4 April 2013

VURUGU KAWE – ALIYEFARIKI NI KIJANA WA MCHUNGAJI





Wananchi wakishuhudia vurugu za Kawe jijini Dar es Salaam


Baada ya Vurugu kubwa zilizotokea huko kawe  baada Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) kudaiwa kumuua dereva wa bodaboda, aliyekuwa akipita eneo iliyodaiwa kuwa raia hawaruhusiwi kupita. Uongozi wa blog hii umeweza kukwasiliana na mzazi wa kijana aliyeuliwa, na kugundua kuwa ni kijana wa Mchungaji Cyprian Mbelwa, wa kanisa la Jerusalem Mito mingi (Moja ya makanisa yanoongozwa na askofu Nyagawa. Kijana huyo wa miaka 18 anajulikana kwa jina la Yohana Cyprian
Kijana huyo alifariki dunia baada mabishano ya muda mrefu kati yake na Askari hao, na kuzuka ugomvi mkubwa ulisababisha kifo chake, ingawa haijajulikana mara moja kama alipigwa risasi ama alipigwa na kitu kizito.
Hata hivyo wananchi wa eneo hilo hawakuweza kuvumilia hali hiyo na kuamua kuingia mitaani na kwenya kuvamia Kituo cha Polisi Cha Kawe kwa ajili ya kumtoa Askari huyo anayeshikiliwa katika kituo hicho. Kitendo cha Wananchi hao kuvai kituo hicho cha Polisi, kiliilazimu Askari Polisi kuwatawanya kwa mabomu ya machozi huku wao wakitumia mawe na kufunga barabara zote zinaao elekea Kawe.
Tuatendelea kukujuza zaidi.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP