10 April 2013

MAHAFALI YA CHUO CHA HUDUMA CHA KIMATAIFA (INTERNATIONAL SCHOOL OF MINISTRY - ISOM) YAFANA DAR ES SALAAM

John shabani akikabidhiwa cheti na askofu kitonga

 Band ya matarumbeta ikiwaongoza wahitimu kuelekea ukumbini

 Bishop Kitonga sambamba na  Mtume Prosper Ntepa


 Mmoja wa watoto wanaolelewa kihuduma na John shabani

Picha na mwakilishi wa Isom kutoka Marekani, Dr Lee


Hatimaye maelfu ya watu wameshuudia mahafali ya kwanza ya chuo cha kimataifa cha huduma (International School of Ministry – Isom).  Chuo hicho chenye makao makuu huko California Marekani, mpaka sasa  kimeenea katika nchi 145 duniani na kufundishwa katika lugha zaidi ya 65 za mataifa mbalimbali.

Mahafali hayo ya kwanza kwa Tanzania yameacha historia, yakiwa yamehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.  Mgeni Rasmi alikuwa Askofu Arthur Kitonga  (Mwanzilishi wa makanisa ya Redeemed, kanisa linaloongoza kwa wingi nchini Kenya na kuenea duniani kote). Pia aliyeleta vyeti kutoka marekani  ni Dk. Lee (Mwakilishi wa isom kutoka Marekani)

Mgeni rasmi alimwaga sifa za chuo hicho,kwamba mtaala wake ni wa kimataifa na kinafundishwa na watumishi wenye huduma zinazotikisa Dunia. Baadhi ya waalimu wanaofundisha katika chuo hicho ni: Mwinjilist Rehnard Bonnke, Joyce Meyen, T. L Hosborn na wengine kibao.
Hivyo watu mbalimbli wamehamasishwa kujiunga na chuo hicho chenye mtaala wa kimataifa.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP