10 August 2012

Kampuni ya Msama Promotions yapaswa kuungwa mkono katika hili .



 Mkurungezi wa kampuni ya MSAMA PROMOTION, Bw. Alex Msama (kulia) akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) Cd za video na Audio Cd za Muziki wa aina mbalimbali pamoja na Kompyuta za kudurufu kazi za wasanii kwa njia ya wizi kwenye  kituo kikuu cha Polisi mkoani Dodoma,mara baada ya kukamilisha zoezi la kusaka na kuwakamata wezi  wa kazi za wasanii


MKURUNGENZI wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama akishirikiana na Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata watu mbalimbali, baada ya kudurufu kazi za wasanii zenye thamani ya milioni ya shilingi
Hakika juhudi hizo za Msama zinahitaji kupongezwa na kuungwa mkono. Mfano halisi ni wa vijana kadhaa waliokamatwa hivi karibuni,  vijana hao walikamatwa katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam. Waliokamatwa katika tuklio hilo ni Malik Sultan, Ally Msangi, Edward Michael na Sijali Andrew ambao walikuwa na CD feki 322 za wanamuziki mbalimbali na wasanii wengine.
Pia watu 8 walikatwa hivi karibuni baada ya kudurufu kazi mbalimbali za wasanii  zenye dhamani ya milioni 25, Watuhumuwa hao walipelekwa katika Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam.
Taarifa zilizotufikia jana ni za ukamataji mkubwa wa mitambo na  Cd za video na Audio Cd za Muziki wa aina mbalimbali pamoja na Kompyuta za kudurufu kazi za wasanii kwa njia ya wizi kwenye kituo kikuu cha Polisi mkoani Dodoma,mara baada ya kukamilisha zoezi la kusaka na kuwakamata wezi wa kazi za wasanii,ambapo jumla ya Cd na Computer zenye thamani ya shilingi milioni Sitini na saba zilikamatwa kwa msaada wa Jeshi la Polisi mkoani humo
Pia, miongoni mwa watu ambao wamekuwa na uchungu na wizi wa kazi za wasanii, ni pamoja na Mwl John Shabani, ambaye hivi karibuni kwa juhudi zake binafsi akishirikiana na polisi kituo cha mwenge, aliwakamata watu kadhaa wanaojihusisha na wizi wa kazi  za wasanii kwa njia ya computer na kuwafungulia taarifa yenye namba MNG/1695/2002 katika kituo cha Polisi Mwenge Sokoni Jijini Dar es salaa.

Uongozi wa Blogu hii pamoja na waimbaji mbalimbali wa Injili, tunampongeza sana na kuahidi kuwa nyuma yake, ili kuhakikisha wasanii nchini wanaheshimika na kunufaika na kazi zao.

0 comments:

HEART OF WORSHIP

HEART OF WORSHIP