Muhando,Christina Shusho.




 David Robert akihojiwa na Samweli Sasali.



Ni kawaida kusikia Kanisa flani lina fanya maombi kwajili ya Taifa au Mkutano fulani ulioandaliwa kwa sababu ya kuombea nchi. Hivi ndivyo imetokea kwa baadhi ya waimbaji wa muziki wa injili kukutana na kutengeneza wimbo mmoja wenye lengo la kuiombea amani Taifa la Tanzania, hii ni kwa mujibu wa David Robert ambaye ndiye msimamizi wa shughuli nzima ya uandaaji wa wimbo huo.

WAZO LA KUWAKUTANISHA WAIMBAJI
"Siku Moja nikiwa na Bahati Bukuku Likatujia Wazo Kwanini Tusifanye Wimbo Wa Kuombea Amani Tanzania, It was very strong in our hearts, then tukaanza utaratibu wa Kuwatafuta Wanamuziki na Kuwasiliana nao walipo, Ilipata Muitikio Mkubwa sana, Rose Muhando, Bahati Bukuku, Florah Mbasha na wengine wengi unaowajua tukakaa pamoja tuka record, na Jana ndio tumemaliza shooting ya wimbo Huo, kwa sasa tunasubiri tu Kukamilika Kisha tutauweka Wakfu wimbo huo"..Haya yalikuwa ni baadhi ya Maneno Ya David Robert akihojiwa na Samweli Sasali.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP